UNABII WA 12

BINTI WA HATIMA, NJOONI!

Imepewa kwake Mtume Sherrie Elijah

* * * * * * *

Binti Wapendwa wa Unabii msitembee katika amani yenu, lakini katika amani ya YAHUSHUA ipitayo akili zote. Msitembee katika nguvu yenu lakini katika nguvu ya MUNGU mnayemtumikia. Usibaki katika mashua Binti YANGU lakini toka ukatembee majini, NAMI. Unayofikiria haiwezekani, Nitatengeneza njia. Kinachokufungia njia na kukuzuia, Nitakitoa. Ingawa mawimbi yatakaa ni kama yanataka kukuzamisha, na upepo unavuma, weka macho yako kwa Mwokozi wako na hautazama. Umekadiriwa kuwa mtembea majini na sio mkaa mashuani.

Kimbia mbele ya Goliathi kama Daudi. Daudi hakumtoroka Goliathi ingawa alimkejeli na kumshtua, ingawa aliwapita wanaume wote kwa urefu. Daudi alikimbia mbele yake Goliathi. Daudi hakuonyesha hofu kwa kuwa aliweka imani yake sio katika binadamu au mfalme, lakini katika MIMI NIKO mkuu na sikumfeli, wala sitakufeli. Hofu ni kinyume ya Imani. Nisikize MIMI. Hofu ni adhabu ambayo huwa situmi. Daudi alipokejeliwa na kutishwa hakujibu ni nini atakachofanya lakini ni nini MUNGU wake atakachofanya. Daudi hakutarajia kumwua adui na yale mawe matano laini, kwa kuwa mawe haya hata hayakuwa makali. Daudi alijua kuwa silaha zake hazitamwua Goliathi, ni ghadhabu ya YAHUVEH zitakazomwua Goliathi. MIMI Niliweka ghadhabu YANGU katika mawe hayo. Nilimwua Goliathi kupitia kijana mchungaji mchanga aliyekejeliwa na watu alipokuja dhidi ya adui na wakasema, “Kwa kweli atafariki, atafeli. Kijana mdogo yuawezaje kumwua jitu?” Haya maneno wanayasema kwa Binti WANGU sasa.

Adui huzungumza katika njia mingi na husema utafeli. Utafariki ukienda dhidi ya adui huyu, wewe ni mdhaifu na haufai kuhubiri katika Jina la YAHUVEH. Lakini Binti WANGU wa Unabii Nimewachagua nyinyi, Nimewakadiri, Nimewapa nguvu. Wanaume wasema ukweli; mkifanya haya katika uwezo wenu na nguvu mtafeli. Mnaweza kufa, lakini hamjasimama katika uwezo wenu, na nguvu yenu. Mmesimama katika upako WANGU, katika Neno LANGU, katika Jina LANGU, mkiiva Vazi LANGU Takatifu la Vita, liliooshwa katika Damu YANGU iliyomwagwa pale Kalvari. Binti WANGU, Ninawaita Binti WANGU wa Unabii siku hii. Je, si MIMI NDIYE mwanzo na mwisho? “MIMI NIKO” mkuu Ndiye Mungu wa Unabii.

Alpha na Omega Ndiye Mungu wa Unabii kwa kuwa Nimetabiri mwanzo na Nimetabiri mwisho. Nani ila “MIMI NIKO” yuaweza kufanya haya? Nitafichua siri ZANGU kwa Binti WANGU na pia kwa Wana WANGU. Binti WANGU Nimewachagua kufanya kama Daudi alivyofanya. Adui atakejeli na kuchochea, atawatumia wengine kutisha na kuangamiza. Utatukanwa kwa ajili YANGU. Adui hawa watakapokuja dhidi yenu msiogope ni nini mtasema au kufanya, maneno mtakayoyazungumza hayatakuwa yenu lakini ni Maneno YANGU mtakayoyazungumza. Wadogo WANGU Wapendwa, msifikirie kabla ya wakati ni nini mtafanya. Msiwe na hofu yoyote mtakapoona nyuso zao. Wanadhani kuwa mnafaa kudhibitiwa na binadamu, na badala ya haya hamdhibitiwi na mfalme wa ardhi hii, mnaongozwa na Mfalme wa Wafalme. Daudi alitupa vazi la vita la dunia hii na badala yake akasimama na vazi la vita, Vazi la Vita LANGU, Mwenyezi MUNGU. Hata nyinyi mtafanya vivyo hivyo. Msilie adui anapoanguka. MIMI Nipo nanyi na hakuna yeyote atakayefanya chochote ambacho sijaruhusu. Ninakupenda Binti YANGU Mpendwa.

Jihadharini nyote mnaojitokeza dhidi ya Binti WANGU wa Unabii. Kwa kuwa jinsi Goliathi alivyoanguka, ndivyo watakavyoanguka wote wanaohuzunisha Binti WANGU wa Unabii. JIHADHARINI! Kwa kuwa Ninatazama, Ninasikia. Nitawahukumu wote wanaohukumu Binti WANGU kwa kuzungumza Maneno YANGU. Kama wanaume wanavyowalinda wanawake na MIMI huweka Roho hiyo ndani yao kufanya vivyo hivyo, je, ni vipi tena zaidi Nitakavyowalinda Binti WANGU wa Unabii? Kwa kuwa imetabiriwa katika hizi nyakati za mwisho Nitamwaga Roho WANGU katika Handmaidens WANGU na Watatabiri.

Yeyote atakayewaguza watakatifu WANGU na kuwaumiza hawa Nabii, kwa kweli Nitawahukumu kwa haraka. Ni heri watubu kabla ghadhabu YANGU iwake dhidi yao. Sasa sizungumzi juu ya nabii bandia kwa kuwa wao huja katika umbo la mwanaume au mwanamke. Kama wao ni bandia, basi lazima haya yafichuliwe ili wengine hawatachafuliwa. Lakini msidhubutu kuwashika au kuwakatisha tamaa au kuweka fikra zenu za binadamu kuhusu ni nini Nitakachofanya, na ni nani Nitakayetumia katika Binti WANGU wa Unabii. Msiseme YAHUVEH hawezi kuwatumia wanawake hawa kwa kuwa hawafanani na mnavyotarajia; eti hawana ruhusa yetu kuzungumza. Nyinyi ni nani O wanaume wa dunia hii kuwanyamazisha Binti WANGU wa Unabii? MIMI huchagua wale walio na uwezekano mdogo wa kuchaguliwa. MIMI hutumia wale ambao husema, “Hapana YAHUVEH, kwa kweli hautaki Nizungumze haya, au kufanya haya?” Lakini bado Binti WANGU husikia sauti YANGU kwa uwazi kushinda Wana WANGU. Nina huzuni kwa machungu ambayo Binti WANGU wa Nabii watapitia kwa ajili ya Jina LANGU. Kumbukeni, Niliteswa kwa ajili yenu. Kama Binti YANGU wa Unabii, utaleta nafsi wengi KWANGU MIMI, na ushafanya hivyo.

Sio Binti wote wa Unabii watakuwa na leseni. Umenifanyia MIMI mengi kushinda wale wanaojiita wahubiri, na wao sio wahubiri hata. Kwa hivyo, usihuzunike wanaume watakapokataa kukukadiri. MIMI Nimekukadiri. Ni haya tu yaliyo muhimu. Nitakulinda na kubariki yote unayoyafanya na kusema. Usifungiwe nira na wasioamini katika chochote ufanyacho. Kumbuka kama wao si WANGU, wapo dhidi YANGU. Macho yako yataona yale ambayo hautataka kuona, utayasikia yale ambayo hautataka kusikia, lakini haitakuwa macho yako, au masikio yako ya mwili yatayohisi uchungu, itakuwa macho na masikio yako ya kiroho. Utajua Baraka zilizopita ndoto zako zote, na utajua huzuni. Nitawatumia nyinyi Binti WANGU wa Unabii kuwalinda wachanga, kuwapa moyo na kuwafunza. Kama tayari mlivyokuwa na hii silika Niliyowabariki nayo. Nitawatumia kukemea, kwa kuwa tena Nimeiweka tayari Roho hiyo ndani yenu kama mama anavyokemea, pia mtakemea hii taifa la wapagani na wote waliopotezwa, na wale wanaowapoteza kondoo WANGU.

Binti WANGU wa Unabii mtakuwa na ujasiri kama wa mama simba anayewalinda wanawe. Nitawatumia kutibu walioumia, kwa kuwa ni mama yupi ambaye hana hii Roho ya huruma ambayo Nilimpa tayari? Mtatumia hizi karama za mama, mwalimu, shujaa, na karama zote za RUACH ha KODESH alizowapa nyote kwa ukarimu. Nimehifadhi kilicho bora zaidi kuwa cha mwisho. Kwa sababu wanaume wamesema, “Hauwezi kutumia mwanamke.” Itakuwa wanawake ambao watakuwa na huduma zenye nguvu zaidi katika nyakati hizi za mwisho na wa mwisho watakuwa kwanza. Nitakuwa nanyi. Ninakupenda Binti YANGU, unaposoma haya utajua kuwa ni ya kwako. Kama haujui kama haya ni ya kwako, basi ni kweli, acha kusoma, haya si ya kwako. Kwa wote wengine watakaopokea ujumbe huu Ninawakumbatia, kunong’ona masikioni mwenu na Ninawaambia, sikiza, ujumbe huu ni wa kwako. Nimewapa Binti WANGU wa Unabii Roho ya Daudi. Sasa nendeni na mkachukue yale ambayo shetani ameiba katika Jina LANGU. Hivi ndivyo Asemavyo YAHUVEH, Mungu wa majeshi.

* * * * * * *

Imepewa kwake Mhubiri Sherrie Elijah Bibi Arusi wa YAHUSHUA



CLICK HERE or the image below to go directly to her youtube channel
YAHSladyinred