Unabii 127
UVUKAJI WA BAHARI YA SHAMU KWA Huduma za Amightywind: Kutoka Kwake Elisheva Eliyahu SEHEMU ZA UNABII HUU ZIMEFUNGWA
*******
ZIKINGOJA KUTUBU KWA EREZ (Ezekieli 33:13, 18:30-32)
SEHEMU ZILIZO WAZI ZINAMTAJA KALEBU SIO EREZ
Ezekieli 33:13 KAMA NIKIMWAMBIA MTU mwenye haki kwamba hakika utaishi, lakini akategemea hiyo haki yake na kutenda uovu, hakuna tendo lo lote la haki alilotenda litakalokumbukwa, atakufa kwa ajili ya uovu alioutenda. […]
Ezekieli 18:30-32 ‘‘Kwa hiyo, Ee nyumba ya Israeli, nitawahukumu, kila mmoja sawasawa na njia zake, asema BWANA MWENYEZI YAHUVEH. Tubuni! Geukeni kutoka katika makosa yenu yote, ndipo dhambi haitakuwa anguko lenu. 31Tupilieni mbali makosa yenu yote mliyoyatenda, nanyi mpate moyo mpya na roho mpya. Kwa nini mfe, Ee nyumba ya Israeli? 32Kwa maana sifurahii kifo cha mtu awaye yote afaye katika uovu, asema BWANA Mwenyezi YAHUVEH. Tubuni basi, mkaishi.
Imeandikwa/Imezungumzwa katika Upako wa ROHO MTAKATIFU (RUACH HA KODESH)
Kupitia Nabii Elisheva Eliyahu
Aprili 29, 2016 – Siku ya Mwisho ya Pasaka kule Israeli
* * * * * * *
Unabii huu una MAJINA ya KIEBRANIA
ya MUNGU:
YAH/YAHU ni JINA TAKATIFU la MUNGU
yaani “Alleluia” au “Hallelu YAH,”
ambayo humaanisha “Sifu YAH”:
YAHUVEH/YAHWEH MUNGU BABA;
YAHUSHUA/YAHSHUA MWANA WA PEKEE WA MUNGU –
HA MASHIACH inamaanisha “MASIHI”;
ELOHIM inamaanisha “MUNGU.”
Ufunuo wa “SH’KHINYAH GLORY”
– kama JINA BINAFSI ya RUACH HA KODESH,
Kwa Kiiengereza Anaitwa “HOLY SPIRIT” – pia ipo kwenye tovuti hii.
(HA SH’KHINAH {SHEKINAH} ni Kiebrania kumaanisha UWEPO wa MUNGU UNAODUMU na wa UUNGU.)
Kuongezea, ABBA YAH inamaanisha “BABA YAH” na IMMA YAH inamaanisha “MAMA YAH.”
Maandiko yaliyotajwa ni ya KJV au NKJV isipokuwa pale palipotajwa vinginevyo.
* * * * * * *
Maneno ya YAHUVEH kwake Elisheva yafaa kuongezwa kabla ya Unabii:
NILIKUONYA KITAMBO ELISABETH [ELISHEVA],
KUTOITA HUDUMA HII KWA JINA LA MWANAMUME AU MWANAMKE.
HATA KABLA KUWEPO NA HUDUMA, NILIIWEKA NDANI YA ROHO YAKO.
KWA KUWA HAKUNA LOLOTE KWA HAYA LILILOFANYIKA KWA MKONO WAKO.
HAKUNA LOLOTE LILILOTOKA KWENYE KINYWA CHAKO.
ILITOKA KWENYE KINYWA CHA YAHUVEH ALIYEIZALISHA.
ILITOKA KWENYE KINYWA CHA YAHUSHUA, MASIHI WAKO ALIYEIZALISHA.
ILITOKA KWENYE KINYWA CHA RUACH HA KODESH, IMMAYAH WAKO ALIYEIZALISHA.
KAMA INGEKUWA TU KWA MKONO WAKO, INGEKUWA IMEFELI KITAMBO.
NI KWA UPEPO WA SHKHINYAH GLORY UNAOVUMA KOTE DUNIANI, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO.
SIO KWA PUMZI YAKO, AU INGEKUWA IMEFELI.
“MIMI NDIYE BWANA YAHUVEH: HILO NDILO JINA LANGU:
NA UTUKUFU WANGU SITAMPA MWINGINE,
AU SIFA ZANGU KWA
SANAMU ZA KUCHONGA.”
ISAYA 42:8
(UNABII WA 105)
Katika mwezi wa Julai 2010, YAHUVEH MUNGU pia Alisema kuongezwe yafuatayo kama onyo kwa wale wanaokejeli:
LAKINI WALIWADHIHAKI WAJUMBE WA MUNGU, NA KUYADHARAU MANENO YAKE, NA KUWACHEKA MANABII WAKE, HATA ILIPOZIDI GHADHABU YA BWANA JUU YA WATU WAKE, HATA KUSIWE NA KUPONYA.
—2 MAMBO YA NYAKATI 36:16
* * * * * * *
Unabii huu ulirekodiwa kwa kinaza sauti. Hii ndiyo
Nakala ya yaliyozungumzwa.
[Ezra anapiga pembe ya kondoo wa kiume.]
[Ezra:] Endelea.
[Ombi la Mwanangu1:] BABA YAHUVEH MPENDWA! Tunakuja mbele ya Kiti CHAKO cha Enzi katika JINA lenye NGUVU la YAHUSHUA MASIHI na kuufunga na kuusulubu miili yetu– na kumfunga shetani mbali nasi, mbali na wakati huu – watawala, nguvu na viongozi wa giza katika maeneo ya juu, chini, maji, ardhi – [tunawafunga wote mbali nasi] miunganisho ya mtandao, hewa, teknolojia, kila kitu BABA YAHUVEH. Tunamfunga na kumvunja shetani mbali katika JINA lenye NGUVU la YAHUSHUA MASIHI – na tunajipaka DAMU ya YAHUSHUA ILIYOMWAGWA kutufunika sisi na kutujaza sisi, nyoyo zetu, akili zetu, miili, roho na nafsi zetu. [Ndimi Takatifu.]
Na tunakufunga na kukukemea ewe shetani katika JINA LA YAHUSHUA MASIHI – na mbali na Mama Rm2 na mbali na Huduma hii yote, hii Huduma ya Amightywind BABA YAHUVEH. Kwa kuwa inavuma kama Upepo Mkuu kote duniani. Na tunaomba kuwa WEWE Utatubariki na kutujaza na Upako WAKO. BABA YAHUVEH tuongoze na SHEKHINYAH WAKO [SHEKINAH] RUACH HA KODESH, ROHO MTAKATIFU.
Naomba BABA YAHUVEH kuwa ndimi zetu zitajazwa na moto, na midomo yetu na Maneno YAKO – itamwaga Maji YAKO ya Uzima BABA YAHUVEH wa MBINGUNI, kuwa WEWE Uzungumze kwetu sisi na Utuonyeshe yote ambayo WEWE wataka tuone. Fungua macho yetu ili tuweze kuona, kiroho, na fungua masikio yetu BABA YAHUVEH ili tuweze kusikia.
Pasikuwe na baridi wala nta juu yetu sisi, BABA YAHUVEH. Ninaomba tu kuwa Upako wa RUACH HA KODESH utakuwa kwenye nyuso zetu. Baridi ya pekee BABA YAHUVEH itakuwa baridi dhidi ya shetani, ugumu dhidi ya dhambi, chuki kwa yote yaliyo maovu. BABA YAHUVEH!
Na huyu mwanamume aliyelaumiwa ambaye kwa wakati mmoja alikuwa kiongozi msaidizi wa Huduma hii lakini sio tena. Ameuacha mwito wake. Amegeuka, BABA YAHUVEH! Na kama tu vile Yudasi alivyogeuka – na YAHUSHUA – alipobadilika hakukuwa na wokovu tena. Hakuna ukumbusho wowote wa wokovu (wa hapo awali) wa binadamu anapotenda dhambi katika maovu na kugeuka. Kwa hivi ndivyo maandiko yanasema BABA YAHUVEH.
Na tunaomba kuwa Umjaze Mama Rm na upako na Utujaze sisi na upako siku hii. Na tunakufunga na kukukemea ewe shetani mbali nasi. Na asante kwa kutuongoza, kutulinda, katika JINA la YAHUSHUA MASIHI, tunaomba.
[Kila mtu:] Amina.
[Elisheva aomba:] BABA YAHUVEH naja kwako tu katika JINA la YAHUSHUA. Sijui niseme nini. Hawa ndio “Wakanyaga pepo wa YAHUSHUA.” 3 Kama unavyojua BABA – mara kwa mara – Nafungua mdomo wangu, na WEWE huniambia niseme nini. Nakuhitaji sasa. Nakuhitaji sasa. Jaza mdomo wangu, BABA YAH!
UNABII UNAANZA:
Aprili 29, 2016 – Siku ya Mwisho ya Pasaka Israeli
Binti YANGU mpendwa Elisheva! Fungua moyo wako tu. Kwa kuwa “Wakanyanga pepo wa YAHUSHUA” wameona moyo wako. Umekuwa hapo kwa kila mmoja wao – hata kama hukuweza kuwa hapo kimwili. Hawana shaka yoyote kuwa wewe ni WANGU. Wamehisi mikono yako ikiwakumbatia na umehisi wao wakikukumbatia. Kwa kuwa wewe ni zaidi ya Nabii tu. Wewe ni zaidi ya Mchungaji tu. Wewe ni mama yao. Unawashauri. Unawapenda – kushinda mchungaji mwingine katika dunia hii. Sio upendo wako tu, ni Upendo WANGU. Ni Upendo wa YAHUSHUA. Na ni Upendo wa IMMAYAH. Hawahitaji hata kukuona kimwili kwa sababu hawana shaka kuwa unawapenda.
Unawapigania kwa maombi, – nyakati zingine kwa muda wa masaa nane kwa siku, wewe na Kathrynyah mnaomba – mkiwapigania kila mmoja. Na sasa Nimemleta Ezra WANGU, anayechukua maombi yao yote na kuyaleta mbele ya Kiti cha Enzi. Anawapenda pia. Ndio sababu yeye husema, “Nahitaji picha za nyuso zao” kuambatana na maombi.
Ninachukua Huduma hii katika mwelekeo mpya. Ninawatupa mbali waliolaumiwa – lakini (hata hivyo,) wewe ndio umekuwa kiongozi wa pekee kwa miaka nyingi. Hakuwa wakati wote Yezebeli, lakini alipoasi na kufanya yote awezayo kuharibu Huduma hii: akikufunga mdomo wako; akishikilia unabii; akikutukana zaidi kila siku ambapo ulilia na kusema, “haya ndiyo ‘mazuri’ Unayoweza kufanya WEWE?” Je, haukuniahidi mimi ‘mazuri kwa mwanamume’ ambapo ‘nimejua mabaya?’
Siku baada ya siku Nilipokuona ukitusiwa, siku baada ya siku imani yako ikiharibiwa – “Uko wapi YAHUSHUA?” Yu wapi mwanamume atakayesimama kando yangu? Yu wapi baba uliyeahidi kwa ‘Wakanyaga pepo wa YAHUSHUA’? Wanampa upendo na yeye hawarudishii!”
Badala ya haya, anajaribu kutenga mama na watoto – anajaribu kuwafanya wamkosee heshima – NILICHOKA! Hilo ndilo sababu alienda! Nilimrarua kutoka nafsi yako tarehe ya Machi 7.
Haya ndio uyajuayo. Na mdomo wake mwenyewe alisema alikuwa anajifanya, alikuwa anajifanya kwa miaka nyingi hadi hakuweza tena kujifanya. Na baada ya miaka kumi na nne, aliondoka. Na Nilikuambia Elisheva hautamwona tena – katika ile cheo alipokuwa. Lakini hata hiyo ilikuwa njozi! Kwa sababu hakuwahi kuwa hapo! Iliendelea kwa miaka saba. Na kila mwaka ulificha. Kwa kuwa haukutaka kuumiza imani ya wengine. Uliogopa aibu itakayokuja kwenye Huduma hii tena.
Lakini Elisheva Nilituma YAHUSHUA kwako – ulipolilia YDS, tena na tena. Wameona mama yao akiathirika katika afya. Hawakujua yule aitwaye ‘Nikomia’ – kila siku – alikuwa anazungumza kifo juu yako. Hamna, hamna hata ombi ili uishi na usife. Badala ya haya, kila siku alisema, “Ni maajabu uko hai!” [imezungumzwa kupitia machozi yake Elisheva].
Lakini “kwa ajili ya watoto” wasema, “Mimi ni Mchungaji. Lazima niwalinde watoto. Siwezi kuwaambia.” Na waliandika na kukuuliza, “Mama, tuambie nini kinachoendelea?” Lakini uliyashikilia ndani machungu haya.
Nilimrarua kutoka nafsi yako! Alipodharau JINA LANGU! Nilimrarua kutoka nafsi yako! Kisha Nikamweka mwingine – yule Niliyemwita hapo awali “Kalebu” kwa kuwa bado yeye ni Kalebu katika Macho YANGU.
Lakini mwaka wa 2007 ulipouliza maombi kwake kwa sababu ya ndoto – Nilitumia [maombi] hayo, Natumia ndoto hiyo. Nilitumia Maneno hayo kumwita mwanamume aitwaye Ezra, na bado hakuwa amepiga magoti KWANGU. Hivi ndivyo Unabii huu wa [94] una nguvu.
Hata ulimi wako umepewa nguvu kwa jina la Kalebu! Anazungumza maisha juu yako na sio kifo. Mwaka uliopita, shetani alijaribu kuchukua maisha yako – kwa sababu ya matusi haya yote, kwa sababu ya kukata tamaa – Niliwainua “Wakanyaga pepo wa YAHUSHUA” kwa wakati huu. Usiyafikirie haya kuwa ya ajabu! Kumbuka Yudasi hakuwa wakati wote Yudasi. Yezebeli alidhani kuwa ana ushindi – yeye [aliyeitwa hapo awali ‘Niko’] alifikiria ana ushindi.
O! Lakini Nilikuwa na mpango mwingine! Na huo ni – inahusu yule mwanamume Mtakatifu: yule atakayechukua nafasi yake. Na hakuna kitu chochote Elisheva ambacho sitakomboa.
Nilikuambia alipotisha ataondoka – mara kwa mara – Nilikuambia, sitaruhusu Unabii zingine zizuiliwe. Nilizungumza Maneno YANGU na kukupa wewe Ufunuo! Lakini alikutisha na kukutusi, kwa hivyo uliyakalia tu. Ulisema, “Siwezani na matusi haya.” Na sasa Ninakuambia safisheni [futa] jina lake katika kila ukurasa. Sasa Ninakuambia safisheni [futa] jina lake kutoka kwa kila Unabii. Kwa sababu yote yamefutwa. Kama vile alivyo katika ‘Kitabu Cha Waliofutwa’. Hili ni funzo. Matunda yasipomea kwenye mzabibu na unapocheza na wokovu wako, shetani ataingia. Utakapoingia katika uasi na kusema, “Nitafanya kila kitu nitakavyo,” umo hatarini!
Sasa Ninawaambia haya. Msiwahi tena kumwita “Baba ‘Niko’” – hamtaki – pepo hii yaweza kuwajia! Choma huu – uhusiano wa nafsi chafu! Haya ndiyo Ninayowaamuru kufanya.
Lakini sasa kuna mwanamume mpya Mtakatifu, ambapo yule mwingine aliacha Utakatifu. Na jina lake ni Ezra. Na atakupenda. Na anakupenda. Na mtakuwa na kiongozi mwingine anayesimama kando ya Elisheva ambaye mnaweza kumwamini, kumwamini kwa kweli. Kwa kuwa yeye ni mwanamume anayetafuta Moyo WANGU. Na Elisheva, sikuiacha nafsi yako pekee yake. Kwa kuwa aliingia ndani ya nafsi yako. Na hata ndimi zake Takatifu hukuzunguka, hukufunika. Ulikuwa tu na “Wakanyaga pepo wa YAHUSHUA,” wana wako [wakikufunika katika maombi] – lakini sasa nakupa mwanamume Mtakatifu – na siongei juu ya mabinti. Sasa Nazungumzia wanaume.
Na Niliichukua nafsi yake na Nikaiunganisha pamoja na yako. Na kwa Mikono ya Daktari wa Upasuaji na kwa Upako Ezra WANGU anayo. Kwa uzi wa dhahabu kutoka Mbinguni, Niliwaunganisha pamoja. Na mtaenda pamoja kuhubiri kote humu duniani na Upako mpya na upendo mpya. Ninaichukua Huduma hii katika mwelekeo mpya-shetani alidhani angeweza kuharibu. Lakini sasa huu mzao mpya, mwanzo mpya utaenda mahali ambapo Huduma hii haijawahi kuenda hapo awali. Na nyinyi wapya, hamkukuwa pale mwanzoni. Hamkukuwa pale kwenye ‘Vita vya Youtube’. Kama mngekuwa pale, mngeona kuwa hakufanya lolote kumsaidia Elisheva WANGU. Lakini alijaribu kusema, “Msimsaidie. Msisaidie Huduma hii”-alijaribu kunyamazisha wote waliokuwa wanafanya haya-alijaribu kuwageuza Adam na Kathrynyah dhidi yake. Lakini alipowaguza Adam na Kathrynyah hapo ndipo ilipokuwa mwisho. Na Kilio cha Vita kikasikika! Na ilikuwa dhidi yake! 4 Na kifo na maangamizi ndiyo aliyoyasikia. Na bado hakutubu.
Alimkejeli [Elisheva] na kusema kwa miaka mingi, “Sipendi vile unavyoomba. Sitaki kuomba na wewe. Sitaki kufanya ushirika na wewe. Sitaki kufanya ushirika kabisa. Upako ni kupoteza wakati.”
Matusi! Matusi! Matusi! MIMI ABBA YAHUVEH, YAHUSHUA na IMMAYAH hatukuweza kuvumilia vilio visivyokoma KWANGU, “Nilichojua tu maishani mwangu ni unyanyasaji kutoka kwa mwanamume. Wapi ‘yule mzuri’?” Wapi kiongozi? Huduma hii inapoendelea kukua, Kathrynyah na Adam wanaweza kusaidia vile wawezavyo, kama anavyoeleza. Wapi kiongozi kusimama kando yake? Wapi kiongozi kumkaribisha Ezra! Wapi kiongozi kuwakaribisha wale wapya! Wapi kiongozi wa kutushauri na kutufunza!
Ezra WANGU amefanya mengi katika huu wakati mfupi wa Aprili kumshinda yule [yule aliyefutwa] aliyoyafanya kwa miaka 14, mwezi mmoja tu. Jaribu kufikiria yale ambayo Nitakayoyafanya. Jaribu kufikiria yale ambayo Nitakayoyafanya-Ninapowaleta hawa Wayahudi wawili pamoja, na mmoja alizaliwa pale Israeli- jaribu kufikiria yale ambayo Nitakayoyafanya. Jaribu kufikiria yale ambayo Nitakayoyafanya.
Na kila mmoja wenu mnapovunja uhusiano huu wa nafsi chafu kwa yule [aliyefutwa]-Upako, Upako, Upako, utawajia juu yenu. Sio tu kutoka kwa uhuru mpya mama yenu anayotembea ndani yake, lakini uhuru mpya kutoka kwa Baba yenu Ezra anayotembea ndani yake! Jaribu kufikiria yale ambayo Nitakayoyafanya wakati nafasi hii inapojazwa na upya-mwanzo mpya, mzao mpya! Na Niliyafanya haya baada ya miaka 21.
Enyi mliothaminiwa “Wakanyaga pepo wa YAHUSHUA,” mnavyonifurahisha MIMI! Kwa wengi wenu mtakaosikia Maneno YANGU, hamtashtuka. Mlikuwa na hofu ya kuzungumza. Hamkuweza kuelewa-jinsi mtu anaweza kuanguka sana!-na ni kwa nini hamkuwahi kusikia kutoka kwake. Sasa mnajua. Sasa mnajua. Sasa mnajua.
Hata Nilimwita ‘Neeky’! Nilijua kuwa atanisaliti MIMI-mara kwa mara katika Unabii Nilimwonya! Lakini alizidi kuwa mgumu zaidi. Alifika mahali aliacha kusikiliza. Alipita mpaka hadi kwa kufuru.
Na vilevile tu alivyonitetea MIMI kule Mbinguni kwa muda mfupi tu katika vita na shetani [ona Unabii 71], vivyo hivyo ilibidi ifanyike tena, itendeke [na kutendwa] tena hapa duniani. Kwa wote wanapigania wokovu wao kwa hofu na kutetemeka (Wafilipi 2:12). Nafsi yako inajua uamuzi uliyoufanya.
Na kutakuwa na upako mpya na kumeanza kuwa na Upako mpya juu ya Nabii WANGU, Mtume anayezungumza. Kutakuwa na afya mpya. Ni mwanzo tayari. Yote kwa sababu sasa ana ufuniko wa maombi wa Mwanamume Mtakatifu ambao sio kama mwingine. Na Elisheva hakuelewa kutoka wakati wa kwanza alipoona mwanamume huyu. Kwa kuwa Nilimsongea hiyo siku kwa njia tofauti na Nikatumia kicheko siku hiyo. Aliona upendo juu yake-kila wakati alipozungumza jina lake-kila wakati alitaja jina lake, bila kumwona, na bado aliona upendo huu. Na akaniambia MIMI, “Huyu mwanamume ni nani? Je, anaweza kuwa ‘Calev’ [Kalebu kwa Kiebrania]?” Kwa hivyo Nikampa ishara baada ya ishara. Nilizungumza Unabii baada ya Unabii, hakuna yeyote aliyesikia. Lakini katika wakati wake mtasikia. MIMI NDIYE NINAYELETA WATU PAMOJA. Ninajua ni nafsi gani inapostahili. Na kwa nyinyi mlio na wachumba na mnaogopa, “Na mimi je? Nina mchumba. Utanirarua kutoka kwa nafsi yake pia?”
Hapana, hapana, hapana watoto WANGU! Njia ya pekee ya haya kufanyika ni mnapogeuka dhidi ya MIMI BABA YAHUVEH, YAHUSHUA na IMMAYAH kwa sababu sitaunganisha waliolaaniwa na nafsi Takatifu. Nitawararua wanapopita mpaka.
Lakini msiogope. Haya hayatafanyika hapa. Lakini mnaposikia ujumbe huu-mtampenda Mchungaji wenu zaidi, mtampenda Nabii huyu zaidi, mtampenda mama yenu zaidi. Na mtamkaribisha Ezra WANGU. Na mtanisifu MIMI. Yule ambaye hapo awali aliitwa ‘Niko’, sasa aitwaye ‘Paul’ amebadilishwa. Na mtanisifu MIMI! Upako wa mwanamume huyu [Ezra] inapowajia nyinyi! Haya ndiyo Niliyowaahidi nyinyi!
Sasa Ninakuunganisha pamoja na Ezra. Huyu ndiye baba yenu wa kiroho. Huyu ndiye kiongozi mnayeweza kumwamini. Hakuulizia haya. Lakini Nilimwambia ya kwamba kutakuwa na mishangao. Na Ninaunganisha Huduma hii pamoja [Huduma moja, Ezra na Elisheva tayari ni roho moja]. Mtaona miujiza ikifanyika. Kwa kuwa mwanamume huyu ana upako wa miujiza. Hata kama Ninafuta jina la ‘Nikomia’-hiyo ilikuwa tu jina la kiroho-lakini huyu ndiye mwanamume, Ninayeita “Kalebu.” Yeye ni msaidizi wa YAH. Na ana upako anapoomba, na anapoinua Gogo lake kuwafukuza maadui. Kama yeye na Elisheva walivyothibitisha kuwa wanapoweka mikono yao kwenye Gogo hilo, Mbinguni ipo makini. Na miujiza itatokezea, kwa hivyo leo, wanavyovuka Bahari ya Shamu-ni kama leo, amemwambia Paul, “Haunishtui mimi kamwe!”
Aliiba fungu la kumi na matoleo. Alimnyanyasa. Na sikuweza kubaki kimya tena. Hakuweza kuyabeba haya pekee yake-sasa “Wakanyaga pepo wa YAHUSHUA,” Ninawainua! Na mtalinda kwa njia ambayo hamjafanya hapo awali. Je, mngefanya hivi kama hamkuwa mnajua? Sasa mnajua. Kila mtu amekatazwa-yeye [Paul, aliyejulikana kama ‘Niko’] akiwaandikia, msisome. Kwa kuwa pepo zimewekwa ndani. 5 Nimewapa amri hizi. Ole kwa yeyote atakayetotii tumaini hili na tayari Ninajua ni nini Nilichoweka ndani ya kila mmoja wenu. Ni miaka ngapi mmemwombea Elisheva-mwaona hata Nimebadilisha jina lake.
Kwa kuwa ana mwanzo mpya. Wakati uu huu Ninamfuta yule aliyelaaniwa, Ninampa jina mpya na Upako mkuu utakaokua kila siku. Ni mara ngapi mliomba, ni machi ngapi ya Yeriko-hata kufunga kwa sababu yake. Sasa mnajua. Sasa mnajua. Na sasa Ninaweza kumponya. Kwa sababu ilibidi Niitupilie mbali sababu ya kuumia kwake. Alimtisha. Na akasema, “Wafikiria YDS hawatajua? Wafikiria maadui hawatajua?”
Na akalia na kusema, “Usiumize imani ya watoto!” Alimfunga shetani na kumwambia, [yeye] hajaruhusiwa kuzungumza. Na akafunga pepo. Kwa mshangao, alimtusi MUNGU na maneno mabaya ya matusi. Alilitusi JINA LANGU mara kwa mara! Kwa hivyo Nikaiweka Kilio cha Vita kwenye mdomo wake! Kilio cha Vita ambayo hakuna yeyote aliyewahi kuisikia!
Alikuwa mbele ya Kiti cha Enzi Mbinguni na MIMI BABA YAHUVEH na YAHUSHUA na IMMAYAH Tulizungumza Maneno ya Ghadhabu. Na ataangamizwa kwa kila neno anasema! Elisheva anasema, “Lakini kutafanyikaje na wale watu wanaoomba baraka juu yake? Kwa WEWE Ulisema kuwa tumbariki ‘Niko’. Nifanye nini na haya?” Alafu Nikampa moyo hata wakati huo-ingawa bado hakuwa amenigeuka MIMI-Nilijua wakati ambapo baraka hizi zitabadilika kuwa laana. Ingawa wote duniani [wanapoomba baraka juu yake], hadi jina lake litakapofutwa kabisa-kila Baraka iliyotolewa kwake sasa litakuwa laana! Kumbukumbu la Torati 28 halidanganyi. Na sasa yupo katika laana za Kumbukumbu la Torati 28! Na wakati huo wakaribia.
Nitachukua maisha yake. Na anajua kuwa kila kitu alichokuwa nacho kimepewa kwa mwanamume mwingine. [Yeremia 8:10] Basi Nitapeana bibi zao kwa wengine, na shamba zao kwa wale watakaozirithi.]
Ndiposa Nilimwambia Elisheva kuweka uso wa Ezra kwenye ukurasa wa mbele! Kuna Upako mpya! Kuna usafishaji mpya! Hayuko tena na yule aliyelaaniwa! Furahieni leo kwa ushindi! MIMI Ninakubariki katika njia mpya na mwanzo mpya, na kukupa tamanio la moyo wako kuwa na baba wa kiroho. Atacheka nanyi. Yeye hajitengi! Unanisikia Ezra? Haufai kujitenga. Nilikupa hiyo furaha na kicheko wakati hapo awali, ulikuwa unaogopa watu wengine watasema nini. Kwa vile Elisheva amekuwa mfano kwako, wale wanaompenda watamheshimu daima. Na Ninakupa Baraka ii hii kwako pia.
Kumbuka Ezra, hawa ni watoto tu. Nenda polepole na mafunzo mapya ambayo unayo. Na kama wewe na Elisheva mtakuwa na mafunzo tofauti, kumbuka MIMI BABA YAHUVEH, Ndiye Nitakayekuwa na Neno la mwisho. Na mnajua Sauti YANGU na hili ndilo sababu Ezra WANGU ni mwanamume anayetafuta Moyo WANGU! Ni Unabii-Unabii nyingi za kibinafsi, zinazoongoza na kuelekeza nyayo mnazochukua pamoja kwa umoja.
Na Ezra wewe humwombea yeye kuenda mbele tu, kumsukuma yeye kuwa bora zaidi-katika njia zote-wewe humpa moyo mahali yeye alikuwa hana raha. Unaomba maisha mahali yule mwingine aliomba mauti. Unaomba ushindi mahali yule mwingine aliomba kishindo. Wewe hautamruhusu kukata tamaa. Wewe hata huchunga maneno anayoyasema [kumkumbusha]: “Usione mabaya tu Elisheva!” Utakuwa mtulivu na mwanamke huyu ambaye amejua tu matusi. Utakuwa mtulivu na upendo ambao Nimekupa. Utakuwa mtulivu na “Wakanyaga pepo wa YAHUSHUA.” Utakumbuka kuwa wanahitaji upendo wa baba wa kiroho.
Hii ndiyo baraka Niliyokupa leo hii! Unapovuka Bahari ya Shamu! Hii ndiyo Pasaka Ninayowapa leo hii! Unapovuka Bahari ya Shamu! Lakini haivuki yeye pekee! Ninawainua “Wakanyaga pepo wa YAHUSHUA.” Na Ninamwinua yule ambaye-ameishikilia lile Gogo-aliye na Upako kama wa Musa. Na kama Eliya na Musa-Eliyahu [na Moshe]-wanavyotembea mkono kwa mkono, wakiongoza njia, mtaona Huduma hii ikizaliwa upya leo hii. Elisheva na E[zra] waliugua maumivu. Miili yao-ilihisi uchungu. Na Ezra alipigana na shetani na pepo, shetani alipojaribu kumfukuza! O lakini siku hii ni ya ushindi! Leo hii ndiyo siku mnanipa MIMI utukufu! Tazama Ninafanya mambo mapya! Tazama Ninafanya mambo mapya!
Wakati ni mfupi sana! Wakati ni mfupi sana! Wakati ni mfupi sana!
Hakuna kuchelewa tena. Kwa kuwa sasa hiyo mikono iko kwenye Gogo hilo! Hakuna umbali katika ROHO-Niliwapa ishara na maajabu-na waliihisi. Ezra WANGU huchukua haya kwa uzito! Yeye huwa hachezi na maombi! Elisheva hachezi na maombi! “Wakanyaga pepo wa YAHUSHUA,” lazima mchukue maombi kwa uzito! Dhambi hairuhusiwi. Ninazungumza na “Wakanyaga pepo wa YAHUSHUA.” Ninawaonya sasa. Sitaki dhambi. Sitaki dhambi. Sitaki dhambi mnapotembea katika mwanzo huu mpya. Sisemi kuwa nyinyi mtakuwa kamili! Lakini mnajua Ninamaanisha nini: sitaki dhambi ya maksudi, ya uasi. Hakuwezi kuwa na shimo kwenye vazi la vita, kwenye Dirii ya Haki! Kama mnafanya haya, njooni kwa uongozi. Kwa kuwa wao wana huruma. Msiruhusu hii dhambi kukua! Chukueni funzo kutoka kwa yule aliyelaaniwa. Msinilazimishe MIMI kuwakata kutoka kwa mzabibu! Lazima mwendelee kukua! Je, mnataka kuwa Bibi Arusi wa YAHUSHUA? Lazima mwendelee kukua! Msiichukulie wokovu wenu kama kitu kidogo. Hakuna hata mmoja wa “Wakanyaga pepo wa YAHUSHUA” ambaye hanifanyii MIMI kazi. Kwa kuwa mavuno ni makubwa lakini wafanyikazi ni wachache.
Msifikirie kuwa mtakaa tu pale na kujiita “Mkanyaga pepo wa YAHUSHUA” na kukosa kufanya chochote. Ninatarajia mengi sana kutoka kwenu na sio machache kwa mwanzo huu mpya, kwa mzao huu mpya.
Kwa hivyo Elisheva haukujua maneno utakayoyasema. Na ukaomba na kuomba. Na Maneno yakaja. Hii ni kwa sababu MIMI, BABA YAHUVEH, Nimezungumza maneno haya! Sio lazima kuelezea jinsi ile ndoa ilivyokuwa mbaya. Kwa kuwa katika macho YANGU haukuwa umeolewa- katika macho YANGU haujaolewa. Umeolewa na YAHUSHUA MASIHI! Na shetani anapojaribu kusema kuwa sio haki yako kumpenda huyu Ezra! Ezra hauna haki kumpenda huyu mwanamke, Ninawaambia kuwa hakuna ‘ndoa’ yoyote ila tu kijikaratasi kisichokuwa na thamani!
Kilichokuwa pale awali, sasa kimekwisha! Kumbukeni Amri Takatifu ya Talaka [Unabii 111], Nilipeana Unabii huo kwako kwa wakati huu, kwa sababu hii! Usiache yeyote akushtaki. Nilikuambia lazima iwe hivi. Siwezi kuwatumia nyote hadi msingi ujengwe katika jiwe la uaminifu na upendo. Kwa hivyo Ninawambia siri hii kwa “Wakanyaga pepo wa YAHUSHUA,” iliyotabiriwa mwaka 2005, na Malaika Watakatifu- Elisheva aliwaona.
Na Ninawaamini. Na Ninawaamini. Na Ninajua ni nini Nilichokiweka ndani ya kila mmoja wenu. Ninawaamini. Na leo hii, upendo wenu umekua. Hakuna yeyote! Yeyote, anayeweza kuchukua imani yenu! Hakuna mwanamume au-mwanamke yeyote! Yote yalimalizwa pale Msalabani! Hakuna mwanamume yeyote, mwanamke yeyote aliyekupa imani hiyo na hakuna mwanamume au mwanamke yeyote atakayeichukua! Sasa mnayajua tu yale maneno Niliyoyazungumza sasa. Fanyeni mengi zaidi KWANGU na sio machache! Inueni jina la YAHUSHUA! Acheni bendera ionekane! Mtukuze YAHUSHUA! Leteni nafsi KWAKE! Ruhusu upako wa IMMAYAH kutiririka-na watu hawataelewa-Upako Mpya. Lakini ni kwa sababu ya ufuniko mpya wa Mwanamume Mtakatifu Niliyemwunganisha na huyu Mwanamke Mtakatifu, unayeweza kumwamini!
Hongera! Hongera! Hongera! Hongera! Hongera! Hongera! Maneno yamekwisha. Nilikuambia jana kuwa kutakuwa na Neno. Na Nimeizungumza. Na siwezi kudanganya. MIMI ni YAHUVEH! MIMI ni MUUMBA! Na Niliyoyazungumza leo imekuja kutendeka! Na uongozi huu sasa, ndio wa kwanza kusikia Upako mkuu ipo juu yenu! Na majukumu makuu yapo juu yenu kuongoza na kuelekeza!
Na msimame na viongozi! Na mnapomheshimu Elisheva, Ninawaamuru kumheshimu Ezra! Waona Bibi Arusi wa YAHUSHUA sio kama bibi arusi wengine. Hakuna ulinganishi. Mwaona mnataka mengi zaidi na sio machache. Bibi arusi bandia husema, “Mimi ni Bibi Arusi.” Lakini ni roho, ni tunda- utakalolijaribu. Utajua kama ni Yezebeli, wale ambao ni bibi arusi bandia-hakuna Bibi Arusi, hakuna Bibi Arusi ila tu wa Ufunuo 14 na 7-[kumbukeni haya] wanapojaribu kuja na mafunzo mengine. Hawa ndio Bibi Arusi wa YAHUSHUA na hakuna yeyote anayeweza kulinganishwa, ni nini Nilichokiweka ndani ya kila mmoja wa Bibi Arusi wa YAHUSHUA!
Na MIMI BABA YAHUVEH Ndiye Ninayemjulisha MWANA WANGU, “Huyu ndiye Bibi Arusi WAKO. Nenda Ukamchukue Bibi Arusi WAKO! Lakini nyote lazima mjue, bado Ninafanya kazi ndani yenu nyote. MIMI BABA YAHUVEH Nasema, tazameni dunia! Kwa kuwa mwanzo mpya umetendeka leo hii katika Huduma hii ya Amightywind! Tazameni dunia! Ninapoweka mikono yao yote kwenye Gogo! Kwa kuwa Elisheva ndiye aliyekuwa wa kwanza kulipokea, lakini ilibidi angojee lile nusu lake! Nitawaambia siri “Wakanyaga pepo wa YAHUSHUA.” Kwa kuwa mnahitaji ishara, maajabu na miujiza ili kuwa na imani ya kuamini, lakini itakuwa katika wakati WANGU. Na itasaidia imani yako kukua. Kwa kuwa Ninajua ni nini Nilichokiweka ndani ya kila mmoja wenu.
Sasa Elisheva nenda kwa amani. Usimwogope tena, huyu adui. Kwa kuwa hawezi kufanya chochote ambacho sijamruhusu kufanya na hata ikifanyika, itarudi kwa njia ya ukombozi kwako kubarikiwa, kwa wote kubarikiwa, wanaotembea katika Nyayo ZANGU!
Mwisho wa Neno/Rekodi.
Imezungumzwa, Imeandikwa, chini ya Upako wa RUACH HA KODESH kwake Mtume Elisheva Eliyahu. Ikiwakera wengi, na baraka kwa wengine, Mtoto, Shujaa, Bibi Arusi wa YAHUSHUA MASIHI.
1 ”Mwana wa kiroho katika YAHUSHUA: Sina furaha iliyo kuu kuliko hii, kusikia ya kwamba watoto wangu wanakwenda katika kweli” (3 Yohana 1:4).
2 Mama Rm ni jina la upendo kwake Nabii Elisheva. Rm ni ufupi wa “Ringmaiden” na yeye ni mama wa kiroho kwa wale ambao wako katika Huduma hii ya Amightywind. YAH alimwinua Nabii Debora aliyekuwa Mwamuzi/Kiongozi, “mama [wa kiroho] pale Israeli” (Waamuzi 4:4; 5:7) na Mtume Paulo (Shaul wa Tarsus) alikuwa baba wa kiroho kwake Timotheo, “Kwa Timotheo, mwanangu hasa katika imani: Neema na iwe kwako, na Rehema, na Amani, zitokazo kwa MUNGU BABA na kwa YAHUSHUA MASIHI BWANA. (1 Timotheo 1:2)
3 ”Wakanyaga pepo wa YAHUSHUA” (YAHUSHUA’s Demon Stompers) ni jina kutoka Mbinguni iliyopewa kwa waombezi wa Amightywind wanaoishi katika Utakatifu-na wako kote duniani. Wengi hata hatujui majina yao, lakini Mbinguni inawajua wote.
4 Kathrynyah alipokuwa anayaandika haya, alisikia: “Kusanyeni askari kwenye kuta!”
5 Usitoe haya au kupeana kwa yeyote. Ifute bila kuisoma. Jifunike na damu ya YAHUSHUA. Tupilia mbali hizo laana. Mkemee shetani. Chukueni vita vya kiroho kwa uzito, kwa kuwa akikuandikia, shetani anaita, anataka nafsi hiyo.