MUWE NA SHEREHE YA PASAKA ILIYOBARIKIWA WAPENDWA WA KONGAMANO LA AMIGHTYWIND
(Maelezo mafupi ya vile neno hili lilivyokuja)
Usiku uliopita (Aprili 1, 2023) nilichukua usiku mzima kuhudumia dada zangu wapendwa katika YAHUSHUA MASIHI waliokuwa wanahitaji kutiwa moyo na mwongozo. Nilipomaliza ilikuwa Saa 6 Asubuhi na nilikuwa tayari kulala.
Nilishinda nikisikia sauti kama mpigo mkubwa wa moyo kwenye masikio yangu. Nilifikiria kuwa labda nimechoka au nina shida na nikafikiria kuwa moyo wangu unapiga haraka na kwa sauti kubwa kwa hivyo nikaipuuza na kujaribu kuenda kulala wakati sauti hiyo ilipotea. Nilipokuwa ninalala nikaisikia tena kwa sauti kubwa na nikainuka na kuketi na nikauweka mkono wangu kwenye kifua changu na nikagundua ya kwamba sauti hiyo ya mpigo wa moyo masikioni mwangu ilikuwa tofauti na vile moyo wangu na mshipa ulivyokuwa unapiga.
Nikagundua ya kwamba haikuwa mpigo wa moyo wangu niliousikia lakini nilikuwa naisikia katika kiroho. Nilipogundua haya, nikasikia kwa sauti kubwa na uwazi, “MIMI Nimejawa na hasira na moyo WANGU unahuzunika!” Nilidhania ya kwamba nilikuwa nimefanya jambo fulani au kusema kitu ambacho kilimkera YAH. Nikaanza kuomba na kumuuliza BABA YAHUVEH kama kuna kitu kibaya ambacho nimefanya kumfanya YEYE kukasirika? Alafu kukawa na amani na kimya, utulivu na huo mpigo ukaacha. Baada ya kuomba nilijua kuwa ninahitaji kupumzika, kwa hivyo nikaenda kulala.
Nilipoamka na kujitayarisha kwa siku, nikaanza kuisikia tena na kusikia BABA YAH akisema vile Alivyokuwa na hasira. Sikuweza kuelewa kwa nini na nikaendelea kuomba nilivyokuwa ninaenda jikoni kutafuta kitu cha kukula. Ndipo nilipohisi kuwa nilikuwa na uzito mkuu kwenye Kiroho na nilijua lazima niombe. Nilijua Neno linakuja na nikamwambia Mama kuwa nilikuwa ninasikia Neno likija. Nikaanza kuomba katika ndimi na neno hili likatoka siku ya 2 Aprili 2023.
Ninaomba kuwa YAHUSHUA MASIHI anataka tuwe na uhusiano NAYE. Sio tu dini au ibada, ni uhusiano na kuwa na uwezo wa kutoa nyoyo zetu KWAKE. Hatuwezi kusema, “Moyo wangu ndio huu YAHUSHUA MASIHI,” na tena kuichukua kutoka kwa Mikono YAKE. Ninaelewa kuwa Unabii huu waweza kuwakera wengine na kuwabariki wengine. Kama Mama Elisheva amesema, hii ndiyo gharama lazima tulipe kwa Upako huu, lakini sio kitu ukilinganisha na kile ambacho YAHUSHUA MASIHI Alipitia Alipotoa maisha YAKE kwetu sisi wakati huu Mtakatifu. Nimebarikiwa na kunyenyekea sana kuwa BABA YAHUVEH Amechagua kuzungumza kupitia MIMI kwa Utukufu na Heshima YAKE pekee.
YAHUSHUA MASIHI Awabariki tunaposherehekea pamoja Sherehe ya Mkate usio na chachu kuheshimu Mbinguni. Katika jina na upendo wa YAHUSHUA MASIHI, Grace.
UNABII – Acheni Michezo! YAHUVEH Amekasirika!
Aprili 2, 2023
Grace anaomba katika Ndimi Takatifu, akilia.
O NIMEKASIRIKA! NIMEJAWA NA HASIRA! Moyo WANGU umehuzunishwa kwa watu-wanaojiita WANGU, mnajaribu kutoa visingizio ili msisherehekee Sherehe ZANGU Takatifu!
NIMEJAWA NA HASIRA! Vile moyo WANGU umehuzunika kwa sababu ya kizazi hiki! Na wewe binti yangu umehisi hasira yangu siku mzima, malalamiko yangu.
Nyinyi watu mmekuwa mkisherehekea sherehe ZANGU kwa miaka, HATA HAMNA HAYA KUNIULIZA MIMI KAMA NI SAWA KULA CHACHU!
NYINYI WATU MNAOTOA VISINGIZIO ILI MSISHEREHEKEE SHEREHE TAKATIFU, HAMNA HAYA!
KAMA MNATAMANI DUNIA SANA, NYINYI SIO BIBI ARUSI WANGU!
KAMA MNAKATAA KUTII MIMI YAHUVEH, NYINYI SIO BIBI ARUSI WANGU!
NYINYI MNAOOGOPA DUNIA ZAIDI YA MIMI, NYINYI SIO BIBI ARUSI WANGU! KWA KUWA BIBI ARUSI WANGU WANAJUA SAUTI YANGU! WANATII MBINGUNI!
KAMA MNAKATAA KUTEMBEA KATIKA UTAKATIFU, NYINYI SIO BIBI ARUSI WANGU!
KAMA MNAKATAA KUSHEREHEKEA SHEREHE ZANGU TAKATIFU, NYINYI SIO BIBI ARUSI WANGU!
KAMA MNAKATAA KUEPUKA DHAMBI, NYINYI SIO BIBI ARUSI WANGU!
KAMA MNAKATAA KUNITII MIMI YAHUVEH NA KUMKATAA SHETANI, NYINYI SIO BIBI ARUSI WANGU!
NIMECHOKA! WAKATI UNAENDA! SICHEZI MCHEZO HUU NANYI TENA KWA KUWA MWANA WANGU YUAJA HIVI KARIBUNI! NA NI BIBI ARUSI WANGU TU NA WATOTO WANGU, WANAOSIKIA SAUTI YANGU WANAVYOKUJA! KWA KUWA MOYO WANGU UMEHUZUNIKA! UMEHUZUNIKA! KUWA MNAWEZA KUWA WABINAFSI KUJIFIKIRIA NYINYI WENYEWE, WAKATI MIMI, NILIMTUMA MWANA WANGU, MWANA WANGU WA KIPEKEE KWA DHAMBI ZENU NA HAMNA HAYA KUULIZA KAMA MNAWEZA KULA CHACHU LAKINI BADO MSHEREHEKEE PASAKA? HILO NI SWALI LA AINA GANI? SIO SHEREHE YA MKATE USIO NA CHAHU KWA KUWA MMECHAGUA KULA CHACHU!
NENDENI! NENDENI! NENDENI! NENDENI! ENYI WAFANYIKAZI WA SHETANI KWA KUWA SIJAWAHI KUWAJUA!
KAMA MPO HAPA TU KUPOTEZA WAKATI WANGU, BASI NENDENI!
MSINIKASIRISHE MIMI YAHUVEH! MKICHAGUA KUTOTII SHEREHE TAKATIFU, NITAPAMBANA NANYI KWA KUWA WAKATI HUU NI WAKATI MTAKATIFU SANA! NA BADO, KILE TU MNACHOFIKIRIA NI NYINYI WENYEWE.
AIBU KWENU! AIBU KWENI! AIBU KWENU!
KAMA MNATAMANI DUNIA, NENDENI! MSIRUDI!
NYINYI WATU MNAOSEMA MNANIPENDA MIMI YAHUVEH, LAKINI HAMNITII, NYINYI SIO WANGU!
NYINYI AMBAO MNAKANYAGIA DAMU YA MWANA WANGU, YAHUSHUA MASIHI, NYINYI SIO BIBI ARUSI WANGU!
NYINYI MNAOPANGA KUTENDA DHAMBI, NYINYI SIO BIBI ARUSI WANGU!
KAMA MNAKATAA KUACHA DHAMBI ZENU NA KUEPUKA MAOVU, NYINYI SIO BIBI ARUSI WANGU!
MSIPOTEZE WAKATI WANGU! MSIPOTEZE WAKATI WA WAHUDUMU WANGU KWA KUWA KUNA NAFSI WENGINE WANAOHITAJI KUHUDUMIWA ZAIDI! CHAGUENI LEO NI MUNGU MGANI MTAKAYEMTUMIKIA!
HUU SIO WAKATI WA MICHEZO! SICHEZI MICHEZO NANYI! NA MNAFIKIRIA KUWA SIONI, MNAFIKIRIA KUWA SISIKII, MNAFIKIRIA KUWA SIONI NIA ZA NYOYO ZENU.
NINAWAONYA NYINYI WATU TENA, ROHO MTAKATIFU, RUACH HA KODESH MPENDWA, IMMAYAH, HATAKAA KWENYE CHOMBO KICHAFU!
CHAGUENI LEO NI MUNGU MGANI MTAKAYEMTUMIKIA!
KAMA NI DUNIA, BASI CHUKUA VIRAGO VYENU NA TOKENI! LAKINI KAMA MMECHAGUA MBINGUNI BASI TUBUNI DHAMBI ZENU NA ZIACHE NYUMA NA MSITENDE DHAMBI TENA! (1 Petro 1:16)
Michezo imeisha! Michezo imeisha! Kwa kuwa wakati Mtakatifu waja! Na mkumbukeni kile ambacho MWOKOZI wenu aliwafanyia! Mkumbukeni nini MIMI YAHUVEH nilichowafanyia!
Nyinyi ambao mnataka kutoka, kama mnataka kutoka kwenu, basi kwanza lazima mjisalimishe. Lazima mjisalimishe kwa YAHUVEH! Sitaki nyoyo nusu! Nimechoka na nyoyo nusu! (Mathayo 12:25)
Je, mwaona wazimu ulio kote duniani! Nyinyi wazazi ambao mna watoto wachanga, ni jukumu lenu kuwafunza watoto wenu kama bado ni wachanga! Ni jukumu lenu kuwafunza watoto wenu kuhusu Utakatifu, kuhusu hizi Sherehe Takatifu! Kwa kuwa Mwanzo wa Hekima ni Kumcha YAHUVEH! (Mithali 9:10) Msiache kumcha MUNGU!
Ninawaita Bibi Arusi WANGU, NJOONI! NJOONI! Kujeni pamoja! NJOONI! Kama tu kulivyokuwa na mafuriko makuu ya maovu, njooni Bibi Arusi WANGU, kwa kuwa nitainua kiwango dhidi yake! (Isaya 59:19) Lakini sitawapokea watu wa roho nusu tena!
Jisalimisheni! Jisalimisheni! Kondoo WANGU wanajua sauti YANGU! Na ninasema, njooni! Njooni! Njooni katika Safina yenu ya usalama! Kwa kuwa mafuriko ya uasi utazidi kuwa mbaya zaidi! Njooni! Njooni! Njooni kwenye Mikono YANGU! Njooni kwenye Safina yenu ya usalama! (Zaburi 132:8) Na nyinyi wachache ambao hamna shukrani kwa yale ambao Nimewapa, jihadharini! Msidhanie kuwa michango yenu pekee itawaokoa! Ni nyoyo zenu ninazotaka! Sio pesa zenu! Hamwezi kusema, “YAHUSHUA Ninakupenda” alafu bado mmeshikilia na kukatalia dunia! Jisalimisheni! Jisalimisheni! Jisalimisheni kwa yote! Leo ndiyo siku yenu ya wokovu! Kesho yaweza kuwa mmechelewa!
Mwisho wa Neno
Halleluyah! Asante! Asante! Asante BABA YAHUVEH, YAHUSHUA MASIHI na MAMA IMMAYAH! Poleni sana kuwa nyoyo ZENU zimehuzunika! Twaomba watoto WAKO Watakatifu, watoto WAKO wa kweli, Bibi Arusi WAKO wajisalimishe kwako! Amina! Amina!
Maandiko:
1 Petro 1:16
“Kwa maana imeandikwa: “Mtakuwa watakatifu, kwa kuwa Mimi ni mtakatifu.”
Mathayo 12:25
“Yesu alijua walichokuwa wakiwaza, akawaambia, ‘‘Kila ufalme ukigawanyika dhidi yake wenyewe huangamia. Hali kadhalika kila mji au watu wa nyumba moja iliyogawanyika dhidi yake yenyewe haiwezi kusimama.”
Mithali 9:10
“Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima na kumjua Mtakatifu ni ufahamu.”
Isaya 59:19
“Kuanzia magharibi, watu wataliogopa jina la BWANA na kuanzia maawio ya jua, watauheshimu utukufu wake.
Wakati adui atakapokuja kama mafuriko, Roho BWANA atainua kiwango dhidi yake na kumfukuza.”
Zaburi 132:8
“Inuka, Ee BWANA, uje mahali pako pa
kupumzikia, wewe na sanduku la nguvu zako.”
Bonyeza hapo chini kusikiza kinaza sauti cha unabii