Unabii 13

Waambie Mtoto WANGU, Waambie kwa Niaba YANGU

Imepewa Mchungaji Sherrie Elijah (Elisheva Sherrie Eliyahu) Januari 24, 1998

Hii ni kutoka unabii 105, YAHUVEH Alisema niweke maneno haya katika Manabii yote kutoka sasa: Nilikuonya kitambo sana Elizabeth (Elisheva) kutoita Huduma hii jina la mwanaume au mwanamke hata kabla hakujakuwa na Huduma. Niliweka hii kwa nafsi yako kwa kuwa hakuna chochote kimefanyika kwa mkono wako, hakuna chochote kimetokana kwa mdomo wako. Ni kutoka kwa Mdomo wa YAHUVEH Aliyeizalisha. Ni kutoka kwa Mdomo wa YAHUSHUA wako MASIHI Aliyeizalisha. Ni kutoka kwa mdomo wa RUACH ha KODESH IMMAYAH wako Aliyeizalisha. Kama ingekuwa kwa mkono wako pekee, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa ajili ya Upepo wa SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, Upepo Mtakatifu wa Uamsho, sio kwa pumzi yako, au ingeshindwa. ( Isaya 42:8)

Mwezi wa Julai 2010, YAHUVEH MUNGU Alisema kongezwe yafuatayo kabala ya kila unabii:

2 Mambo ya Nyakati 36:16, '' Lakini walikejeli Watume wa MUNGU, Wakadharau Maneno YAKE, na wakachekelea manabii WAKE, mpaka mori ya BWANA ikaamka dhidi ya watu WAKE, mpaka hakukuwa na suluhu.''

*******

Wakati wa maombi leo, 1/23/98, nilikuwa naomba na rafiki wangu Sharon. Nilikuwa namwambia kuhusu Gabrieli na vile bado naona taswira akiwa ameshikilia tarumbeta kwa kinywa chake, akingoja ishara ya kuipuliza kutoka Baba YAHUVEH Aliye kwenye kiti cha enzi.

Akaniambia,"oh Sherrie (Elisheva Sherrie) umeona hayo?'' Na nilipojaribu kumjibu, badala yake ndimi takatifu zikatoka kwangu! Lakini zilikuwa ndimi tofauti, ndimi za dharura; Machozi ya joto yakanitoka usoni. Kisha RUACH ha KODESH Akanionyesha YAHUSHUA. Alikuwa Amepiga magoti kwa ardhi. Alikuwa Anaangalia upande wa Gabrieli, na Amefunika uso wake na mikono YAKE na Analia. Analia kilio kigumu. Aliongea na nilisikia maneno haya. Kilio kilipasuka kutoka kwangu kanakwamba YEYE Alikuwa Analia kupitia kwangu. Nikaacha machozi yakauke kwa uso yangu, yalikuwa joto sana. Nikielewa kwa namna fulani kuwa haya hayakuwa machozi ya kawaida bali machozi yalikuwa yanatoka kwa YAHUSHUA. Bado nayasikia kwa uso yangu ni kama yalikaukia hapo na kukaa hapo.

Haya ndiyo maneno RUACH ha KODESH Anayaweka ndani ya nafsi yangu tena kwani nimeamrishwa, ''Waambie Mtoto WANGU, waambie kwa niaba YANGU.'' 1/24/1998 imepewa huyu Mtoto, Shujaa na Bibi Harusi wa YAHUSHUA ha MASHIACH.

*******

Japo Nashangilia kuja kuwachukua Watoto WANGU kutoka dunia hii mbovu, kuwabeba Bibi Harusi Wangu nyumbani kwa mikono YANGU, Nalia kwikwikwi kwa kuwa Nimegawika unusu. Wengi sana wataachwa nyuma, wengi sana ambao wanajiita WANGU ilihali Roho WANGU hayuko ndani yao. Wataachwa kuteseka kwenye ghadhabu ya Mwenyezi Mungu YAHUVEH! Waambie Binti YANGU, waambie kwa niaba YANGU. Waonye. Wengi wataskiza na kutii unabii huu. Nalilia makanisa ambayo yamejaa pomoni na watu husimama foleni ili kuingia ndani ya makanisa.

Bali RUACH ha KODESH (Roho Mtakatifu) WANGU hayuko ndani ya makanisa haya. Hawa watu hujiita Wangu lakini hawanijui. Ni wa kanisa ya wanafiki. Waambie Mtoto WANGU, waambie kwa niaba YANGU. Wataachwa kuteseka kwenye ghadhabu ya Mwenyezi Mungu YAHUVEH kama hawataTUBU! Hio itakuwa mkasa mkuu. Waambie Mtoto WANGU, Waambie kwa niaba YANGU, YAHUSHUA ha MASHIACH ANAKUJA HARAKA! Nawalilia mabwana ambao wataacha mabibi zao wapagani. Nawalilia mabibi ambao wataacha mabwana zao wapagani. Nawalialia kwa sababu walijaribu lakini wenzi wao wapagani hawakusikiliza.

Waambie Mtoto WANGU; Waambie kwa niaba YANGU kwa kuwa Nakuja haraka sana. Nawalilia ambao wanafikiri Nawachukia. Ilihali kwa dhambi zao Nilikufa na kufufuka kwa ajili yao. Waambie mtoto WANGU; Waambie kwa niaba YANGU kwa kuwa Nakuja sasa kwa haraka sana. Najua itaonekana ni kama watu wachache wanaskiza na wengi watafunika masikio yao, kuliko wasikie. Lakini hakuna chochote kimebadilika. Si walifanya hayo KWANGU pia? Si walinitazama MIMI Nikiwa Nimesulubishwa pale Kalvari? Si ni wale wale walioona miujiza YANGU, walipiga yowe Nisulubishwe kwa ule mti? Ingawa yote Niliyokuwa Nikitaka ni kuwa baraka kwao na kwenu, na Nilikufia wote ili kutoka kwa mkono wa Ibilisi uwekwe huru milele.

Japo ni vinywa ngapi bado vinalaani, vinakana, vinatotii, vinakejeli, na kunifuru? Binti YANGU, utakuwa kama sauti inayolia jangwani, itakuwa ni kama unasikia tu mwangwi wako ukirudi kwa masikio yako. Bali si mwangwi wako, lakini mwangwi YANGU dunia itasikia ukitoka kwa kinywa chako ambacho Nimetakasa na kupaka mafuta ili kunena Maneno YANGU, sio maneno yako.

Gharama imekuwa kuu ambayo wewe na wengine ambao Nimetakasa, kupaka mafuta ili kuongea maneno YANGU, dhabihu kuu umelipa. Lakini matuzo yako yatakuwa kuu. Hakuna chochote unachosalimisha kwa niaba YANGU kitaenda bila kutuzwa. Chochote ambacho umeteseka kwa ajili ya Jina LANGU. Nitakutuza sio duniani pekee bali milele Mbinguni. Waambie Mtoto WANGU; Wambie kwa niaba YANGU kwa kuwa Nakuja haraka sana.

Baraka kuu Nimehifadhia wale wote ambao huhudumia na kutii, huzaka, wale walio watakatifu na kuniabudu MIMI. Waambie mtoto WANGU; Waambie kwa niaba YANGU kwa kuwa Nakuja haraka sana. Nakwambia wengine watasikia mwangwi wa unabii hii kote duniani. Na hawataskia sauti ya mwanamke akiongea bali watasikia sauti ya Mwenyezi Mungu YAHUVEH Akiongea. Hawatasikia sauti moja lakini wengi watakuwa wakimwangwi sauti YANGU.

Hata wapagani watalazimishwa kusikia sauti YANGU. Si unaweza sikia mwangwi ukiwa mbali sana? Hata kama wanaziba masikio yao, watasikia sauti YANGU Ikiongea. Ni chaguo lao kama watatii, lakini Nitawalazimisha kusikiza. Usiogope chuki, mori ama kukataliwa, na matishio ya adui. Vile dunia Ilinichukia hivyo ndivyo watakuchukia na wale wote ambao ni WANGU wa kweli. Waambie Mtoto WANGU, waambie kwa niaba YANGU ili roho ziweze kwa Jina na Damu YANGU kuwekwa huru kutokana na mori ya YAHUVEH Mwenyezi ambayo inakuja duniani haraka sana. Kwanza Nakuja kuwapeleka Watoto WANGU nyumbani kwa upendo mwingi sana! Najua wale ambao ni WANGU; Wale walio na Roho WANGU ndani yao tayari wana mabawa ya kupaa yasioonekana.

Waambie mtoto WANGU; Waambie kwa niaba YANGU, kwa kuwa Nakuja haraka sana. Wale ambao Nawaita Watoto WANGU wataskia na kubaini sauti YANGU. Wale ambao si Watoto WANGU bali ni wa kanisa la wanafiki wataziba masikio yao na waseme enda mbali. Hatutaki kusikia Unachosema. Hata wakati Ninachotabiri kitakuja kutimia mwishowe, watakulaumu wakisema ni wewe umefanya kitendeke. Kwa sababu ulizungumzia na unachotabiria wengine kitatendeka haraka sana.

Hii dunia haitawahi kuwakumbatia Watoto WANGU. Hii dunia ni ya dhambi na uvundo puani YMWNGU. Uvundo wa dhambi Marekani na katika viongozi wa hii nchi na dunia inaniziba MIMI. Na kutokana na huu uvundo Nitakuwa huru. Ndio maana Nakuja kuwachukua Watoto WANGU salimini nyumbani haraka. Kisha hukumu ya YAHUVEH itaangukia dunia hii kwa njia ambayo haijawahi otwa wala haitatendeka hivyo tena. Na itatendeka kwa hii ardhi kafiri. Lakini kama dunia inakukumbatia wakati Nitakapokuja, basi jua hili na tahadhari kwa kuwa wewe si Mtoto WANGU. Wewe ni wa shetani na jina lako halijaandikwa katika kitabu cha Uzima cha Mwanakondoo chini ya andiko kombolewa. Unafaa tu hukumu na mori ya Mwenyezi Mungu YAHUVEH! Jehanamu ndio tu utaona.

Kuna Kitabu cha Uzima cha Mwanakondoo kilichoumbwa kabla ya dunia kutengenezwa, na Nilijua mapema ni jina gani itaandikwa na chini ya kichwa gani. Kunavyo vichwa vitatu tu pale. Waliokombolewa.... waliofutwa..... waliolaaniwa. Jina lako liko pale tayari katika moja ya maeneo hayo. Hata wale waliotajwa kwa kukombolewa wanaeza futwa majina yao, na kama imefutwa, ni kwa sababu ulijua uzuri wa YAHUVEH Baba, na bado ukachagua kuabudu mungu wa dunia hamu ya kimwili na ukanigeukia kimgongo MIMI na kujifanya tu kunipea mioyo na maisha yenu MIMI. Nilijua haya yote mapema yale uchaguzi utafanya, kwa kuwa MIMI ni Mungu wa hekima na maarifa yote na huwa sishangazwi na chochote kinachotendeka.

Kumbuka chochote, yeyote unayependa zaidi ndiye Mungu unayeabudu. Mick Jagger dunia inamkumbatia na kumpigia makofi, japo anaabudu mungu mwingine. Mungu wa uovu na hata kama Nimekubali hio umaarufu na mali, hii ndio tu atawahi jua kwa kuwa aliuza roho yake jehanamu kitambo sana. Sasa anatafuta kuchukua wengine pahali anapoenda. Wanamuziki mashujaa wengi wa “Rock” wanavyoitwa, hata hili jina shetani ananikejeli nalo kwa sababu anajua Mwamba ni moja tu la Uzima na ni MIMI Bwana yako YAHUSHUA ha MASHIACH. Jua hivi; muziki wa ‘rock’ si muziki wa Mwamba wa uzima! Wanamuziki hawa wa “Rock” hawana roho ya Mwamba wa uzima. Wameuza roho zao kupata sifa na mali. Wamefanya maagano na shetani ambayo Ninaeza vunja kirahisi na huwa navunja mara nyingi. Japo tu wanaweza tubu, geuka, na Niwaoshe kwa Damu YANGU Iliyomwagika ya Kalvari.

Watumbuizaji, mmeuza roho zenu. Mnalipwa kulaani yote ambayo ni takatifu na Jina LANGU ili kupata umaarufu na mali hafifu ya kidunia. Bali huwezi nunua njia yako kuingia Mbiguni. Matajiri na wenye sifa wa hii dunia si matajiri na maarufu katika macho ya Mweneyezi Mungu YAHUVEH. Nyinyi ni mafukara na hamjui. Mnakufia njaa Mkate wa Uzima, bali hamjui. Mnakufia kiu Maji ya Uzima lakini hamjui. Mko uchi, na hamna mavazi, bali hamjui. Mnaelekea jehanamu na hamjui. Nyinyi ni tajiri kwa mali ya kidunia, lakini fukara kwa zawadi za kiroho. Pesa zenu haziwezi nunua kile ambacho Nimewapa Watoto WANGU bila malipo. Watoto WANGU huniabudu MIMI, na huniweka kwanza katika maisha yao, wanaishi takatifu kwa niaba YANGU, na wanashahidi kwa niaba YANGU, wanateseka kwa ajili ya Jina LANGU. Watoto WANGU wanazaka, wanapeana sadaka kusaidia kazi ambayo Nimeamrisha watume wengine kufanya, wakitumia zaka na sadaka takatifu.

Kwa sababu ya hii Nitawanusuru siku ya hukumu. Watoto WANGU hawaogopi kusimamia utakatifu. Watazungumzia dhidi ya ushoga, na utoaji mimba, pornografia na jinsi zote za dhambi. Si Nilipenda kiasi tosha kuwaonya wafarisayo? Wewe je? Ni mara ngapi zaidi inakupasa? Watoto WANGU jua Nimeahidi, tuzo hio hio huyu mtume atapokea mbinguni kwa kuhudumia watu, kuleta maroho KWANGU, kuomba, kufunza, kuweka huru mateka kwa Jina LANGU. Kuongea dhidi ya uovu na kutangaza ujumbe wa unabii WANGU.

Hazina hio hio imewekewa yeyote anayesaidia, anayepea moyo, na anayeombea hawa watume, wanabii, wainjilisti, wachungaji, walimu wale wanaoweka mateka huru kwa niaba ya utukufu WANGU. Watapokea zawadi hizo hizo walizohifadhiwa huko Mbinguni.

Nawashawishi, pandani mbegu zenu tu katika huduma zinazohubiri na kufunza ukweli wote, hata kama inakuchukiza. Waombee hao wahudumu na muwasaidie. Sizungumzi kuhusu leseni za kibinadamu ambazo dunia hii huita cheti za kiroho. Wengi wanazo hizi na wanazo makanisa makubwa, ilhali wanazitumia kupotosha watu. Mwenyezi Mungu YAHUVEH pekee, ndiye Anayeagiza, sio binadamu.

Ninaifahamu Roho ya huyo mwanamume au mwanamke, Najua kama wanafaa kuwa kiongozi wa kiroho. Sasa tena, mwanadamu anacheza akijifanya mungu. Wengi wanaitwa lakini wachache wanachaguliwa na MIMI. Kwa hivyo usikubali shetani akudanganye. Utawaajibika kama unapeana zaka na sadaka kwa kanisa ambayo unajua haihubiri injili ya ukweli ya YAHUSHUA. Kama huyo mchungaji anafunza kasoro na anapotosha wengine na unamsaidia na zaka na sadaka zako utahisi hatia hata sasa unaposoma haya, na utajua sijafurahishwa. Kwa kufanya hivyo umesaidia adui kufanya Watoto Wangu kushindwa.

Ninafurahishwa unapopeana zaka na sadaka kwa wale ambao kila siku hulaza maisha yao chini kwa ajili YANGU. Ambaye kila siku ni mtumishi kwa watu na KWANGU. Mara mingi wanatusiwa, wanakataliwa, wanachukiwa kwa kusimamia utakatifu na kutangaza ujumbe ZANGU.

Watume wengi sana wanabeba mzigo wa kifedha pekee yao. Wako wapi Watoto WANGU wale ambao Nimebariki? Mbona mnapanda mbegu kwa mchanga mgumu na mkavu uliyo tasa? Mbona hamuombi na kuuliza pahali mtapanda zaka na sadaka zenu takatifu? Ndio, Nimefichua bandia wa Shetani wanaonipora MIMI na kwa kuiba zaka na sadaka takatifu na wanazitumia tu kwa makusudi yao. Mbwa mwitu katika mavazi ya kondoo wanafichuliwa na watasimama mbele ya Mwenyezi Mungu YAHUVEH waliyempora Siku ya Hukumu. Ole wao watume hawa.

Omba Nitakuonyesha halisi kutokana na bandia wa shetani. Nilikuwa na mfuasi mlafi, mwana wa jehanamu, japo haimaanishi wafuasi wangu wote ni wasaliti sio? Kwa hivyo ni ukweli tena. Umeuliza, "Mbona sibarikiwi kwa kupeana fungu langu la kumi"? Nitakuambia, ni kwa sababu unapanda mbegu katika mchanga mgumu mkavu unaofunza kasoro na kupotosha wengine kuelekea tumboni mwa jehanamu. TUBU LEO! Kama wewe ni Mtoto WANGU na haupeani zaka na sadaka basi haunitii MIMI? TUBU LEO! Ili Nikubariki kama miujiza ya mikate na samaki. Ili maombi yako yapate majibu ya kasi.

Watoto WANGU wengine Naskia wakisema, ''oh hapana, siendi kupeana pesa ZANGU zozote kwa huduma, siamini kutoa zaka,'' na wengine watasema, '' napeana kwa huduma, siipendelei na nakubali napeana kwa kusita lakini napeana si mingi lakini napeana''. Hapa ndio jibu LANGU kwa kikundi cha kwanza wanaojiita WANGU. Jiangalie mwenyewe, kama hautii neno la YAHUVEH, utaweza aje kusema RUACH ha KODESH WANGU ako ndani yako? Unaweza aje kusema unanipenda MIMI na usinitii MIMI? Kwa wale wanapeana kwa uchache na kusita nawaambia, Nitawarudishia kwa uchache na kwa kusita.

Kwa kipimo hichohicho unachopeana, na mtazamo huohuo ndio mtazamo huohuo Nitakurudishia. Kwa hivyo sasa mna majibu yenu. Wakati Sijibu maombi yenu haraka, sasa mnaelewa kwa nini. Inapoonekana mifuko yako yana mashimo, na mlaji anakuja na kuia mbegu zako ndio usiwe na ya kutosha kulipa wadeni wako, unaelewa sasa ni kwa nini. Kuna laana kwa fedha zote kwa ambao hawakumbuki kupeana asilimia kumi ya zaka. Sadaka ni kitu chochote ilio juu ya hio. Inapoonekana mambo yote yanayoenda mrama kwa maisha yako yanaenda mrama. Sasa unajua ni kwa nini.

Umeibia YAHUVEH! Malaki 3 haibadiliki. Watumishi mashuhuri wa hii dunia si kila mara wanaongea ukweli lakini kagua wanachosema, inaendanisha na neno la YAHUVEH ama wanafanya kombo maandishi. Inalainishwa na neno la YAHUVEH ama inageuzwa kuwa taswira ya mwanadamu? Zaka na sadaka zenu haijalishi ukubwa wa dhabihu si takatifu KWANGU, kama unaipanda kwa ufalme wa shetani. Na hivyo ndivo unafanya kama unasaidia mtu anayefunza kasoro, na anayefunza kanuni za mwanadamu, sio neno Takatifu la YAHUVEH ambalo haliongei uongo. MIMI Ndiye Neno Aliyefanywa binadamu. Unawaajibika sasa kwa kile ambacho haukujua ama haukufunzwa.

TUBU LEO!

Naweza fanya pesa zinyeshe kutoka Mbinguni kusaidia mahitaji ya watumishi, ila sichagui kufanya hivi bali Nataka uwe sehemu katika baraka kwa kupeana asilimia kumi ya zaka na sadaka kusaidia kazi ya YAHUSHUA. Wengi wenu mnafikiri zaka hukuja baada ya ushuru, baada ya kulipa bili zako lakini soma Malaki 3 kwa utaratibu, na utaona ni kile bora zaidi sio mabaki. TUBU, hapo awali haukujua afadhali, sasa unawaajibika kwa kile unachojua. Utajua wewe ni WANGU kikweli, unapokuwa na hamu ya kuzaka na unasisimuka unapoingisha hii kwa nafsi yako. Unapotoa zaka unaweka sehemu ya baraka Mbiguni iwachiliwe wakati inahitajika na upate majibu ya kasi ya maombi yako. Nijaribu MIMI uone kama MIMI ni Mungu wa kudanganya. Soma Malaki 3 kisha uniweke MIMI kwa jaribu.

Kwa sababu Najua wengi wenu hawatachukua nafasi kusoma, Nitamsimamisha Mtumishi WANGU hapa aipige chapa kwa kusudi lako. Kumbuka shetani amekupumbaza akitumia watumishi wake kukudanganya kwamba watumishi wote wanaendesha Rolls Royce, na wana jeti binafsi, na wanalainisha mifuko yao na fedha na dhahabu. Wale wanaofanya hivi wanaiba zaka na sadaka kutoka watumishi wanaohitaji, na wale watu WANGU Niliowaambia wawatolee zaka na sadaka. Mbona Naongea haya kupitia ujumbe huu wa kinabii? Ni kwa sababu hautasikia ukweli haya kwa huduma zenye mali, wanaogopa kukwaza binadamu. Hawatawaonya pahali mbwa mwitu wako. Hawatawaambia dhambi ni dhambi, YAHUVEH hajabadilika, mwanadamu amebadilika. Watumishi tajiri wanachukua pesa za kafiri na hawajali kuwaambia wanapaswa kutubu kwa sababu wako njiani wakielekea jehanamu.

Watumishi Ninaoinua wataongea maneno yangu; Hawana mali ya dunia ili waogope kupoteza. Lakini nyakati hizi za mwisho wanapaswa kuwa na usaidizi wako. Itakuwa hawa watumishi watakuwa na ujasiri wa Yohana Mbatizaji. Wengi wa Watoto WANGU wanafikiri kwa sababu watumishi tajiri na wenye sifa wana makanisa yaliyojaa pomoni, milaini ikisimama kuingia, kwa runinga na redio majina yenye sifa, basi zaka itatoa mbegu zaidi ikipewa mtu anayefanya kazi YANGU, lakini hawana sifa ama nyenzo za mali zilizotajwa. Watumishi WANGU waaminifu husaidia huduma kutoka kwa fedha zao wenyewe. Wananitegemea MIMI kuelekeza mioyo ya watu kupanda mbegu kwa huduma nyenyekevu. Nimeongelesha huyu mtumishi ambaye namtumia kufikisha huu ujumbe aliponiuliza MIMI mbona situmi samaki walio na sarafu za dhahabu kwa midomo yao. Ndipo asemavyo Mwenyenzi Mungu YAHUVEH kwa watumishi na watume WANGU wote waliouliza swali hili. Nimewatuma, Nimewaambia wapeane, lakini hawangetii.

Kwa hivyo Nitainua watumishi watiifu watakao panda mbegu zao kwa huduma zenye rutuba zinazoshinda roho. Ndio hata huduma hii kwa kuwa mfanyikazi anastahili malipo. Ni kwa nini wakati mtu ana kazi ya kidunia, kila mtu anafikiria, ndio wanapaswa kulipwa kazi yao ngumu. Lakini wakati mtu ananifanyia kazi MIMI na anafanya kazi ngumu zaidi. Kwa kuwa mtumishi hufanya kazi kila uchao, na kila siku ya maisha yao. Japo ni wachache wanaelewa wanastahili kulipwa pia. Ama hawastahili? Hii ndio kazi ya zaka. Si Niliamrisha zaka ya kwanza iende kwa kuhani Haruni? Soma Malaki 3 yote na uniulize MIMI Nikufunze mbona kuna baraka katika hili, si kwa mchanga pekee mbegu ilipopandwa, bali kwa anayepanda mbegu. Wewe ambaye unasoma hii RUACH ha KODESH WANGU Anakusadikisha na kukuonyesha kama wewe ni mtiifu au la. Malaki 3:6-18. MIMI YAHUVEH Sibadiliki. Ili nyinyi wazao wa Yakobo, msiangamizwe.

Tangu enzi za mababu zenu mmekiuka kanuni ZANGU na hamjaziweka. Rudini KWANGU Nami Nitarudi kwenu, asema Mwenyezi Mungu YAHUVEH. Lakini mnauliza niaje tutarudi? Mtu ataibia YAHUVEH? Japo mnaniiba MIMI. Lakini mnauliza, tunakuibia aje? Kwa zaka na sadaka. Mko chini ya laana, nchi mzima, kwa sababu mnaniibia MIMI. Leteni zaka yote kwa ghala, ndio kukuwe na chakula kwa nyumba YANGU. Nijaribu kwa hili, asema Mwenyezi Mungu YAHUVEH na uone kama Sitafungua madirisha ya Mbiguni (floodgates) na Niwamwagie baraka nyingi sana mpaka hautakuwa na nafasi tosha ya kuiweka. Nitazuia wadudu kukula mimea, na mizabibu kwa mashamba yenu hayatatupa matunda yao asema Mwenyezi Mungu YAHUVEH. Kisha wote watakuita aliyebarikiwa, kwa kuwa ardhi yako itakuwa ya kupendeza, asema Mwenyezi Mungu YAHUVEH na umesema mambo makali dhidi YANGU asema YAHUVEH.

Japo wauliza, ''Ni yepi tumesema dhidi YAKO?'' Mmesema, '' Ni bure kumuabudu YAHUVEH, ni faida gani tumepata kwa kufanya mahitaji YAKE na kujiendesha kama waombolezaji mbele ya Mwenyezi Mungu YAHUVEH?'' Lakini sasa tunaita fidhuli mbarikiwa. Bila shaka muovu anafanikiwa, na wale wanaomchangamoto YAHUVEH wanaponyoka. Kisha wale wanaomuogopa YAHUVEH wakaongea mmoja kwa mwingine, na YAHUVEH Akasikiliza na kusikia, na kunjo ya ukumbusho ilikuwa imeandikwa mbele ZAKE kuhusu wale waliomuogopa YAHUVEH na kuheshimu JINA LAKE. Watakuwa WANGU asema Mwenyezi Mungu YAHUVEH, siku ambayo Nitafanya hazina zangu za mali Nitawanusuru, vile mtu hunusuru mwanawake ambaye humtumikia na mtaona tofauti kati ya mwenye haki na muovu, kati ya wale hutumikia YAHUVEH na wale ambao hawamtumikii. Wale ambao wanasaidia huduma ZANGU zinazonena Neno LANGU, wanafanya hivo sio kwa sifa zao, heshima na utukufu wao, Lakini kwa sifa YANGU, HESHIMA na UTUKUFU. Ndio uzuri wao uwe mwangazo wa Mungu wanayeabudu. Nyinyi ni wa furaha KWANGU.

Oh aibu ambayo Ninayo kwa wale husaidia watumishi WANGU na wanafanya hivyo ili wapate kupunguziwa ushuru. Ukweli hawatapata baraka zingine isipokuwa hii. Chunga wale wanapeana kwa misaada ili wapate pesa zao tena za ushuru. Najua mioyo zenu. Ziko mbali na MIMI. Hii ni uvundo wa dhabihu ambao hauridhishi puani MWANGU. TUBU LEO! Nina mamilionea wengi ilhali ni wachache tu husaidia wale hudhubutu kuwa Watumishi WANGU. Watawajibika siku ya Hukumu.

TUBU LEO!

Wekeza uchumi kwa roho za watu. Hauwezi chukua pesa na mali unapotoka duniani. Nitauliza wale wamebarikiwa tele, '' Ulitumiaje pesa zako kwa utukufu WANGU, na Watoto WANGU?'' Utasemaje? Shetani anafanya watu wapande mbegu kwa kazi za uovu, wachungaji waovu wanakunja maneno YANGU, wanaongea maujumbe yasiyo kwaza kasoro wateseke kifedha, ama wapoteze hadhi yao ya kutolipa ushuru. Ama wanaogopa kukwaza makafiri na hawaogopi kukwaza Mwenyezi Mungu YAHUVEH. Ole wako. Nimepandisha cheo Watumishi ambao hawana mali ya kidunia. Lakini kwa ujasiri hunena maneno YANGU, wakibariki watu WANGU na MIMI.

Naongea kwa mioyo ya watu WANGU, Nasema toa zaka, peana sadaka za upendo na wanajifanya kiziwi na kipofu kwa mahitaji ya watumishi WANGU. Ole wenu nyinyi watoto waasi! Nitachukua kile ambacho Nimewapa kutoka kwenu na Nipe mmoja wa Watoto WANGU ambao si walafi. Kazi unayo Nimekupa, si kuweka sehemu endapo utahitaji siku fulani, bali ni kuitumia kuhubiri Injili duniani. Ninaongelesha mioyo za wale wameabudu mali za nyenzo kuliko MIMI. Wale wameabudu pesa kuliko MIMI. Hizi vitu hazitakunusuru wakati Nitakuja tena. Jenga hazina zako Mbinguni, pahali nondo na kutu hazitaangamiza, pahali wezi hawawezi ziiba. Ni wangapi wenu wanafanya hivi? Unawavalisha nguo walio uchi? Unawalisha maskini? Sio kwa jina lako bali kwa Jina LANGU! Sio kwa utukufu wako bali kwa utukufu WANGU.

Waigizaji na matajiri hupeana kwa namna zote za misaada wakifikiria hii itatuliza hasira YANGU, bali sivyo. Wengi wanafanya haya mambo, wanapeana kidogo kutoka kwa tele zao kwa sifa zao, heshima na utukufu sio kwa WANGU katika majina yao sio Majina YANGU. Kweli, hii ndio tuzo yao pekee. Pesa haiwezi jaza utupu ambao Nilikuwa Niujaze. Kila mtu ana utupu; Ni ufyonza uliowekwa ndani ya kila binadamu aliyeumbwa kwa taswira YANGU kunipenda MIMI na kuwa na hamu ya kupenda Muumbaji wao. Ila wanadamu wanajaza utupu huu na mambo mingi ya kidunia, nyenzo nyingi wakitafuta miungu wengine, ila ni MIMI pekee Naweza jaza utupu huo. Nahuzunika kwa kuwa dunia inafikiria mtu akifa ambaye ni tajiri ama mwenye sifa na kila mtu anajua jina la huyo mtu, huyu mtu kwa sababau ya sifa ama mali yake duniani atarithi ufalme wa mbinguni. Japo ni uongo kutoka jehanamu! Kama matajiri na wenye sifa wanapendwa na hii dunia, na hawakataliwi kwa kuwa WANGU, basi tena nasema hawana Roho wa Mungu Aliye Hai ndani zao!

Waambie Mtoto WANGU; Niambilie wao kwa niaba YANGU, Je, kweli hii ni thamani ya bei ya jehanamu milele? Waambie Kunitumikia pekee na Kuniabudu na Kunipenda YAHUSHUA ha MASHIACH, kKunieka MIMI mbele kwa maisha yao, kKunitii MIMI, kuishi takatifu, kupigania utakatifu, kupenda wengine tosha kuwaonya, hii itawafikisha Mbinguni. Waambie mtoto WANGU; Waambie kwa niaba YANGU, wameiba upendo na ibada iliyokusudiwa kuwa YANGU. Waambie mtoto WANGU; Waambie kwa niaba YANGU, wakitaka wokovu inakuja kwa njia ya Damu Niliyomwaga Kalvari.

Waigizaji hufanya kazi nyingi nzuri sana, bali hawazifanyi kwa niaba YANGU, kwa sifa, heshima na utukufu WANGU. Waambie mtoto WANGU; Waambie kwa niaba YANGU. Waambie waTUBU; Wageuke dhambi zao, kwani kuna msamaha katika Damu YANGU Iliyomwagika Kalvari. Niliwakufia wao pia ili wawekwe huru. Waambie, mtoto WANGU; Waambie kwa niaba YANGU kwa kuwa haujatumwa kwa maskini pekee, na kondoo walionyanyaswa, umetumwa kwa wale ambao wamejiweka juu ya wastani wanaoamini utangazaji wao walinunua. Umetumwa kwa viongozi wa hii nchi, na [nchi] zingine. Waambie mtoto WANGU, waambie kwa niaba YANGU kwa kuwa tajiri na maskini wote ni sawa KWANGU. Nilimwaga Damu YANGU kwa ajili yao pale Kalvari, ili kutoka jehanamu wawekwe huru. Waambie mtoto WANGU, waambie kwa niaba YANGU kwa kuwa Nakuja kwa kasi! Imani bila matendo imekufa! Matajiri wengi na wenye sifa hawajaweka imani yao KWANGU, ila umaarufu wa dunia. Kwa nguvu za aliye na pesa nyingi.

Ata mwenyeji wa tamasha inayopendwa ya kuongea ambaye dunia inajua alikuwa WANGU mara moja lakini sasa amepotoka. Dunia inamkumbatia kwa kuwa anasimamia dunia. Hasimamii tena utakatifu, anachekelea kile ambacho anajua ni takatifu. Anadharau Neno la YAHUVEH ambalo aliamini mara moja anatafuta miungu mingine kwa nyege za masikio yake. Amekuwa kahaba wa miungu mingine, ila mwambie ATUBU na anirudie MIMI, kwani ni MIMI Nimempa neema na utangazaji, ndio aongoze wengine kwa Damu YANGU ya Kuokoa ya Kalvari. Mwambie haya Oprah Winfrey. Mwambie mtoto WANGU, mwambie kwa niaba YANGU kwa kuwa hatima ya binti mfalme Diana itakuwa yake milele kama hatatubu upesi na arudi kwa YAHUSHUA ha MASHIACH, Aliyelipa gharama, ndio awekwe huru kutoka mkono wa shetani. Mwambie Oprah Winfrey, arudi Kalvari arudi kwa mizizi ya mababu zake pale anapofaa. Mwambie hakuna ambaye anaeza mpenda kama Ninavyompenda.

Mwambie Nimembariki na hamu yote ya moyo wake, na hakuna chochote kinaweza kujaza utupu uliotengenezwa na Mungu ila MIMI. Namgojea arudi japo anajiita WANGU, na Roho WANGU Ako mbali naye. Mwambie kwa niaba YANGU binti YANGU, Namlilia! Nalilia hii dunia anayopotosha. Mwambie Oprah, Mtoto WANGU, mwambie kwa niaba YANGU hata kama atadharau, atajua kwa nafsi yake nabii wa YAHUVEH amemuonya na yule Nimetuma ni wewe. Mwambie mtoto WANGU, mwambie kwa niaba YANGU, rudi kwa Mungu wa Utakatifu uliyemwabudu mara moja, YAHUSHUA ha MASHIACH Aliyelipa gharama ya Kalvari. Mwambie anapaswa kuishi kwa Neno Takatifu la YAHUVEH, ama hatawahi ona familia yake inayomgoja huko Mbinguni. Mwambie, mwambie Binti YANGU, kwa niaba YANGU kwa kuwa Nimekuita uhudumie mwenyeji wa tamasha ya kuongea ya dunia Oprah Winfrey.

Mwambie alikuwa amekusudiwa kuwa WANGU, ila amenitoroka MIMI mara kwa mara. Mwambie binti YANGU, mwambie kwa niaba YANGU. Watoto WANGU wote ambao humtazama kila siku, na humfanya tajiri, hunukuu maneno anayosema, sasa nawaweka wazi sana na ujumbe kama huu. Unajiita na jina LANGU, japo unamtazama kila siku akichukua maana ya utakatifu na kuchafua. Inuka na umwambie, mwambie kwa niaba YANGU, nyinyi pia ni sauti ZANGU zinazopaswa kumrudisha kwa Roho ya kutubu kupitia Damu YANGU iliyomwagika Kalvari. Mwambie watoto WANGU; MWAMBIE kwa ajili YANGU ni nyinyi anajaribu kuwafurahisha si MIMI.

Nasherehekea nyinyi, Watoto WANGU mlio tajiri kwa imani. Hamuweki imani yenu kwa tajiri za dunia. Huwezi hudumia bwana wawili. Utamchukia mmoja na umpende mwingine. Huwezi hudumia dunia mbili, dunia ya kimwili, na dunia ya ufalme wa Mbinguni. Ni wale tu wanakataa kimwili na wanaishi na kutembea ndani ya RUACH ha KODESH ndio Nitanusuru. Waambie mtoto WANGU, kuwa sauti YANGU na uwaambie kwa niaba YANGU. Kwa yule YAHUSHUA Amempa masikio na macho ya kiroho, na huu ujumbe atawekwa huru. Waambie mtoto WANGU, waambie kwa niaba YANGU. Kondoo WANGU mweusi, haijalishi umbali umepotoka, rudi kwa mchungaji wa pekee mzuri, rudi KWANGU.

Kemea shetani na kutoka hawa ibilisi wa uovu toroka na Mbinguni utaona. Waambie mtoto WANGU; waambie kwa niaba YANGU, YAHUSHUA Alilipa gharama pale Kalvari. Nimefanya yote Niliyohitaji kufanya; sasa Nawaachia uchaguzi kwenu. Waambie, wote wenye masikio ya kuskiza, na macho ya kuona, pitisha ujumbe haya Nimekunenea, ndio uwe thamani siku inayokuja, Ninapokusanya WANGU wasiotingizika kwa mikono YANGU na kuwapeleka nyumbani, utajua kwa sababu ya maneno yako hauendi pekee yako. Waambie watoto WANGU; Waambie kwa niaba YANGU, YAHUSHUA ha MASHIACH Anakuja upesi. Kwa kuwa Gabrieli ana macho yake kwa Baba YAHUVEH, pembe ikiwa kinywani, anagoja tu ishara ya Baba YAHUVEH, alafu YAHUVEH Atanigeukia Aniambie, ''Enda, sasa ndio wakati, endea Bibi Harusi wako!" Hadi itakapotimia, Nangoja, Natazama na kuskiza Nikijua nani atatii, na apitishe onyo kuhusu Siku ya Hukumu inayokuja.

Waambie Watoto WANGU, waambie kwa niaba YANGU. Pamoja wacha sauti zenu zivume na nabii huyu WANGU wakati nafasi ipo. Waambie Watoto WANGU, waambie kwa niaba YANGU. Waambie mtoto WANGU, waambie kwa niaba YANGU. Kuwa na imani KWANGU ndio funguo la hatima yao. Lakini haitoshi tu kuamini MIMI ni nani, watoto WANGU sharti watii, wapende, watumikie Mungu Mkuu YAHUVEH ''I AM!'' Waambie mtoto WANGU, hata kama wengi hawatasikiza, waambie kwa niaba YANGU! Mbinguni ama jehanamu ni milele. Waambie watoto WANGU, waambie kwa niaba YANGU. Umeonywa siku ya leo, utafanya aje? Nitasema, ''Umefanya vizuri wewe mtumishi mzuri na mwaminifu, karibu ndani,'' ama Nitasema, ''Ondoka KWANGU wewe mfanyikazi wa uovu na dhambi, RUACH ha KODESH wa Baba YANGU haukuwa Naye ndani yako. Umetumikia mungu wa dunia hii na dhambi sasa umetumikia shetani utateseka naye milele.'' Waambie watoto WANGU, waambie kwa niaba YANGU. YAHUSHUA ha MASHIACH ANAKUJA UPESI! Waambie mtoto WANGU, waambie kwa niaba YANGU!

Imepewa huyu mtoto, shujaa, Bibi Harusi wa YAHUSHUA, Nabii Sherrie Elijah (Elisheva Sherrie Eliyahu)

Unahitaji maombi ama wokovu? Una maoni ama maswali?

Tafadhali mwandikie Mtume Mnabii Elisheva Eliyahu!



CLICK HERE or the image below to go directly to her youtube channel
YAHSladyinred