UNABII WA 4

MSIWE NA SHAKA WAKATI AMBAPO HAMNIHISI KANDO YENU!

Alipewa Rev. Sherrie Elijah Februari 5, 1997

*******

Leo tu nilisema “YAHUVEH, ni nini kinachofanyika hadi siwezi kuhisi kuwepo kwako kama nilivyoweza hapo awali?” Nimetubu dhambi yoyote niliyotenda bila kujua, lakini bado kuwepo kwako sio sawa. YAHUVEH hazumgumzi sana na nina wasiwasi. Si kwa ajili ya tunayoyafanya, kwa kuwa bado tunamjua YAHUSHUA na atatupenda sote milele, bali tunafanya yote iwezekanavyo kumfurahisha na kumwabudu. Tunajua lazima kwa imani tuamini neno lake YAHUVEH. Hajatuaacha.

Hatufuati hisia zetu, hisia hutudanganya, lazima tufuate imani yetu. Kwa kuwa wale walio wema wataishi kwa imani pekee, sio hisia. Lilikuwa jambo kuu tulipokubaliwa kuhisi kuwepo kwake, lakini kuna kitu kinachobadilika katika eneo ya kiroho na ingawa YAHUSHUA bado yupo nasi, ni kama amelala kwenye mashua, na tunaangamizwa na dhoruba za maisha na sisi ndio wanafunzi wanaosema, “YAHUSHUA, amka kabla tuangamie”. Alafu YAHUSHUA huamka na kusema, “Enyi mlio na imani kidogo” na kukemea dhoruba. Bado ninamngoja akemee dhoruba nzito ambazo nimekabiliana nazo kwa muda mrefu sasa inaonekana. Tunajua kuwa kuna wakati uliotengwa kwa ukombozi wetu. Ninavyonakili haya ninapata upako. Nimeacha na kuomba katika Roho na nitafanya jambo hili wakati mwingine, baada ya kuchukua mamlaka juu ya shetani. Kama YAHUVEH kweli anataka kuzungumza kupitia mimi tena, atafanya vivyo hivyo. Nakupa mikono yangu YAHUSHUA na akili yangu, masikio yangu ya kiroho na macho yangu ya kiroho.

Tafadhali zungumza nami sasa ili niwape neno la kumpa moyo ndugu yangu mdogo. Katika jina lako YAHUSHUA nauliza na kwa nguvu za RUACH ha KODESH, kupitia damu ya YAHUSHUA ha MASHIACH wa Kalvari. Je, kuna neno ambalo unataka kuzungumza kwa watu wako? Kama ndivyo RUACH ha KODESH paka mafuta mikononi mwangu sasa kama ulivyozungumza kupitia upako huu usio wa kawaida katika jumbe (3) za unabii zilizopewa mbeleni. Kwa kuwa unawajali watu walio katika Mtandao ambao hawana njia nyingine ya kusikia ujumbe wako kwa uwazi ili waelewe na ghasia zisiwakamate katika udhibiti wa shetani. Upako unanijia katika mikono yangu sasa na tena sauti ya YAHUSHUA inazungumza nami. Sifa kwake YAHUSHUA!

******

Waambie mtoto WANGU; waambie siwezi tena kushikilia hasira za Baba YANGU. Nimejaribu. Nimelilia huruma kwa wale wanaochafua yote yaliyo Takatifu kwa makusudi; wale wanaokataa kufahamu kuwepo kwa jambo kama dhambi. Wale walio katika mimbari wanaotoa visingizio kwa ajili ya dhambi, je, hata kisingizio bora kinawezaje kufunika uweusi wa dhambi? Lakini bado Ninapowaomba watubu, wageuke kutoka kwa dhambi, wananikejeli MIMI na kusema YAHUVEH hajali, Anaelewa. Wanaambia Manabii na Mitume WANGU wanyamaze na kuwaacha, wayaweke maneno yao kati ya wao wenyewe. Hawatawaruhusu kuongea katika kanisa, na kuruhusu roho za ibada ya pepo chafu kuingia katika kanisa hadi nabii hayuko salama akiomba. Hizi pepo mbaya hungoja, zikijua manabii waja kutoa onyo ZANGU, na wanazuiwa na ndio, wengine hata huumizwa. Onyo likiwa kuu, upinzani mkuu utatoka kwa adui.

Shetani anajaribu sana kuwanyamazisha Manabii na Mitume WANGU na wale ambao wameambiwa waonye watu. Waonye juu ya MUNGU katika Nahumu 1 inayosema YEYE huongea katika dhoruba na mitetemeko ya ardhi. Waonye kuwa YAHUVEH ni MUNGU aliye na wivu na hataruhusu miungu nyingine mbele YAKE. Waonye, kuwa ghadhabu yake YAHUVEH haifurahishwi virahisi. WAONYE! Bado MIMI YAHUSHUA huwatuma Wajumbe WANGU kuwaonya na kama katika bibilia wanapigwa na wengine hata wanauliwa. Nimezungumza kuhusu wapelelezi wa shetani waliomo katika kanisa: hakuna yeyote anayesikiliza.

Ni wachache sana hata wanaodhubutu kuwafichua. Nimewaonya kuwa shetani yumo katika makanisa na anapigania funzo la uongo, roho za uasi, roho ya kudanganya kanisa kuwa dhambi si dhambi. Lakini MIMI ni MUNGU MTAKATIFU na Ninadai nyote muwe watakatifu kama MIMI Nilivyo MTAKATIFU. Nimeweka Roho YANGU ndani yenu ili mjue lipi ni ukweli na lipi ni uongo. Dhambi ni nyeusi, sio kijivu, Utakatifu ni nyeupe na sio rangi nyingine. Wengine sasa watamruhusu shetani kuyachukua haya na kutengeneza matusi ya kirangi. Acheni jambo hili sasa, mnajua ni nini Ninachomaanisha. Ni nyekundu pekee itakayoosha dhambi hii kutoka kwa akili zenu, na hii ni Damu ya YAHUSHUA ha MASHIACH hapo Kalvari. Ninaonya sasa kuwa linalosababisha kuwepo KWANGU kutohisiwa kama hapo awali ni kwa sababu Ninaomboleza. Ninalia kwa yale ambayo lazima Nifanye hivi karibuni.

Je, walimsikiza huyu Nabii ambaye sasa Ninamtumia wakati Niliwaonya kabla ya wakati kuwa uchina utaonja hasira ZANGU kupitia mitetemeko ya ardhi, mtetemeko mkubwa zaidi bado haujatokea lakini waja. Wamewaua Watoto WANGU wengi sana, na kuwatesa na kuwaweka jela Watoto WANGU, Wajumbe WANGU, kwa haya, serikali italipa vikuu na nchi hii itararuliwa na mitetemeko ya ardhi huku wakijaribu kuwagawanya Watu WANGU na kuwaongoza mbali NAMI kwa hofu ya kuabudu kwa uwazi MUNGU ambaye hapo awali walimtumikia na sasa wanaogopa kumtumikia kwa uwazi. Kama walivyogawanya Watu WANGU ndivyo Nitakavyogawa ardhi yao.

Ninawalinda wale ambao ni WANGU, na Ninajua nani ni WANGU. Hata Nimetingiza milango ya jela kama katika nyakati za kale, ili wafungwa waliohubiri injili, kwa kuwa hili ndilo lililokuwa hatia yao pekee, wakuwe huru. Naja kwa njia kuu na mwaka huu ingawa vituo vya habari vya nyumbani kwenu vinakataa kukubali ule uharibifu na hasira ambayo MIMI Nishaonyesha mwaka huu. Nitaanza kuwaonyesha kwa njia ambazo hawataweza tena kudharau. Wanalaumu mama ardhi. Kuna Muumbaji mmoja tu na MIMI ndiye Baba wa viumbe vyote. MIMI NIKO AMBAYE NIKO. Hakuna mwingine. MIMI sigawi utukufu WANGU na mtu yeyote kama vile mama ardhi. Nimetuma onyo katika vipindi vya televisheni, ndio, mwamba amelia, lakini je wanasikiliza, ni wachache sana, wachache sana. Msifikirie kuwa Ninafurahia kwa haya ambayo lazima Nifanye kwa sababu Sijafurahia, lakini lazima Niyafanye, kwa kuwa watoto wanafikiria sasa wanatawala mzazi.

Volkano kadhaa zitalipuka wakati mmoja, itakuwa moto WANGU nyekundu itakayomwagika na kuonyesha hasira ZANGU. Ni wachache ambao wanajaribu kuwa Watakatifu. Wanadhani kuwa MIMI Nitaafikiana na dhambi zao. Kama tu wangeweza kutubu. Kama tu wangefahamu kuwa MIMI ni MUNGU ambaye habadiliki. Mimi niko sawa jana, leo na milele. Ni lazima nyinyi mbadilike, sio MIMI NIKO AMBAYE NIKO’ MKUU, ‘MIMI NIKO AMBAYE NIKO’ na siombi msamaha kwa lolote Ninalofanya. Simpi majibu yeyote. YAHUVEH mkuu amekasirika na hata Mwana WANGU, yule Niliyewapa kama Mwokozi hawezi kuzuia hasira ZANGU tena. Nipo karibu kuonyesha hasira ZANGU, jihadharini nyote mlionikejeli MIMI na neno la YAHUSHUA na kuwanyamazisha wale walio na upako wa wajumbe WANGU na kuwatusi, kuwatesa na kuwaweka jela katika jela za binadamu. NIMEKASIRIKA! Niliwaonya Sodoma na Gomora na Ninawaonya sasa tena. Dunia hii ni Babeli wa kisasa, dunia hii. MIMI ni Muumbaji anayeamuru Utakatifu; Niliweka ndani ya kila binadamu mahali panapotamani Utakatifu na uhusiano na Muumbaji wao.

Sitatuma tu volkano zitakazolipuka moja baada ya nyingine, lakini Nitatingiza ardhi hii kama mzazi anavyotingiza mtoto mtundu. Sitatingiza tu sehemu moja ya ardhi hii moja kwa moja, lakini sehemu nyingi za ardhi wakati mmoja. Nitatuma miguu YANGU yatakayokanyaga ardhi kwa hasira. Kwa kuwa hasira zangu ni kuu kwa wale waasi walionitingizia ngumi zao usoni MWANGU, na kusema wanakataa kutii kitabu na sheria zilizoandikwa elfu za miaka kale. Kwa wale wanaotumia JINA LANGU kama tusi. Kwa wale wanaokejeli Damu ya MWANANGU iliyomwagwa kwa sababu yao pale kalvari. Nitatuma vimbunga kuonyesha machozi iliyonitoka juu ya watoto WANGU wasiotubu na juu ya wale Niliowaumba waliofaa kuwa Watoto WANGU lakini wakakataa kunikubali MIMI kama Baba.

Wale waliojiingiza katika mambo yasiyo takatifu, na hata hawakujaribu kunifurahisha MIMI au kunisaka MIMI. Mafuriko yatakuja na kufunika sehemu zote za ardhi wakati mmoja. Hii itakuwa ishara ya machozi YANGU, kwa kuwa wengi wamechagua Jehanamu juu ya Mbinguni. Wale waliochagua shetani juu ya YAHUSHUA. Nitazituma tufani na itakuwa ngumi YANGU inayotuma upepo unaopepea. Sitayaonyesha haya katika sehemu moja tu, mkiziona zote zikija pamoja mtajua Ninaongea na Nimekasirika na hasira ZANGU hazifurahishwi virahisi.

Kumekuwa na mitetemeko ya ardhi, mafuriko, tufani, vimbunga hapa na pale duniani lakini mkiziona moja baada ya nyingine zikifuatana kwa mtindo huu, nyingi kwa wakati mmoja basi mtajua huu ndio wakati Niliowaonya juu yake. TUBU SASA, kabla wakati haujaisha. Nimekuwa nikizishikilia hasira ZANGU kwa muda mrefu sasa. Kwa sababu ya MWANANGU na maombi YAKE kwenu nyinyi watu, Nimeshikilia ghadhabu YANGU. Lakini shetani ananikejeli MIMI na kunidharau MIMI kwa sababu Sijawaadhibu. Anatumia viumbe vyangu kunikejeli na kunidharau MIMI. Midomo Nilizoumba. Midomo nilizozipa upako wakati mmoja. Ndio, hata katika kanisa ZANGU Ninakejeliwa huku neno Takatifu linabadilishwa kufuata umbo la mwanadamu. Sio umbo la MUNGU Mtakatifu. Wanafunza kuwa ushoga umetoka KWANGU, SIO DHAMBI, ni kosa la YAHUVEH, ni kasoro ya kuzaliwa.

Roho za kudanganya na kuchanganyisha zinatoka kwa wale walio na umbo la utakatifu, lakini hawana utakatifu ndani yao. Nitapambana MIMI Mwenyewe nao hawa wachungaji waovu kwa njia ambazo zitawaonyesha watu kuwa MIMI sio MUNGU wa kukejeliwa. MIMI sio MUNGU wa kukasirishwa ovyo. Nitapambana vikali na utawaona wakianguka wakifa mimbarini, wale wanaokubali vitu hivi na kutoa mimba. Niliwajua nyote kabla muwe tumboni mwa mama zenu. Niliumba na kuunda na kupanga vile Nilivyotaka maisha yenu yawe. Ilikuwa chaguo lako kuwa vile MIMI nilivyotaka. Usinilaumu MIMI, kwa kuwa Nilikutakia mazuri tu. Hata nyinyi mlioteseka, na kuishi maisha yaliyokaa ni kama hayakuwa yamebarikiwa, Nitawatumia na Nimewatumia kwa Utukufu WANGU, katika mateso yako umenipa MIMI Utukufu wengine wakiona kuwa bado unanisifu MIMI, kunitumikia MIMI na kuniabudu MIMI. Upako WANGU unamwagwa katika maisha yenu, hata kushinda wale wanaoishi maisha yao yaliyo na matatizo machache. Maisha yako hayajapewa baraka za wengine, lakini si kwa sababu Sikupendi kama wengine, ni kwa sababu kama YAHUSHUA alivyowekwa katika ardhi hii kuteseka juu ya wengine, kwa hivyo hata wewe pia, na tuzo zako zitakuwa kuu mbinguni kama utabaki mwaminifu mpaka mwisho.

Watoto WANGU wengine wamejawa nyongo wanavyoona wapagani, wale ambao hawajawahi kupiga goti, au kuomba wakinipa MIMI asante, na Watoto WANGU husema huyu ni MUNGU wa aina gani? Nawaambia, msiwaonee wivu matajiri ambao hawanikubali MIMI, au waovu. Inakaa ni kama wanazo baraka zote maishani kwa kuwa haya ndiyo yote ambayo watawahi kupata, na alafu itakuwa laana ya milele, na jehanamu ya milele na mateso. Walitupilia mbali maisha ya milele Mbinguni kwa miaka michache hapa ardhini ambapo walitenda dhambi za kila aina, sanasana dhambi ya kufikiria kwamba hawahitaji Mwokozi.

Lakini wewe, ukibaki mwaminifu utaona Mbinguni na kwa wakati mfupi kwenye ardhi utaona mateso, chuki na matusi, lakini usijawe na nyongo, usiende mbali NAMI. Ni heri uje KWANGU. Angalia Nilivyo Baba aliye na upendo. Nimewaonya mapema ili wakati vitu hivi vitakavyokuja kwenye ardhi mtakuwa mshaonywa mapema, ili muweze kutubu na kuwaonya wengine kabla hasira ZANGU hazijaonekana. MIMI hutuma Manabii WANGU kuonya kabla Sijatuma uharibifu. Lakini nyinyi mnaonipenda, kunitumikia MIMI kwa uaminifu na kujiosha katika Damu ya YAHUSHUA ha MASHIACH ili mbaki watakatifu mbele YANGU, hamna chochote cha kuogopa katika wakati huu, hamtapatikana kama hamko tayari.

Nitalinda yote ambayo ni YANGU, na Ninajua yapi ni YANGU. Ninajua kila moja ya nyoyo zenu zote, na Ninazo roho zenu mikononi MWANGU kwa kuwa mmenipa MIMI maisha yenu na roho zenu mlipomkubali YAHUSHUA kama Bwana na Mwokozi. Mmeleta miili zenu kama dhabihu hai kwa utukufu WANGU. Sijawakasirikia. Ninawapenda, na Nitawafunika na kuwalinda. Ndio, hata mkiona dunia imetingizwa katika hasira YANGU, Nililie MIMI. Nitakuwa papo hapo kuwakumbatia.

Sababu linalofanya wengi wenu msihisi kuwepo KWANGU sasa, si kwa sababu yenu. Ndio, hata huyu Ninayemtumia kuzungumza maneno haya na hajui ni nini ataandika kutoka neno moja hadi lingine linalofuata, ana tatizo kuhisi kuwepo KWANGU tangu Nilipomtumia kuwaonya watu WANGU mwisho. Nimempa upako huu usio wa kawaida kushika tahadhari ya watu WANGU, ambao hangekuwa na njia nyingine ya kuwaongelesha, kwa kuwa Nimewatawanya kote duniani. Manabii WANGU na Wajumbe watasikia, na wanazo masikio za kiroho na macho na mdomo jasiri kuwaonya watu ambao hawasikii.

Nawaambia tena Manabii na Watoto WANGU, msiwe na shaka na kufikiria Nimewaacha wakati ambapo hamwezi kunihisi MIMI kando yenu. Sijaenda pahali popote, bado Nipo hapa; Nimekimya tu kwa kuwa huu ndio utulivu kabla ya dhoruba. MIMI huwa kimya kabla Niachilie hasira ZANGU kwa kuwa Ninajaribu kushikilia ghadhabu zangu, lakini tangu mafuriko ya Noah imekuwa ikipanda na tena Nina huzuni wakati Ninapoona yote Niliyoyafanya, hata kumpa MWANANGU wa pekee kama Dhabihu. Abrahamu alikuwa na dhabihu nyingine; Niliwapa MWANANGU, kuwa Mwokozi wenu. Ni wachache sana ambao watamkaribisha YEYE. NIMEKASIRIKA! Niliwapa Mwili WAKE ili mponywe. Ni wachache sana ambao wataamini kuwa kuna uponyaji kwa sababu ya vile viboko viliyolazwa kwenye Mwili WAKE. Niliwapa Damu YAKE, ili msamehewe. Ni wachache sana ambao watakubali zawadi hii pale Kalvari. Niliwapa maisha YAKE, ili mwokolewe. O, hii ndiyo sababu inayofanya mhisi upungufu wa kuwepo KWANGU. Hamjawahi kukasirika na watoto wenu hadi mkapoteza hamu ya kuongea, kwa hofu ya hasira zako mwenyewe? Hamjawahi kuhuzunishwa sana hadi mkataka tu kuwa kimya au kukasirika sana hadi mwataka tu kuwa kimya. Ukiogopa kuachilia hasira zako kwa hofu ya mambo ambayo yanaweza kutokea. NIPO HAPO!

Sijawakasirikia wale wanaotamani kuhisi kuwepo KWANGU. Nimewakasirikia wale ambao hawajahisi kuwa Niko kimya, na kuwepo KWANGU hautamanwi. Kwa wale ambao mnahisi kuwepo KWANGU haupo, na mna huzuni kwa sababu ya haya, na mnatubu na kushangaa ni nini kibaya mlichofanya, sasa Ninazungumza kupitia Handmaiden WANGU na kuwaambia nyinyi, mmefanya yote ambayo ni sawa, ndio sababu mnahisi kukimya KWANGU na hamhisi kuwepo KWANGU. Sizungumzi na wale walio katika dhambi na hawajawahi kunijua MIMI au kunitamani MIMI, kutoka mwanzoni. Mnajua ni nani Ninaowazungumzia. Ni Watoto WANGU tu ambao wataelewa. Kwa wale kati yenu, ambao mlikuwa Watoto WANGU lakini mkawa na uvuguvugu, rudini sasa Nawaomba. Nitamani MIMI na kuweni na hamu ya kuisikia sauti YANGU tena. Sijawaacha, ni nyinyi mliotenda haya.

Tubuni kufunza uongo. Tubuni kufunza kuwa, dhambi sio ukosefu wa utakatifu na kuwa hamna kitu kama dhambi, kwa kuwa YAHUVEH anayependa wote atawasamehe kwa kila mtakachofanya. Hakuna haja ya kutubu, au kugeuka kutoka kwa dhambi. Hamwoni kuwa huu ni uongo wa shetani. Shetani husema, “hauhitaji Mwokozi, zawadi YANGU, MWANANGU mpendwa YAHUSHUA.” Hamwoni, Ninalia Ninapofikiria gharama Mpendwa WANGU aliyolipa kwa sababu yenu? Mkisema ya kwamba hamna kitu kama dhambi, na kila kitu kinakubaliwa NAMI kwa kuwa MIMI ni MUNGU ambaye hajali tena ni nani ulalaye naye au nini ulalacho nacho.

Ni damu ya nani asiye na hatia inayomwagwa? Hata wale ambao hawajazaliwa, ‘si dhambi kuwaua kama hauwezi kuwaona’. Hata wakati mnapoweza kuwaona kama wanawaua watoto hawa wasio na hatia ili kuokoa maisha ya wengine, haijalishi, wao ni muhimu kwa kitu fulani. Huu ni uuaji na hii ni dhambi. Wahubiri mtanijibu MIMI nyinyi wenyewe kwa kuwa mmesema, mnanifanyia kazi MIMI, lakini mmekuwa mkifanya kazi dhidi YANGU. Ushoga ni DHAMBI! Kutoa mimba ni DHAMBI! Uuaji ni DHAMBI! Uasi ni DHAMBI! Uchawi ni DHAMBI! Nyote mnajua DHAMBI ni nini! Someni amri 10. Wahubiri, Mitume, Manabii, Walimu, Wainjilisti, rudini kufunza kuwa dhambi ni dhambi. Ni mtenda dhambi aliyetubu tu ndiye atakayesamehewa.

Hamna tena, kila mtu fungeni macho yenu hatutaki kumwaibisha mtu yeyote, ili waweze kuinua mikono yao na kumkubali YAHUSHUA ha MASHIACH kama Mwokozi wao. Je, mnaelewa vipi jambo hili lilivyonikasirisha? Tangu lini ikawaje ni aibu kuja kwake YAHUSHUA kwa kusamehewa kwa dhambi zenu. Hakuwezi kuwa na Wokovu bila kuungama dhambi zako kwa wengine. Kukiri kwa dhambi hubadilika kuwa wokovu. Nawaambia msiponiungama MIMI mbele ya binadamu, YAHUSHUA hatawaungama mbele YANGU, Baba. Watoto WANGU, Wainjilisti WANGU, Manabii, Wachungaji, Walimu na Mitume wamefanya hivi.

O, uchungu huu. Huzuni niliouvumilia juu ya haya. Mnafikiria hawa watu ambao walikuwa na aibu kuu ya kusimama na kuungama kuwa wanahitaji Mwokozi, watabaki waaminifu kwa muda mgani? Papo hapo adui ataiba lile mbegu ndogo lililopandwa. Wale kati yenu, mliofanya haya, TUBUNI! Kataa kufanya haya tena kwa uwazi. Kwa kuwa mtajibu kwa zile roho zilizopotea ambazo zingekuwa zimeokolewa. Wale kati yenu mlionifanya MIMI kukaa kama MUNGU wa mchanganyiko mnaposema wanaweza kuinua mikono yao kisiri na kusema YAHUSHUA njoo moyoni mwangu, bila kuwafunza kwanza lazima walie na kutubu dhambi zao, na kugeuka kutoka kwa dhambi hizo. Kubali kumweka YAHUSHUA kwanza maishani mwao, na kufuata Utakatifu, sio ukosefu wa utakatifu. Mtanijibu MIMI mwenyewe pia, na kwa wale wote waliofikiria, kuwa ukishaokolewa umeokolewa, sasa tunaweza kufanya chochote kile tunachotaka kwa sababu dhambi zetu zote zimefunikwa. Hamkuwafunza, ‘kwa nini mnasema mnanipenda MIMI na hamnitii MIMI?’

Wale kati yenu mliotumia roho za udanganyifu kupata watu kuinua mikono yao kama macho ya kila mtu imefungwa alafu kuwaita waje wasimame mbele ya watu baada ya kuwafanya waamini kuwa wanaweza kufanya haya kisiri. Mmewaonyesha kuwa YAHUVEH ni MUNGU wa mchanganyiko na udanganyifu. MIMI SIO! Kwa haya mtalipa, msipotubu. Ndio, kabla ardhi haijaanza kutingizika, hata sasa Ninatingiza na kuwagawa wasio waaminifu na walio waaminifu katika zile zinazofaa kuwa Kanisa ZANGU, Hekalu ZANGU. Ninazungumzia sehemu za kukusanyika sasa kwa kuwa Kanisa na Hekalu za Kweli ni watu WANGU.

Lakini katika mijengo ya kanisa mtaona ni nini kinachofanyika kwa wale wanaowachanganya Kondoo WANGU. Au wale waliotaka kuwa kondoo lakini wakabadilishwa kuwa mbuzi, kwa kuwa mchungaji mwovu ni mbwa mwitu aliyetumwa kati ya Kondoo WANGU kuwaangamiza kwa ukosefu wa maarifa na utambuzi. NIMEKASIRIKA! Katika mijengo ya kanisa mshaona mgawanyo ukianza. Ninafichua adui kati ya kambi zenu. Tahadhari, simama, angalia, na sikiza sauti ya RUACH ha KODESH. Tena endeleeni kuniita MIMI na kusema ninatamani kuwepo KWAKO kwa kuwa hawa ndio wale waliozoea kuhisi kuwepo KWANGU na waliozoea kusikia sauti YANGU kila siku na sasa wanahisi kunyamaza KWANGU.

Lakini Sitabaki kimya wakati wote Wapendwa WANGU, ni kwa muda mfupi tu ambapo mtahisi huzuni WANGU, na lazima msifuate hisia zenu kwa kuwa hayo ni ya mwili. Lazima mfuate imani yenu kwa kuwa hii ni ya Roho. Siku hii Nimechagua kuzungumza kupitia huyu Handmaiden, msigombane kati yenu na kusema, “Kwa nini YAHUVEH alizungumza kupitia mwanamke au kuweka upako mikononi mwake.” Nawaacha na haya, Nachagua kumtumia yeyote Ninayechagua kumtumia, na sijibu binadamu yeyote na kama Ningeweka upako mdomoni mwake pekee kama alivyozoea, na singeweka upako mikononi mwake kwenye kibodi, je, mngekuwa mmenisikia MIMI Nikizungumza ujumbe huu kupitia kwake siku hii? Mmejijibu maswali yenu.

Sasa tafadhali onya watu, ingawa katika nyakati za Noah wengi hawakusikiza. Bado, msiwe na damu mikononi mwenu kama Ezk 3:17-21 husema, “Msiwache damu ipatikane mikononi mwenu.” ONYA WATU! Bado kuna muda mfupi uliobaki, kwa ajili ya MWANANGU Nimekuwa na huruma kwa watu, lakini wakati wa kulipiza kisasi na wa hukumu unakaribia haraka. Waonye, na mnitafute MIMI kama bado Ninaweza kupatikana. Tia maanani tarehe hii na mwangalie matukio katika dunia, 2/25/1997. Nimemkataza Handmaiden WANGU, Sherrie Elijah, kubadilisha hata neno moja Nililolizungumza. Ingawa anajua si wote watakaokubali yote Niliyoyazungumza.

Tena, Ninawaonya wale walio maadui WANGU lakini hujifanya kuwa hao ni rafiki ZANGU, akina Yuda jihadharini, kwa kuwa mnapotafuta kumwumiza huyu mjumbe mnamwumiza yule aliyemwumba na kumpa upako. Mtakuwa wa kwanza watakaohisi ghadhabu YANGU na mtajua kuwepo KWANGU kwa njia ambazo hamngependa kujua. NIMEKASIRIKA, na nyinyi mlioniomba MIMI kuzungumza mmesikia sauti ya upendo, uhakika, huzuni, na hasira kuu. Mmesikia sauti ya YAHUVEH Mkuu, ‘MIMI NIKO’ akizungumza kupitia chombo kilichopasuka cha udongo siku hii. Ombea wale wote ambao umejaribu kuzifikia nyoyo zao, na bado hunisukuma MIMI mbali. Omba watubu leo kwa kuwa kesho wakati unaweza kuwa umepita.

Alipewa Rev. Sherrie Elijah katika siku ya 2/5/1997

*******

Ndugu Noel, nimemsomea mwanangu mwasi haya, na nikasema kutakuwa na watu kote duniani watakaokuwa wakiomba na kumtafuta YAHUVEH kuona kama nilichoandika ni ya YAHUVEH. Je, kweli ilikuwa YAHUVEH Baba aliyezungumza kupitia kwangu katika upako wa RUACH ha KODESH? Haya yatajaribiwa na kuthibitishwa na manabii, wachungaji, mitume, walimu, wainjilisti. Kabla wathibitishe jumbe zile zingine za kiunabii za mwaka huu alizonipa YAHUVEH, sasa nakuuliza mwanangu, hii ilikuwa sauti ya YAHUVEH iliyozungumza kupitia kwangu? Na thibitisho bora kwangu mimi ilikuwa wakati ambapo mwanangu alisema, “Ndio.”

Sifa kwake YAHUSHUA! Nilimwambia kuwa bado kuna matumaini. Kwa kuwa hata kijana mwenye uasi anaweza kusikia sauti ya YAHUVEH. Hii ilikuwa jaribio kuu na sina shaka kuwa YAHUVEH mwenyewe alizungumza maneno haya ili niyaandike siku hii. Tafadhali nakili haya na itume kwa kila mtu RUACH ha KODESH atakuambia umtumie. Ipeleke katika kanisa yako, hata kama hawatasikiza.

www.allmightywind.com

www.almightywind.com

Contact AmightyWind



CLICK HERE or the image below to go directly to her youtube channel
YAHSladyinred