UNABII WA 11
INUKENI, ZUNGUMZENI, AMBIENI SHETANI ANYAMAZE KATIKA JINA LANGU!
Imepewa kwake Mtume Sherrie Elijah
* * * * * * *
Haya yanatoka kwenye Unabii 105, YAHUVEH Alisema iwekwe mbele ya Unabii zote kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], Kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote kwa haya lililofanyika kwa mkono wako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako iliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY Unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)
Katika mwezi wa Julai 2010, YAHUVEH MUNGU pia Alisema kuongezwe yafuatayo kama onyo kwa wale wanaokejeli:
2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii Wake, hata ilipozidi Ghadhabu ya Bwana juu ya watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”
* * * * * * *
Msizuie karama ambazo Nimewapa, wengi huitwa, wachache huchaguliwa. Vikosi vya Gideoni waliitwa, lakini wachache walichaguliwa. Baba YAHUVEH aliwaondoa. Mpendwa WANGU, hivi ndivyo asemavyo YAHUVEH, jua haya, Sijakuita kufeli, bali kufaulu katika JINA LANGU. MIMI huwa sianzi kazi nzuri halafu siimalizi. Huu mwito si wa kwako bali ni WANGU. Je, si Neno LANGU husema, “MIMI huchagua wale wadhaifu ili nguvu YANGU idhahirike?”
Wote watajua kuwa si wewe unayefunza lakini MIMI Ninayefunza kupitia viombo vya udongo vyenye upako. Sherrie (Elisabeth) hawezi na hachukui sifa kwa chochote anachonifanyia MIMI, kwa kuwa anajua si ya kwake bali ya KWANGU. Anajua sasa hivi kuwa Ninazungumza kupitia kwake hadi kwenu. Madaktari ambao huchanganya akili za watu wangesema huu ni ugonjwa wa akili, lakini kujitoa kwa yule aliyekupa mdomo, hisia, na akili si ugonjwa wa akili.
Lakini kwa kukubali au hata kuamini YAHUVEH anaweza hata kuzungumza kupitia mtu, ambaye madaktari wanafikiri kuwa ni ugonjwa wa akili. Hakungekuwa na Bibilia kama wangefaulu kuwashawishi Wanafunzi WANGU juu ya haya. Ndio, kuna bandia na hawa watu ni wagonjwa akilini lakini Nabii WANGU si mmoja wao. Shetani husababisha ugonjwa wa akili na walio wagonjwa akilini wanahitaji ukombozi. Je, si wangemshtaki Petero aliyetembea majini kama anayetaka kujitoa uhai? Udanganyifu mkuu. Watoto watatu wa Kiebrania, si wangesema, hao watoto wa Kiebrania waliotupwa ndani ya tanuu yenye moto, walikuwa na akili ya shahidi na pepo za kujitoa uhai?
Lakini mwili upo katika vita kila wakati na RUACH ha KODESH (ROHO MTAKATIFU) ndani yako. Lazima uushinde mwili ili kuhudumu. Unaweza kufaulu ukifanya haya katika JINA LANGU. Lakini kuna vita kila wakati. Baada ya kila Unabii Nabii WANGU hupigana dhidi ya miili yao inapoinuka na kusema, unadhani wewe ni nani kuzungumza kwa watu wa YAHUVEH na kusema YEYE Ameizungumza? Haya yasipofanyika kwa Nabii WANGU na wakatae kukubali kuhusu vita hii, basi MIMI sizungumzi kupitia kwao.
Ishara kamili kuwa Roho WANGU Amezungumza au ameandika kupitia mtu ni kama wamekutana na ile sauti, inayowafanya wafikirie huyu ni wewe kweli YAHUVEH? Huyu anayewaandikia sasa, dada yenu huwa na hii vita mara kwa mara kwa kuwa anahisi hastahili kutumiwa kwa njia hii. Lazima Nimkumbushe Nitakavyowakumbusha wengine kwa kufanya haya yapewe kwa wengine, je, mnafikiri kweli kuwa mnaweza kuzungumza vizuri hivi, na mkiwa mmejazwa na nguvu za upako? Je, mnafikiri kweli kuwa mna hekima hii yote? Daima Nabii WANGU wa Kweli lazima waseme, “Ni kweli, haya hayawezi kuwa mimi.” Je, mnadhani kweli kuwa mna ujasiri wa aina hii?
Basi sema, “Nisamehe, Baba wa Mbinguni lazima huyu ni wewe, kwa kuwa siwezi, wala sina hamu ya kufanya kitu kama kusema, hivi ndivyo Asemavyo YAHUVEH wakati huo sio ukweli.” Hii ndio ishara ya Nabii wa kweli; wao hushuku mwili, lakini huamini RUACH ha KODESH anayewatumia. Wanajua kuwa hawawezi kufanya chochote au kuwa na hamu ya kufanya chochote bila RUACH ha KODESH kuwapa upako wa kuyafanya. Acheni kuogopa karama Nilizowapa. Sitawalazimisha kuwalisha Kondoo WANGU na bado mtaenda Mbinguni, lakini zawadi zenu hazitakuwa kuu na Nitamwinua mwingine kujaza nafasi ambapo ulifaa uwe. Kuna nafsi wanaokungoja uwahudumie.
Uoga ni kinyume ya imani. Tena Ninazungumza thibitisho, lakini msiendelee kunijaribu MIMI, kwa yale ambayo tayari Nimedhibitisha. Wakati ni mfupi. Kuja KWANGU ni kwa muda mfupi, fanyeni mtakayonifanyia MIMI sasa, sio baadaye. Sasa ndipo Ninapohitaji Wahudumu WANGU, Mashujaa WANGU. Sasa ndipo Ninapohitaji wale waliochaguliwa kukusanya mavuno ya nafsi. Sasa ndipo Ninapohitaji nyinyi kuwa wavuvi wa wanaume na wanawake. Sasa ndipo Ninapohitaji Nabii WANGU kuzungumza. Sasa ndipo Ninapohitaji wainjilisti, Roho kama Yohana Mbatizaji kujitokeza. Sasa ndio wakati wa wokovu, kesho waweza kuchelewa. Ni wengi sana walioitwa hungoja hadi kesho mpaka vile hali itakapokuwa sawa kwao. Kumbe kesho na hali sawa hazitawahi kuja kwao. AMKENI, hii ni hila ya adui.
Hila nyingine ya adui ni, “Mimi sistahili kufunza Injili ya YAHUSHUA, nina shida nyingi sana. Nina mambo ya kale ambayo yananiletea aibu, hauwezi kunitumia mimi”. AMKENI, MIMI Ndiye Ninayechagua ni nani atakayenitumikia MIMI, sio nyinyi. Je, sikumchagua Paulo kunitumikia MIMI na yeye alikuwa muuaji wa maelfu wa Wakristo. Je, mambo yake ya kale yawezaje kuwa mbaya zaidi ya hayo? Lakini bado, Nilichukua mambo hayo ya kale na Nikaitumia kwa Sifa, Heshima na Utukufu WANGU. Kile shetani alipangia kwa mabaya Nimeigeuza kwa uzuri wenu. Haya ndiyo MIMI hufanya; MIMI siwaiti watu katika huduma hii ambao hawajateseka. Hawangeweza kuhisi mateso ya watoto WANGU. Hamjui vipi kidonda kinavyoumiza, hadi wewe mwenyewe ukajeruhiwa.
Ni nani bora wa kuwachunga kondoo wangu walioumia kushinda yule ajuaye uchungu huo? Hautajua vipi ya kumleta mtu kutoka kwa dhambi na kwenye msalaba wa Kalvari, kama wewe mwenyewe haukuwa na chochote kile cha kufanana nao. Mwenye dhambi aliyeokolewa kwa neema. Je, utahudumu vipi kwa wale walioanguka kama wewe mwenyewe hata wakati mmoja ulifikiria kuwa umepoteza imani KWANGU. Udhaifu wako mkuu Nitafanya iwe nguvu yako kuu, kwa kuwa Nitaitumia hiyo udhaifu na kukusaidia kuishinda, na kuthibitisha uwepo wa YAHUSHUA. Nitakapothibitisha kuwa umechaguliwa, usisimame pale na kuniuliza MIMI, “Mbona mimi?” Jua tu MIMI ni ‘MIMI NIKO’ mkuu na MIMI sifanyi makosa. Ingawa, bado chaguo ni lako kama wataka kunitii. Lakini hautakuwa na amani yoyote na kamwe utakumbuka kuwa haukutii mwito WANGU maishani mwako utakapoikataa.
Ndiyo Nilisema, “Wengi huitwa na wachache huchaguliwa.” Utachugua gani? Ninajua tayari ulichochagua. Je, si Neno LANGU husema, “Wale wanaoweka mikono yao kulima na kuangalia nyuma, hawastahili?” Wekeni mikono yenu kulima; acheni mambo yenu ya kale kwenye msalaba wa Kalvari. Niliruhusu mambo yaliyotendeka kukufanya uwe na nguvu KWANGU, sio mdhaifu. Kwa kuwa una ushuhuda uliotengenezwa na dhahabu sio shaba. Itumie kuwaleta nafsi KWANGU, itumie kuniletea MIMI, Sifa, Heshima na Utukufu.
MIMI Bwana wako YAHUSHUA MASIHI Ninarudi hivi karibuni kushinda mnavyofikiria. Uovu unavyozidi kuongezeka katika dunia hii, na wale waovu wanaotenda dhambi usoni MWANGU wakisema, “Utafanya nini YAHUSHUA?” Nitawaonyesha ni nini Nitakachofanya juu yake. Ninavyowaonyesha watoto WANGU Ninapowachapa, Nitawaadhibu wale wanaodharau amri ZANGU, ushoga, usherati, na Bibilia katika uso WANGU na huthubutu kunikejeli MIMI. Inakuja, hasira ZANGU zaja katika ardhi hii zisizo na kipimo.
Wanavyowafunza watoto kutenda dhambi na eti Maneno YANGU si ya leo tena, watalipa katika njia kuu. MIMI Nilikuwa dhabihu ya Mwana-kondoo mara moja tu; Ninarudi kama Shujaa Mkuu wakati ujao. Lakini kwanza Nitawakusanya Watoto WANGU nyumbani. Hasira YANGU imewekwa kwa maadui WANGU sio Watoto WANGU. Watoto WANGU, wale wanaonipenda na kunitumikia MIMI, ambao dhambi zao zimeoshwa katika Damu iliyomwagwa Kalivari, hawana chochote cha kuogopa.
Lakini maadui WANGU hawatajua hofu kuu kama hii. Kwa yale waliyoogopa yatakuja juu yao na yote ambayo hawakuogopa itawamaliza. JINA LANGU linavyotumiwa kama laana hewani na yote ambayo ni Takatifu yanakejeliwa kote hewani, Nitathibitisha kuwa MIMI ni Mwenyezi MUNGU, YAHUVEH mkuu ‘MIMI NIKO’ na sio MIMI Ambaye Anakejeliwa na kulaaniwa. Ni nyinyi ambao mnaosikiliza haya na hamhisi huzuni kwa kuyasikia, na mmefanya mioyo yenu iwe ngumu, na kuruhusu haya na hamjazungumza dhidi ya haya. Watoto WANGU chukueni hewa, katika JINA LANGU. Hamsikii Buddha akilaaniwa, au shetani au Mohammed lakini mnasikia jina la Yesu Kristo (YAHUSHUA MASIHI) likilaaniwa. Mnasikia MUNGU mnayemtumikia Akilaaniwa. Sio MUNGU Mwenyezi Aliyelaaniwa; ni wale wanaozungumza hizi laana juu yao wenyewe. Ni Damu ya YAHUSHUA pekee itakayowaosha safi kutoka kwa dhambi hii.
Ninawaambia angalieni volkano na mitetemeko ya ardhi, vitisho kwenye anga na mtajua jinsi kuja KWANGU ulipo karibu. Ninavyochukua mamlaka ya kitu kimoja ambacho binadamu hawezi na hatawahi kuchukua mamlaka, yale yaliyo angani na hali ya hewa. Binadamu hawezi kuzuia volkano, mitetemeko ya ardhi, theluji au baridi au joto, tufani, vimbunga, mafuriko kutoka mvua kubwa, waovu wanapozidi kuwa waovu zaidi na wazuri wanakuwa Takatifu zaidi. Ninawatenga Watu WANGU sasa, na kuja KWANGU upo karibu. Fanyeni mtakachonifanyia MIMI haraka.
Wazee wanapaswa kutunzwa kwa upendo na heshima kwa kuwa hao ni wazee ambao ni ghala za maarifa mengi. Wao ndio hazina ZANGU hapa duniani, lakini ni wangapi ambao wamesahauliwa, kufungwa, na kufananishwa kama takataka. Watoto wao wenyewe hutumia sheria kuwaua wale walio wagonjwa au walemavu. Wao ni mizigo kihela “Acheni maskini wafe, ondoa ustawi, uzuri wao ni nini?” Je, si Nilisema, “Maskini watakuwa nanyi kamwe?” Lakini mnapaswa kugawa mlicho nacho nao. Walishe maskini; wavishe walio uchi, ndugu na dada zenu. Wale walioitwa kwa JINA LANGU, mliooshwa kwa Damu YANGU na mnajifanya hamwezi kuwaona. Ninawaona, Ninasikia vilio vyao, MIMI huiruhusu ili nione ni wangapi watajali. Lakini kwa neema ya MUNGU YAHUVEH, mnawapita. Unafaa kuwa mlinzi wa ndugu yako. Sehemu moja ya mwili wa YAHUSHUA inapoteseka, mwili wote huteseka. Acheni kupuuza uchungu.
Kama mauaji ya watoto wasio na hatia ambao bado wapo tumboni mwa mama zao wanararuliwa kiunyama na mnafikiria kwa sababu dunia hii imeihalalisha, kuwa ni halali KWANGU. Hata wauaji wenu walio katika hukumu ya kifo, mnajaribu kufikiria vifo vya huruma na haraka kwao. Sheria inawapa angalau miaka 10 zaidi katika kesi nyingi kwa gharama ya walipa ushuru, pesa zenu za ushuru, kurefusha maisha yao. Kutengeneza njia za huruma zaidi za kuwaua wale waliochukua maisha bila huruma. Lakini watoto ambao ni wa thamani KWANGU sana, watoto Niliohesabu siku hadi wazaliwe, Nikaweka Roho YANGU ndani yao, Nikasababisha wao kukua na nguvu na afya katika tumbo la mama zao, na hawa watoto wasio na hatia hawakuwahi kujua mabaya waliteswa kama vilio vyao visiosikika hulia masikioni MWANGU.
Wale waliofanya hizi kuavya mimba na hawajakiri haya na kuuliza msamaha na kuachana na dhambi hii, daima watasikia vilio vya watoto hao. Kama mojawapo ya adhabu zinazowangoja jehanamu na kamwe hawatakuwa na kikomo kutoka kwa vilio hivi vya watoto waliouwawa, au vilio vyao. Je, si mwajua jinsi mtoto anayelia hukera? Jaribu kufikiria mamilioni masikioni mwako milele.
TUBUNI SASA, wauguzi, madaktari na wanawake wanaofanya vitu hivi kwa kujifikiria wewe mwenyewe. TUBUNI SASA, wanasiasa waliopitisha amri hizi. Korti Kuu, nyinyi sio wakuu machoni MWANGU. Nyinyi hampo juu ya amri ZANGU. MUNGU YAHUVEH MWENYEZI pekee Ndiye Mkuu. MUNGU YAHUVEH MWENYEZI pekee Ndiye hakimu, mwamuzi na Anayetekeleza hukumu. YAHUSHUA MASIHI Alikuja ili muwe na maisha na maisha bora. TUBUNI! Acheni dhambi hii kwa kuwa MIMI Nitahakikisha kuwa mmewajibika. Damu ya watoto wasiozaliwa ipo mikononi mwenu.
Kwa nini, kwa sababu Nimewapa wanadamu chaguo? Chaguo la kutii lile ambalo ni silika iliyopewa kwa kila mwanamke na mwanamume, kulinda watoto, kuwatunza watoto na bado wanauwawa kinyama. Ole kwa wale wanaosema kuwa haya ni halali. Ole kwa madaktari na wauguzi wanaojihusisha katika mauaji haya. Ole kwa wale wanasiasa wanaopitisha amri hizi za watoto wasio na hatia kuuwawa. Ole kwa nyinyi mliokaa kimya kwa muda mrefu sana. Kwa sababu Ninasikia vilio vyao. Nafsi za watoto hawa hurudi zilikotoka Mbinguni. Lakini nafsi zao zimeraruliwa kutoka dunia hii bila huruma. Ukatili usio na kifani. Ninaruhusu nafsi hizo kuondoka kuthibitisha ukatili wa binadamu kwa binadamu. Nikijua ni chaguo gani mama alikuwa tayari amefanya. Nikihuzunika na kumpa kila nafasi ya kutubu. Nikijua hatatubu, Nikiwa na hasira kuwa hatatubu.
Waambie, waambie binti YANGU. Mara nyingine ingawa hata wale wanaojiita kwa JINA LANGU bado hawafanyi chochote ila kutingiza vichwa vyao tu na wengine Nina furaha sana kuwaita Watoto WANGU huweka maisha yao chini, sifa, na fedha ili kulinda watoto wasio na hatia katika tumbo za mama zao. Hawa ndio Nitakaowatuza. Je, mbona makanisa haziwasaidii wale walio na hamu ya kutoa yote walio nayo kufanya maandamano dhidi ya mauaji haya ya watoto wasio na hatia?
Wanapoteza kazi zao, wanawekwa gerezani, wanakejeliwa, na kwa nini? Kwa sababu walisikia sauti YANGU, na thibitisho LANGU lililosema, “Zungumza, usinyamaze.” Nimeyasikia maombi yao, Nimeona machozi yao, na Nimeihisi uchungu wao, wewe je? Kila mkutano wa kanisa unapaswa kuwaombea hawa. Kila mkutano wa kanisa unapaswa kuombea thibitsho LANGU, hukumu YANGU kwa wale wanaofanya vitu kama hivi, wanaoruhusu haya mauaji, lakini ni wachache sana wanaofanya vivyo hivyo. MIMI NINA HASIRA KUU kwa kuwa mnasema nyinyi ni WANGU na mnapuuza vilio vya watoto ambao hawajazaliwa, na vilio vya wale wanaotoa yote yao kulinda na kukomesha mauauji ya watoto ambao hawajazaliwa. Inukeni! Zungumzeni! Katika JINA LANGU! Ombeni, Ombeni, Ombeni hadi muone hofu hii imekwisha.
Mnataka kujua ni kwa nini Niliruhusu haya kuendelea, kwa sababu Nimekuwa Nikiwangoja Watoto WANGU kuliita JINA LANGU kukomesha haya. Kuthibitisha kuwa wanajali. Sio tu wachache, lakini mamilioni wanapaswa kuzungumza wakati sheria hizi zilizo dhidi ya amri ZANGU zinapitishwa. Hakufai kuwa na mkutano wa kanisa wowote bila kuwa na ombi hili. Wachungaji, mtawajibika. Mmeonywa. Kongamano muonye wachungaji wenu. Wanapaswa kuwa wananiwakilisha MIMI. Waombe kuwa katika kila mkutano wanapaswa kuomba kuwa hofu hii iishe, kwa kuwa hukumu YANGU itakuja juu ya wale wanaokataa kutubu. Acheni kunipa MIMI maombi vuguvugu. Sitazisikia. Nipe MIMI maombi yaliyo na shauku na moyo unaojali. Acheni maombi ya ibada ambayo tu ni maneno ya kurudia, sitasikia. Haya yanatoka akilini na mdomoni, sio moyoni mwenu.
Mashimo makubwa yatafunguka na ardhi itameza hizi kliniki za kuavya mimba. Sio chochote ambacho mwanamume amefanya bali tu kwa mkono WANGU Nitaigonga dunia hii. Pale ambapo damu zaidi imemwagwa, damu ya wasio na hatia. Kwa kuwa, hata vitani damu ya wasio na hatia haimwagwi vile. Lakini katika madhabahu ya shetani hawa watoto wanachinjwa kwa minajili ya urahisi, kwa ubatili, ubinafsi, kwa hofu na kwa ulafi. Nitawapa kitu cha kuogopa, wataogopa MWENYEZI MUNGU YAHUVEH Aliyeumba nafsi hizi ambazo wamawaua kikatili. Wataogopa YAHUVEH Yule Ambaye wanamkejeli na kusema ni halali. Wataogopa wale ambao wameweka Wakristo nyusoni mwao kuwaonya kuwa haya ni mauaji. HII NI DHAMBI. Kwa kuwa haitakuwa chochote ambacho Wakristo wamefanya kuwasababisha waogope, bali tu kuomba na kusongeza mkono wa YAHUVEH kupitia maombi haya.
Lakini wanawake, madaktari, wauguzi, wanasiasa, wale wanaoshangilia mauaji haya ya nafsi ZANGU zisizo na hatia wataona uso WANGU na Roho WANGU juu ya watoto WANGU waliotumwa kama majeshi kuomba. Kumbukeni kuwa haikuwa mikono ya binadamu iliyoangusha kuta za Yeriko. Hivi ndivyo itakavyokuwa tena na hawataweza kujenga kliniki hizi kwa haraka. Waambie Mtoto WANGU na wafunze.
Bado kuna wakati wa kutubu, lakini hivi karibuni hakutakuwa na wakati wowote. Kumbukeni Sodoma na Gomora, haikuwa Mikono ya binadamu iliyoleta moto na kiberiti, ilinyesha kutoka Mbinguni ambapo imewekwa na itakuja tena. Enyi waovu, mnaofanya mambo haya na hata mabaya zaidi, mmeonywa. Sheria zenu zinaweza kuhalalisha ndoa za kishoga lakini Nilikadiri kuwa ni dhambi. Hii ni kejeli ya ndoa na yale Niliyoumba kuwa Takatifu. Haijahalalishwa katika macho YANGU. Wachungaji, wengine wenu mmejiunga katika hizi sherehe za mapenzi za ushoga kwa kutosema chochote, mmejiunga nayo. Inukeni! Zungumzeni! Ambieni wapagani wanyamaze katika JINA LANGU! Msisikize uongo zao tena. Wanawataka watoto, mmeonywa, watoto wenu wenyewe.
Lazima mtubu sasa au nyinyi pia mtapitia yale yajayo na yanakuja haraka. Mmeonywa. Mna wasiwasi kwa sababu ya hali yenu ya kutolipa ushuru lakini hamjali kile ambacho MUNGU mnayesema kuwa mnamtumikia Atakachowafanyia, kwa kutoomba dhidi ya haya na kutosongeza mkono WANGU kuyakomesha haya. Tena hakufai kuwa na mkutano wa kanisa ambao unaisha bila maombi ya kukomesha roho hii iliyotumwa kuchafua kila kitu kilicho Takatifu. Maombi vuguvugu sisikizi na Ninachukia. Ni aidha uko moto au baridi lakini usije KWANGU vuguvugu kwa kuwa Nitakutema nje ya mdomo WANGU.
Usiseme wewe ni WANGU na hausimami kwa yale yaliyo Takatifu au kukaa kimya unapoona wengine wakisimamia Utakatifu na wanateswa kwa ajili YANGU, na hauwasaidii katika njia yoyote kwa kuwa unahofia kupoteza hali yako ya kutolipa ushuru. Utapoteza mengi zaidi ya hali yako ya kutolipa ushuru. Mtapoteza mengi zaidi ya maisha yenu. Mtapoteza NAFSI zenu! Mmeonywa. Wakati ni sasa! Inukeni! Zungumzeni! Ambieni wapagani wanyamaze katika JINA LA YAHUSHUA! Mmoja na YAHUSHUA upande wao ni wengi. Mamilioni bila YAHUSHUA upande wao ni wachache. Wakati ni sasa.
* * * * * * *
Chombo cha udongo kilichovunjika, lakini Shujaa Mkuu wa YAHUSHUA MASIHI!
Mchungaji Sherrie Elijah
Kutoka sasa Nimeamriwa kuandika wakati ndani. Sijui sababu. Pia nilipokuwa nikiandika Unabii huu, Intaneti ilipotea, nilijaribu kuirudisha lakini nikapata laini za simu zinashambuliwa kwa njia moja au nyingine, imekuwa masaa mawili. Sasa na hii haijatumwa. Ni saa 3:37 mchana na siwezi hata kufikia opereta.
Kwa masaa inasema, “Laini ni busy.” Haya hayajawahi kufanyika hapo mbeleni. Ninafunika tarakilishi hii, na barua pepe iliyo na ujumbe wa kinabii na Damu ya YAHUSHUA MASIHI wa Kalivari. Kwa imani, ninaamini kuwa wale RUACH HA KODESH Anayetaka wapate ujumbe huu wataipata. Sijaweza kutumia Intaneti usiku mzima na kuituma usiku huu. Siwezi hata kumfikia opereta, au kupiga simu ya mbali. Kitu kimefanyika angani ninapoandika haya. Ni simu tu za karibu zinazopatikana.
Hii ndiyo mara ya kwanza niliwahi kuambiwa kuweka saa, mtaona kitu kikifanyika kikiambatana na tarehe hii au saa hii. Sijui ni nini. Ninauliza kuwa popote unabii huu utawekwa, au kutumwa, tuma ukurasa mzima.
Kwa kuwa kuna sababu na tena ninajua ni YAHUVEH Anayeniamuru kusema, msibadilishe au kutoa neno hata moja, acha ilivyo ninavyoituma. Shetani lazima amekasirika. Kwa kuwa haya yanatumwa kupitia hewa na Bibilia husema kuwa shetani ni mkuu na ana mamalaka juu ya hewa na falme zake. Lakini ninafunika hewa ambayo hii inapitia na tarakilishi hizi na damu ya YAHUSHUA iliyomwagwa, na huduma za simu na huduma za Intaneti. Damu ya YAHUSHUA wa Kalivari, na Nazareti ipo dhidi yako shetani.
Na pepo, hamwezi kupita Damu. Katika jina la YAHUSHUA. Laini za simu zinafanya kazi sasa 11:15 usiku. Sasa inaweza kutumwa. Wale walio na masikio ya RUACH HA KODESH watasikia sauti ya Mwenyezi MUNGU YAHUVEH Wetu, wote wengine watabaki viziwi. Katika jina la YAHUSHUA MASIHI, RUACH HA KODESH tuma jumbe hizi kwa wote wanaotambua sauti ya Bwana na Muumba wetu.
Pekee kwa Sifa, Heshima, na Utukufu,
YAHUSHUA ninauliza. Amina.