UNABII WA 8
JE, MTATHIBITISHA UPENDO WENU KWANGU?
Ilipewa Rev. Sherrie Elijah Mei 28, 1997
*******
Hivi ndivyo asemavyo YAHUSHUA (YESU KRISTO), basi ndivyo mtakavyokuwa. Kwa kuwa Ninaziona nyoyo zenu. Nazisikia vilio vyenu KWANGU. Ninahisi machungu yenu wakati ambapo kiongozi mliomwamini anawadanganya. Lakini, Nimewaita na Nimewakadiri. Nitakuhifadhi. MIMI, YAHUSHUA na RUACH ha KODESH (ROHO MTAKATIFU) tunawatayarisha. Sitawatuma kwenye mistari ya mbele mpaka ambapo mtaweza kusimama imara na kuvumilia majaribio ambayo mtapitia. Lakini baraka zenu zipo kwa wingi.
Roho nyingi zitakuja KWANGU, Nikiimarisha imani yenu na mkienda katika JINA LANGU kufanya mambo makuu katika JINA la YAHUSHUA na wote watajua kuwa sio wewe lakini ni upako wa RUACH ha KODESH anayeleta madhihirisho haya ya ukombozi na uponyaji. Nitawatumia kuzungumza Maneno YANGU na mtafanya haya kwa ushupavu, ila wengi watakerwa. Haya ni Maneno YANGU, sio maneno yenu; hamtawajibika kwa ajili ya yale Nisemayo au Ninavyofikiria. Kwa kuwa njia ZANGU ni kuu kushinda njia zenu, au sio?
Sizungumzi tu nanyi, lakini tena Ninazungumza kwa Manabii na Mitume wote ambao huhubiri katika JINA LANGU. Njia haijakuwa rahisi na haitakuwa rahisi. Lakini shikilieni kwa nguvu kwenye kipimo cha imani yako Niliyowapa kila mmoja wenu. Kwa kuwa ni mengi juu ya haya ambayo yatakuhifadhi katika wakati huu wa mwisho wa dunia. Kwa kuwa Bwana Arusi yuaja, ndio hata Nipo kwenye upeo. Mnaweza kunihisi MIMI saa uu huu, mkae tayari.
Mfanye yale ambayo Nimewaita kufanya, na mweke mikono yenu kwenye vyombo vya kulima na msiangalie nyuma lakini mwangalie mbele. Endeleeni kukimbia mbio za haki kwa njia ya mwito wa juu. Msidanganywe, dhiki bado haijaanza. Omba kuwa utaponea haya, kwa kuwa dhiki hii sio ya Bibi Arusi WANGU. Je, Nitampigaje au kumwumiza Bibi Arusi WANGU Mpendwa? Nawezaje kumuua mke WANGU, Bibi Arusi WANGU anayemngoja Bwana Arusi wake? Bibi Arusi WANGU akiwa amevaa johari zake akiwa amepambwa vizuri, na anayeniabudu MIMI pekee, anayeishi kwa sababu YANGU pekee. Singeweza.
Nawaambia yeyote anayesema, Nitaruhusu mpitie katika dhiki kuu hazungumzi Maneno YANGU. Wanazungumza maneno ya hofu na uongo. Ninawajia Bibi Arusi WANGU kuwabeba kwa utaratibu na kuwalinda kwa upendo. Hafai kuonja ghadhabu YANGU, kwa kuwa ananipenda na kuniabudu MIMI. Ananiamini MIMI. Ananitegemea MIMI kumwokoa. Msiogope chochote ambacho hawa wajuaji husema, na wao husema, “Mtakuwa hapa wakati wa ghadhabu ya Mwenyezi MUNGU YAHUVEH.” Haya si ya KWANGU. Ninawapenda Bibi Arusi WANGU, watoto WANGU, juu ya yote. Nilitoa maisha YANGU ili mwokolewe.
Mkininiamini MIMI kuwalinda mbali na jehanamu, Niamini pia kuwalinda mbali na uharibifu ujao wakati mkuu wa hofu, ujao hapa ardhini kwa nguvu zote za ghadhabu ya Mwenyezi YAHUVEH. Watoto WANGU, omba kwa kuja kwa haraka KWANGU kwa kuwa hukumu lazima ianze na watoto WANGU alafu wapagani watahukumiwa. Huu ndio wakati mkuu wa hofu Ninayozungumzia. Lolote Nililokuita ufanye, lifanye sasa kwa kuwa muda ni mfupi.
Wekeni macho yenu angani mashariki na mjue kuwa kufika KWANGU upo karibu. Je, Hamhisi furaha kwa kuwa Bwana Arusi wenu yuaja? Lakini kwa nyinyi Bibi Arusi WANGU hamna hofu, bali kushangilia tu. Waogopee wale wanaonikejeli au kunikataa MIMI. Waogopee wale kondoo waliopotea. Waogopee wale wapotovu na fedha iliyokataliwa. Kama walivyonikataa MIMI, pia Nitawakataa. Mtajua fedha iliyokataliwa; kwa kuwa mtajua RUACH ha KODESH hawavuti. RUACH ha KODESH hatapingana kamwe na binadamu kwanza katika nyakati hizi za mwisho wa dunia.
Wewe Daniel ulikuja ukitafuta neno. Wewe Daniel umetuzwa siku hii. Tena Nilikutumia kuzikoroga karama za Roho Mtakatifu ndani yake Handmaiden WANGU. Nyote hamkujua kuwa Nilikuwa Nimechagua wakati ambapo mtakutana kwenye mtandao, lakini Nilitenda. Ujumbe huu sio wako pekee Daniel lakini tena Mwanangu Mpendwa wa kiume, Nimekutumia kuzungumza kwa Watoto WANGU wote.
Msiogope, Bwana Arusi wenu yuaja. Shikilieni kabisa kwenye imani yenu, kwa kuwa ingawa Nimenyamaza Ninawajaribu wale ambao hutangaza upendo wao KWANGU. Lakini kwa kuwalisha, kuwaonya Kondoo WANGU mtakuwa mnathibitisha upendo wenu KWANGU. Kwa kuwa tayari kupitia mateso, chuki, kukataliwa kwa JINA LANGU, mnathibitisha upendo wenu KWANGU. Kwa kushikilia kabisa kwenye imani yenu ingawa kwa macho yenu hamwezi kuona jibu la maombi yenu, mtakuwa mnathibitisha upendo wenu KWANGU mkisema, “YAHUSHUA hata kama hautawahi kujibu ombi langu nitakuabudu kwa wewe ulivyo, kwa yote uliyonifanyia pale Kalvari.”
Haya yatathibitisha upendo wenu KWANGU, kwa kuwa tayari kuweka chini sifa zenu kwa ajili YANGU na kama iwezekanavyo kutoa maisha yenu kama dhabihu kwa ajili ya Injili ya YAHUSHUA. Haya yatathibitisha upendo wenu KWANGU, kwa kunitii MIMI, kunisaka MIMI, na kuniungama kwa uwazi na kuniabudu MIMI. Kwa kufichua wale mbwa mwitu walio katika pango ya kondoo wanaokuja kuwala kondoo, kwa kuchukua upanga WANGU wa RUACH ha KODESH na kuwatetea Kondoo WANGU mtathibitisha upendo wenu KWANGU. Mnasema kuwa mnanipenda MIMI Watoto WANGU? Basi kwa kusimama katika utakatifu na kwa ukweli na sio uongo, kwa kufanana na umbo LANGU na sio la dunia mtakuwa mnathibitisha upendo wenu KWANGU. Namalizia haya na swali moja, “Je, Mtathibitisha upendo wenu KWANGU?
Ninatazama na mmezungukwa na wingu la mashahidi. Hata adui wa roho zenu anatazama kwa hofu. Je, Mtathibitisha upendo wenu KWANGU kwa kupendana? Wale ambao watafanya haya, jua wewe ni WANGU na utalijua. Je, Mtathibitisha upendo wenu KWANGU kwa kuwapa makao na kupendana na kunyoosha mikono yenu kwao katika maombi? Haya yatathibitisha upendo wenu KWANGU. Kondoo WANGU wanajua sauti YANGU; hawatamwendea mchungaji mwingine. Je, Mmesikia sauti YANGU siku hii? Basi ujumbe huu ni wako. Nimethibitisha Upendo WANGU kwenu pale Kalvari. Sasa, mtathibitisha upendo wenu KWANGU?
*******
Alipewa huyu Handmaiden wa YAHUSHUA,
Nabii Sherrie Elijah Mei 28, 1997.
NDIO, nitathibitisha upendo wangu KWAKO YAHUSHUA. Asante kwa kuzungumza kupitia chombo hiki cha udongo mara nyingine. Tafadhali RUACH ha KODESH naomba uweke upako mkubwa kwenye maneno haya kwa Utukufu wa YAHUSHUA. Tafadhali saidia wale kondoo kutambua sauti ya YAHUSHUA. Tafadhali, RUACH ha KODESH, tusaidie kuthibitisha upendo wetu kwa Bwana wetu, Mtawala, Mwokozi, Mfalme wa Wafalme, Bwana Arusi anayekuja. Tunakuabudu, Kukusifu na Kukupenda wewe YAHUSHUA ha MASHIACH. Mimi wako Handmaiden, Mtoto, Shujaa, Bibi Arusi.
www.allmightywind.com
www.amightywind.com