UNABII 72
SAYARI X
Umepewa Mtume Elisheva Eliyahu Julai 12, 2003
Onyo la YAHUVEH la kuongezwa kabla ya Unabii:
Nilikuonya kitambo Elisheva,
kutoita Huduma baada ya jina la mwanaume au mwanamke.
Hata kabla kuwepo na huduma, Niliweka ndani ya roho yako.
Kwa kuwa hakuna lolote kwa haya ambalo limefanyika kwa mikono yako.
Hakuna lolote kwa haya ambalo limetoka kwenye kinywa chako.
Limetoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH ambaYE amezaa.
Limetoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA,
MASHIACH wako ambaYE amezaa.
Limetoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH,
IMMAYAH wako ambaYE amezaa.
Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo.
Ni kwa UPEPO wa SHKHINYAH GLORY
unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO.
Sio kwa pumzi yako au ingekuwa imefeli.
“MIMI NDIMI BWANA YAHUVEH: hilo ndilo JINA LANGU:
Sitampa mwingine UTUKUFU WANGU,
Wala sanamu SIFA ZANGU.” Isaya 42:8
(Unabii 105)
Julai 2010 MUNGU YAHUVEH pia Alisema yaongezwe haya ili kuonya wale wanaodhihaki:
Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, wakayadharau Maneno YAKE,
na kuwacheka Manabii WAKE, mpaka Ghadhabu ya BWANA
ikawa kubwa dhidi ya Watu WAKE, na hakukuwa na namna ya kuituliza.
—2 Nyakati 36:16
*******
[Sayari itafanya Uharibifu Mkubwa Onyo la Kinabii. Je, hii ni ile Sayari X [eks] ambayo wengi sana wanaonya kuhusu? Sijui kama ndiyo au sio wala sijui data hiyo ya kisayansi, lakini najua kile YAHUVEH Aliniambia na upako ulinigonga wakati nilikuwa nikiandika yaliyo hapa chini.]
UNABII 72
Mtu mjinga kufikiria unaweza tumia hisabati kuhesabu tarehe ambayo MIMI, YAHUVEH NItatumia sayari katika ghadhabu YANGU kufanyia uharibifu mkubwa maadui WANGU. Neno la onyo la kinabii kwa matajiri na wenye nguvu ambao wanafikiria watakuwa salama katika miji ya chini ya ardhi iliyojawa na hazina zenu zilizohifadhiwa, mapochopocho ya vyakula, n.k. Hiyo miji ya chini ya ardhi mliyojenga na bado mnajenga itakuwa makaburi yenu ya maji na mtakufa na hazina zenu za dunia na MIMI, YAHUVEH, NImechelewesha hukumu hiyo kwa ajili ya maombi ya waumini wa kweli katika Jina la YAHUSHUA, wale watiifu, wanatembea Takatifu mbele ZANGU wataepushwa na NImekuwa na huruma umbali huu kwa ajili ya Watoto WANGU ambao wanalilia muda zaidi kufikia Ufalme wa Mbinguni nafsi zaidi.
Hukumu imecheleweshwa lakini haijasimamishwa na ni MIMI, YAHUVEH, pekee ambaye NItakokotoa tarehe ya wakati ghadhabu YANGU itapiga dunia. MIMI, YAHUVEH, NImechelewesha hukumu ili kufadhaisha na kuaibisha wale ambao wamejenga miji ya chini ya ardhi wakijifikiria wenyewe tu, NIkithibitisha kuwa MIMI, YAHUVEH, pekee ni Hakimu juu ya nani ataishi na nani atakufa na nani ataingia Mbinguni na nani ataenda jahannamu.
Kumbukeni MIMI, YAHUVEH, Natuma Mitume na Manabii WANGU kuonya kabla NItume ghadhabu YANGU. Ni chaguo lenu kama mtasikiza na kutii lakini jueni hili, wote watavuna kile walipanda mbegu nzuri na mbegu mbaya sawasawa.”
MWISHO WA ONYO LA KINABII
Limepewa Elisheva Eliyahu, Julai 12, 2003