Unabii 101

MIMI, YAHUVEH, Nasema, “Matendo Yako Yazungumza Zaidi ya Maneno Yako.”

Imeandikwa/Kuzungumzwa katika upako wa RUACH ha KODESH Kupitia Mtume Elisabeth Elijah (Elisheva Eliyahu) Oktoba 2, 2008 Saa tisa asubuhi

Rosh HaShanah

Haya yanatoka kwa Unabii 105, YAHUVEH Alisema kuyaweka haya katika Unabii zote kutoka wakati huu: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote kwa haya lililofanyika kwa mkono wako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye kinywa cha RUACH ha KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa Upepo wa SHKHINYAH GLORY Unaovuma kote duniani, Upepo Takatifu wa Uamsho. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)

Katika mwezi wa Julai 2010, YAHUVEH MUNGU pia Alisema kuongezwe yafuatayo kutoka Kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati kabla kila Unabii:

2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi ghadhabu ya BWANA juu ya watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

* * * * * * *

[Msimamizi wa tovuti] alikuwa anafanya kazi kwa maelezo ya Siku 10 za Hofu kuiweka kwenye mtandao wa Huduma na akaniuliza mimi kama nilikuwa na kitu cha kuongezea pamoja na maelezo ya vile YAHUSHUA MASIHI wetu Anavyohusiana na huu wakati Mtakatifu. Nilipoanza kumuuliza YAHUVEH niseme nini, funzo hili likaja, pia kwa mshangao wangu, Unabii mpya ulizaliwa katika siku ya kwanza ya Rosh haShanah, Oktoba 2, 2008.

Haya ndiyo niliyoyasikia kuhusu funzo la Siku 10 za Hofu.

Huu ni wakati tunatafakari uhusiano wetu na YAHUVEH na YAHUSHUA na kama tuna uhusiano wa upendo na wa kutii nao. Sisi sote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa YAH kwa sababu hakuna yeyote ambaye ni kamili aliyetembea duniani humu ila tu YAHUSHUA MASIHI wetu. Hata fikra mbaya ni dhambi. Wayahudi Halisi hawaamini kuwa Masihi Amekuja kwa hivyo hawana dhabihu ya damu kwa upatanisho wa dhambi zao. Wanamkataa YAHUSHUA MASIHI wetu kama MASIHI na kama mwana wa kipekee wa YAHUVEH.

Wakati huu Mtakatifu sio wakati tu wa kusherehekea lakini ni wakati wa hofu kuu kwa wale ambao hawajui kama majina yao yameandikwa katika Kitabu cha uzima cha MwanaKondoo. Sisi tunaomtumikia na kumuabudu YAHUSHUA MASIHI wetu Aliyefufuka tunajua kuwa kuna mwombezi mmoja tu mbele ya Muumba YAHUVEH na njia ya pekee hadi mbinguni kupitia jina la MASIHI wetu YAHUSHUA na Damu iliyomwagwa pale Kalivari. YAHUSHUA MASIHI wetu Ndiye dhabihu ya damu. Sisi Wayahudi wa Kimasihi sio lazima tulie au kuhuzunika wakati wa Yom Kippur kwa sababu hatuna kifuniko cha dhambi zetu, kama wale wanaomkataa YAHUSHUA wanavyofanya.

MIMI, YAHUVEH, Nasema, “Matendo Yako Yazungumza Zaidi ya Maneno Yako.”

Hapa ndipo YAHUVEH Alivyoanza kuzungumza.

Hivi Ndivyo Nisemavyo MIMI, YAHUVEH, msingoje kutubu dhambi zenu, fanyeni haya haraka. Msiwe na mfano wa utakatifu, lakini hamna utakatifu ndani yenu. Kila fikra lilete KWANGU MIMI, YAHUVEH. Msipange kutenda dhambi, epukeni maovu, na msitoe visingizio vya dhambi. Acheni kumlaumu shetani kwa fikra zenu na matendo, kwa kuwa hawezi kufanya chochote bila nyinyi kumruhusu kuyafanya haya kuwapitia. Ninazungumza maneno haya kwa nyinyi mnaosema kuwa nyinyi ni wa YAHUSHUA MASIHI, mnaosema kuwa mmeoshwa katika Damu ya YAHUSHUA MASIHI iliyomwagwa, mnaoomba katika jina la YAHUSHUA MASIHI na bado MIMI, YAHUVEH, Ninawaonya sasa kwa wale wanaodai upendo KWANGU MIMI na Mwana WANGU YAHUSHUA, Ninajua nyoyo zenu na matendo yenu yanazungumza zaidi ya maneno yenu!

Acheni kumjaribu RUACH ha KODESH, acheni kumhuzunisha Roho WANGU. Dunia hii inasimama kwenye mwisho ya jabali, na jabali hili ni Dhiki Kuu. Iteni YAHUSHUA MASIHI sasa kama bado kuna wakati. Katika Yom Kippur katika Siku hizi 10 za Hofu kumbukeni, Ninasikia tu maombi ya wale ambao ni wanyenyekevu moyoni. Msiwe na kiburi katika wokovu wenu.

Katika nyakati za kale watoto wa Israeli walitenda dhambi dhidi YANGU. Walichukua dhahabu yao na fedha Niliyowapa kama Baraka na wakaitengeneza kuwa ndama ya dhahabu kuiabudu na kuiinamia, hakuna tofauti hata sasa hivi. Dunia hii huchukua dhahabu na fedha na huinama kwa wale matajiri na kuwaabudu, lakini Ninawaonyesha Ninapotingiza dunia hii kama mnavyopika popcorn kwenye meko na wale ambao wamejawa na kiburi, wale matajiri, waliosema kuwa wao ni mungu, hawahitaji mungu mwingine, wanakejeli Maneno YANGU Takatifu, wanakejeli Amri ZANGU Kumi, wanachafua yote ambayo ni takatifu, na kama popcorn zilizopikwa sana mtanusa uvundo huo mtakapowaona wamechomeka.

Ole kwa wale waovu, wanaume waovu wanaojiita wachungaji. Nyinyi mliochukua jina la kanisa na kuwatumia watu walio na njaa ya kiroho kujenga ufalme zenu za pesa. Mtachomeka na ufalme zenu za pesa MIMI, YAHUVEH, Nitazirarua na Mikono YANGU na mtafunuliwa kwa uovu ambao mnao. Sitawapa pole Sodoma na Gomora, ole kwa dunia hii ambao wanafuata nyayo zao! Mko kwenye mwisho wa jabali na ni wale tu walio na uhusiano wa upendo na wa kutii na MIMI, YAHUVEH, na YAHUSHUA MASIHI watakaookolewa. Tubuni leo kwa kuwa kesho mtakuwa mmechelewa.

Mipango ambayo maadui wanayo, katika serikali na katika ufalme wa shetani ni ya uovu, kuiba, kuua na kuharibu. Kuwafanya muwe njaa, kuweka sumu kwenye hewa mnayopumua. Kufanya jaribio na maji mnayokunywa, ambapo aina tofauti ya sumu tayari zinachafua maji yenu. Matajiri wanataka kupunguza idadi ya watu hapa duniani, kuhifadhi rasilimali kwao wenyewe, lakini MIMI, YAHUVEH, Nasema, ni MIMI Nitakayekuwa na neno la mwisho. Sitakejeliwa MIMI. Nitawalinda wale ambao ni WANGU na silaha zao maadui zitawaangamiza.

Sasa ndio wakati wa kusimama na kuchukua hatua kwa Utakatifu kama bado mwaweza. Acheni kucheza na shetani na watumishi wa shetani. Ogopeni kunikera MIMI, YAHUVEH, zaidi ya kuwakera wanadamu tu.

Mwisho wa Neno la Kinabii.

Kumbukumbu la Torati 31:8 – YAHUVEH Mwenyewe huenda mbele yenu na Atakuwa nanyi, hatawahi kuwaacha. Msiogope, msife moyo.

Imepewa kupitia Mtume Elisabeth Elijah (Elisheva Eliyahu)

Rosh haShanah Oktoba 2, 2008 Saa tisa asubuhi



CLICK HERE or the image below to go directly to her youtube channel
YAHSladyinred