Unabii 120

Usife Moyo! Usikate Tamaa! Unabii wa Urejesho wa Sukkot kwa Mfasiri Mwebrania, Wayahudi wa Kimasihi & Waumini Wote.

Imeandikwa/Kuzungumzwa chini ya Upako wa ROHO MTAKATIFU (RUACH HA KODESH) Kupitia Mtume & Nabii Elisabeth Elijah (Elisheva Eliyahu) Oktoba 19, 2011 Siku ya 6 ya Sukkot wakati Mwezi Mpya ulipoonekana; Au siku ya 7, Hoshana Rabbah kama ilivyo kwenye kalenda rasmi ya Israeli

Unabii huu una Upako wa urejesho, nguvu na ujasiri. Kwa hivyo kama umechoshwa na vita, acha YAHUSHUA Akuburudishe na Unabii huu wa Sukkot wa Urejesho kwa wote wanaomuabudu YAHUSHUA na kuishi katika Utakatifu. Ina Upako wa urejesho-akili,mwili,nafsi na roho, afya, fedha na katika njia zote!

Tunakusifu EWE, BABA YAHUVEH kwa Upako katika Unabii huu utakaovunja nira na utumwa kwa Sifa, Heshima na Utukufu WAKO.

Waumini wote waliookoka, kujazwa na ROHO MTAKATIFU, wanaoabudu, kumtumikia na kumtii YAHUSHUA BWANA MWENYEZI MUNGU & MWOKOZI, wanaoteswa, kutukanwa, kukataliwa, kuchukiwa-nyinyi ambao mmechoka maovu kuitwa yanayokubalika na mazuri kuitwa maovu: Msife moyo enyi Waombezi Watakatifu, Bibi Arusi wa YAHUSHUA. Msikate tamaa hata wakati shida za dunia hii zinawafanya kuhisi ni kama mmezidiwa, wakati shetani anawashambulia, wakati maadui ni wengi waliokuzunguka! Usife moyo, usikate tamaa! Dunia hii sio Nyumbani kwetu! Usiachilie imani yako katika Jina la YAHUSHUA! Utapata ushindi!

Haya yatarejesha vikosi ambao wamepigwa. Morale ya vikosi hivi vinahitaji kujengwa. Hamna uvumilivu kule Israeli kwa wale wanaoamini na kumfuata YAHUSHUA.

Elisheva anasema, “Ilichukua Myahudi aliyeteswa kuweza kukoroga upako katika huyu Myahudi aliyeteswa. Kama umechoka na umepigwa, tafadhali soma haya na usikize. Kuna Upako wa urejesho ndani yake. Kuna Upako mkuu katika Neno lililozungumzwa. Tafadhali sikizeni rekodi ya sauti kwenye video, au someni kwa sauti kama mnaweza.

Tafadhali oneni pale mwisho, kulikuwa na muujiza na kinaza sauti. Betri ilikuwa imejaa tu na nguvu ya kurekodi urefu wa Neno lenyewe. Kama mawasiliano ya simu ingerekodiwa kutoka mwanzo, Neno lote halingekuwa limerekodiwa mpaka mwisho. Lakini Sifa kwa YAHUSHUA, kinaza sauti kilianza kwa wakati kamili wa YAHUVEH na Neno lote lilirekodiwa!

* * * * * * *

Yafuatayo ni Unabii ulivyokuja:

—na Nabii Elisheva, akizungumza katika "Ndimi Takatifu," kama ROHO wa MUNGU Alivyomjalia kutamka (Matendo ya Mitume 2:3-4) kwa lugha za wanadamu na malaika (1 Wakorintho 13:1). Elisheva anazungumza katika ndimi Unabii ukitokea (1 Wakorintho 14:6).

Tunatumia Majina ya Kiebrania ya MUNGU:

YAH/YAHU יה ni JINA TAKATIFU la MUNGU, kama vile “Alleluia” au “Hallelu YAH” הללו–יה ambayo humaanisha “Msifu YAH”: YAHUVEH/YAHWEH י-ה-ו-ה MUNGU BABA; YAHUSHUA/YAHSHUA יהושוע MWANA WA PEKEE WA MUNGU—(HA MASHIACH המשיח inamaanisha “MASIHI”; ELOHIM אלוהים inamaanisha “MUNGU.”)

Ufunuo wa “SH’KHINYAH GLORY” שכניה תפארה —kama Jina la Kibinafsi la RUACH HA KODESH רוח הקדש, (katika Kiingereza “ROHO MTAKATIFU”) —upo kwenye tovuti hii. (HA SH’KHINAH {SHEKINAH} ni Kiebrania ya UWEPO WA MUNGU, UWEPO MTAKATIFU.)

Zaidi ya hayo, ABBA YAH אבא יה humaanisha “BABA YAH” na IMMA YAH אמא יה humaanisha “MAMA YAH.”

Maandiko yaliyotajwa yametoka KJV/NKJV isipokuwa pale palipotajwa vinginevyo. Bonyeza nambari za footnote kufungua ukurasa mwingine.

* * * * * * *

Unabii 120 Unaanza:

Oktoba 19, 2011

Unanifurahisha MIMI, mtoto WANGU. Usisite kuniita MIMI BWANA MUNGU MWENYEZI kwa kuwa ROHO WANGU yupo ndani yako!

Wewe ni WANGU! Umeoshwa na DAMU!

Umenunuliwa na DAMU! Na wewe ni WANGU.

-akili, mwili, roho na nafsi zote ni za

YAHUSHUA MASIHI! MIMI ni MASIHI wako!

Elisheva: O nina joto! [Moto Mtakatifu wa Upako wa RUACH HA KODESH mara nyingi hujionyesha kwa njia hii.]

Na sasa Ninakujaza na Mafuta Mapya kutoka Mbinguni ili utembee katika Upako mkuu kuzungumza na ujasiri mkuu, kama Yohana Mbatizaji.

Kutoka kichwani mwako hadi kwenye nyayo ya miguu yako!

Mana kutoka Mbinguni, Ninawapa mle!

Wewe ni mpendwa WANGU! Mpendwa WANGU ni WANGU!

O mpendwa WANGU! Nisaidie MIMI, Nisaidie MIMI, Nisaidie MIMI!

Walishe kondoo na wana kondoo WANGU! Fanyeni kazi kando ya Nabii huyu.

Kwa kuwa wakati ni mfupi sana!

DAMU YANGU imelowa kwenye mchanga wa Israeli. Tone moja tu ndilo linalotakikana kuosha dhambi. Asante kwa kuwa hamjaibika kwa sababu YANGU. Asante kwa kuwa tayari kuteswa kwa sababu YANGU! Asante kwa kunikubali MIMI- hata kama inamaanisha kuwa familia yako itakuacha, wale wa familia yako ya damu, lakini sio familia ya DAMU YANGU!

Familia YANGU ya DAMU inakukumbatia kama huyu dada Nabii yenu anavyowaita leo hii! Familia YANGU ya DAMU, wale ambao wanafanya mapenzi ya BABA WA MBINGUNI, wanakukumbatia na kukupenda-wanakutambua wewe kwa wewe ni nani ndani YANGU! KUMBUKA HAYA DAIMA! Ninakupenda! Na ninakushukuru. Ndio, BWANA MUNGU wako, MWOKOZI wako, MASIHI wako Anakupenda! Kamwe, kamwe, kamwe, kamwe usimruhusu yeyote kuchukua haya kutoka kwako!

Ninazungumza nawe kwa kimya ya usiku. Ninakupa Ufunuo. Na ufunuo mkuu utakuwa nao!

Kumbuka mpendwa WANGU, “Mayudasi” WATAKUJA na “Mayudasi” wataenda. Mimi Nilikuwa na “Mayudasi” WANGU. Wewe una wako. Elisabeth [Elisheva] ana wake. Wote, wote, wote wanaonifuata MIMI, kama hawateswi katika JINA LANGU, heri wajiulize, “Mbona sivyo?” kwa kuwa mtumishi sio mkuu kushinda BWANA (Yohana 13:16). Ni wote… wote hawanipendi MIMI. [Sio wote wanaonipenda MIMI]. Usitarajie kuwa wote watakupenda wewe-kwa kuwa kama bado Ninateswa-katika dunia hii Ninachukiwa kushinda vile Ninavyopendwa! Ninakejeliwa zaidi ya vile Ninavyokubaliwa! Lakini Nililipa GHARAMA pale Kalivari. Na Israeli-O, Israeli-ni hadi lini, hadi lini, hadi lini, hadi lini Nitawangoja mnikubali MIMI-kunipenda MIMI?

O Ninajua itachukua muda mgani! Na Ninajua gharama Israeli itakayolipa! Na itakuwa gharama nzito-kwa kuwa watawajibika zaidi. Kwa kuwa Nilitembea barabara za Yerusalemu. DAMU YANGU, DAMU YANGU, DAMU YANGU imelowa kwenye ardhi yenu. O Ninavyohuzunika! O Ninavyoomboleza!

Lakini kuna mabaki! Nina mabaki! DAIMA MIMI huwa na mabaki! Wao ni wachache, lakini wao ni WANGU! Na kama tu nina nyinyi pia kuna wengine Israeli. Na wameenea kote duniani na watasimama na watalinda! Wanalinda yale ambayo ni Takatifu! Na wanafunua na kukejeli yote yasiyo takatifu na wanaonya kuwa mpinga kristo yupo njiani- lakini haitafanyika hadi Niwachukue Bibi Arusi WANGU wa kweli.

Kwa hivyo Ninachukua fursa hii kusema, “Asante.” Ninamtuma huyu Nabii WANGU kusema, “Asante.” Hamna hata chozi moja liliomwagika wakati ambapo limefanyika kwa ajili ya JINA LANGU, halijawekwa kule Mbinguni katika chupa ya thamani, iliyo na gems na johari ya aina tofauti (Zaburi 56:8). Na jinsi mateso yalivyo makuu-Ninawaambia haya, Wapendwa WANGU, Bibi Arusi WANGU-ndivyo harufu nzuri yazidi. Harufu nzuri ipo ndani ya chupa hiyo iliyo na machozi yako. Imekuwa dhabihu KWANGU, YAHUSHUA wako, BABA MWENYEZI na RUACH HA KODESH Aliyethaminiwa.

O ni hadi lini, hadi lini, hadi lini, hadi lini, hadi lini, hadi lini Nimengoja kuweza kuwakumbatia Bibi Arusi WANGU! Lakini haitakuwa muda mrefu sasa! Haitakuwa muda mrefu sasa! Mtakuwa Mikononi MWANGU! Mtasikia Sauti YANGU!

Msife moyo! Msikate tamaa! Kwa kuwa mmetoka mbali! Msife moyo! Msikate tamaa! Msiafikiane na uongo wa dunia hii!

Dunia hii ikizidi kukuambia kuwa wewe sio mtakatifu, jua kuwa wewe ni Mtakatifu! Wakizidi kukukejeli na wanacheka-kwa sababu unafuata Sheria za Torati- jua wewe ni WANGU!

Ukizidi kulinda Sabato, Shabbat na kusema, “Sio Jumapili”-jua tu wewe ni WANGU! Usife moyo. Usikate tamaa. Ingawa mateso ni mazito na ingawa yatazidi kuwa mazito, kumbuka ni kwa sababu ya JINA LA NANI unateswa! Kumbuka ni kwa sababu ya NANI unachukiwa!

O watatumia jina lako na jina lako watalitumia vibaya na kuzungumza maovu mbalimbali kulihusu, lakini sio jina lako kwa kweli wanalolichukia. Ni NANI unayemwakilisha. Ni kwa sababu ya wewe ni nani ndani YANGU. Ni Jumbe unazopeana zinazotoka Mbinguni.

Kwa hivyo usife moyo! Usikate tamaa!

Kwa kuwa Nitalipiza Kisasi kwa hawa maadui! Na wataomba milima kuwafunika-kutoka kwa yule Aliyeketi kwenye kiti cha enzi (Ufunuo wa Yohana 6:15-17)! Na MWANA KONDOO MTAKATIFU Aliyechinjwa, kusulubiwa na kufufuka tena! YAHUSHUA MASIHI ni JINA LAKE!

Na Ninawaambia MSIFE MOYO! NA MSIKATE TAMAA! Kwa kuwa MIMI niko nanyi.

Fikieni watu WANGU. Fikieni watu WANGU. Sizungumzi tu na watu kule Israeli lakini Ninazungumza na watu kote duniani. Fikieni watu WANGU. Endeleeni kuwalisha kondoo WANGU na wana kondoo. Endeleeni kutoaibishwa na ushuhuda wenu kwa ushuhuda wenu sio wewe ni nani, USHUHUDA wenu ni MIMI NI NANI-ndani yenu! Haya ndiyo shetani anayochukia! Haya ndiyo maadui wenu wanayochukia!

Lakini USHUHUDA uo huo unathibitisha MIMI NI NANI-kwa kuwa Ninabadilisha maisha! Na makuu, makuu, makuu, makuu, makuu, makuu, makuu ni zawadi zinazowangoja wale-Mbinguni-waliokuwa tayari, tayari kuweka sifa zao chini, majina yao chini, waliokuwa tayari kuteswa kwa sababu ya JINA LANGU! Makuu, makuu, makuu, makuu, makuu ni zawadi zenu zinazowangoja nyinyi Mbinguni.

Utaona mpendwa WANGU. Utaona UTUKUFU WANGU, UTUKUFU WANGU, UTUKUFU WANGU. Na macho wako mwenyewe! Utaona! Sio mbali sasa! Usife moyo unapoona wanaotunga tarehe wakija na kuenda. Sikiza tu na utaona. Ufunuo mpya zitakuja kwako.

Simameni na wengine wenu! Sasa sio wakati wa kusimama pekee yenu. Ninaleta Bibi Arusi WANGU pamoja kutoka mwisho mmoja hadi mwingine [wa] dunia kupitia Intaneti, au nyinyi wawili mnaozungumza sasa hamngekuwa mmekutana. Na bado, ni kama mpo katika chumba kimoja kwa kuwa nyinyi mna Roho moja.

Mtajua nani ni WANGU. Watapigana kando yako. Watalinda yale yalio Takatifu. Watafichua mbwa mwitu walio katika mavazi ya kondoo. Msidanganyike. Wote wanaodai kuzungumza katika “Jina la ‘YESU KRISTO’” kwa kweli sio [wote] wanaozungumzia MIMI. Yeyote atakayesimama dhidi ya Huduma hii Takatifu, Huduma hii iliyokadiriwa na YAH… Ole kwa hawa maadui wanaosimama dhidi ya Utakatifu! Kwa kuwa mnasimama dhidi ya MUNGU MWENYEZI!

Kwa hivyo mpendwa WANGU, jua kuwa Nimekuchagua. Jua kuwa wewe ndiwe Mfasiri Mwebrania na kuna wengi wanaokuja, lakini wamecheleweshwa. Kwa hivyo hii ni zawadi yako leo hii. Ulitaka Neno. Umepata Neno.

Elisabeth [Elisheva] ulisema, “Sijui ni nini nitakachosema!” Ulivyosema ni sawa binti YANGU, kwa sababu haya sio maneno ya mwili! Maneno haya yametoka Mbinguni-kubariki Mfasiri Mwebrania atakayechukua Maneno YANGU kwa watu Waebrania [na] atafanya kazi kwa bidii. Na Nitabariki kwa wingi!

Ninakupenda! Ninakupenda! Kamwe, kamwe, kamwe, kamwe, kamwe usisahau Ninakupenda. Ninajua KILA MMOJA & machozi YOTE uliyomwaga! Ninajua kila wakati jina lako linalaaniwa hapa duniani, lakini sio MIMI.

Kwa kuwa Ninatuma Baraka!

Ninatayarisha meza MBELE YA MAADUI WAKO (Zaburi 23). NA NINAKUBARIKI!!!! Na WOTE jehanamu WAMEKASIRIKA kwa sababu HAWAWEZI KUNYAMAZISHA SAUTI ya YAHUVEH MWENYEZI wako ANAYEISHI!

Kwa hivyo [maadui] sageni meno yenu kwa ghadhabu!!!!

MIMI sio MWANA KONDOO

Aliyechinjwa tena! Hiyo ilikuwa wakati mmoja tu!

Sasa MIMI ni SIMBA kutoka Kabila ya YUDA

Na NINAKUJA KUWARARUA maadui WANGU!!!!!

KWA KUWA MIMI & BABA NI MOJA!

Sote tunabariki na Sote tunalaani!

Kumbukumbu la Torati 28, Baraka na Laana:

Baraka kwa wale WANAOTII!

Laana kwa wale WASIOTII!

Mnatembea katika Baraka ZANGU. WALE AMBAO HUFANYA MAPENZI ya BABA MWENYEZI hutembea katika Baraka ZANGU.

Ninawajaribu. Ninajua tayari ni yupi anayestahili kuepuka Dhiki Kuu. Nyinyi wote mpo katika majaribio! Sasa una Unabii mpya Elisabeth Elijah [Elisheva Eliyahu]. Umengoja na kungoja na maadui wameogopa lakini Nimengoja na kungoja mpaka sauti hii ukaisikia-ya Mfasiri Mwebrania-kukoroga Upako ndani yako.

Kwa Israeli, Ninawapenda.

Je, Mnanisikia MIMI, O Israeli?

Ninawapenda. Nina hamu ya kuwaokoa.

Chaguo ni lenu.

Itachukua mateso

-kama ya yale ya huyu unayezungumza naye sasa,

ameteswa na wengine wengi.

Lakini nina Bibi Arusi pale Israeli.

Wao ni Bibi Arusi waliofichwa.

Hamna tu Israeli ya kimwili na

-kuna Israeli ya Kiroho.

Na nina Bibi Arusi WANGU.

Kwa kuwa Israeli ya Kiroho wapo Israeli pia.

O Hazina WANGU!

Someni Wimbo ya Solomoni.

Oneni Upendo WANGU kwenu. Oneni Upendo WANGU kwa Bibi Arusi WANGU.

Hamjui jinsi Ninavyotaka kuwakusanya Kando YANGU!

Na haitakuwa muda mrefu! Kwa kweli haitakuwa muda mrefu!

Ninaona machozi yenu. Ninasikia huzuni yenu. Ninatazama mnapolia na kupiga mayowe,

“Sitaki kuishi kwa dunia hii tena.”

Mmezungumkwa na maovu pande zote.

Lakini, mnafikiria Ninahisi vipi?

Wakati JINA LANGU Linachukiwa?

Haitakuwa muda mrefu.

Msife moyo! Msikate tamaa!

Kazi nzuri Niliyoianza, Nitaimaliza.

Mwisho wa Unabii

[Elisheva:] HalleluYAH! Sifu YAHUSHUA! Ndio! [KICHEKO cha furaha]. O BABA YAHUVEH, YAHUSHUA, RUACH HA KODESH MPENDWA, Asante! Asante! Asante! Asante! Asante! Asante! Asante! Asante! Kila mtu alingoja na kila mtu akasema, “Elisabeth [Elisheva], imekuwa muda mrefu tangu kuwe na Unabii mwingine. Je, Unabii upo wapi? Wewe una Unabii zilizohifadhiwa.”

Lakini BABA YAHUVEH katika JINA LA YAHUSHUA, tunakushukuru na kukusifu WEWE sasa hivi! Huu ndio Unabii unaofuata na ilichukua Mwebrania kutoka Israeli kuiachilia, katika JINA LA YAHUSHUA MASIHI! HalleluYAH! E bwana, nina joto! Tunakusifu WEWE YAHUSHUA! Woo hoo! Sijui inasema nini, inasema nini?

[Mazungumzo yanaendelea, jibu halisikiki vizuri, kwa muda mfupi hadi betri inapoisha].

Elisheva: O sawa, betri inaonyesha kuwa imeisha, lakini hakikisha kuwa ujumbe upo pale… O Tafadhali MUNGU MWENYEZI…”

Rekodi inaisha hapa.

Ilizungumzwa kupitia chombo cha udongo, lakini shujaa mkuu wa YAHUSHUA

Imezungumzwa, imeandikwa siku hii

Ya Oktoba 19, 2011 Saa Sita Usiku.

* * * * * * *

Unahitaji maombi au Wokovu? Je, Una maoni au maswali? Tafadhali Wasiliana na Mtume Nabii Elisheva Eliyahu!



CLICK HERE or the image below to go directly to her youtube channel
YAHSladyinred