Unabii 89
SIRI ZA RUACH ha KODESH
Imeandikwa/Imezungumzwa katika upako wa RUACH ha KODESH Kupitia Mtume Elisabeth (Elisheva) Elijah Januari 27, 2007 Saa Kumi na Moja Jioni
Sabato – Port Alfred, Afrika Kusini
Bonyeza kiungo ifuatayo kuona Vitabu Vya Hekima
http://www.allmightywind.com/treadure/wisdommain.htm
* * * * * * *
(Kwenye Kinaza Sauti)
Elisabeth Akiomba: Sote twataka kukujua MAMA RUACH. Binadamu hukuita mwanaume kwa kuwa hawakutaka kukutambua kutoka zamani. Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu… tunakuita MAMA RUACH HA KODESH. Tafadhali jidhihirishe kwangu? Tafadhali jidhihirishe kwetu?
Unaweza kumpa mume wangu maono kama vile tu waweza kunipa mimi. Unaweza kumpa upako kujua vitu hivi kama vile tu waweza kunipa mimi. Kathy ana maandiko mazuri ambayo najua unayaandika kupitia kwake katika sauti tofauti. Wewe ni mpole. Wewe ni kila kitu ambacho mwanamke anafaa akuwe. Kama mwanamke matakwa yangu ni kuwa kama wewe. Wewe ndiye maana ya neno kike. Hata ABBA YAHUVEH na YAHUSHUA huonya, “Msimwumize.”
Neno kutoka kwa RUACH ha KODESH:
Ngoja, ngoja, ngoja, sasa bado sio wakati wa MIMI kudhihirisha katika njia uliyoniuliza MIMI kudhihirisha. Lakini Nitayafanya haya na utayafunza haya na uongo wote utamalizwa! Ni MIMI Niliyekupa hamu kujua MIMI ni nani. Kwa kuwa ni MIMI uliyenilalia mabegani Mbinguni (Ndoto ya Meza ya Karamu). Nilikupa mtazamo uone vile wanaopenda YAHUSHUA NAMI nawapenda pia. MIMI ndiye MAMA wa UUMBAJI. Wanawake waliumbwa katika mfano WANGU. Mimi sizeeki. Mimi ni MSAIDIZI katika UUMBAJI. Familia ni nakala ya kilicho Mbinguni. Je, mnafikiria ilitoka wapi? Mama, Baba na watoto.
Haya hayamaanishi kuwa Mbinguni kuzaliwa ni kama ilivyo duniani. Haikupangwa kuwa hivyo. Ilikuwa kwa sababu ya dhambi za Eva na Adamu ikawa mchakato mchungu. Hakuna ugomvi Mbinguni. Hakuna uchungu Mbinguni. Kuna tu upendo, amani na furaha. Kuna tu furaha.” (Elisabeth asema: Kuna mengine MAMA, ni yapi unayotaka kuniambia?)
Elisabeth, wewe uliyetamani upendo wa mama tangu ulipozaliwa, hata tumboni mwa mama yako ulinililia MIMI. Hili ndilo sababu Ninakujaza katika njia Ninayofanya na upako usio wa kawaida kati ya nyinyi wawili. Basi hautawahi kuhisi utupu huo tena. Niko, haukupata usikivu. Mama yako duniani alifanya yote aliyoweza na roho aliyokuwa nayo. Lakini MIMI pia hukujaza na upendo WANGU.
Elisabeth, unapobembea na kuomba, ni MIMI Ninayekubembeza. Endelea kujitahidi kujua MIMI ni nani. Nitadhihirisha mengi kwako. Nitakukumbusha vile kulivyokuwa Mbinguni ulipoona Uso WANGU. Kwa kuwa MIMI hukaa karibu na BABA yako Aliye Mbinguni. YAHUVEH ni MUME WANGU. YAHUSHUA ni MWANANGU. Hakuna tu kiti kimoja cha enzi, kuna viti vitatu vya enzi Mbinguni na SOTE twatawala pamoja. Je, mnafikiria maombi yenu hufikaje masikioni mwa ABBA YAHUVEH wenu? Ni MIMI huzituma KWAKE kwa kuwa Nimo ndani ya Waumini, wale wanaompenda MWANANGU, YAHUSHUA. Ni MIMI, UPEPO ulio na upako huzivuma KWAKE (YAHUVEH) Nikivumisha busu Mbinguni. Ninaongea katika mfano ili muelewe. Mnapoinua sala, ni kama busu zinavumishwa kwake BABA YAHUVEH wenu. Mnapoomba katika JINA LAKE MWANANGU, kwa kuwa inahitaji sote watatu ili msikike na mjibiwe. Huu ndio mwanzo wa funzo hili.
Ni ya wale tu Ninaokuambia uwaambie, bila shaka, familia hii yote, utawaambia haya. Lakini Nitakuongoza kwa tahadhari, tofauti na Neno lingine lililozungumzwa. Kwa kuwa hizi ni siri shetani hakutaka zidhihirishwe na atapambana nawe na vita ambayo hujawahi kuona. Hili ndilo sababu bado sio wakati wa kupa dunia Neno hili.
Nitazungumza nawe katika mambo ambayo mwanamume au mwanamke yeyote hajasikia. Je, unadhani ni kwa nini shetani alikuja na kumjaribu Eva kwanza? Ilikuwa kunikejeli MIMI kwa kuwa Eva aliumbwa kwa mfano WANGU kama vile Adamu aliumbwa kwa mfano wa YAHUVEH kama vile Abeli aliumbwa kwa mfano wa YAHUSHUA, mtakatifu, ufananuzi wa upendo. Kwa hivyo, ni kwa mkono wa shetani Kaini alimwua Abeli. Kama vile ilivyokuwa kwa roho ya mkono wa Kaini, shetani tena alikuwa anamsulubisha MWANANGU YAHUSHUA, ingawa ilikuwa katika mpango wetu. Kwa nyinyi nyote ambao majina yenu yameandikwa katika Kitabu cha Maisha cha Mwana-Kondoo, Mbinguni mnaweza kurudi, hakukuwa na njia ingine. Kwa hivyo, Agano Jipya la Damu lilizalishwa siku hiyo kubadilisha Agano la Kale la Damu ambalo halikuweza simama.
Mnataka kujua jambo ambalo hunihuzunisha MIMI. Mnataka kujua jambo ambalo hunikera MIMI? Elisabeth, unapohisi kukasirika KWANGU na hasira ZANGU, zinazungumzia hasira za BABA, hasira za BABA YAHUVEH, hamwelewi kabisa hasira za MAMA wa UUMBAJI! Mna tu kiwango kidogo cha hasira ZANGU! Mnapohisi volkano hiyo tayari kulipuka vichwani mwenu na ni katika jina la utakatifu, mna tu kiwango kidogo cha hasira ZANGU!
Mnaposoma katika Neno ambalo limefasiriwa na wanadhubutu kumwita MWANANGU YAHUSHUA, mwana wa binadamu. YEYE hajawahi kuwa mwana wa binadamu. YEYE ni MWANA wa YAHUVEH! MWANA wa YAH! Mkiyaona haya katika fasiri, kwa muda mgani Nimetuma muwe na huzuni na hamjawahi kuwa na amani katika haya na bado mnaeleza kuwa fasiri zote hufanya hivi. Hayakuwa kwa mkono WANGU! Huu ni kwa mpango wa shetani. Ingawa YEYE alizaliwa katika umbo la binadamu, ingawa alihisi uchungu kwenye msalaba, YEYE hajawahi, hajawahi, hajawahi kuwa mwana wa binadamu. YEYE Ndiye MWANA wa YAHUVEH na JINA LAKE, kutangazwa kote duniani. Mnadhani ni kwa nini katika fasiri shetani, amejaribu kumzuia na kumpa YEYE jina la binadamu. Nimeyaruhusu haya na katika wakati huu, kabla ya Dhiki Kuu, jina la Yesu litasimama.
O, lakini katika Dhiki Kuu wale waliookolewa sasa na wamekuwa wakiishi kwa Utakatifu mbele YANGU, roho YANGU ipo ndani yenu, kama vile mlivyookolewa katika Jina la Yesu, bado mngekuwa mnamwita katika Jina hilo. Na msikose kunielewa MIMI, kuna nguvu, nguvu ya Mbinguni inayoinua Jina hilo kwa sababu ya huruma ya BABA yenu YAHUVEH. Lakini katika Dhiki Kuu wengi watafariki, hata kama wameokolewa sasa, wengi watashangaa ni kwa nini maombi yao hayajibiwi. Sio kwa sababu SISI hatuwapendi. Na MIMI sizungumzii wale watakaoenda katika Kanisa za Jumapili na kuchukua ALAMA, Ninazungumzia wale watakaolia katika Jina la Yesu, wanaojua kuwa YEYE Ndiye aliyesulubishwa na kufufuka tena kutoka kifoni na katika siku ya tatu alifufuka.
Wangojee Mbinguni. Lakini lazima waelewe ingawa sasa kuna nguvu katika Jina hilo, baadaye hakutakuwa na nguvu katika Jina hilo. Haya hayamaanishi kuwa wale bado wanaotembea kwa Utakatifu mbele YANGU hawatarudi Mbinguni, lakini inamaanisha kuwa MIMI siwezi kuwajibu kwa kuwa Nilisema huu ni upako WANGU, ni kama kutuma busu kwake BABA YAHUVEH ili maombi yao yajibiwe lakini katika siku hiyo MIMI sitaweza kuyainua maneno yao wanayoyasema kwa kuwa kutakuwa na mwingine katika sura ya dunia hii atakayesema, “Mimi ndiye Yesu.” Na ingawa Nitajua ni Yesu mgani wanaomzungumzia na kumwita, kwa sababu jina hilo litakuwa kama laana, maombi yao hayatafika Mbinguni na watashangaa ni kwa nini. Hii ndiyo sababu unawaonya sasa. Huu ndio umuhimu wa hilo JINA la Kiebrania. Mnaona shetani hataki kutumia hili JINA YAH. O, Nina maadui wengi huko nje wanaodhubutu kuongoza huduma zao na kutumia hili JINA YAH kuwachanganya mbwa mwitu na wana-kondoo. Lakini mwana wa shetani hataki kutumia hili JINA YAH, anataka kutumia jina ambalo dunia limezoea na hilo ni jina la Y-E-S-U.
Kwa hivyo, ingawa wale ambao majina yao yameandikwa katika Kitabu cha Maisha cha Mwana-Kondoo, katika Dhiki Kuu, watarudi mbinguni. Itamaanisha kuwa lazima watapeana maisha yao lakini hawatawahi, kamwe kuingia katika kanisa la Jumapili au majina yao kufutwa. Na hakutakuwa na wokovu wakati huo katika jina la Y-E-S-U; itakuwa tu katika YAHUSHUA. Wengine watasema YAHSHUA. Lakini JINA YAH halitaachwa nje.
Kwa wale 144,000 walio na upako hawatakuwa wakifundisha jina la Y-E-S-U. Hii ni sasa. Baadaye utakuwa wakati tofauti. Nimekupa ujumbe huu kuonya tena. Ni kama sasa hivi, haimanishi kuwa wote wanaohudhuria kanisa za Jumapili sio WANGU, na hawajajazwa na Roho YANGU, lakini inamaanisha kuwa katika Dhiki Kuu haitaruhusiwa kwa kuwa hapa ndipo watakapojiuza kwake Mnyama. Je, mnaelewa? Roho zinaokolewa sasa katika Jina la Y-E-S-U. Ninawapa upako katika Jina la Y-E-S-U. Ninaponya katika Jina la Y-E-S-U. Ninakomboa katika Jina la Y-E-S-U. Lakini baadaye haya hayatakuwepo.
Waonye! Nitawezaje kuwajibu? MWANANGU YAHUSHUA atawezaje kuwajibu? Wanapopiga mayowe, “Yesu, nisaidie,” na mwanaye shetani yupo hapo, na kusema, “Nipo hapa.” Watasema, “Yesu niokoe, nisamehe dhambi zangu!” Na mwanaye shetani atasema, “Nipo hapa.” Je, hamwezi kuona hatari iliyomo? Je, hamwezi kuelewa? Hamjui huzuni Nitakaouhisi wakati wale ambao majina yao yamo katika Kitabu cha Maisha cha Mwana-Kondoo, wanaojua bora zaidi kuliko kuenda katika kanisa za Jumapili, watakimbia na kujificha, na lazima watapoteza maisha yao kwa sababu watakuwa wanalia kilio kuu na watakataa kusema JINA la YAHUSHUA. Watayashikilia yale waliyofundishwa na watasema Jina la Yesu na maombi yao hayatafika Mbinguni kwa kuwa Sitayatuma kama busu kwa sababu mwanaye shetani atajibu, “Nipo hapa.” Haya hayamaanishi kuwa majina yao yamefutwa. Yamaanisha tu kuwa Siwezi kuokoa maisha yao. Siwezi kuwaficha. Siwezi kuwalisha. Siwezi kuwakomboa.
Hili ndilo sababu MIMI huinua huduma kama hii zinazofunza JINA la YAHSHUA, zinazofunza JINA la YAHUSHUA. Haijalishi. Wengi hukataa kutamka jina hili Nilivyowapa lakini JINA la YAH haliwezi kuachwa nje kwa kuwa hata JINA LAKE linamaanisha “YAH Huokoa.”
Nilikupa ndoto wakati mitambo ya angani itakapokuja, kweli itakuwa jeshi la shetani lakini wana haki kwa wale ambao watalia katika jina lisilo sawa kwa sababu yeye (mwanaye shetani) atadai “Nipo hapa.”
Kwa hivyo, jihadharini, tayari ishaanza. Kuna mmoja ambaye amejitokeza. Ana wafuasi kote duniani na yeye hujiita Yesu Kristo. Lakini jambo la muhimu ni, yeye hutupa yote yaliyo Takatifu nje. Jihadharini na Yule ajaye, kwa kuwa huyu ni mwanadamu tu, lakini jihadharini na yule ajaye kwa kuwa itakuwa ni kama Yuda amerudi tena na yeye kwa kweli ni mwanaye shetani, mwana wa shetani.
Waonye sasa. Kuna wakati na kuna msimu. Utajua wakati wa kuachilia Neno hili. Lakini Elisabeth, hautawahi tena kutamani pendo la mama kwa kuwa Nimekuonyesha kuwa Nimeujaza utupu huo.
Kuwaelimisha wengine, Kuwaudhi wengi, Mtume Elisabeth (Elisheva) Elijah
www.allmightywind.com
www.almightywind.com
(maoni kwenye kinaza sauti)
Niko: Elisabeth alikuwa akiomba kwa kiroho, akimwulizia RUACH ha KODESH, MAMA RUACH na akitaka kumjua yeye na MAMA RUACH akazungumza. Yale ndiyo maneno MAMA aliyoyazungumza. Haya basi Adamu. Ulitaka thibitisho, rafiki umeipata. Inakaa ni kama sisi wanaume mara nyingine tumeaibishwa na hawa wanawake!!!
Elisabeth: Ni lazima niseme ufunuo aliyonipa, wakati wanaume waliposhinda wakisema katika bibilia wakimtaja RUACH ha KODESH, "he, he, he," (yaani, kumfananisha na mwanaume) jina hili likiwa linakosa herufi moja tu (yaani “s” ili iwe “she” kumaanisha YEYE ni mwanamke) kwa sababu wanaume walikuwa wakisema kila wakati, “Sisi tumeumbwa kwa mfano wa MUNGU,” na waliweza kujishangilia kwa mwanamke wakisema, “Wewe haujaumbwa kwa mfano WAKE, ni mimi.” Kwa hivyo, MAMA RUACH amethibitisha sasa hivi ukweli, kuwa wanawake, wanawake, Eva, waliumbwa kwa mfano WAKE na YEYE huketi upande mwingine wa YAHUVEH na YEYE ni MSAIDIZI katika UUMBAJI! Kwa hivyo, sisi tumeumbwa kwa kweli kwa mfano wa MUNGU RUACH ha KODESH, kwa mfano wa MAMA wetu. Tafakari hayo wanaume wa dunia!
Haya ni maandiko kadhaa yanayomtaja RUACH ha KODESH.
Jinsia yake RUACH ha KODESH (Roho Mtakatifu)
Maandiko katika Bibilia yanayomtaja RUACH ha KODESH:
Isaya 63:10
Zaburi 51:11
1) Jinsia ya Kike – ‘SHE’
RUACH ha KODESH – CHOKMAH (hekima) jina la kike katika Kiebrania
Mithali 1:20… HEKIMA huita kwa sauti kuu barabarani,
Hupaza sauti YAKE (HER) kwenye viwanja vikubwa.
Mithali 1:21… Hutoa hotuba YAKE (HER).
Mithali 1:23… Kama mngekuwa mmeitikia karipio LANGU,
ningekuwa nimemimina ROHO YANGU kwenu.
Mithali 3:18… YEYE (SHE) ni mti wa uzima kwa wale wanaomkumbatia.
Mithali 4:6… Usimwache HEKIMA NAYE (SHE) atakuweka salama,
mpende, NAYE (SHE) atakulinda.
Mithali 4:13… Mshike maana YEYE (SHE) ni uzima wako.
Mithali 9:1… HEKIMA amejenga nyumba YAKE (HER),
amechonga nguzo ZAKE (HER) saba.
Ufunuo wa Yohana 4:5… Roho Saba za YAH. (Je, hizi ni sawa na nguzo saba za HEKIMA?)
Mathayo 11:19… Lakini HEKIMA huthibitishwa kwa haki ya matendo YAKE. (HER)’’
Mithali 7:4… Mwambie HEKIMA, “Wewe ni dada yangu.’’
(Maandiko haya yote yametoka kwenye KJV Mpya.)
(Kutoka Kitabu cha Hekima – Bibilia ya Yerusalemu)
http://www.allmightywind.com/treasure/wisdommain.htm
Kitabu cha Hekima 1:6… HEKIMA ni ROHO, rafiki kwa binadamu, ingawa YEYE (SHE) hatayasemehe maneno ya kafiri, kwa kuwa YAH huona sehemu ya ndani kabisa, yake…
Kitabu cha Hekima 7:11… Kwa kuwa NAYE (HER), mambo yote mazuri hunijia mimi.
Kitabu cha Hekima 7:12… Haya yote mimi huyafurahia, kwa kuwa HEKIMA huyaleta, lakini bado sikuwa nimejua kuwa YEYE (SHE) ndiye MAMA yao.
Kitabu cha Hekima 7:22-30… Kwa ndani Yake (HER) kuna roho aliye na akili, Mtakatifu, wa kipekee, tabia mbalimbali, mwenye hila, anafanya kazi, ana usahihi, msafi, anaeleweka, ana nguvu, ana wema, mkali, hututendea, ana upendo kwa binadamu, yeye ni imara, anaweza kutegemewa, asiyeweza kutingizika, mwenyezi, anayapima yote.
Kitabu cha Hekima 6:12-22… HEKIMA anameremeta na haachi kumeremeta. Kwa wale wanaompenda, YEYE (SHE) huonekana virahisi, na kupatwa na wale wanaomtafuta. Kwa haraka yeye huwatarajia wale wanaomtaka, yeye hujitokeza kwao.
BABA na MAMA wa Mbinguni?
(Nukuu kutoka KJV Mpya.)
Mithali 1:8-9… Mwanangu, sikiliza mwongozo wa BABA yako, wala usiyaache mafundisho ya MAMA yako. Hayo yatakuwa taji la maua la neema kichwani pako, na mkufu shingoni mwako.
Mithali 6:20-23… Mwanangu, yashike maagizo ya BABA yako na usiache mafundisho ya MAMA yako.
Mithali 6:21… Yafunge katika moyo wako daima, yakaze kuizunguka shingo yako.
Mithali 6:22… Wakati utembeapo, yatakuongoza, wakati ulalapo, yatakulinda, wakati uamkapo, yatazungumza nawe.
Mithali 6:23… Kwa maana maagizo haya ni taa, mafundisho haya ni mwanga.
(Kuna maandiko mengine sawa inayopatikana katika Zaburi 119, ikimzungumzia ELOHIM.)
Zaburi 119:105… Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga katika njia yangu.
(Kutoka kwa haya, tunatamatisha kuwa taa na mwanga pengine hutoka kwa BABA wa Mbinguni wetu, na MAMA RUACH ha KODESH wetu wa Mbinguni, ELOHIM wetu.)
Nani ndiye MAMA wetu?
Wagalatia 4:26… Lakini Yerusalemu wa juu ni huru, nayo ndiye Mama yetu.
Asili ya ROHO MTAKATIFU
Matendo ya Mitume 1:8… Lakini mtapokea nguvu Roho Mtakatifu atakapowajia juu yenu, nanyi mtakuwa mashahidi Wangu katika Yerusalemu, Uyahudi kote na Samaria, hadi Miisho ya Dunia.
Waefeso 5:18… Pia msilewe kwa mvinyo, … bali mjazwe na Roho.
Matendo ya Mitume 2:2-4… Ghafula sauti kama mvumo mkubwa wa upepo uliotoka mbinguni, ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi. Zikatokea ndimi kama za moto zilizogawanyika na kukaa juu ya kila mmoja wao. Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, Roho alivyokuwa akiwapa maneno.
Luka 1:35… Malaika akamjibu, ‘Roho Mtakatifu atakujia juu yako, nazo nguvu Zake YEYE ALIYE JUU zitakufunika kama kivuli.
Warumi 8:9… Lakini ninyi, hamtawaliwi na mwili, bali na ROHO, ikiwa ROHO wa MUNGU anakaa ndani yenu. Mtu yeyote ambaye hana ROHO wa KRISTO, yeye si WAKE.
Yoeli 2:28… Hata itakuwa, baada ya hayo, nitamimina ROHO WANGU juu ya wote. Wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto na vijana wenu wataona maono.
Isaya 40:13-14… Ni nani aliyeyafahamu mawazo ya BWANA, au kumfundisha kama MSHAURI WAKE? Ni nani ambaye BWANA ametaka shauri kwake ili kumwelimisha, naye ni nani aliyemfundisha njia iliyo sawa? Ni nani aliyemfundisha maarifa au kumwonyesha mapito ya ufahamu?
Warumi 8:26-27… Vivyo hivyo, ROHO hutusaidia katika udhaifu wetu. Kwa sababu hatujui kuomba ipasavyo, lakini ROHO mwenyewe hutuombea kwa njia isiyoweza kutamkwa.
Ezekieli 36:27… Nami nitaweka ROHO WANGU ndani yenu na kuwafanya ninyi kutembea katika amri ZANGU na kuwafanya kuwa waangalifu kuzifuata sheria ZANGU.
Waefeso 5:15-21… 18Pia msilewe kwa mvinyo, ambamo ndani yake mna upotovu, bali mjazwe na ROHO, mkizungumza ninyi kwa ninyi kwa Zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, mkimwimbia na kumsifu BWANA mioyoni mwenu.
Ezekieli 37:14… Nitatia ROHO WANGU ndani yenu nanyi mtaishi, nami nitawaweka katika nchi yenu wenyewe…
Matendo ya Mitume 8:17… Wakaweka mikono yao juu ya wale waliobatizwa, nao wakapokea ROHO MTAKATIFU.
Matendo ya Mitume 16:6… Paulo pamoja na wenzake wakasafiri sehemu za Firigia na Galatia, wakiwa wamekatazwa na ROHO MTAKATIFU wasihubiri neno huko Asia.
Matendo ya Mitume 10:44… Wakati Petro bado akiwa anayanena maneno haya, ROHO MTAKATIFU aliwaangukia wote waliokuwa wakisikiliza neno.
2 Timotheo 1:7… Maana MUNGU hakutupa ROHO ya woga, bali ya nguvu, ya upendo na ya akili timamu.
Mwanzo 2:7… BWANA MUNGU alimwuumba binadamu kutoka vumbi ya ardhi akampulizia Pumzi ya Uhai puani mwake, binadamu akawa kiumbe hai.
Wagalatia 5:16-26… 16Kwa hiyo nasema, Tembeeni katika ROHO, na hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. 22Lakini tunda la ROHO ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu.
Waefeso 6:18… Mkiomba kwa Roho siku zote katika sala zote na maombi katika ROHO, mkiwa waangalifu kwa uvumilivu na mkiwaombea watakatifu wote.
1 Wakorintho 12:4-11… 4Basi kuna aina mbali mbali za karama, lakini ROHO ni yule yule; 7Basi kila mmoja hupewa ufunuo wa ROHO kwa faida ya wote; 8Maana mtu mmoja kupitia ROHO hupewa neno la hekima na mwingine neno la maarifa kupitia ROHO yule yule; 9Kwa mwingine imani kupitia huyo ROHO na mwingine karama za kuponya; 10Kwa mwingine matendo ya miujiza, kwa mwingine unabii kwa mwingine kupambanua ROHO, kwa mwingine aina mbali mbali za lugha, kwa mwingine tafsiri za lugha; 11Haya yote hufanywa na ROHO yule yule mmoja, ROHO naye humgawia kila mtu, kama apendavyo mwenyewe.
Mwanzo 1:2… Sasa Dunia ilikuwa haina umbo tena ilikuwa tupu, giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji, naye ROHO wa Mungu alikuwa ametanda juu ya maji.
Mwanzo 6:3… Ndipo BWANA akasema, “ROHO wangu hatakaa ndani ya mwanadamu milele, kwa kuwa yeye ni wa kufa….’’
Hesabu 11:25… Kisha BWANA akashuka katika wingu na kunena na Mose, naye akachukua sehemu ya ROHO iliyokuwa juu ya Mose na kuiweka hiyo ROHO juu ya wale wazee sabini. ROHO alishuka juu yao, wakatabiri, ingawa hawakufanya hivyo tena.
Zaburi 104:30… Unawatuma ROHO wako, wanaumbwa, nawe huufanya upya uso wa dunia.
Isaya 42:1… MIMI… Nimeweka ROHO WANGU juu yake…
Isaya 48:16… Sasa MWENYEZI MUNGU na ROHO WAKE wamenituma.
1 Samweli 16:13-14… Basi Samweli akachukua ile pembe ya mafuta na kumtia mafuta mbele ya ndugu zake, kuanzia siku ile na kuendelea ROHO wa BWANA akaja juu ya Daudi kwa nguvu. Kisha Samweli akaenda zake Rama. Basi ROHO wa BWANA alikuwa ameondoka kwa Sauli, nayo roho mbaya ikaachiwa nafasi na BWANA ili imtese.
1 Wafalme 22:23… Kwa hiyo sasa BWANA ameweka roho ya kudanganya ndani ya vinywa vya hawa manabii wako wote. BWANA ameamuru maafa dhidi yako.
Zekaria 4:6… Si kwa nguvu, wala si kwa uwezo, bali ni kwa ROHO WANGU, asema BWANA WA MAJESHI.
Asili ya HEKIMA (Kitabu cha Mithali, NKV)
1. Hupewa na MUNGU …Mithali 2:6
2. HEKIMA huita kwa sauti kuu barabarani, hupaza sauti yake kwenye viwanja vikubwa. Kwenye makutano ya barabara za mji zenye makelele mengi hupaza sauti, kwenye malango ya mji hutoa hotuba yake …Mithali 1:20-33
3. YEYE huwapa utambuzi na ufahamu na maarifa ya MUNGU na ufahamu wa utakatifu na haki …Mithali 2:1-9
4. Kwa maana HEKIMA ana faida kuliko fedha na mapato yake ni bora kuliko ya dhahabu safi …Mithali 3:14
5. YEYE ni mti wa uzima kwa wale wanaomkumbatia …Mithali 3:18
6. Kwa HEKIMA BWANA aliiweka misingi ya dunia …Mithali 3:19
7. HEKIMA ni bora kuliko vyote, kwa hiyo jipatie hekima. Hata ikikugharimu vyote ulivyo navyo, pata ufahamu. Mstahi, naye atakukweza, mkumbatie, naye atakuheshimu. Atakuvika shada la neema kichwani mwako na kukupa taji ya utukufu …Mithali 4:7-9
8. MIMI HEKIMA, nakaa pamoja na busara, ninamiliki maarifa na busara. Kumcha BWANA ni kuchukia uovu, ninachukia kiburi na majivuno, tabia mbaya na mazungumzo potovu. Ushauri na hukumu sahihi ni vyangu, nina ufahamu na nina nguvu. Kwa msaada wangu wafalme hutawala na watawala hutunga sheria zilizo za haki …Mithali 8:12-15
9. Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona …Mithali 8:17
10. BWANA aliniumba mwanzoni mwa kazi yake, kabla ya matendo yake ya zamani. Niliteuliwa tangu milele, tangu mwanzoni, kabla ya dunia kuumbwa. Wakati huo nilikuwa fundi stadi kando yake nilijazwa na furaha siku baada ya siku, nikifurahi daima mbele zake, nikifurahi katika dunia yake yote nami nikiwafurahia wanadamu …Mithali 8:22-31
11. Kwa maana yeyote anipatae MIMI amepata uzima na kujipatia kibali kutoka kwa BWANA …Mithali 8:35-36
Asili ya HEKIMA (Kitabu Cha Hekima, Bibilia ya Yerusalemu)
http://www.allmightywind.com/treasure/wisdommain.htm
1. HEKIMA ni ROHO, rafiki wa binadamu… Hekima 1:6
2. HEKIMA anameremeta na haachi kumeremeta. Kwa wale wanaompenda (HER), YEYE (SHE) huonekana virahisi, na kupatwa na wale wanaomtafuta (HER)… Hekima 6:13
3. Kwa ndani YAKE (HER) kuna roho aliye na akili, Mtakatifu, wa kipekee, tabia mbalimbali, mwenye hila, anafanya kazi, ana usahihi, msafi, anaeleweka, ana nguvu, ana wema, mkali, hututendea, ana upendo kwa binadamu, yeye ni imara, anaweza kutegemewa, asiyeweza kutingizika, mwenyezi, anayapima yote, hupenya yote, aliye na akili, Roho safi na zenye hila; YEYE (SHE) ni mwepesi kwa hoja kuliko mwendo zozote; YEYE (SHE) ni msafi, huenea kote na hupenya vitu vyote… Hekima 7:22-24
4. YEYE (SHE) ni pumzi ya nguvu zake BWANA, maonyesho masafi ya utukufu wake MWENYEZI; kwa hivyo hamna chochote kisichokuwa safi kinachoweza kutafuta njia ndani YAKE… Hekima 7:25
5. YEYE (SHE) ni mfano wa mwanga wa milele, kioo cha nguvu zake MUNGU kisichobadilika, mfano wa uzuri WAKE. Ingawa pekee yake anaweza kufanya yote; mwenyewe habadiliki, YEYE (SHE) hufanya vitu vyote viwe mpya… Hekima 7:27