UNABII WA 2

GHADHABU YANGU NI KUU KAMA PENDO LANGU!

Alipewa Rev. Sherrie Elijah Januari 8, 1997

* * * * * * *

Hivi ndivyo asemavyo Bwana MUNGU wa Majeshi, “MIMI nitaonyesha kuwa MIMI hutuza wale wanaonitafuta MIMI kwa bidii. Nithibitishe MIMI na uone huu ndio mwaka uliongoja. Mjiunge pamoja kote ulimwenguni kupitia muujiza wa tarakilishi, unganeni pamoja, simameni pamoja na mtaona kumwagwa mkuu wa RUACH ha KODESH (Roho Mtakatifu) kushinda hapo awali.

Kwa kuwa mtaziamsha zawadi zenu kati yenu wenyewe zilizokuwa zikilala kwa kutotumika au zile ambazo hazitumiwi sana. Mtaunganishwa pamoja katika Roho hata bila kupanda ndege, mtakuwa kitu kimoja kwangu MIMI na kupitia muujiza wa teknolojia ya tarakilishi kwa kuwa ingawa shetani huitumia kwa uovu wake, Ninaitumia tena zaidi kwa Sifa, Heshima na Utukufu WANGU. Manabii WANGU wataitumia kupasha ujumbe WANGU kwa hivyo msikize kwa makini mwaka huu ndio mjue kutarajia nini kabla haijatendeka. Nitatuma Manabii kabla Nitume ghadhabu YANGU.

Omba kuwa nikupate ukinitafuta MIMI kwa bidii, ukinipenda MIMI na ukitii Neno LANGU. Usiseme unanipenda MIMI kama haunitii MIMI. Ingawa dhambi zako zimeoshwa na Damu Inayookoa, usinijaribu MIMI kwa kuwa Najua ni nani aliyeokolewa na ni nani anayejifanya tu.

Hapo awali Nilimwambia Nabii WANGU aseme hukumu huanza katika nyumba ya YAHUVEH. Sasa siku hii ya Jan. 8 1997, Hukumu umeanza katika nyumba ya YAHUVEH kwa njia kuu tena zaidi kushinda hapo awali. Tazama na sikiza kwa makini, kuwa tayari. Nitazame MIMI nikisafisha hekalu kama wakati Mwana WANGU alivyoichana hekalu, ilikuwa ya mambo yajayo na imeanza. Wachungaji waovu na wachungaji walio na unyama, manabii bandia, jihadharini; ghadhabu kuu na hodari inawajia mwaka huu.

Kimbieni kama bado mwaweza. Mmefanya vitu katika JINA LANGU, mmewadhuru Kondoo WANGU Wadogo, mmewachinja na kuwasulubu Kondoo WANGU kwenye miguu ya shetani; kwa haya mtalipa. Mmewatia moyo wale waovu na kuwakatisha tamaa wale watakatifu. Mmesema Nilizungumza uongo, na mmeona maono lakini hata hamnijui MIMI. Kwa hivyo mmenionaje MIMI au kuniskia MIMI. Mmewadanganya wengi na hata kutumia Neno LANGU Takatifu kwa faida yenu na utukufu wenu.

Jitayarisheni kupigana kwa kuwa hamtakuwa mnapigana na Mwenyezi MUNGU YAHUVEH pekee, lakini pia na kizazi kipya cha mashujaa WANGU walio na upako wa RUACH ha KODESH (Roho Mtakatifu). Sikilizeni kilio chao cha vita. Wamejazwa na hasira za YAHUVEH kwa yale yote ambayo adui amefanya. Wanawasaka kondoo waliofukuzwa na adui. Kuwaleta kwenye miguu ya Mchungaji Bora wa pekee, YAHUSHUA ha MASHIACH (Yesu Kristo) wa Nazareti na Kalvari. YAHUSHUA ha MASHIACH ni JINA LAKE na liko katika midomo yao, pia limeandikwa kwenye vipaji vyao (akili) na moyo.

Ninawezesha huduma yangu ya mizizi mitano kwa njia wasiozijua bado na wakati wote watasikia sauti YANGU na kuona kuwa MUNGU wanayemtumikia ni hodari katika vita. Watoto WANGU hamna chochote cha kuogopa, kwa kuwa Najua Kondoo WANGU na mnajua Mchungaji wenu. Hamna chochote cha kuogopa. Tena Nawaambia, angalieni juu, ukombozi wenu umekaribia. Kuja KWANGU upo karibu kushinda mnavyowaza, lakini adui anajua haya na sasa hujaribu kuharakisha uovu.

Kumbuka wakati adui atakapoingia, kama mafuriko Nitainua kiwango dhidi yao. Wale wanaosimama nyuma ya mimbari na kuhubiria Kondoo WANGU wanasikia sauti YANGU. Nimewaita kuwa mashujaa wa YAHUSHUA na sio waoga. Chukua kile ambacho adui amekuibia katika JINA LANGU. Shetani yuaja kuiba, kuua na kuangamiza. Acheni kumruhusu. Tena Nasema nimewaita kuwa Mashujaa WANGU, sio waoga.

Msimpe nafasi shetani na shetani hatakupa nafasi pia. Siku hii, kanisa ambayo sio mjengo tu wala mchungaji bali ni Watu WANGU, wanaoitwa kwa JINA LANGU, lazima wajitokeze na kusema “Sisi ni mashujaa wa YAHUSHUA ha MASHIACH; tunajua kuwa sisi ni zaidi ya washindaji kupitia JINA LAKE YAHUSHUA. Vita ni ya YAHUVEH, ushindi ni wetu kwa Sifa, Heshima na Utukufu wa YAHUSHUA ha MASHIACH na YAHUVEH.”

Kabla hatujafika mwisho kwa kila kipengele mtaniona MIMI nikiwatenganisha wale ambao sikuwaunganisha pamoja, nyinyi wenyewe ndio mliofanya hili jambo. Lakini itachukua mkono WANGU pekee kutenganisha kile ambacho hakikuwa kinafaa kuunganishwa. Je, ng’ombe dume na panya wanaweza kuvuta mkokoteni? Na bado zaidi ya haya, je, ng’ombe dume au mchwa wanaweza kuvuta mkokoteni iliyojaa matunda? Omba kwangu MIMI na RUACH ha KODESH atakuonyesha ni wapi yule mchwa au panya ameunganishwa kwako. Halafu kubali vile Nitakavyochagua, na yupi Nitakayechagua kutenganishwa nawe.

Kwa kuwa mmeshangaa kwa nini maombi yenu ilizuiwa, ni kwa sababu kuna wale ambao hawajaunganishwa kwa usawa kwa njia nyingi tofauti. Haya inawahusu pia Wahubiri WANGU na huduma, pia maisha yao ya kipekee. Hakuna yeyote atakayetoa chochote kwa ajili YANGU, ambacho sitakirudisha zaidi yake mara mbili katika maisha haya na mbinguni. Niamini MIMI na kuwa myenyekevu kama Abrahamu alivyofanya na kuwa na imani. Sema, “YAHUVEH, chochote kinachonizuia kuwa yote niliyoitwa kuwa, na yote niliyochaguliwa kufanya, naitoa kwako kama sadaka, chochote kinachosimama njiani mwa matakwa yako kamili kutendeka maishani mwangu.

Toa kwangu MIMI yote ambayo wewe uliyo, na yote ambayo wewe sio na nitazame MIMI nikifanya muujiza hodari wa ukombozi katika maisha yenu na yale ya wapendwa wenu. Mwaka huu Nitawapatia tamaa za nyoyo zenu kwa kuwa najua tamaa za nyoyo zenu ni tamaa Nilizowapatia.

* * * * * * * *

Ilipewa siku hii kwake Rev. Sherrie Elijah 1/8/97 kupitia upako wa RUACH ha KODESH kwa utukufu wa YAHUSHUA, mwana wa PEKEE wa YAHUVEH.

Kumbukumbu kutoka kwake Rev. Sherrie:

Omba katika nguvu za ndimi ya RUACH ha KODESH na haswa kwa zawadi ya kutabiri ijitokeze ndani yako. Sisi Manabii tunahitaji kutabiriwa pia. Nahubiria wengine, lakini wachache hunihubiria. Inaweza kuwa kwamba wewe ni mmoja wao.

Ndio mtetemeko wa ardhi unakuja pia huku Marekani. Nimepata ndoto nyingi na nimeona mkoa wangu wa Indiana ikikaribia kuwa magofu. Itakuwa 8.9 katika mizani ya Richter na katika wakati huo pia kutakuwa na vimbunga na mafuriko. Itagonga karibu mikoa 15 na Indiana wakati moja.

Nilimsikia MUNGU Baba akisema katika ndoto yangu ya kushtua sana, watu wakifanya usafishaji na kufikiria imeisha. “Mwisho wa raundi 1, sasa ni raundi 2.” Lakini tumsifu YAHUSHUA, kwa kuwa amenionesha katika ndoto hiyo ingawa nyumba kadhaa zitabaki zikisimama itakuwa kama wakati wa Musa na wale watu wanaomwabudu YAHUSHUA, katika roho na ukweli, nyumba zao na maisha yao yataokolewa.

Malaika wa kifo atawapita na hatawashika au nyumba zao. Kliniki za uavya mimba zitaanguka katika mashimo kubwa yaliyozama wakati ardhi itakapofunguka na kuwameza. YAHUVEH mwenyewe ataonyesha ni nini kitakachowatendekea wauaji wa watoto wasio na hatia kama bado wapo katika tumbo za mama zao.

Ushoga ni roho chafu ya tamaa iliyopotoka na sio kitu inayotokana na kuzaliwa na kasoro yoyote lakini ni dhambi na imetumwa na shetani kukejeli muungano wa YAHUVEH inayoitwa ndoa. Lakini tena Mwenyezi YAHUVEH atalipisha kisasi kwa njia zitakazothibitisha kuwa Yeye hakejelewi virahisi. Na ole wale wanaomkejeli, kwa kuwa YAHUVEH sio MUNGU wa huruma pekee na upendo lakini wa ghadhabu kwa maadui wake.

Taifa na watu wamepoteza kuogopa kwa YAHUVEH tena zaidi hapa Marekani na kwa wale wasiomwogopa; atawapa jambo la kuogopa. Lakini wale kati yetu, bibi arusi wa YAHUSHUA hawana chochote cha kuogopa, bali tu tufanye yote iwezekanavyo kumtii, kusikia sauti yake, na kumwabudu katika Roho na ukweli. Waonye wengine ndio damu ya Ezekiel 3:17-21 haitakuwa mikononi mwako. Ole wao wanaosikia lakini hawasikizi. Kwanza kutakuwa na hukumu katika nyumba ya YAHUVEH, halafu wapagani.

Mali ya waovu na kazi zao zitapewa watoto wa kweli wa YAHUSHUA wanaomwabudu na walio na imani, na wanaojaribu kumtii na kumtumikia, wakieneza Injili ya YAHUSHUA kwa wokovu wa roho. Walio na mamilioni watajitokeza kwa wingi kushinda hapo awali na itakuwa ni watoto wa YAHUVEH walio na mali, kampuni za ndege, vituo vya ununuzi.

Nimeitwa pia kuwa mpanda kanisa na mchungaji wa kanisa nyingi. Haya yanahitaji pesa ambazo sina kwa sasa, lakini naamini kwa imani kuhusu haya kabla mwisho wa mwaka. Tafadhali wape moyo ndugu na dada zetu kote ulimwenguni, waambie YAHUSHUA atatetea kanisa yake kwa njia kuu kushinda hapo awali. Shikilieni papo hapo na tazameni maadui wakianguka.

Uchina utakuwa na mtetemeko wa ardhi mkuu na mapigo zitawakabili na viini ambazo hakuna binadamu yeyote anayeweza kuponya, na watateseka katika haya yote kwa kuwatesa watoto wa YAHUSHUA. Tena YAHUVEH atathibitisha kuwa yeye sio kipofu wala kiziwi na kuwa amesikia kilio cha watoto wake. Mwone adui akisema kuwa YAHUVEH hayupo. Lakini chunga shetani kwa sababu ukombozi wa watu wa YAHUSHUA upo njiani hata sasa hivi haya yakiandikwa.

Wale ambao wamewatesa Wakristo wa kweli ndio watateswa sasa. Wale waliotuma roho za uharibifu, umaskini, kukata tamaa na kifo ndio wataangamizwa na hizi Roho kwa njia kuu zitakapowarudia. Maadui wetu wataangamia wasipotubu mbele ya MUNGU anayewahukumu wote. Mali itachukuliwa na imeanza kuwekwa kwa mikono ya watakatifu kupitia YAHUSHUA ha MASHIACH. Itakuwa muda mfupi pekee kabla YAHUSHUA wetu aje tena na pesa hii itumike kukusanya mavuno ya roho.

YAHUSHUA wetu yuaja! Kwanza lazima apate kanisa yake tayari bila doa wala kunyazi. Viongozi Watakatifu wasio na kiburi yoyote kwa kuwa itafanyika katika nguvu za RUACH ha KODESH ili mtu yeyote asichukue utukufu wa YAHUSHUA. Nguvu ya upako mkuu kushinda hapo awali itawajia wale watumishi wake waliochaguliwa na ishara kuu, maajabu na miujiza zitawajia waabudu wa kweli wakiona kwamba YAHUSHUA wetu bado anafanya miujiza leo kwa njia kuu.

Wengine watakuwa na upako mkuu hadi vivuli vya watumishi wengine vitafukuza mbali shetani na pepo mbaya na kuponya wagonjwa na kufufua waliofariki kwa utukufu wa YAHUSHUA pekee. Mwaka wa 1997 utakuwa hatua ya kugeuka wa kanisa, kanisa zinazokataa mvinyo mpya watakuwa tupu au wamejawa na nguvu za ibada ya uovu. RUACH ha KODESH hatavumilia tena kanisa zilizogawanywa kwa ubaguzi. Sisi wote ni kitu kimoja na hatufai kuona rangi yoyote isipokuwa nyekundu tu. Sisi ni watu – tuliooshwa na Damu na kusafishwa na Damu inayookoa ya YAHUSHUA ha MASHIACH wa Kalvari.

Ndugu na dada zetu haijalishi rangi, jamaa, au lugha yao; ni wale waliookolewa, waliotakaswa, na kujazwa na RUACH ha KODESH. Tutawajua kwa matunda yao na kujiunga na roho zao. Shetani amejaribu kufanya watu wa rangi tofauti kufikiria wao ni bora, hii ni kiburi na YAHUVEH husema kuwa kitu kimoja anayochukia ni kiburi.

Yeye hana upendeleo. Anajua watoto wake ni nani na wale walio watoto wa shetani ni nani. Hataruhusu wateule wake kudanganywa tena. Tazameni wale bandia wakianguka kwa njia kuu na YAHUVEH akiwainua manabii, wainjilisti, wachungaji, mitume na walimu wa kweli kuchukua nafasi za wale bandia.

Waliotajwa mwisho watakuwa na upako mkuu kushinda waliotajwa kwanza (bandia), kwa sababu watathibitisha kuwa si kwa uwezo au nguvu zetu lakini kwa nguvu za RUACH ha KODESH pekee. Kupitia jina la YAHUSHUA ha MASHIACH na ni kwa kupitia Damu Yake ndio ukombozi utakuja. Ni upako utakaovunja nira na utumwa, kupitia nguvu za RUACH ha KODESH.

Kuna mashujaa wengi walioanguka. Hawana nguvu yoyote au imani ndani yao. Shetani amewadanganya na wanafikiria YAHUSHUA haoni machozi yao au kusikia kilio chao mwaka huu. Shikilieni papo hapo, sasa si wakati wa kukata tamaa. Huduma mlizopewa zitafanikiwa na yote mliyoyangoja itakuwa ukweli. Msife moyo.

www.allmightywind.com

www.almightywind.com

Contact AmightyWind



CLICK HERE or the image below to go directly to her youtube channel
YAHSladyinred