Unabii 63

O Israeli, Dhabihu Yenu Ya Damu Iko Wapi?

Niliamka na maneno haya Tarehe Septemba 16, 2002 na Bwana Aliniambia Niyaandike.

Ilipewa kwake Mtume Elisabeth Elijah (Elisheva Eliyahu) siku ya Yom Kippur

* * * * * * *

Haya maneno yanatoka kwenye Unabii wa 105, YAHUVEH Alisema yaongezwe kwenye Unabii zote kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote lililofanyika kwa mikono yako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASHIACH wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)

Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH pia Alisema kuongezwe yafuatayo mbele ya Unabii zote kutoka Kitabu cha pili cha Mambo ya Nyakati:

2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

* * * * * * *

O Israeli, O Ninavyowalilia. Ndio, MIMI, YAHUVEH, Muumba wa yote, Muumba wa hata wakati. Ninalia kwa kuwa Nimemwaga upendo WANGU, Nimemwaga huruma YANGU, Nimewapa mazuri YANGU yote, Mwana WANGU Mpendwa YAHUSHUA. MIMI, YAHUVEH, Niliwapa YAHUSHUA Aliyemwaga Damu YAKE kukomboa dhambi za Adamu na Hawa. O Israeli, Damu ya YAHUSHUA bado imelowa kwenye mchanga. Je, mnafikiria ni kwa nini shetani anawachukia kushinda watu wengine au taifa lingine? Kwa sababu MIMI, YAHUVEH, Nilikuja katika mwili kupitia Mwana WANGU YAHUSHUA, Mwana WANGU Mpendwa.

Abrahamu alifikiria tu kuwa alikuwa amtoe Isaka kama dhabihu. Abrahamu alihisi tu hisia za huzuni kuu alipoishika ile kisu juu ya mwanawe mpendwa akifikiria kuwa hakutakuwa na kondoo wa kumtoa kama dhabihu, kama dhabihu ya damu. Lakini kwa imani Abrahamu akiwa tayari kumtoa mwanawe Isaka uhai aliamini kuwa MIMI, YAHUVEH, Nitamfufua Isaka kutoka kwa wafu kama yahitajika, kama Nilivyomfanyia Mwana WANGU YAHUSHUA. Ni kwa sababu ya MIMI, YAHUVEH, ni nani. Kwa sababu ya MIMI ni nani, kwa sababu ya upendo WANGU usio na mwanzo wala mwisho kwa wale walioitwa Watoto WANGU na wale pekee wanaoitwa Watoto WANGU ni wale wanaonililia MIMI katika Jina la Mwana WANGU YAHUSHUA. Ni MIMI pekee Niliyemzuia Abrahamu kumtoa uhai mwanawe Isaka. Nilitoa kondoo aliyekuwa amejificha kutoka kwa mtazamo wa Abrahamu mpaka wakati uliostahili.

Abrahamu hakuwa kamili. Isaka pia. Israeli sasa inalipa gharama ya dhambi ya Abrahamu aliyoileta kupitia Ishmaeli na mbegu ya Ishmaeli. Abrahamu pia alihitaji dhabihu ya damu. Ni yule kondoo aliyekuwa mfano aliyekamatwa pale kichakani. Ilikuwa mfano wa Mwana WANGU YAHUSHUA, Mwanakondoo wa pekee wa YAHUVEH, Mwanakondoo kamili bila dhambi au doa au waa. Kondoo yule alikamatwa kichakani. Mwana WANGU YAHUSHUA Alinililia MIMI. YEYE alikuwa Amekamatwa katika kichaka cha mapenzi YANGU. “Baba, kama inawezekana, chukua kikombe hiki kutoka KWANGU, lakini sivyo Nitakavyo, lakini mapenzi YAKO yatimizwe.” YAHUSHUA Alifananishwa na kondoo yule, kama ile dhabihu ya damu ambayo Abrahamu alitoa siku hiyo iliyochukua nafasi ya Isaka.

Dhabihu ya Damu ya YAHUSHUA ni dhabihu ya binadamu ya pekee iliyo Takatifu ya kutosha kuosha dhambi za wanadamu wote. Kama tu wanadamu watakubali na kutii Agano jipya la Damu Niliyowapa pale Kalvari kupitia Mwana WANGU YAHUSHUA, hii ndiyo ahadi YANGU kwa watoto WANGU waaminifu wanaompenda YAHUSHUA na kukubali hili Agano jipya la Damu. Kama vile sikumwacha Mwana WANGU Mpendwa katika lile kaburi, Nilimfufua YEYE kutoka kwa wafu na Akapanda Mbinguni, basi Nitawafanyia yaya haya pia. Wanachotakikana kufanya Watoto WANGU wote ni kupokea, kuamini, kupenda na kujaribu iwezekanavyo kutii amri ZANGU. Je, haya ni magumu sana?

Ninazungumza kwa wale wanaokataa Mwana WANGU YAHUSHUA kama MASIHI. Je, dhabihu yenu ya damu iko wapi? Wote wanajua kuwa lazima kuwe na dhabihu ya damu kwa msamaha wa dhambi. Je, ni mnyama yupi aliye kamili? Binadamu yupi? Hakuna, bali tu ya Mwana WANGU Mpendwa YAHUSHUA. MIMI, YAHUVEH, Niliiondoa agano la damu la kale kuwapa binadamu agano la damu bora zaidi. Hii ndiyo njia ya pekee Ninavyoweza kusamehe dhambi zenu. Hamna njia nyingine kwa kiti CHANGU cha enzi, kwa MIMI kuyajibu maombi yenu, ila tu kupitia Damu YAKE iliyomwagwa pale Kalvari kwa msamaha wa dhambi. Hakuna mwombezi mwingine mbele YANGU ila tu Mwana WANGU YAHUSHUA. Mohammed hawezi kukuokoa. Kumlilia Abrahamu haitakuokoa. Allah hawezi kukuokoa. Someni Torah kama Nilivyozungumza kupitia huyu Binti. Wale wanaofikiria kuwa kufuata Torah pekee itawaokoa lazima watambue kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na Utukufu WANGU [Warumi 3:23]. Kuvunja amri moja ni sawa na kuvunja amri zote. Mnahitaji Mwokozi. YAHUSHUA Ndiye Masihi huyo. Wale wanaokataa kumkubali YAHUSHUA kama Bwana na Mwokozi, MASIHI wa wanadamu wote, watahukumiwa na YAHUSHUA, lakini watasimama mbele ya Musa atakayefungua Kitabu cha Hukumu bila huruma. Kwa kuwa alionya Israeli kuwa kutakuwa na agano jipya lijalo, Agano jipya la Damu. Alijua ya kwamba haikuweza kufurahisha ghadhabu ZANGU. Haya yalikuwa ya muda mfupi tu kwa dhabihu za wanyama.

O Israeli, Niliituma Agano jipya la Damu kuzaliwa katika nchi yenu. Nilifanya miujiza kupitia Jina la YAHUSHUA. Nilimtumia Yeye kuwa dhabihu ya binadamu, dhabihu ya damu ya binadamu, dhabihu kamili ya pekee ya damu kwa msamaha wa dhambi. Na Nilimfufua YEYE kutoka kwa wafu katika nchi ya Israeli.

Katika siku hii ya Yom Kippur, 2002, Ninazungumza kwake Israeli na Ninawaambia kuwa Ninasikia maombi yao ya toba, wakiuliza msamaha WANGU. Ninaona kufunga kwenu. Ninahisi hofu yenu mnapotambua dhambi zenu ni uvundo kwenye pua LANGU. O Israeli, mnajua kuwa “MIMI NIKO” Adonai na Nitawahukumu kwa tamaa za miili yenu. O Israeli, mnajua ya kwamba hakuna dhabihu ya damu. Mna hamu ya kujenga hekalu hiyo iliyo na kuta ili mweze kutoa dhabihu za wanyama kwa msamaha wa dhambi, mahali kuhani mkuu wenu atalia kwa huruma kwa sauti ya juu. Na bado, mmekataa kupokea zawadi Niliyowapa, hekalu bila kuta iliyojawa na RUACH ha KODESH, iliyojawa na upendo WANGU na hukumu YANGU. Hekalu isiyotengenezwa na mikono ya binadamu, kamili, takatifu, hekalu bila dhambi. Jina Lake ni YAHUSHUA. Jina LANGU [YAH] lipo katika Jina LAKE. Nguvu zipo katika Jina LAKE Takatifu, nguvu zipo katika Majina YETU Matakatifu.

YAHUSHUA Ndiye Hekalu lile. YAHUSHUA Ndiye Dhabihu ya Damu Nitakayokubali. YAHUSHUA Alikuja Israeli kama mtoto. YAHUSHUA Alikuwa Dhabihu yenu ya Damu. YAHUSHUA Ndiye Dhabihu pekee Takatifu ya Damu. O Israeli, Nisikizeni MIMI, Damu ya YAHUSHUA ilimwagwa pale kwenye mchanga wa Israeli na bado ikajaza kona zote za dunia. O Israeli, Nisikizeni MIMI, kwa sababu mnakataa Agano hili lipya la Damu, Niliwapa pia mataifa, Nikawapandikiza kwenye shina, Nikiwangoja mtubu na kumkubali YAHUSHUA kama MASIHI. Je, itachukua nini, o Israeli? Nina mabaki wachache sana pale Israeli. Ninavyozungumza maneno haya kupitia huyu binti, kutakuwa na wanafunzi wapya watakaojitokeza na kupeleka neno hili hadi Israeli. Kwa kuwa Ninawaambia sasa, mna ushahidi unaomwagika kutoka kwa ukuta wa kilio ambapo mfano wa Maji YANGU ya Uzima yanamwagika.

Je, haya Maji ya Uzima yanatoka wapi? MIMI, YAHUVEH, Ninawapa zawadi hii tena, kama RUACH ha KODESH Alivyoachiliwa kupitia YAHUSHUA pale Israeli. Sasa inamwagika kupitia ukuta huo ambapo Israeli hupiga goti, kulia, kupiga mayowe na kuomba. Kubali YAHUSHUA kama MASIHI wenu. Ukuta huo wa hekalu unavimba na kuharibika mbele ya macho yenu. Je, hamwoni o Israeli kuwa agano la kale limepita. Sitaki dhabihu za wanyama.

Ni Damu ya Mwana WANGU Mpendwa YAHUSHUA pekee Aliyekuja kutoka kwa kabila la Yuda inayoweza kuwa Agano la Damu la Israeli na damu ya msamaha wa dhambi kwa dunia mzima. Kuna tu dhambi moja ambayo haiwezi kusamehewa, kumkataa YAHUSHUA na maisha na Damu YEYE Alitoa pale Kalvari. Jihadharini, kumkejeli na kukataa RUACH ha KODESH ni kukufuru. Hakuna msamaha wa dhambi hii.

Kubalini maisha ya YAHUSHUA na Damu na [jueni] kupitia Jina LAKE ndiyo msamaha wa dhambi. Niliwapa zawadi hii pale Kalvari; Niliwapa dunia hii zawadi hii. Na Israeli, katika siku hii Takatifu, MIMI, YAHUVEH, Nazungumza kupitia Binti huyu Myahudi. O Israeli, nyinyi mliowapiga mawe, kuwaumiza, kuwauwa mitume na manabii, nyinyi mliowauwa Watoto WANGU Niliowatuma kuwahubiria. O Israeli, hata damu ya waliouwawa imelowa kwenye mchanga. Ni MIMI pekee Israeli Ninajua, ni kiasi gani cha damu yenu itakayomwagwa kabla ya kumkubali Masihi Anayeweza kuwaokoa. YAHUSHUA bado Anawalilia kama Alivyofanya kwenye bustani ya Gethsemane.

Macho ya dunia ipo kwenu, o Israeli. Macho YANGU daima hayawaachi. Nguvu ya kuokoa ipo katika Jina mnalokataa, lile jiwe kuu la pembeni hekaluni mnalolikataa. Lakini lazima mkubali YAHUSHUA kama MASIHI. Ni kupitia Jina la YAHUSHUA, Neno na Damu. YAHUSHUA Ataokoa Israeli. O Israeli, YAHUSHUA Alifunga kwa sababu yenu kwa siku na usiku arobaini. Je, mnafikiria kuwa kufunga siku moja tu yatosha kufunika dhambi zenu? Watoto WANGU waliomkubali YAHUSHUA kama Elohim na Masihi hufurahia kuwa dhambi zao zimelipwa zote pale Kalvari.

MIMI, YAHUVEH, Ninawangoja Israeli. O Israeli, nyinyi mnaofuata na kukumbuka Karamu za Kiyahudi na siku takatifu, je, hamwoni kuwa YAHUSHUA yupo katika zote? O Israeli, rudini KWANGU kwa Utakatifu. Acheni dhambi zenu katika toba ya kweli katika Jina la Mwana WANGU YAHUSHUA. O Israeli, Ninalia kwa uchungu wenu. Lakini kumbukeni, kama Nilivyo Mtakatifu, pia nyinyi lazima mjitenge na kuwa Watakatifu.

Je, mnataka kuhukumiwa na amri Nilizompa Musa, na pia Musa kuwahukumu bila huruma. Sasa mnavyomkataa mwombezi wa pekee, Mwanakondoo Kamili wa pekee wa YAHUVEH, YAHUSHUA Atasema kwa wale wanaotegemea agano la damu la kale kuwaokoa. Wale wanaotegemea agano hili la damu, jihadharini! YEYE Atasema, “Mlichagua kuhukumiwa na agano la damu la kale, mtahukumiwa na Musa.” Na kwa sababu hakuna yeyote aliye kamili, ole kwa wale watakaohukumiwa na Musa. Hakuna yeyote atakayeepuka. Jehanamu na Ziwa la Moto litakuwa nyumbani kwao milele. Kila mtu anajitayarishia mahali pake atakapokaa milele.

Hakuna yeyote aliyehakikishiwa sekunde nyingine ya kuishi. Wote walio katika huruma YANGU MIMI, YAHUVEH, leo ndiyo siku yenu ya wokovu. Kesho mnaweza kuchelewa.

* * * * * * *

Imezungumzwa, imeandikwa, siku ya Yom Kippur, Septemba 16, 2002. Imepewa kwa mtumishi huyu, Mtume Elisabeth Elijah (Elisheva Eliyahu)

* * * * * * *

Mathayo 10:18-42

18Nanyi mtaburutwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili Yangu, ili kuwa ushuhuda kwao na mbele ya watu Mataifa. 19Lakini watakapowapeleka humo, msisumbuke kufikirifikiri mtakalosema, kwa maana mtapewa la kusema wakati huo. 20Kwa sababu si ninyi mtakaokuwa mkinena, bali ni Roho wa Baba yenu atakayekuwa akinena kupitia kwenu. 21“Ndugu atamsaliti ndugu yake ili auawe na baba atamsaliti mtoto wake, watoto wataasi dhidi ya wazazi wao na kuwafanya wauawe. 22Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya Jina langu. Lakini yeye atakayevumilia hadi mwisho ataokoka. 23Wakiwatesa katika mji mmoja, kimbilieni mji mwingine. Amin, amin nawaambia, hamtamaliza miji yote ya Israeli kabla Mwana wa Adamu hajaja. 24“Mwanafunzi hawezi kumzidi mwalimu wake wala mtumishi hamzidi bwana wake. 25Yatosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake na mtumishi kuwa kama bwana wake. Ikiwa mkuu wa nyumba ameitwa Beelzebuli, je, si zaidi sana wale wa nyumbani mwake mwenyewe! 26“Kwa hiyo msiwaogope hao, kwa maana hakuna kilichofichika ambacho hakitafunuliwa, wala hakuna siri ambayo haitajulikana. 27Ninalowaambia gizani, ninyi lisemeni mchana peupe na lile mnalosikia likinong'onwa, masikioni mwenu, lihubirini kwenye paa la nyumba. 28Msiwaogope wale wauao mwili lakini hawawezi kuua roho afadhali mwogopeni yeye awezaye kuiangamiza roho na mwili katika jehanamu. 29Je, shomoro wawili hawauzwi kwa senti mbili tu? Lakini hakuna hata mmoja wao atakayeanguka pasipo Baba yenu kujua. 30Hata nywele za vichwa vyenu zote zimehesabiwa. 31Hivyo msiogope, kwa maana ninyi ni wa thamani kubwa zaidi kuliko shomoro wengi. 32“Kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, mimi nami nitamkiri yeye mbele za Baba yangu aliye mbinguni. 33Lakini ye yote atakayenikana mimi mbele ya watu, mimi nami nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.’’ 34“Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali upanga. 35Kwa maana nimekuja kumfitini mtu na babaye, binti na mamaye, mkwe na mama mkwe wake. 36Nao adui za mtu watakuwa ni wale watu wa nyumbani kwake. 37‘‘Yeyote ampendaye baba yake au mama yake kuliko anavyonipenda mimi, hastahili kuwa wangu. Yeyote ampendaye mwanawe au binti yake kuliko anavyonipenda Mimi, hastahili kuwa wangu. 38Tena yeyote asiyeuchukua msalaba wake na kunifuata, hastahili kuwa Wangu. 39Ayang’ang’aniaye maisha yake atayapoteza, lakini yeye atakayeyatoa maisha yake kwa ajili yangu atayaona.” 40“Mtu yeyote atakayewapokea ninyi atakuwa amenipokea mimi na yeyote atakayenipokea mimi atakuwa amempokea Yeye aliyenituma. 41Mtu yeyote anayempokea nabii kwa kuwa ni nabii, atapokea thawabu ya nabii na mtu anayempokea mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapokea thawabu ya mwenye haki. 42Kama yeyote akimpa hata kikombe cha maji mmoja wa hawa wadogo kwa kuwa ni mwanafunzi wangu, amin, ninawaambia, hataikosa thawabu yake.’’

Mathayo 12:50

Kwa maana yeyote afanyaye mapenzi ya Baba Yangu wa mbinguni, ndiye ndugu Yangu, dada Yangu na mama Yangu.’’

Mathayo 21:42-46

42YAHUSHUA akawaambia, “Je, hamjasoma katika maandiko kwamba: “Lile jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni, Bwana ndiye aliyefanya jambo hili, nalo ni la ajabu machoni petu?’ 43‘‘Kwa hiyo ninawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu na watapewa watu wengine wawezao kuzaa matunda yake.’’ 44“Yeye aangukaye kwenye jiwe hili atavunjika vipande vipande, lakini yule litakayemwangukia atasagikasagika kabisa. 45Viongozi wa Makuhani na Mafarisayo waliposikia mifano Yake, walitambua kuwa alikuwa akiwasema wao. 46Wakatafuta njia ya kumkamata lakini wakaogopa ule umati wa watu kwa kuwa wao walimwona kuwa ni nabii.

Mathayo 23:29-39

29“Ole wenu, walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Mnajenga makaburi ya manabii na kuyapamba makaburi ya wenye haki. 30Nanyi mwasema, ‘Kama tungaliishi wakati wa baba zetu, tusingalikuwa tumeshiriki katika kumwaga damu ya manabii!” 31Hivyo mnajishuhudia wenyewe kwamba ninyi ni wana wa wale waliowaua manabii. 32Haya basi, kijazeni kipimo cha dhambi ya baba zenu! 33“Ninyi nyoka, ninyi uzao wa nyoka wenye sumu! Mtaiepukaje hukumu ya jehanamu? 34Kwa sababu hii tazama nawapelekea manabii na wenye hekima na walimu. Baadhi yao mtawaua na kuwasulibisha, wengine mtawapiga mijeledi katika masinagogi yenu na wengine mtawafuatia kutoka mji mmoja hadi mji mwingine. 35Hivyo ile damu ya wenye haki wote iliyomwagwa hapa duniani, tangu damu ya Abeli, ambaye alikuwa hana hatia, hadi damu ya Zekaria mwana wa Barakia, mliyemwua kati ya Patakatifu na madhabahu, itawajia juu yenu. 36Amin, nawaambieni, haya yote yatakuja juu ya kizazi hiki.’’ 37“Ee Yerusalemu, mnaowaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwenu! Mara ngapi nimetamani kuwakusanya watoto wako, kama vile kuku akusanyavyo vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka! 38Tazama nyumba yako imeachwa tupu na ukiwa. 39Kwa maana nawaambia, hamtaniona tena mpaka siku ile mtakaposema, ‘Amebarikiwa Yeye ajaye kwa Jina la YAHUVEH.”

Mwislamu Aokoka Baada Ya Kuona Mikono ya YAHUSHUA Yenye Damu Katika Mpira wa Moto!!!

* * * * * * *



CLICK HERE or the image below to go directly to her youtube channel
YAHSladyinred