Unabii 80

Bibi Arusi wa YAHUSHUA, Ombeni Kuwa MIMI, YAHUVEH, Nitume Maadui Wenu katika Shinikizo Kubwa la Ghadhabu YANGU!

Imeandikwa/Imezungumza katika upako wa RUACH ha KODESH Kupitia Mtume Elisabeth Elijah (Elisheva Eliyahu) Januari 18, 2006 Saa 1:40 Asubuhi

Haya yanatoka kwa Unabii 105, YAHUVEH Alisema kuyaweka haya katika Unabii zote kutoka wakati huu: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote kwa haya lililofanyika kwa mkono wako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha. Ilitoka kwenye kinywa cha RUACH ha KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa Upepo wa SHKHINYAH GLORY Unaovuma kote duniani, Upepo Takatifu wa Uamsho. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)

Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH pia Alisema kuongezwe yafuatayo kutoka Kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati kabla kila Unabii:

2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi ghadhabu ya BWANA juu ya watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”

* * * * * * *

Bibi Arusi wa YAHUSHUA, msiendelee kutupa lulu zenu mbele ya nguruwe wa dunia hii. Nguruwe wengine wamejificha nyuma ya mimbari, wale matajiri na wanaojulikana wanaojiita Wakristo, hata kwenye hewa yenu. Hawa nguruwe wapo katika kila dini. Kama vile Mafarisayo hawakumuelewa YAHUSHUA na walitaka afe, basi hata wale na pepo za kidini ambao ni sehemu ya makanisa ya Babiloni hatawaelewa sasa. Wataikataa nuru yako ya Shkhinah Glory.

Bibi Arusi wa YAHUSHUA, mwaka huu wa 2006 mnafaa kuombea amani ya Yerusalemu kwa njia ambayo hamjafanya hapo awali. Tambueni kuwa mnapoombea amani ya Yerusalemu, mnaombea Mfalme wa Amani Ambaye ni Mwana WANGU YAHUSHUA kuharakisha kuja KWAKE na kutawala dunia hii kama Mfalme wa Wafalme, Akiondoa kila kitu kisicho kitakatifu kutoka duniani humu kwa muda uliopangiwa na kukadiriwa. Bibi Arusi wa YAHUSHUA, tambueni kama MIMI, YAHUVEH, Ninavyowaamuru kuyafanya haya, tambueni kuwa YAHUSHUA hawezi kurudi na kutawala hadi Israeli iteseke sana. Malalamiko mengi, kulia, mateso, na damu itamwagika na MIMI, YAHUVEH pekee Ndiye Niliyejua hapo awali ni nini kitatokea kufanya Israeli tena kutembea katika utiifu kwa Amri ZANGU za Torati Nilizowapa kupitia Musa, na kunipenda MIMI, YAHUVEH, ambapo hawataogopa kuzungumza Jina LANGU Takatifu ambamo mna Nguvu za upako.

Watakemea uongo ambazo walipewa wao na wengine. Israeli itatambua YAHUSHUA sio tu kama Mwana wa YAHUVEH pekee lakini pia kama MASIHI wa pekee. Watakubali Dhabihu ya Damu Takatifu ambayo ni zawadi ya YAHUSHUA Aliyowapa pale Kalivari, nguvu ya kuokoa, kukomboa, kuponya, kufufua katika Damu ya Mwana Kondoo kamili wa YAHUVEH. Israeli haitamwona Mfalme wa Amani Akija tena katika nchi yao hadi haya yafanyike. Shetani atatuma amani bandia kwa muda mfupi kuwadanganya lakini itakuwa ni kama Jehanamu imejimwaga kote duniani wakati wakati huo mfupi utakapokwisha.

Israeli, mtarudi kwa Muumba wenu na upendo na kunitii MIMI tena. Israeli, kumbukeni Mfalme Daudi wa kale na kumbukeni alifanya nini kushinda vita zote alizoshinda. Alinyenyekea mbele ya MIMI, YAHUVEH, na Sifa na Ibada ndizo zilizoleta ushindi zote kwa Wanaisraeli wa kale. Bibi Arusi wa YAHUSHUA, lazima muombe kuwa Israeli watakuwa na hamu ya viongozi Watakatifu wanaonipenda na kunitii MIMI, YAHUVEH. Israeli watakaponipenda na kunitii MIMI, YAHUVEH, kama Abrahamu, Isaka na Yakobo walivyofanya, basi Nitarudisha yale yaliyoibwa kutoka Israeli, na tena Nitawakomboa Israeli kutoka kwa Mikono ya maadui. Israeli ni kikombe cha kutetemeka kwa dunia hii mzima, kwa kuwa hapo ndipo vita vya nyakati za mwisho vitakapopiganiwa, mazuri dhidi ya maovu. Shetani atatuma mwana wake kutawala dunia hii kutoka kwa nchi hii kwa sababu shetani hunikejeli MIMI na hufanya bandia kila kitu MIMI, YAHUVEH hufanya.

MIMI, YAHUVEH, Nilituma Mwana WANGU YAHUSHUA na Roho WANGU kuongoza nafsi Mbinguni na shetani hutuma pepo zake kudanganya wote watakaosikiza na kufuata pepo ya uasi dhidi ya yote ambayo ni Takatifu, ikiwaongoza hadi Jehanamu, ikiwavutia na Alama. Kama YAHUSHUA Alivyowapa alama wale ambao ni WAKE kwa kweli, ambao majina yao yamendaikwa katika kitabu cha Uzima cha Mwana Kondoo kabla ya kuumbwa kwa dunia hii, pia shetani amewapa alama wale ambao ni wake na pia kimwili atawapa alama tena, akithibitisha kuwa wale wanaomfuata wana majina yao katika kitabu cha waliokataliwa au kitabu cha waliofutwa. Hakuna yeyote atakayechukua alama ya shetani, ataingia katika Ufalme wa Mbinguni.

Israeli hawatawahi kujua amani ya kweli hadi waseme, “Baraka kwa YEYE Anayekuja katika Jina la YAHUSHUA MASIHI.” Ninatuma Bibi Arusi wa YAHUSHUA sasa kuombea Israeli na kwa kila mmoja wao na MIMI, YAHUVEH, Nazungumza mahari kupitia huyu handmaiden ya upako mpya iliyopewa kwenu na YAHUSHUA kwa Bibi Arusi WAKE kama tu wataamini katika imani.

Bibi Arusi wa YAHUSHUA, sasa lazima muamini kwa imani kile neno hili lililozungumza, lakini kwa muda mfupi hata hamtakikana kuwa na imani kuzungumza haya, mtajua kuwa mnajua, kwa kama Eliya alivyowaona maadui wake wakiangamizwa mbele ya macho yake, hata nyinyi mtayaona haya pia. Mtatembea juu ya majivu ya maadui wenu wa utakatifu na hamtaangalia nyuma tena.

1 Wafalme 18:40

Kisha Eliya akawaamuru, “Wakamateni hao manabii wa Baali. Msimwache hata mmoja atoroke!’’ Wakawakamata, naye Eliya akawaleta mpaka Bonde la Kishoni na kuwachinja huko.

MIMI, YAHUVEH, Nimekadiri vita juu ya dunia hii ambapo maovu yamezidi. MIMI, YAHUVEH Ninawapa mamlaka haya mapya. Mnaponiomba MIMI katika Jina la Mwana WANGU YAHUSHUA njooni kwa ujasiri mbele YANGU na ulizeni kuwa maadui wa Israeli warushwe ndani ya shinikizo kubwa la Ghadhabu YANGU. Wakati unakuja hivi karibuni, kwa hivyo Ninawaonya Bibi Arusi wa YAHUSHUA na Wageni katika Karamu ya Arusi ya Mwana Kondoo kupitia huyu Ringmaiden wa YAHUSHUA. Shetani atatuma amani yake bandia, kwanza kumkejeli Mfalme wa Amani, akijaribu kudanganya na kuweka alama dunia hii na Alama yake. Shetani pia ana siku ya wiki ambayo ameitenga kwa Alama hii kupewa. Wale walio na masikio wasikie, Jihadharini na Sabato ya binadamu. Nimewatuma Manabii WANGU kuonya wakati utakuja ambapo wote watalazimika kuchagua ni Mungu mgani wanomtumikia. Hivi karibuni kunakuja mwana mpotovu atakayeua zaidi ya madikteta wenu wabaya zaidi. Huyu mwana mpotovu atakuja na chuki kwa yeyote anayetambua Masihi mwingine. Huyu mwana mpotovu ana chuki kwa kila kitu ambacho ni Kitakatifu kwa kweli na wale waliomkubali YAHUSHUA kama MASIHI.

1 Yohana 2:18

Watoto wadogo, huu ni wakati wa mwisho! Kama mlivyosikia kwamba mpinga Kristo anakuja, hivyo basi wapinga Kristo wengi wamekwisha kuja. Kutokana na hili twajua kwamba huu ni wakati wa mwisho.

1 Yohana 2:22

Je, mwongo ni nani? Mwongo ni mtu yule asemaye kwamba YAHUSHUA si Kristo. Mtu wa namna hiyo ndiye mpinga Kristo, yaani, yeye humkana Baba na Mwana.

1 Yohana 4:3

Lakini kila roho ambayo haimkubali YAHUSHUA haitoki kwa YAHUVEH. Hii ndiyo roho ya mpinga Kristo, ambayo mmesikia kwamba inakuja na sasa tayari iko ulimwenguni.

2 Yohana 1:7

Wadanganyifu wengi, wasiokubali kwamba YAHUSHUA MASIHI amekuja katika mwili, wametokea ulimwenguni. Mtu wa namna hiyo ni mdanganyifu na mpinga Kristo.

Watakatifu WANGU hawatanisaliti MIMI, YAHUVEH, wala YAHUSHUA MASIHI. Ni wale tu wenye pepo kama Yudasi watakaopokea Alama na zawadi zilizopewa na shetani ambazo ni za muda mfupi. Israeli kamwe watasimama. Hakuna yeyote atakayeweza kuwaondoa kwenye ramani, kwa kuwa Mwana WANGU YAHUSHUA Atapachika miguu Yake kwenye Mlima wa Mzeituni na kutawala kutoka Yerusalemu. Nilichukua kiapo na Israeli hawatawahi kuharibiwa kabisa. O vile ilivyo tofauti kwa wale wanaopanga dhidi ya Israeli kama Yudasi au waliosema kuwa watawaondoa kwenye ramani. MIMI, YAHUVEH, Ndiye Ninaye haki ya kumuadhibu Israeli, kama mwana mpotevu. Wale walio na pepo za Yudasi na Hamani (Esta 3:1-6) Hamas wa nyakati za sasa watavuna mabaya yote yaliyowafanyikia Israeli. (Esta 7)

Kama Bibi Arusi wa YAHUSHUA, ambao ni Esta WANGU, wanavyoombea amani ya Yerusalemu, tambueni kuwa mnapofanya haya inaharakisha kila kitu ambayo imekadiriwa. Kukuja kwa mwana wa shetani, aitwaye mwana mpotovu, pia mnaharakisha kukuja kwa Dhiki Kuu, kama mnavyoharakisha kukuja kwa YAHUSHUA kutawala kutoka Israeli na kukaa kwenye Hekalu Takatifu. Mnaposema, “Njoo YAHUSHUA, njoo haraka,” tambueni upako mpya mnapozungumza maneno haya katika maombi ya upako. Kama vile Hamani alitaka kuua kila Myahudi, pia viongozi wa kishetani katika dunia hii wanataka kufanya vivyo hivyo na watataka kumuua kila Myahudi wa kimasihi aliyemkubali YAHUSHUA kama MASIHI. Ezekieli 9 imeanza tayari. Watu WANGU Watakatifu Nishawafunika kwa Mkono WANGU pekee. Ninawaonya sasa kabla ya wakati, uharibifu upo njiani kwa wale waovu na waliokataliwa. Nina mabaki pale Israeli waliojificha na pia ni sehemu ya walio kikundi cha Bibi Arusi wa YAHUSHUA. Sasa ndio wakati wa kuinuka na kumfikia huyu Ninayezungumza kupitia kwake, kwa kuwa nyote ni moja.

Kutoka mwaka huu, mtaona usaliti wa serikali za dunia zaidi ya vile mlivyoona hapo awali. Kile ambacho MIMI, YAHUVEH, Nimekadiri kama chukizo KWANGU kitawekwa mbele ya uso WANGU na waliokataliwa kwa dunia mzima kuona. Mataifa yatageukiana kwa maneno na vita na kiu ya mamlaka, tamaa na damu, na kiu ambayo haiwezi kupunguzwa kama ruba au vampires wanaonyonya damu, wanasiasa wanaotoa visingizio kuuana na kusababisha vita. O ni hadi lini nyinyi watu wa uasi wa dunia hii, mnafikiria mtatingiza ngumi zenu dhidi ya Muumba wenu MIMI, YAHUVEH, na Wanaume na Wanawake Watakatifu mkikanyagia Maandiko YANGU Matakatifu chini ya miguu yenu kwa kejeli na chuki ya yote yaliyo Takatifu? Je, mnafikira kuwa Nitangoja hadi lini kabla nyinyi watu wa uasi muangamizwe na hatima ya sodoma na gomora?

MIMI, YAHUVEH, Nimewapa nafasi kutubu, sanasana nyinyi Marekani, na bado dhambi zenu zinaongezeka kila chukizo ikizidi iliyokuwa hapo awali. MIMI, YAHUVEH Nilikuumba ewe Israeli na Marekani kutengwa na kuwa Takatifu mbele YANGU, Nikimwaga Baraka juu yenu na nchi yenu na watu walifanikiwa na hali ya hewa yenu Nilibariki kwa sababu ya mimea yenu. Kutoka mwaka huu, Nitageuza hali ya hewa dhidi ya sehemu tofauti kwenye ardhi hii Nikiitumia kama adui dhidi ya maadui WANGU katika kipimo kikuu kushinda 2005. O Israeli na Marekani, wewe ni taifa ambalo liliumbwa kuwa kiongozi. Sasa unaongoza mataifa mengine katika uasi na chukizo.

Nyinyi mataifa mengine mliangalia tu na kukataa kusikiza na kutii, kwa hivyo Nikafunga masikio yenu na kufunga macho yenu Nilipozungumza na kunguruma kupitia moto, mvua wa mawe, vimbunga, mafuriko, tufani, ukame, mitetemeko ya ardhi, tsunami, na volkano. Mlikataa kusikia na Nilipokanyaga chini na mguu WANGU mmoja kwenye ardhi na kusababisha ardhi kutingika kwa hofu kuu hadi mzunguko wa ardhi unazunguka kama mlevi. Je, mtasema nini Ninapokanyaga na miguu yote kwa hasira? Mataifa yanayowachinja Watu WANGU Watakatifu ni kama wao ni kondoo wanaopelekwa kichinjioni sasa wanajililia wao wenyewe Nilipotuma mitetemeko ya ardhi na tsunami na hukumu kwa kuwaua Wakristo wasio na hatia ambao hawana damu mikononi mwao, wanaume, wanawake na watoto waliuawa na wanauawa kwa sababu moja, wanakataa kumkana YAHUSHUA MASIHI Ambaye wamwitaye Yesu Kristo Ambaye ni MASIHI na Mwana wa pekee wa MIMI, YAHUVEH.

Mataifa yote kama Indonesia, Nilidai damu yenu na ya wapendwa wenu kwa sababu mlidai na kuchukua maisha ya Wakristo Watakatifu wa kweli. Na kwa hivyo itaendelea kwa watu wa mataifa yote ya dunia hii. Mtavuna kila mlichopanda, mkipanda utakatifu na utiifu kwa Maandiko YANGU Matakatifu na kuniweka MIMI, YAHUVEH, Muumba wenu na kumtambua YAHUSHUA kama Mwana WANGU MIMI, YAHUVEH na MASIHI wenu, mtavuna Baraka ZANGU kutoka Mbinguni. 2006 utakuwa mwaka wa Jubilei kama mtaamini na kuwa na imani katika Jina la YAHUSHUA kuwa MIMI, YAHUVEH, Nitawakomboa kutoka kwa ghadhabu ZANGU zijazo sanasana kwa Bibi Arusi WANGU waaminifu Ninayemwita Esta WANGU.

1 Wathesalonike 5:9

Kwa maana Mungu hakutuita ili tupate ghadhabu bali tupate wokovu kwa njia ya Bwana wetu YAHUSHUA MASIHI.

Haya MIMI, YAHUVEH, Nimekadiri wale wanaopanda maovu, wakitoa visingizio kuishi maisha ya dhambi, wakimwaga damu ya wasio na hatia, kejeli, uasi, nyinyi watoto watumishi wa shetani wanaokataa kutubu uchawi, ushetani, na kila aina ya nguvu za shetani kama wanaoongea na pepo, katika shinikizo kubwa la ghadhabu, katika kisaga CHANGU cha nyama, mtaenda. Nyinyi waliokataliwa mnaopenda kuua na kusababisha vita, mnaoabudu pepo za uasi, kuiba, kuua na kuharibu, mauaji na tamaa. Nyinyi waliokataliwa mnagonga mawe, kutesa, mnaoshambulia na kuwaweka gerezani Mbegu YANGU Watakatifu, mkiwalazimisha kuwa mashahidi, katika shinikizo kubwa la ghadhabu YANGU, katika kisaga cha nyama CHANGU mtaingia.

Ufunuo wa Yohana 19:15

Kinywani mwake mlitoka upanga mkali ambao kwa huo atayaangusha mataifa. Atayatawala kwa ‘‘fimbo yake ya utawala ya chuma.’’ Atalikanyaga shinikizo la mvinyo wa ghadhabu ya YAHUVEH Mwenyezi.

MIMI, YAHUVEH, Nitawabariki wale ambao ni baraka kwa Mwana WANGU YAHUSHUA na wale ambao hubariki Watoto WANGU wa Utakatifu. MIMI, YAHUVEH, Nitawalaani wale ambao ni laana KWANGU na kwa Mwana WANGU YAHUSHUA na Nitawatumia laana za Kumbukumbu la Torati 28 kwa wale wanaowaumiza au kutaka kuwaangamiza na kuwaua Bibi Arusi wa YAHUSHUA, Esta WANGU. MIMI, YAHUVEH, Nitawabariki Watu WANGU Watakatifu na Baraka za Kumbukumbu la Torati 28 zilizohifadhiwa kwa Bibi Arusi wa YAHUSHUA, wanao ndani yao Moto Mtakatifu wa RUACH ha KODESH. MIMI hutoa siri ZANGU kwa mitume na manabii WANGU wa kweli walio na upako. MIMI, YAHUVEH, Nitatuma laana ZANGU za Kumbukumbu la Torati 28 kwa wote wanaodai kumtumikia Mwana WANGU YAHUSHUA lakini kwa neno na tendo wanamtumikia shetani na hukataa kunitii MIMI na huwa ndani yao wana upako bandia inayoitwa moto usio halali na wameuza nafsi zao kama Esau kwa umaarufu na mali, wanaobadilisha Maandiko YANGU Matakatifu, wakifunza uongo na mafunzo ya kishetani.

Ukamilifu wa RUACH ha KODESH WANGU haupatikani kwa mhudumu anayekana yale ambayo anajua ni kweli au kufurukuta maandiko na amri ZANGU ili kubadilishwa kuwafurahisha binadamu au Serikali za dunia hii. Msidanganyike. MIMI, YAHUVEH, sijabadili akili YANGU kuhusu dhambi ni nini au watenda dhambi wasiotubu huenda wapi milele. Maadili yenu na maelezo ya dhambi yaweza kubadilika lakini MIMI NIKO AMBAYE MIMI NIKO na MIMI, YAHUVEH, sibadiliki wala Mwana WANGU YAHUSHUA. MIMI, YAHUVEH, Niliandika kwenye vibao viwili vya sheria vinavyoitwa amri kwenye mawe na kidole CHANGU chenye moto Nikiziandika na Nikampa Musa. (Moshe) Wajinga wanaofikiria kuwa Nilimtuma Mwana WANGU YAHUSHUA kutoka Mbinguni kubadilisha amri hizi zikiwemo amri za Siku YANGU ya Sabato.

Mwaka wa 2006 na baada ya hapa, Watu WANGU watakua katika Utakatifu wakifanya bidii kumtii, kumpenda na kumtumikia Mwana WANGU YAHUSHUA na MIMI, YAHUVEH, katika njia zote. Watu WANGU Watakatifu hawatacheza na adui. Bibi Arusi wa YAHUSHUA ana ruhusa na mamlaka YANGU kuniita MIMI, YAHUVEH, katika Jina la YAHUSHUA na kuniuliza MIMI kuzipeleka pepo zinazowasumbua katika shinikizo kubwa la ghadhabu YANGU la Mbinguni linaloitwa kisaga nyama, pepo zilizotumwa kukusumbua au wapendwa wenu waliokombolewa au kwa watu waliokombolewa. Mmepewa agizo kuomba kwa ukombozi.

Bibi Arusi wa YAHUSHUA, Niiteni MIMI kuwakomboa kutoka kwa watumishi binadamu wa shetani wanaotaka vifo na uharibifu wenu. Njooni mbele ya kiti CHANGU cha enzi kwa ujasiri bila dhambi na Niulizeni MIMI Baba yenu YAHUVEH na katika YAHUSHUA MASIHI kuweka hawa maadui WANGU waliokataliwa na wako katika kisaga nyama CHANGU, Shinikizo kubwa la ghadhabu YANGU. Wale wanaothubutu kutuma laana zao, urogi na hufanya kila aina ya maovu kujaribu kuwaangamaiza au kuwaua Bibi Arusi wa YAHUSHUA ambao ni waliowekwa alama WANGU. Malipo ni YANGU, Ndivyo Asemavyo YAHUVEH. Nitawalipiza kisasi maadui wa Bibi Arusi wa YAHUSHUA na kuwasaga katika njia 7 tofauti.

Bibi Arusi wa YAHUSHUA, haifai nyinyi kulipiza kisasi wakati hawa watumishi binadamu wa shetani wanaumiza. Bibi Arusi wa YAHUSHUA sameheeni hawa maadui binadamu lakini waweke kwenye Mikono YANGU, MIMI, YAHUVEH. Ni jambo la hofu sana kuanguka kwenye mikono ya MIMI, YAHUVEH. Haifai nyinyi kulipiza kisasi lakini Niacheni MIMI, YAHUVEH, kulipiza kisasi kwa niaba yenu. MIMI, YAHUVEH, Nitawasaga maadui wenu wote waliokataliwa kiakili, kimwili, kiroho na kinafsi. Hakutakuwa na chochote kitakachobaki ila tu sauti ya mifupa inayovunjwa wakati MIMI, YAHUVEH, Nimemalizana nao hapa duniani. Adui yeyote wa Bibi Arusi wa YAHUSHUA ni adui wa MIMI, YAHUVEH na YAHUSHUA na RUACH ha KODESH. Wengine wa hawa maadui hutangaza jina la Yesu Kristo na hata hivyo Roho Mtakatifu wa Masihi hayupo ndani yao. Wao na watenda maovu, wanajidanganya wao wenyewe.

Wengine wanaosoma haya watasema, “Je, Bibi Arusi wa YAHUSHUA ni nani?” Ninawaambia haya; matendo yako huzungumza zaidi ya maneno yako. Bibi Arusi wa YAHUSHUA huabudu na kumpenda MIMI na Mwana WANGU YAHUSHUA (mkitupenda sisi juu ya wote) mkiwa na hamu ya mapenzi yetu katika maisha yenu na mkiomba vile vya kututumikia SISI na kutufurahisha SISI, vile vya kuweka tabasamu kwenye uso wa YAHUVEH na YAHUSHUA. Wao hukataa kupuuza ukweli; wanakataa kuamini uongo za shetani. Bibi Arusi wa YAHUSHUA hujitahidi kutii amri ZANGU kama zilivyotajwa katika Maandiko Matakatifu ya Bibilia. Bibi Arusi wa YAHUSHUA huishi kwa Utakatifu kwa sababu wao ni Watakatifu. Wao hukumbatia Uyahudi wa YAHUSHUA wanapotazama na kuheshimu Sabato YANGU na huhesabu Sherehe Takatifu kama Baraka, na huzitazama na kuthibiti kuwa MASIHI YAHUSHUA Bwana Arusi wao, yupo ndani ya kila mmoja.

Kutoka siku hii tukienda mbele, Ninaamuru Bibi Arusi wa YAHUSHUA, Esta WANGU mpya, kutazama Sherehe ya Purim na kufurahia. Sherehekeeni na kunisifu MIMI kwa kumkomboa Esta, kwa kuwa bila yeye, damu yake YAHUSHUA ingekuja vipi? Hakungekuwa na Waebrania wowote katika dunia hii walioachwa kama Hamani angefaulu. Kile ambacho Hamani alijaribu kufanya hapo awali itajaribiwa tena kwa njia iyo hiyo. Zawadi za kuwakamata zitawekwa juu ya Wayahudi na waumini wote wa YAHUSHUA. Pepo iyo hiyo ilikuja tena kupitia Pepo ya Hitler, na itafanyika tena, wakati mwana mpotovu atakapokuja, ambaye ni mwana wa shetani. Bibi Arusi wa YAHUSHUA, someni kitabu cha Esta.

Bibi Arusi wa YAHUSHUA, furahieni, tena MIMI, YAHUVEH Nasema, furahieni. Mwaka huu ni wa Jubilei yenu. Msitazame tu hukumu na kisasi Nitakazomwaga juu ya maadui WANGU, waliokataliwa na wapagani. Kwa wale wanaoabudu, kupenda na kutii Mwana WANGU YAHUSHUA na MIMI, YAHUVEH, mmeokolewa na kuoshwa katika Damu ya YAHUSHUA iliyomwagwa na hamjapangiwa ghadhabu ZANGU, lakini mtabarikiwa kama, katika imani, mnaamini kuwa mtapokea mwaka wenu wa Jubilei.

Bibi Arusi wa YAHUSHUA, wengi wenu mnapambana na miili iliyo dhaifu, na magonjwa au miili yenye uzee ambayo imezeeka hata kabla ya wakati wake kwa sababu ya mashambulizi ya kimwili, kihisia, kiroho na mashambulizi kutoka kwa watoto watumishi wa shetani na pepo zake. Maadui wenu wamewamaliza nguvu kimwili na kiakili lakini kiroho mnaendelea kukua na kukuwa na nguvu zaidi katika Jina la YAHUSHUA na kupitia Damu YAKE iliyomwagwa pale Kalivari.

Furahieni Bibi Arusi wa YAHUSHUA, hivi karibuni na haraka mtanyakuliwa kumkuta YAHUSHUA kule angani mkiwa hai na miili yenu itabadilika ghafla, kufumba na kufumbua. Na mtakaporudi hamtaweza kuzuiliwa katika viombo hivi vya udongo vidhaifu lakini mtakuwa na nguvu isiyo ya kawaida, mtafanana kama vijana na afya bora kwa njia zote. Hakuna chochote ambacho hamtaweza.

Ushindi juu ya maadui wenu wote na kila pepo. Kama mtataka kukula chakula mnaweza kula kile mtakacho lakini sio chakula ambacho kitawatosheleza. Bali itakuwa upako wa RUACH ha KODESH ambao utawatosheleza. Kila Neno la Kiroho litakalotoka mdomoni mwenu kupitia Maandiko Matakatifu litawatosheleza.

Mathayo 4:4

Lakini YAHUSHUA akajibu, “Imeandikwa, ‘Mtu haishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha YAHUVEH.’ ’’

Luka 4:4

YAHUSHUA Akajibu Akamwambia, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu, bali kwa kila neno la YAHUVEH.’ ”

Kama mnataka kulala mnaweza, lakini usingizi hautakuwa wa lazima kurejesha nguvu yenu.

Isaya 40:31

Bali wale wamtumainio YAHUVEH Atafanya upya nguvu zao. Watapaa juu kwa mbawa kama tai, watapiga mbio wala hawatachoka, watatembea kwa miguu wala hawatazimia.

Vyuma vya gereza havitawashikilia; hakuna milango yoyote itakayowazuia kuenda pale Nitakapowaambia muende. Mtakuwa na miili ambayo inaweza kutoonekana kama mnavyotaka; na mnaweza kuwa na sura aina tofauti kama mnavyotaka. Hakuna umbali wowote ambao hautawezekana hata kama ni Mbinguni au sayari nyingine au kwa mwisho wa dunia hii au hata kwenye mwezi. Itakuwa rahisi kama vile kufikiria mahali fulani na utawasili pale pale. Hakuna mwanamume yeyote, mwanamke, pepo, hata pia shetani mwenyewe hataweza kuwazuia kuenda mahali YAHUVEH na YAHUSHUA watawaambia muende.

Yohana 20:19

Ikawa jioni ya ile siku ya kwanza ya juma, wanafunzi Wake walipokuwa pamoja, milango ikiwa imefungwa kwa kuwaogopa Wayahudi, YAHUSHUA Aliwatokea, Akasimama katikati yao, Akasema, “Amani iwe nanyi.’’

Mtakuwa kama Eliya na Enoki wa kale. Bibi Arusi wa YAHUSHUA watakuwa na miili ambayo haitaweza kuumizwa wala kufa isipokuwa Mashahidi WANGU Wawili, ule wakati uliotajwa kwenye maandiko ambapo silaha ya kiroho kutoka jehanamu iliyohamasishwa na shetani itatumika. Lakini siku 3 baadaye, Mashahidi WANGU Wawili watafufuka katika Miili hiyo ya Utukufu na kunyakuliwa kuwa na YAHUSHUA MASIHI, Bwana Arusi.

Watoto wapendwa, msichoke kwa kufanya mazuri na katika kutii kwa MIMI, YAHUVEH, na masihi wenu YAHUSHUA kama wewe ni Bibi Arusi au Wageni. Baraka kwa wote walioalikwa kwenye Karamu ya Arusi ya Mwana Kondoo. Kama mnavyoona, maovu yanakua kwa kiwango kikuu na mipaka. Inaharakisha kuja kwake YAHUSHUA.

Kama mnavyoona, wale matajiri na watu maarufu waovu ambao ni wanaume na wanawake kawaida tu ambao ni njozi tu, sanamu za dunia hii ambao husahau kuwa miili yao imetengenezwa na vumbi katika Mikono YANGU na katika wakati WANGU Nitarudisha miili yao ya udongo kuwa vumbi tena. Lakini miili yao ya kiroho itateseka milele kule jehanamu na alafu kwenye Ziwa la Moto kwa dhambi walizozifanya katika miili yao. Kwa hivyo msitamani kuwa kama wao.

Msidanganyike, kwa kuwa kuna gharama ya milele ya kulipa unapomkejeli YAHUSHUA na MIMI, YAHUVEH. Ni kama kujaribu kudunga sindano ndani ya macho ya MIMI, YAHUVEH, na Nitalipiza. Na Nitawasaga chini ya miguu YANGU Nikitengeneza nyama kutoka kwa maisha yao hadi pumzi yao ya mwisho hapa duniani. Alafu hawa maadui watahisi moto WANGU wa ghadhabu pale Jehanamu na kwenye Ziwa la Moto. MIMI, YAHUVEH, Ninawalinda Bibi Arusi wa YAHUSHUA, waliokombolewa, waliowekwa alama, kwa njia ambayo sijawahi kufanya.

Kwa kuwa ni kwa huu wakati wa mwisho uliokadiriwa na saa mnamo Januari 14, 2006, Nilimuamsha Elisabeth Elijah [Elisheva Eliyahu] na Nikamuambia baada ya adui binadamu kuja kujaribu kumuua alipokuwa analala kupitia ulimwengu wa kiroho, kuomba KWANGU na kuniuliza MIMI Niwapeleke maadui wake waliokataliwa katika Shinikizo kubwa la ghadhabu YANGU pia linaloitwa Kisaga Nyama. Nilimpa upako wakati wa maombi na [nyumba yake] sio kwa [wao tu], lakini kwa Bibi Arusi wote wa kweli wa YAHUSHUA, pia wana mamlaka ya kuniuliza MIMI kufanya yaya haya.

Imetosha! Imetosha! Bibi Arusi wa YAHUSHUA hawafai kukanyagwa chini na watoto watumishi wa shetani. MIMI, YAHUVEH, Ninawapa upako huu mpya kwa Bibi Arusi wa YAHUSHUA. Watoto watumishi wa shetani na bibi arusi wa shetani, wanaoshambulia Bibi Arusi wa YAHUSHUA, watavuna laana za Kumbukumbu la Torati 28, mara elfu, na kuzivaa kama ngozi ya pili. Watalia kwa uchungu na kusema, “Kama isingekuwa kwa bahati mbaya, hawangekuwa na bahati hata.” MIMI mwenyewe Nitawakanyagia chini ya miguu YANGU hawa maadui wa Bibi Arusi wa YAHUSHUA na damu yao itamwagika kama ziwa nyekundu MIMI, YAHUVEH, Ninapowaweka hawa maadui wa Bibi Arusi wa YAHUSHUA katika shinikizo kubwa la ghadhabu YANGU.

Nyinyi mlio Bibi Arusi wa YAHUSHUA, mmepewa upako usio wa kawaida. Ninawapa upako huu kwa kumfanya Ringmaiden wa YAHUSHUA Elisabeth Elijah [Elisheva Eliyahu] azungumze haya kwa maombi yenye upako na kwa maneno yalioyaandikwa. Nyinyi mlio Bibi Arusi wa YAHUSHUA, kama mpo tayari kuamini kwa ujasiri na kupokea mamlaka haya mapya MIMI, YAHUVEH, Ninayowapa, Nitawakomboa kwa ujasiri kutoka kwa maadui wenu na maadui WANGU kwa njia ambayo hamjawahi kufikiria. Bibi Arusi wa YAHUSHUA, Niulizeni MIMI na tazameni kama sitatuma pepo zinazowasumbua katika kisaga nyama cha YAHUVEH ambayo ni shinikizo kubwa la ghadhabu YANGU ambapo Nitawaharibu.

Bibi Arusi wa YAHUSHUA, Ninawapa mamlaka haya mapya na upako huu mpya siku hii mnaponiuliza MIMI katika Jina la YAHUSHUA sio tu kwa niaba yenu Ninawapa upako huu, lakini ni kwa minajili ya Israeli. Je, ni wangapi watachagua kukubali kiwango hiki dhidi ya maovu hapa duniani? Chaguo ni lako. Imewekwa tu kwa Bibi Arusi wa YAHUSHUA. Wengine wote watakaoomba haya hawatakubaliwa.

Tukikera wengine wanaokataa kusikia, tukiwasaidia wengine wanaosikia sauti ya YAHUVEH.

Mtume Elisabeth Elijah (Elisheva Eliyahu),

Januari 18, 2006 Saa 1:40 Asubuhi



CLICK HERE or the image below to go directly to her youtube channel
YAHSladyinred