Unabii wa 101

 

MIMI, YAHUVEH, Nasema, “Matendo  Yako Huzungumza Kwa Nguvu Zaidi ya Maneno Yako”

 

 

 

Imeandikwa/Imezungumzwa katika upako wa RUACH ha KODESH

kupitia Mtume Elisabeth (Elisheva) Elijah.

Oktoba 2, 2008 saa 3.00 asubuhi

Rosh HaShanah

 

Mume wangu Niko alikuwa anatayarisha maelezo ya siku 10 za Hofu ili ayaweke kwenye Tofuti ya Huduma na aliniuliza kama nina chochote cha kuongezea pamoja na maelezo ya jinsi YAHUSHUA, MASHIACH wetu anavyohusiana na wakati huu Takatifu. Nilipoanza kumwuliza YAHUVEH niseme nini, funzo hili lilipewa, na pia katika mshangao wangu, Unabii mpya ulizaliwa katika siku ya kwanza ya Rosh haShanah, Oktoba 2, 2008.

 

Haya ndiyo niliyoyasikia kuhusu mafunzo ya siku 10 za Hofu.

 

Huu ni wakati wa kutafakari juu ya uhusiano wetu na YAHUVEH na YAHUSHUA na kama tuna uhusiano wa upendo na kutii nao. Sote tumefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wake YAH kwa sababu hakuna mtu aliye kamili aliyetembea humu duniani bali tu YAHUSHUA, MASHIACH wetu. Hata fikira mbaya ni dhambi. Wayahudi Halisi hawaamini ya kuwa Masihi ashakuja kwa hivyo hawana damu dhabihu ya upatanisho ya dhambi zao. Wamemkataa YAHUSHUA, MASHIACH wetu kama MASIHI na mwana wa pekee wa YAHUVEH.

 

Wakati huu Takatifu sio tu wakati wa kusherehekea lakini ni wakati wa hofu kuu kwa wale wasiojua kama majina yao yameandikwa kwenye Kitabu cha Maisha cha Mwana Kondoo. Sisi tunaomtumikia na kumwabudu MASIHI wetu YAHUSHUA aliyefufuka tunajua kuwa kuna mwombezi mmoja tu mbele yake Muumbaji wetu YAHUVEH na kuna njia moja tu kuenda Mbinguni kupitia jina lake YAHUSHUA, MASHIACH wetu na damu yake iliyomwagwa pale Kalvari. YAHUSHUA, MASHIACH wetu ndiye damu dhabihu yetu. Sisi Wayahudi wa Kimasihi hatulii wala kuomboleza wakati wa Yom Kippur kwa sababu hatuna kifuniko cha dhambi zetu, kama wale waliomkataa YAHUSHUA wanavyofanya. Tunawapa moyo nyote katika wakati huu Takatifu kumkaribia YAHUSHUA, MASHIACH wetu zaidi ya ulivyofanya hapo awali.

 

                   **********

 

MIMI, YAHUVEH, Nasema, “Matendo  Yako Huzungumza Kwa Nguvu Zaidi ya Maneno Yako”

 

 

Hapa ndipo YAHUVEH alipoanza kuzungumza.

 

Hivi ndivyo ninavyosema, MIMI, YAHUVEH, msingoje kutubu dhambi zenu, fanyeni hivi mara moja. Msiwe na umbo la utakatifu, lakini ndani yenu hamna utakatifu. Basi kila fikira iwe juu yangu MIMI, YAHUVEH. Msipange kufanya dhambi, epuka uovu na usitoe visingizio kuhusu dhambi. Acheni kumlaumu shetani kwa ajili ya fikira na matendo yenu, kwa sababu hawezi kufanya chochote ambacho haujamruhusu kutenda kukupitia wewe. Ninazungumza maneno haya kwa wale kati yenu wanaosema kuwa wao ni mali yake YAHUSHUA ha MASHIACH, wanaosema kuwa wameoshwa katika Damu yake YAHUSHUA ha MASHIACH iliyomwagwa, wanaoomba katika Jina lake YAHUSHUA ha MASHIACH na bado MIMI, YAHUVEH ninawapa onyo sasa kwa wale wanaotangaza upendo wao KWANGU na kwa Mwana WANGU YAHUSHUA, Ninajua nyoyo zenu na matendo yenu huzungumza kwa nguvu zaidi ya maneno yenu!

 

Acheni kumjaribu RUACH ha KODESH, acheni kumhuzunisha Roho WANGU. Ulimwengu huu sasa unasimama katika ukingo wa korongo, korongo yenyewe ni Dhiki Kuu. Mlilie YAHUSHUA ha MASHIACH sasa kama muda ungali upo. Wakati wa Yom Kippur, katika hizi siku 10 za Hofu kumbuka, MIMI husikia pekee maombi ya wale walio wanyenyekevu moyoni. Msiwe na kiburi katika wokovu wenu.

 

Katika zile enzi za kale watoto wa Israeli walitenda dhambi kuu dhidi yangu MIMI. Walichukua dhahabu na fedha Nilizowapatia kama baraka na kutengeneza ndama wa dhahabu kumwabudu na kumwinamia, sio tofauti sasa. Ulimwengu huu huchukua dhahabu na fedha na kuwainamia matajiri na kuwaabudu, lakini MIMI ninawaonyesha nikitingiza ulimwengu huu kana kwamba unapika bisi kwenye jiko na wale waliojigamba katika kiburi wale matajiri wanaosema wao ni mungu, hawahitaji mungu mwingine, wanadharau Maneno YANGU Takatifu, wanadharau Amri ZANGU Takatifu, wanachafua yote yaliyo Takatifu na kama bisi iliyopikika sana mtanusa harufu mbaya mkiwaona wakiungua na kuchomeka.

 

Ole wao walio waovu, binadamu waovu wanaojiita wachungaji. Nyinyi mliochukua jina ya kanisa na kuwatumia wale watu walio na njaa ya kiroho kujenga himaya zenu za kifedha. Mtaungua na mtachomeka, na himaya zenu za kifedha MIMI, YAHUVEH nitazibomoa na mikono YANGU na mtafichuliwa kwa maovu yenu yote mliyo nayo. MIMI sitawaomba msamaha Sodoma na Gomora, ole wale waliomo duniani wakifuata katika nyayo zao! Mpo kwenye ukingo wa korongo na ni wale tu walio kwa ukweli na uhusiano wa upendo na kutii NAMI, YAHUVEH na YAHUSHUA ha MASHIACH watakaookolewa. Tubu leo kwa kuwa kesho inaweza kuwa muda umepita.

 

Zile mipango ambazo wale maadui wanazo, katika serikali na katika ufalme wa shetani ni za uovu, kuiba, kuua na kuharibu. Kusababisha njaa, kuweka sumu kwenye hewa mnayopumua. Kufanya majaribio na maji mnayokunywa, ambapo kila aina ya sumu mbalimbali tayari imeharibu maji yenu. Wale matajiri wanataka kupunguza nambari ya waliomo duniani, kujiwekea wao wenyewe rasilimali, lakini MIMI, YAHUVEH nasema, MIMI nitakuwa na neno la mwisho. MIMI sitakejeliwa. MIMI nitawalinda wale ambao ni WANGU na zile silaha za maadui zitawaangamiza wao wenyewe.

 

Sasa ndio wakati wa kusimama na kuchukua hatua kwa Utakatifu kama bado mna uwezo. Acheni kuafikiana na shetani na watumishi wa shetani. Ogopeni kunikosea MIMI, YAHUVEH zaidi ya kuwakosea binadamu.

 

Mwisho wa Neno la Unabii

 

Kumbukumbu la Torati 31:8 - YAHUVEH mwenyewe atakutangulia naye atakuwa pamoja nawe, kamwe hatakuacha wala hatakutupa. Usiogope wala usifadhaike.

 

Ilipewa kupitia Mtume Elisabeth (Elisheva) Elijah

Rosh haShanah Oktoba 2, 2008 saa 3.00 asubuhi.

 

Kama Unabii huu umekuwa baraka kwako tafadhali nitumie barua pepe unijulishe.

 

Contact Us

www.allmightywind.com
www.almightywind.com

 

Anwani la kutuma Barua:

 

Almightywind
P.O. Box 40893
Upper Hutt
New Zealand 5018

* * * * * * *

Haya ndiyo maelezo ya desturi na imani ya Wayahudi kuhusu siku 10 za Hofu. Tafadhali kumbuka ya kwamba hizi ni desturi za Wayahudi wengi ambao HAWAJAMKUBALI YAHUSHUA kama MASIHI wao. Hizi ndizo desturi na amri za YAHUVEH kutoka kwenye Torati. Hii inaonyesha tofauti kati ya imani ya Wayahudi Halisi na wale ambao wamemkubali YAHUSHUA kama MASIHI na tunayo Damu ya YAHUSHUA inayookoa, iliyomwagika kwa upatanisho wa dhambi zetu.

 

Zile siku 10 zinazoanza na Rosh Hashanah na kuisha na Yom Kippur kwa kawaida Siku za Hofu (Yamim Noraim) ama Siku za Kutubu. Huu ni wakati wa uchunguzi mkuu, wakati wa kufikiria zile dhambi za mwaka uliopita na kuzitubu kabla ya Yom Kippur.

 

Moja ya zile mandhari zinazoendelea katika Siku za Hofu ni ile dhana kuwa YAHUVEH ana “vitabu” anavyoandikia majina yetu, akiandika wale ambao wataishi na wale ambao watakufa, nani wataishi maisha mazuri na nani wataishi maisha mabaya, katika mwaka ujao. Vitabu hivi vinaandikiwa ndani wakati wa Rosh Hashanah, lakini matendo yetu katika Siku za Hofu ndizo zinazoweza badilisha amri ya YAh. Matendo yanayoweza badilisha amri ni “teshuvah, tefilah na tzedakah,” kutubu, kuomba, matendo mema (ukarimu). Hivi “vitabu” hufungwa wakati wa Yom Kippur. Dhana hii ya kuandika katika vitabu ndiyo chanzo cha salamu ya kawaida katika wakati huu “Upate kuandikwa na kufungwa kwa mwaka mzuri.”

 

Kati ya desturi za wakati huu, ni kawaida kutafuta maridhiano na watu ambao uliwakosea katika mwaka. Talmud hutaja kuwa Yom Kippur inapatanisha dhambi kati ya binadamu na YAH pekee. Kupatanisha dhambi kati yako na mtu mwingine, lazima kwanza utafute maridhiano na huyo mtu, kusawazisha yale mabaya uliyomfanyia kama inawezekana.

 

Kazi inaruhusiwa kama kawaida wakati wa Siku za Hofu, kutoka Tishri 3 mpaka Tishri 9, lakini sio Sabato katika wiki hiyo.

 

Sabato inayopatikana wakati huu inajulikana kama Shabbat Shuvah (Sabato ya Kurudi). Hii hufikiriwa kuwa Sabato muhimu sana.

Contact AmightyWind