Ombi La Wokovu.
Jinsi ya Kuirithi Zawadi BURE ya Uzima wa Milele.
Je, Ubatizo ni Jambo Muhimu Kwa Kupata Wokovu?
*******
YAHUSHUA Mpendwa,
Nakukubali sasa kama BWANA na MWOKOZI wangu, Wewe ndiye Mungu ninayependa. Naamini ya kwamba ulilipa
gharama ya dhambi zangu pale Kalvari, ulikufa na kufufuka katika siku ya tatu. Nauliza uje moyoni
mwangu, nisamehe dhambi zangu, nioshe niwe msafi wa udhalimu wote. Pole kwa kutenda dhambi, na
nageuka kutoka kwa dhambi hizo. Asante kwa kunijaza na Roho Mtakatifu wako, na kunipa hamu ya
kukutumikia siku zote za maisha yangu, na uishi maisha yako ndani yangu YAHUSHUA, ili Utukuzwe!
Asante kwa kunipa hamu ya kusoma Bibilia, na kunipa hekima niielewe. Asante kwa Kunipenda na Kuokoa
roho yangu, ikisababisha Imani yangu kukua, ili siku moja nitakuwa na WEWE Mbinguni. Nijaze na Roho
Mtakatifu wako sasa na niokoe kutoka kwa yule muovu katika jina lako YAHUSHUA Naomba! Nisaidie
YAHUSHUA kukumbuka wote wametenda dhambi na kupungukiwa na Utukufu wa YAHUVEH, na ulikuja kutuokoa
sisi watenda dhambi, ndio sababu wewe huitwa MWOKOZI wetu. Amina.
*******
Soma ombi hili alafu isome tena, wakati huu BILA maarifa ya kichwa lakini na moyo wako wote, iamini
kwa IMANI, na kumbuka YAHUSHUA SI Mungu Pekee, lakini YEYE ni rafiki wako wa dhati! Anakujali sana,
Anakupenda sana. Jinsi vile ulivyo. Anachukia Dhambi, lakini Anakupenda WEWE, mtenda dhambi!
YAHUSHUA alilipa gharama ya dhambi zako, sasa hufai kujisikia kama mwenye hatia au aliyehukumiwa
tena! Ungama dhambi zako kwa YAHUSHUA. Zitaje, alafu mwambie pole, muulize akusamehe! Dhambi zako
zote za zamani na sasa. Dhambi ni kitu chochote ulichofanya au unachofanya kinchomchukiza YAHUVEH
Mtakatifu. Hakuna mtu aliye bora zaidi kushinda mwingine! Kumbuka haya!
Soma Agano Jipya ili upate kujua YAHUSHUA ni nani. (Yohana 3:16) Bibilia husema lazima umwungame
Yeye kama BWANA na Mwokozi ili Akuungame mbele yake Baba. Usione aibu kumjua YAHUSHUA, kwani Yeye
HAONI aibu kukujua WEWE. Ambia mtu ya kwamba umemkubali YAHUSHUA wa Kalvari na Nazareti, siku hii na
malaika wote mbinguni wanashangilia.
Turuhusu tushangilie nawe. Kama unahitaji Mchungaji, tuna wengi zaidi ya mmoja. Karibu katika
Familia ya YAHUSHUA! TUNA MATUMAINI YA KWAMBA TUTAKUTANA NAWE MBINGUNI, KAMA SI HAPA DUNIANI!
Tuma Barua Pepe kwa Elisabeth na umueleze juu ya zawadi ya uzima wa milele ambayo umerithi kutoka
kwa YAHUSHUA Masihi wetu Mpendwa!
[email protected]
*******
Rudi Kwa Ukurasa Wa Wokovu
Je, Ubatizo ni Jambo Muhimu Kwa Kupata Wokovu?
Ubatizo, Mto wa Yordani
Mbatizwe. (Ona Matendo ya Mitume 2:38, 39)
Kubatizwa inamaanisha kutumbukizwa kwenye maji. Wakati mwingine, mtu husimama ndani ya maji alafu
hutumbukizwa majini (na Mkristo mwenzake) kisha huinuliwa kutoka majini na kusimama tena. Umuhimu wa
kitendo hiki unaonekana katika Kitabu cha Warumi 6:1-7 na zoezi hili hupatikana katika Kitabu cha
Matendo ya Mitume 8:26-39.
Watu wengine hufikiria ya kwamba ubatizo si moja ya vitendo ambavyo ni ishara ya kumkubali YAHUSHUA.
Hata hivyo, jambo moja ni wazi katika Bibilia. Imani na ubatizo huwa pamoja kila wakati,
hazijatenganishwa. Kwa hivyo, ni wazi ya kwamba Ubatizo ni ishara ya kumkubali YAHUSHUA.
Tunawahimiza wote mtafute sababu za ubatizo katika Bibilia. Mkristo yeyote wa kweli anaweza
kukubatiza.
Kubatizwa na maji ni njia moja. YAHUSHUA alisema, “Yohana alibatiza na maji lakini YAHUSHUA hubatiza
na MOTO wa ROHO MTAKATIFU!” Baada ya kubatizwa na maji, ULIZIA kujazwa kwa MOTO wa ROHO MTAKATIFU!
Hivi ndivyo zawadi za ROHO MTAKATIFU hupatikana! Kwa hivyo, usiamini ya kwamba KAMA hauna hizi
zawadi au huwezi kuzungumza katika ndimi takatifu, hautaenda Mbinguni! Hili ni funzo la uongo! Jambo
hili lingekuwa kweli, basi YAHUVEH angesema vivyo hivyo kwa uwazi ya kwamba wote ambao hawawezi
kuzungumza katika ndimi takatifu HAWATAOKOLEWA! Tena, lingekuwa kweli, hakungekuwa na haja ya
YAHUSHUA kupeana maisha yake na kumwaga damu pale Kalvari! Ni Damu yake YAHUSHUA Pekee inayoosha
dhambi zote kwa wale wanaokubali ZAWADI hii kwa IMANI!
Kanisa zingine hufunza KAMA mtu hajabatizwa, hata mtoto mdogo, basi huyo mtu hataenda Mbinguni!
Jambo hili lingekuwa kweli, kwa nini basi YAHUSHUA alijitolea pale Kalvari? Ubatizo ni ishara wazi
kwa wote kuona ya kwamba tunamfuata YAHUSHUA! Watoto wadogo hawawezi kuyaelewa haya vizuri, kwa
hivyo HAIFAI kuwabatiza mpaka watakapoweza kuelewa gharama ambayo mtu anafaa kulipa ili kumfuata
YAHUSHUA. Inafaa watoto wachanga waletwe mbele yake Baba wanapozaliwa, SI kuwabatiza, kwa sababu
lazima waamue wenyewe wakiwa wamekua.
Kwa hivyo, badala ya kuangalia ubatizo kama kitu ambacho LAZIMA ufanye, bali na kumkubali YAHUSHUA
kama Bwana na Mwokozi wao, ili waokolewe… lazima mtu ATAKE kufanya jambo hili, ili kuruhusu kujazwa
kwa Roho Mtakatifu na kuonyesha kila mtu ya kwamba wana uhusiano na kifo na kufufuka kwa Mwokozi
wao, YAHUSHUA Ha Mashiach!