Unabii wa 105
MIMI, YAHUVEH, Nasema, Katika Mwaka Wa 2009 Nitatingiza Kila Kitu Kinachoweza Tingizika!
Imeandikwa/Imezungumzwa katika upako wa RUACH ha KODESH kupitia Mtume Elisabeth (Elisheva) Elijah. Disemba 29, 2008
Kumbukumbu: Neno hili la Unabii lilipewa kwetu kama Neno la kipekee kwetu. YAHUVEH alisema tuweke sehemu hii ya Neno kwa Waaminifu na Wakweli WAKE hii 2009.
***********
[Aya hii ya kwanza iliongezwa siku ya Januari 8, 2009. Niko alisahau kuiongeza kutoka kwenye Neno ya kwanza iliyopewa siku ya Disemba 29, 2008. Nitafanya nini naye? Natafakari nitamweka tu.]
Nilikuonya kitambo Elisabeth kutoita huduma hii kwa jina la mwanaume au mwanamke hata kabla kuwepo na huduma. Niliiweka ndani ya roho yako kwa kuwa hakuna lolote kwa haya lililofanyika kwa mkono wako au lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye kinywa cha YAHUVEH aliyeizalisha. Ilitoka kwenye kinywa cha YAHUSHUA, MASHIACH wako aliyeizalisha. Ilitoka kwenye kinywa cha RUACH ha KODESH, IMMAYAH wako aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa upepo wa SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, upepo Takatifu wa uamsho, sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)
*********
Katika mwaka wa 2009 nitatingiza kila kitu kinachoweza tingizika. Kama hujajengwa juu ya Mwamba Imara, utajengwa kwenye udongo unaoporomoka. Itakuwa kama mchanga unaozama haraka na utazama. Ninamjaribu Bibi Arusi Wangu. Nilipokuambia enda ulienda, hukusema, “Lakini mbona ni lazime tuende?” ulitii tu. Mimi ndiye Kamanda Mkuu, hufai kuyadharau maagizo YANGU. Unafaa kuenda popote ninaposema uende, unafaa kukaa popote ninaposema ukae, unafaa kutembea ninaposema tembea, unafaa kukimbia ninaposema kimbia, unafaa kuzungumza ninaposema zungumza, unafaa kunyamaza ninaposema nyamaza, unafaa kupigana ninaposema pigana, unafaa kukaa kwa imani ninaposema kaa kwa imani.
Usiwahi sema kuwa MIMI sitafanya kitu kwa sababu MIMI, YAHUVEH, nitakutia fadhaa. Usije kufikiri ya kuwa unajua matakwa YANGU, bali tafuta matakwa YANGU. Kwa wale Waaminifu na walio Kweli, haya ndio Maneno ya 2009 ninayowapa na hata kama bado sio 2009 sehemu hii itawekwa mbele ya dunia. Kupitia tu Jina na Damu iliyomwagwa ya YAHUSHUA, MASHIACH wako ndio mtaweza kusimama.
Tena Ninasema kila kitu na chochote kinachoweza kutingizika kitatingizwa, kwa hivyo jitayarisheni sasa ninapowaonya katika mwaka wa 2008. Chochote ulicho nacho ithamini, ithamini chakula chako, ithamini mshahara wako, ithamini nyumba yako, ithamini familia yako na familia yako ni wale wanaoshiriki katika mwili wa YAHUSHUA MASHIACH. Kwa kuwa utapata maadui wako wabaya tena zaidi wanaweza kupatikana katika nyumba yako kupitia damu yako ya kuzaliwa lakini sio kupitia damu yake ya kuzaliwa YAHUSHUA, MASHIACH wako. Hii ndio familia yako ya kweli, hawa ndio wale ambao hawatakusaliti.
Mnakaribia sasa kama ile tarehe ya mteketeo. Jifunze vizuri kutoka kwa wale walioishi, na kwa wale ambao hawakushikwa. Utii wako ni kwangu MIMI, YAHUVEH, sio kwa sheria za binadamu. Kama hazisikizani na kile Ninachosema zitupe mbali. Unajua Neno linasema nini. Kwa sababu Nitakuambia ufanye kile usichofikiria, Nitakuambia useme kile usichofikiria, Nitakuficha kwa njia usiyofikiria.
Ilipewa kupitia Mtume Elisabeth (Elisheva) Elijah Disemba 29, 2008
Kama Unabii huu umekubariki tafadhali nitumie barua pepe uniambie.
Contact AmightyWind
www.allmightywind.com
www.almightywind.com