UNABII 73

“HUKUMU! HUKUMU! HUKUMU!”

Imepewa kwake Mtume Elisabeth Elijah (Elisheva Eliyahu) Juni 2, 2004

Haya maneno yanatoka kwenye Unabii wa 105, YAHUVEH Alisema yaongezwe kwenye Unabii zote kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote lililofanyika kwa mikono yako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASHIACH wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)

Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH pia Alisema kuongezwe yafuatayo mbele ya Unabii zote kutoka Kitabu cha pili cha Mambo ya Nyakati:

2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

* * * * * * *

Familia wapendwa katika YAHUSHUA,

Onyo hii ya kinabii ilikuja nikiwa naomba baada ya kutazama habari za Bill O’Reilly. Hata yeye anamwogopa Mungu kwa yale yanayojiri na alama za Wakristo zikitolewa kwenye Mhuri wa Kaunti ya Los Angeles. Unabii huu mpya utatumwa kwake na tunauliza wengine kumtumia pia mara moja barua pepe tutakapouweka kwenye mtandao. Labda atamkubali YAHUSHUA na ulinzi WAKE anapoisoma. Tafadhali ombeni afanye vivyo hivyo. Kama jina lake limeandikwa kwenye Kitabu cha Uzima cha Mwanakondoo kabla ya kuumbwa kwa dunia hii, basi atafanya vivyo hivyo. Labda hata atasoma onyo hii ya kinabii hewani.

Watu wanaweza kunikejeli wanavyotaka lakini mimi ninajua ya kwamba nimewaonya watu. Kama Ezekieli 3:17-21 inavyosema, damu yao haitakuwa mikononi mwangu. Baba YAHUVEH Amekasirika ujumbe huu ulipotolewa kuwa kunafaa kuwe na maelezo katika kila sentensi. Mpaka mtakapoisikia video hakuna vile ninavyoweza kuelezea sauti ya Baba YAHUVEH Alivyozungumza nayo, sauti ya hasira kwa maadui WAKE na upendo kwa Watoto WAKE wapendwa. Lazima niongeze, nilikuwa ninaona maono ya mdomo unaolazimishwa kufunguka wazi alafu bomba kubwa imewekwa ndani alafu mkono mkubwa ulikuwa unamwaga damu ndani ya koo. Mimi ni mjumbe tu. Tafadhali msimgonge mawe mjumbe.

* * * * * * *

HUKUMU! HUKUMU! HUKUMU!

HUKUMU, HUKUMU, HUKUMU! Nyinyi ambao hamtapokea Damu ya YAHUSHUA MASIHI iliyomwagwa. Ninazungumza kwa wote wanaonikejeli MIMI. Ninazungumza kwa wote wanaonikufuru MIMI. Ninazungumza kwa wote wanaomkataa Mwana WANGU YAHUSHUA, nyinyi ambao hamtapokea Damu iliyomwagwa kwa sababu yako, basi Nitamwaga damu ndani ya koo zenu. Nitawaangamiza kwa damu yenu wenyewe. Nitawaangamiza nyote kwa dhambi mlizofanya hapa Marekani pekee yake.

Msifikiri kuwa mataifa mengine ya dunia hii hayajanichukiza MIMI. Kwa sababu nabii huyu ametoka Marekani, kwa hivyo Nasema, Ninazungumza hukumu zijazo hapa Marekani. Kama angekuwa ametoka Ujerumani, Ningezungumza Hukumu kwa Ujerumani. Kama angekuwa ametoka Australia, Ningezungumza Hukumu iliyowekwa kwake Australia. Kama angekuwa ametoka Canada, Ningezungumza Hukumu iliyowekwa kwake Canada, kwa kuwa hakuna taifa hata moja duniani humu ambalo sijalipangia hukumu.

Damu itatiririka kwenye mitaa yenu. Damu yaja kwenye pwani zenu. Maradhi ambayo hamjawahi kuyasikia, yaja juu ya maadui ZANGU, wale waliokadiri kuwa wao ni maadui ZANGU. Kwa hivyo mnataka kutoa alama ZANGU za chochote Takatifu msizione, mzitoe kwenye mhuri, kutoka kwa ahadi, kutoka kwa bendera zenu. Mnataka kunifukuza MIMI kutoka kwa mataifa yenu, Nitawaonyesha, Nitawaangamiza kwa damu yenu wenyewe.

Kwa sababu mnafikiria kuwa hakuna chochote kibaya na kumwua mtoto kama angali ndani ya tumbo la mamake, watoto wenu Nitawaua, Nitawachinja mbele yenu. Kwa mkono wa YAHUVEH Mwenyezi Anayeishi, Nitawaonyesha kuwa MIMI si Mungu wa kukejeliwa. Kwa sababu mmenikejeli MIMI kwa huruma ZANGU, hivi karibuni mtaona kuwa hakuna huruma tena. Sitawaambia pole Sodoma na Gomora na miji mingine kando yake. Sitawaambia pole Ninawi, kwa kuwa dhambi zenu ni kuu zaidi kuliko miji hiyo yote pamoja! Uvundo wa dhambi zenu hufika puani MWANGU. Ni wachache sana wanaonyenyekea na kuanguka kwenye nyuso zao. O, isingekuwa Damu ya YAHUSHUA MASIHI, Ningewamaliza nyote wanadamu.

Lakini Ninao wachache, o wachache sana, Ninaowaita Watoto WANGU na hazina YANGU, wanaolia na wanaoomboleza mbele YANGU, wanaosema, “Dhambi hii isihesabiwe kwetu.” Na kama vile Nilivyomkinga Nuhu na familia yake, vile Nilivyomkinga Lutu na familia yake isipokuwa mmoja tu, kama vile Nilivyotoa njia ya kuepuka, njia ya kubariki, njia ya kuwaficha wapendwa WANGU. Nendeni mkajifiche, Watoto WANGU. Njooni chini ya funiko la Mabawa YANGU; mhakikisheni kuwa Damu ya YAHUSHUA imefunika kila dhambi. Kwa kuwa ghadhabu ZANGU ni kuu, kuu kama Jina LANGU na Dhiki Kuu ijayo haipo mbali sana.

Mnataka kuanza vita kwa wale ambao hawajachochea vita. Mnataka kuwakanyagia chini kwa sababu mnaweza. Nimeziona silaha za mwanadamu lakini haziwezi kulingana na silaha za Mbinguni. Mnakejeli filamu iitwayo ‘The Passion of Christ,’ sasa mnakejeli filamu nyingine (The Day After Tomorrow) inayowaambia mbele ya wakati, kwa kuwa Nimeiweka kwenye akili ya mpagani kuwaonyesha Hukumu ijayo. Na wanasiasa wenu wanainuka na kusema, “Msisikilize, hii ni wazimu, haitafanyika” lakini wao ni nani kusema? Je, wanajua ni wapi Ninapoweka mvua? Je, wanajua ni wapi Ninapoweka upepo?

O, wako na mashine yao iliyoundwa na mwanadamu, wanasema wanaweza kumiliki hali ya hewa, lakini MIMI NIKO, MIMI na MIMI pekee Nitawaonyesha Nitakavyofanyia hii mashine yao! Nitavunja kamba za hii HAARP yao! Nitawashangaza wale wanaodhani wao ni wenye hekima sana. Kwa kuwa si MIMI Ndiye mwandishi wa hekima yote na nyinyi hamjaumba chochote, ni MIMI Ndiye mvumbuzi. MIMI pekee Ndiye Muumba na Nitawaonyesha Ninavyofanyia silaha za maangamizi, kwa kuwa mtaona maangamizi kutoka Mbinguni kama vile Sodoma na Gomora na ile miji saba ilivyoona.

Kwa hivyo mnataka kunikejeli MIMI? Sasa Nitawaonyesha ni nini hufanyika wakati MIMI Muumba Ninapowakejeli. Shirika la ndoa lilitengenezwa ili tuwe moja. Haikuwahi kutengenezwa kuwa ya watu walio na jinsia moja. Tufani zaja ambazo hazijawahi kuonekana hapo awali. Mawimbi ya Tsunami yaja kwenye pwani zenu, zitakuwa machozi YANGU. Dunia itatikisika kwa mawimbi kote duniani wakati mmoja. Kama macho yenu yametazama angani, hofu mtaona shetani akija kama amejificha. Kwa kuwa mko katika njia ya mgongano na mtavuna ghadhabu ZANGU kwa kuwa MIMI ni Mungu YAHUVEH Mwenyezi, kuna mmoja tu.

Kwa sababu ya huruma ya Mwana WANGU Nimeshikilia hasira ZANGU. Mkiona taifa moja chini ya Mungu, mhuri za mwisho zikienda, kwa kweli mtakuwa mmefukuza neno, neno Mungu kutoka kwa taifa lenu. Mmeacha wachache, waliochaguliwa na shetani kuchukua uhuru, moja baada ya nyingine. Mnabaki kimya na bado mnakuja KWANGU na kuomba? Adui habaki kimya, adui ananguruma na kujitambulisha mwenyewe kama vile shetani anavyozungukazunguka kote kama simba akimtafuta ni yupi wa kummeza. Kwa hivyo kwa wale ambao dhambi zao hazijaoshwa kwa Damu ya YAHUSHUA iliyomwagwa, kwa wale ambao hawajiniweka MIMI na Mwana WANGU kuwa kwanza katika maisha na upendo wao, mtayaona majanga haya yakija.

O, mnasema kuwa MIMI Ninapepesa macho kwa dhambi hii na dhambi ile, kwa kweli Mungu hajali. Kama wajua bora na mnaendelea kutoa visingizio, mkiyasema maneno yasiyofaa ambayo hata siyasikii, Nitawaonyesha kuwa MIMI ni Mungu Aliye na wivu. Chochote ulichokiweka mbele YANGU mmekifanya kuwa Mungu.

HUKUMU, HUKUMU, HUKUMU. Hata jina lenyewe Hakimu mtaona korti zenu kuu za Marekani, zinazokaa pale mlimani kama wacha mungu, lakini MIMI pekee Ndiye Hakimu na mmoja kwa mmoja watashushwa, kwa kuwa walikunja ngumi zao dhidi ya Mwenyezi YAHUVEH Anayeishi bila kuogopa. Ninawaambia haya Watoto WANGU, ajenda ya shetani imeanza papa hapa. Mfumo wa mpinga kristo umeundwa ukingoja tu wakati unaofaa na msimu wa yeye kujitokeza. Mmeonywa, Watoto WANGU. Jificheni kwa muda mfupi tu. Ninapowaambia msonge, msiniulize kwa nini. Msipoteze wakati au hamtakuwa salama na mtakuja KWANGU na kuniuliza MIMI kwa nini.

Marekani Nimeweka hukumu ya mwisho kwenu. Mnatazama kote duniani na kuchukua taifa moja baada ya nyingine lakini MIMI Nina macho YANGU juu yenu. Ninaona nyoyo zenu, nyoyo za wanasiasa wenu, pesa za damu zilizobadilishwa, vifo vya wanajeshi, wanawake na wanaume wanaokufa bure, wanateseka bure, kwa kuwa wameapa kutii Taifa ambalo haliniwakilishi MIMI. O, nyinyi mataifa mengine mnaosikiliza neno hili, msifikirie kuwa nyinyi mko sawa, kwa tena Ninasema Nimeweka Hukumu ZANGU, na manabii wenu wanazungumza, kwa kuwa nyinyi hamko sawa, ni Marekani tu walio na ujasiri katika maovu yao. Kwa kuwa wamepoteza hofu ya Muumba wao, yule Aliyewatenga.

Sizungumzi onyo hili kwa Watoto WANGU; Siwatishi Watoto WANGU, wale ambao ni wapendwa WANGU, wale ambao ni Watoto, Bibi Arusi, Waliochaguliwa na Wateule. Msiogope ghadhabu ya Baba yenu kama mnafanya yale ambayo Nimewaambia mfanye. Nitawalinda, Nitawaficha chini ya funiko la mabawa YANGU, ni katika upako huo mnaingia ndani.

Mji wa dhambi ndio wa kwanza ghadhabu zitakapoingia, kwa kuondoa msalaba mdogo kutoka kwa mhuri. Inaonyesha nguvu za kanisa katika Mkoa huo. Wana mfano wa Utakatifu, hawana hamu ya Utakatifu, hawana Utakatifu ndani. Wale ambao wapo katika Kanisa hizi ambazo wachungaji wamebaki kimya na kutazama, hata hawakuomba, hawakuwaambia shirika kufunga na kufanya maandamano. Nyinyi ni makahaba, nyinyi ni makahaba katika macho YANGU. Mlijiuza kwa gharama kuu. Ni nini msichokifanya kwa ajili ya hali ya msamaha wa kodi, ambayo Nilitabiri kuwa itatolewa. O, lakini mnangoja ile siku ambayo mtaweza kuendelea kufanya mnavyotaka. Nimewaambia watu kukimbia Kanisa hizi za Babiloni. Lakini bado wanaendelea kusaidia Kanisa hizi, kuwatunza wachungaji hawa, wakihakikisha kuwa wameweka mali ya wale waovu. Hawa ndio walioketi vitini wakivipa joto tu na Nitawawajibisha, kwa kuwa hawakukimbia, lakini waliendelea kusaidia kazi za shetani ambazo ni bandia mbele YANGU.

Kwa hivyo Marekani, Ninatabiri kupitia huyu binti kwa kuwa ametoka Marekani, fungueni midomo yenu wazi kwa sababu wale wasiokubali Damu ya YAHUSHUA MASIHI iliyomwagwa, damu yenu wenyewe Nitawamwagia! Na hakuna hata mtu mmoja ambaye hataweza kusema, wakati ambapo maangimizi yatakuja kwa mawimbi, “Ninajua huyu au yule aliyefariki.” Niliwaonya Marekani, manabii wenu wamewaonya. Nimezungumza onyo baada ya onyo kutoka kwa binti huyu miaka mingi hapo awali. Kote duniani wanaomba, “Nabii huyu ana nini ya kusema?” Nitajirudia MIMI mara ngapi kwa kuwa masikio yenu hayasikii, yana nta, nyinyi ni wagumu wa kusikia. Hata hamjatii Niliyoyasema na bado mnalia, “Nipe mpya!” Hii ni sampuli ndogo tu.

Sasa Ninawapa onyo mpya. Kwa wale wanoamini kuja kwa YAHUSHUA tena, mnatumia jina unyakuo (rapture), kunyakuliwa kwa Wanawake na Wanaume na Watoto WANGU waaminifu. Ninawaonya sasa, JIHADHARINI Watoto WANGU kwa kuwa kuna UNYAKUO BANDIA iliyopangwa na wale mnaowaamini. Wanaposema “Yesu yupo hapa,” wanaposema “Yesu yu pale, njoo mkutane nasi pale.” (Mathayo 24:23-24) Jihadharini Watoto WANGU kwa HOLOGRAMU iliyo angani, itakuwa shetani ajaye kwa kujificha. Kwa kuwa silaha mpya zitawaangamiza. Kwa wale ambao hawasikii, kwa wale ambao hawajui, watayeyushwa, watabaki moshi tu. Kwa kuwa hamhitaji kuenda popote kwa YAHUSHUA kuja, Mwana WANGU Atakuja mlipo.

Jihadharini Watoto WANGU na UNYAKUO wa BLUE BEAM, ambao sio unyakuo, kwa kuwa ni maovu ambayo yatanyakuliwa, walipofikiria kuwa wanakuja kuuona uso wa Yesu. Niliwaruhusu kudanganyika, kwa kuwa kama kwa kweli mlikuwa mnasikia kutoka KWANGU mngelijua neno lenu, mngejua hata wale wateule watadanganyika. Huu ndio mpango, hii ndio njama ya adui, kuwaonyesha tu maovu ni nini. Sio wote watakaokusanyika ni waovu, wengine hawajasikia onyo, wengine hawajui vile ya kusikia sauti YANGU, kwa hivyo Ninawaambia mwaonye. Kwa kuwa Mwana WANGU yuaja lakini shetani hujaribu kuenda mbele yake, kwa hivyo waonye. Jaribu Roho izungumzayo.

Ndio, ni ukweli kuwa waliofariki katika MASIHI watafufuka, na nyinyi mliobaki mtanyakuliwa kwenye anga kukutana naye Mwana WANGU lakini shetani yuaja kwanza. Jihadharini nyinyi mlio na masikio, sikieni, nyinyi mlio na macho ya kiroho, oneni, ndio msidangayike wakati ambapo bandia hii itakapojaribu kujitokeza mbele yenu. Wakati wanasiasa wenu kote duniani watakapoangalia angani na kusema, “Kuna Mungu mkuu ajaye kunishinda MIMI,” wataona mizimu; ndio, watasema wanaona mashine geni (space ships). Itakuwa kwenye habari. Mgeni (Alien) atahojiwa kwenye televisheni. Kumbukeni Watoto WANGU haya yanapokuja, shetani huja mbele ya Mwana WANGU.

Shetani ananikejeli MIMI katika njia zote, kejeli kuu itakuwa kujaribu kuwaiba Watoto, Bibi Arusi, Waliochaguliwa na Wateule WANGU wa kweli. Jehanamu inamwagika na ishara zitakuja kutoka kwa lava itakayomwagika kutoka sehemu tofauti za dunia. Dunia inatikisika kwa ghadhabu ZANGU, kwa kukaribia kwa Mwana WANGU wa kweli kwa kuwa Bibi Arusi WANGU wanajua Bwana Arusi wao yuaja. Kwa hivyo shetani anakejeli na kujaribu kuenda mbele ya Mwana WANGU na kuondoa chochote na vyote vilivyo Takatifu kutoka kwa macho ya watu ili wasahau gharama ambayo Mwana WANGU Alilipa. Kwa kuwa YAHUSHUA MASIHI Ndiye MASIHI wenu wa pekee, mwanga wenu wa pekee unaowaongoza.

Niliwaonya kwenye anga, Niliwapa ishara baada ya ishara mwaka huu. Niliwapa maajabu na mshangao comet zilipokuja katika vipimo tofauti. Ni wachache waliongalia juu na kutambua kuwa ukombozi wenu wakaribia. Lakini kwa maadui WANGU, hukumu, hukumu, hukumu ndiyo mtakayojua. Hukumu kwa wale waliotengeneza njaa ya mwanadamu. Hukumu kwa wale waliotengeneza maradhi. Hukumu kwa wale waliochafua hewa na maradhi. Hukumu kwa wale walioweka sumu kwa chakula na maji.

HUKUMU, HUKUMU, HUKUMU kwa kuwa MIMI pekee Ndiye Hakimu Mkuu na mtaona kuwa MIMi sio Mungu wa kukejeliwa. Mtaona ni nini Ninachowafanyia maadui WANGU, wale wanaokaa kwa mali na kiburi na huwagonga maskini kwenye vumbi.

HUKUMU, HUKUMU, HUKUMU Ninapofungua midomo yenu kwa nguvu, kumwaga ndani ghadhabu ZANGU. Wale wanaopiga kelele, “Mimi ni shoga, na Ninajivunia.” Maradhi yatawajia, mapigo yatawajia, watu watawakimbia kwa hofu na mtajificha na mtaogopa na mtapiga kelele, “Niue kwa kuwa uchungu huu siwezi kuuvumilia tena.”

HUKUMU, HUKUMU, HUKUMU sio tu Marekani pekee lakini katika kila Taifa ambalo limenikataa MIMI, katika kila Mji na katika kila Mkoa, haijalishi ilivyo ndogo, kutoka Mji, kutoka Vijijini hadi Vitongojini, Ninajua nyote mko wapi. Nitawapata papo hapo.

HUKUMU! HUKUMU! HUKUMU! Kwa nyinyi ambao ni watakatifu katika Jina la Mwana WANGU, hukumu hii haitakuja karibu nanyi. Mtatazama na kuona kwa hofu, mtawaona wale mnaowajua wakivuna Hukumu ZANGU hata wakiwa familia, rafiki au adui. Kama Nilivyoweza kuwalinda Watoto wa Israeli kutokana na mapigo ya wakaazi wa Misri ndivyo Nitakavyofanya tena. Kwa kuwa MIMI Ndiye Hakimu Mwenyezi Anayeishi, MIMI ni Muumba Mwenyezi Anayeishi na Nitavuna Hukumu, kwa maadui WANGU watazivaa kama nguo, kama ngozi ya pili.

Kwanza Ninalia alafu MIMI hukasirika na sasa Watoto WANGU jificheni kwa muda mfupi tu kwa kuwa BABA yenu amekasirika sana. Lakini sijakasirika nanyi Watoto WANGU, sio nyinyi mnaomwita Mwana WANGU, sio nyinyi mnaojaribu kufanya vile mnavyoweza kuliweka tabasamu kwenye uso WANGU na Mwana WANGU. Sio nyinyi mnaosema “O tunaona haya kuwa sisi ni mmoja wa binadamu ambao wanaletea Baba yetu wa Mbinguni aibu.” Ninapapasa vichwa vyenu, Ninawapa busu kwenye paji la nyuso zenu, Ninasema “Jificheni Watoto WANGU kwa muda mfupi tu” wakati Hukumu yaja juu ya maadui WANGU. Kote duniani, bahari hadi bahari, Hukumu yaja juu ya maadui WANGU.

* * * * * * *

Imezungumzwa, Imeandikwa Tarehe Juni 2, 2004 Saa 7:00 Usiku

Mtume Elisabeth Elijah (Elisheva Eliyahu)

www.allmightywind.com

www.almightywind.com

TAFADHALI TOENI HAYA KWA WALE AMBAO WANAJALI. MSITUPE LULU ZENU KWA NGURUWE WATAKAOKEJELI!

* * * * * * *



CLICK HERE or the image below to go directly to her youtube channel
YAHSladyinred