UNABII WA 116

 

Mnapaswa Kuwa Wanaotembea Majini Kwa Imani!

 

Imeandikwa/Imezungumzwa katika upako wa RUACH ha KODESH kupitia Mtume Elisabeth (Elisheva) Sherrie Elijah

Ilipokewa Septemba 30, 2009 mwisho wa Yom Kippur

Ilitolewa Oktoba 14, 2009

 

 

(Kutoka Unabii wa 105, YAHUVEH alisema ujumbe huu uwekwe katika kila unabiii kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth kutoita huduma hii kwa jina la mwanaume au mwanamke hata kabla kuwepo na huduma. Niliiweka ndani ya roho yako kwa kuwa hakuna lolote kwa haya lililofanyika kwa mkono wako au lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye kinywa cha YAHUVEH aliyeizalisha. Ilitoka kwenye kinywa cha YAHUSHUA, MASHIACH wako aliyeizalisha. Ilitoka kwenye kinywa cha RUACH ha KODESH, IMMAYAH wako aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa upepo wa SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, upepo Takatifu wa uamsho, sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8))

 

*******

 

Maelezo ya jinsi Unabii huu ulivyopokewa: Adam na Elisabeth walikuwa wanazumgumza kwa simu. Walianza kuombea kusafiri salama kwa Adam na Kathrnyah waliokuwa wanasafiri kwenda kuwatembelea Elisabeth na Niko kwa ajili ya sherehe za Sukkot.

 

Unabii wote haupo katika kinaza sauti. Sauti iliyorekodiwa inaanza takriban theluthi moja (1/3) wa Unabii ukiwa unaendelea.

 

*******

 

Neno la Unabii linaanza:

 

Waambie waje tarehe tano kwa kuwa hata kama watano hawakusanyiki, inasimamia watano wenye busara (Matayo 25: 1-13). Kwa sababu ya Neno jipya lililopokewa, Niko asikose kuzingatia haya. Kwa kuwa nimempa jukumu la kuandika yale yatakayosemwa.

 

Na hili Neno ni tofauti na yale mengine kwa kuwa MIMI nimeshalithibitisha huku nikitetemesha dunia hii kwa hasira ZANGU katika siku hii ya Hukumu!

 

Kuweni tayari kuona dhumna yakianguka. Kumbuka Zaburi 91, hata ingawa unaona 10,000 wakianguka karibu nawe na itaonekana kana kwamba wote karibu nawe wanaanguka, kwa kuwa ni MIMI, YAHUVEH, ninaowagonga chini.

 

Ninaitetemesha dunia hii kwa hasira ZANGU!

 

Lakini wote walio WANGU hawapaswi kuniogopa. Kwa kuwa mpo katika kiganja cha mkono WANGU na mkono WANGU mwingine unawafunika. Nyinyi ni kama vifaranga na ninawaambia haya sasa ili mabawa yenu yasiharibiwe kwa kuwa mtayaona yale msiotaka kuyaona na mtasikia yale msiotaka kuyasikia.

 

Lakini msiruhusu uoga kuwatawala, kumbukeni pahali imani yenu ipo. Msiweke imani yenu katika uchumi, fedha, sio katika kazi ulipoajiriwa au biashara mnazozimiliki. Wekeni imani yenu kwangu MIMI tu, ABBA YAHUVEH na Mwana WANGU wa pekee YAHUSHUA, MASHIACH wako na mpendwa RUACH ha KODESH. Wekeni imani yenu na macho yenu kwa ahadi nilizowapa. Kuweni wanaotembea majini kwa imani. Petro hangejua ya kwamba anaweza kutembea juu ya maji kama hangetoka kwenye dhau na kuchukua ile hatua ya kwanza kutembea kule alipokuwa YAHUSHUA. Ni uoga uliomfanya aanze kuzama, lakini macho yake yalipomwangalia YAHUSHUA tena, aliweza kutembea juu ya maji tena. Hili ndilo jambo ninawaulizia.

 

 

Matayo 14:28-31

28        Petro akamjibu akasema, "Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji."

29        Akasema, Njoo. Petro akashuka, chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu.

30        Lakini alipouona upepo, akaogopa, akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe.

31        Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika na akamwambia, "Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka?

 

Mnapaswa kuwa wanaotembea majini kwa imani kwa kuwa yale mtakayoyaona katika dunia hii , hasa katika mwaka wa 2010, yatafanya nyoyo za wengi kuzirai kwa uoga. Msiweke imani yenu kwa serikali za dunia hii. Msiweke imani yenu kwa mwanasiasa yeyote, kwa kuwa nia zao ni kujitumikia wao wenyewe. Haya ndio maneno ninayowaambia, kwa kuwa nimeanza mtetemeko WANGU na hautakoma. Nakataa kuomba msamaha wa Sodoma na Komora. Nchi hizi zinazoendelea kuhalalisha dhambi, tazama nitakachowafanyia. Wale wanaojiita Wakristo na wanaendelea kunyamaza kimya, msininung’unikie wakati uhuru hamna tena, kwa kuwa mlinyamaza kimya. Mliwaacha wachache walalamike. Mliwaachia wengine wajitolee kuongea. Hamuoni ya kwamba maadui hawajanyamaza? Hamuoni kuwa wale wanaotangaza dhambi hawajanyamaza? Wanapiga kelele kwa sauti za juu hata kama wako wachache. Watumishi wa shetani hawajanyamaza. Kwa nini watumishi wa YAHUSHUA wamenyamaza kimya? Na ninapoongea kuhusu watumishi, sizungumzi kana kwamba wewe ni mtumishi vile mnavyolitumia neno hilo. Ninazungumza na wale wanaomtumikia YAHUSHUA. Ni wachache sana wanaojitolea kuongea. Ni wachache sana wanaotetea yale ambayo ni takatifu.

 

 

Kumbukeni hukumu huanza katika Nyumba la Bwana (1 Petro 4:17). Kwa nini Kanisa zote hawalalamiki? Ni Kanisa ngapi zipo? Katika kila nchi kwa nini Kanisa hawalalamiki dhidi ya hizi sheria za machukizo zinazopitishwa? Wanainua tu na kushusha mabega yao. Wanazingatia tu yale yanayowahusu. Kwa hivyo msishangae, nyinyi kanisa zilizopangwa, wakati serikali itakapowafuata na kuchukua uhuru zenu za kuhubiri na kuweka ishara za kufungwa kwenye Kanisa zenu. Msishangae wakati ardhi yenu itakaponyakuliwa. Msishangae nyinyi mnaoringa na mamilioni zenu.

 

Nazungumza sasa na matajiri – Mnaweka imani yenu katika fedha zenu, msishangae wakati itakapokuwa kama udongo kavu inayotokana -jivu mikononi mwenu. (Mathayo 19:24, Luka 16: 19-31).

 

Nitawaonyesha.

 

Nitaionyesha dunia hii.

 

Wengi wataanza kupata ujumbe kuanzia mwaka wa 2010, lakini watoto nawaonya sasa ili msiseme Baba yenu hakuwaonya. Nawatayarisha sasa ili msishtuke na nawafariji sasa kwa kuwa ABBA wenu hataki nyoyo zenu zifadhaike, kwa sababu nawapenda. Kama vile ilivyokuwa katika siku za kale, nilitenda miujiza na hakuna kitu kilichobadilika. Kwa hivyo mshikilie kabisa pindo la vazi la YAHUSHUA.

 

Mzidi kuoshwa na damu yake aliyomwaga.

 

Simameni katika mavazi YAKE ya utakatifu na ninawahakikisha, maombi yenu yote yanasikika Mbinguni.

 

Tembea katika utakatifu ili shetani asiweze kukushtaki. Tembea katika utakatifu ili usililete aibu kwa jina la YAHUSHUA ha MASHIACH.

 

Masikio YANGU yamefunguliwa kwa hali ya kipekee, tena Elisabeth umezungumzia hili ulipoomba. Ni kana kwamba ungeweza kusikia sindano ikianguka, kwa kuwa siku hii ni ya kipekee kwa wale wote wanaozingatia Yom Kippur nilipowaona mkitubu chochote kisichonipendeza. Wakati kila hitaji la maombi yenu yaliletwa KWANGU wakati mmoja hasira ZANGU zilitetemesha dunia. Kama tu zile nyakati za kale na Musa, wana wa Israeli walilindwa na wale walioabudu muumbaji mwingine hawakulindwa. Hakuna kilichobadilika. Nitawabariki wale ambao ni baraka KWANGU. Nitawalaani wale ambao ni laana KWANGU, na kwa hivyo nimezungumza siku ya leo, ABBA YAHUVEH wenu.

 

[Kama thibitisho hapo awali katika siku hiyo Kathrynyah alikuwa akiomba na katika ulimwengu wa kiroho aliwaona waumini katika YAHUSHUA kama vifaranga wadogo wakihitaji kuongozwa na YAHUSHUA. Alinyoosha mkono WAKE na alikuwa anatuongoza kama vifaranga wadogo.]

 

 

Kwa hivyo imezungumzwa, kwa hivyo imeandikwa Septemba 29, 2009

Mwana, Shujaa, Bibi arusi wa YAHUSHUA ha MASHIACH,

Mtume Elisabeth S. Elijah Nikomia

 

Contact AmightyWind

 

www.amightywind.com

www.almightywind.com

 

Anwani la kutuma Barua:

 

Amightywind

Sanduku La Posta, 40007

Upper Hutt

New Zealand 5018

 

Zaburi 2

 

1 Mbona mataifa wanafanya ghasia, Na makabila wanatafakari ubatili?

2 Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya YAHUVEH, Na juu ya Masihi wake,

3. Na tuvipasue vifungo vyao, Na kuzitupia mbali nasi kamba zao.

4. Yeye aketiye mbinguni anacheka,YAHUVEH anawafanyia dhihaka.

5. Ndipo atakaposema nao kwa hasira yake,na kuwa fadhaisha kwa ghadhabu yake.

6. Nami nimemweka mfalme wangu juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.

7 Nitaihubiri amri; YAHUVEH aliniambia, ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.

8. Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, na miisho ya dunia kuwa milki yako.

9. Utawaponda kwa fimbo ya chuma, Na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi.

10. Na sasa, enyi wafalme, fanyeni akili, Enyi waamuzi wa dunia, mwadibiwe.

11. Mtumikieni YAHUVEH kwa kicho, Shangilieni kwa kutetemeka.

12. Shikeni yaliyo bora, asije akafanya hasira, nanyi mkapotea njiani, Kwa kuwa hasira yake itawaka upesi; heri wote wanaomkimbilia.

 

Yeremia 26:3

 

3: Labda watasikia, na kughairi na kuacha kila mtu nia yake mbaya; ili niyaghairi mabaya niliyokusudia kuwatenda, kwa sababu ya uovu wa matendo yao.

 

Kumbukumbu la Torati 13:4

 

4: Tembeeni kwa kumfuata YAHUVEH, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kusikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.

 

Matayo 25: 1-13

 

1Wakati huo, Ufalme wa Mbinguni utakuwa kama wanawali kumi waliochukua taa zao na kwenda kumlaki bwana arusi.

2Watano wao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye busara.

3Wale wapumbavu walichukua taa zao lakini hawakuchukua mafuta ya akiba,

4lakini wale wenye busara walichukua taa zao na mafuta ya akiba kwenye vyombo.

5Bwana arusi alipokawia kuja wale wanawali wote wakasinzia na kulala.

6Usiku wa manane pakawa na kelele: Tazameni, huyu hapa bwana arusi! Tokeni nje mkamlaki!

7Ndipo wale wanawali wote wakaamka na kuzitengeneza taa zao.

8Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara, Tupatieni mafuta yenu kidogo, taa zetu zinazimika.

9Lakini wale wenye busara wakawajibu, Sivyo, hayatutoshi sisi na ninyi pia. Afadhali mwende kwa wauzao mkajinunulie mafuta yenu.

10Nao walipokuwa wakienda kununua mafuta, bwana arusi akafika. Wale wanawali waliokuwa tayari, wakaingia ndani pamoja naye kwenye karamu ya arusi na mlango ukafungwa.

11Baadaye wale wanawali wengine nao wakaja, wakaita, Bwana! Bwana! Tufungulie mlango!

12Lakini yeye bwana arusi akawajibu, Amin, amin nawaambia, siwajui ninyi!

13Kwa hiyo kesheni, kwa sababu hamjui siku wala saa.

 

Luka 16: 19-31

 

19Palikuwa na mtu mmoja tajiri aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, ambaye aliishi kwa anasa, kila siku.

20Hapo penye mlango wake aliishi maskini mmoja, jina lake Lazaro, mwenye vidonda mwili mzima.

21Huyo Lazaro alitamani kujishibisha kwa makombo yaliyoanguka kutoka mezani kwa yule tajiri. Hata mbwa walikuwa wakija na kulamba vidonda vyake.

22Wakati ukafika yule maskini akafa, nao malaika wakamchukua akae pamoja na Abrahamu. Yule tajiri naye akafa na akazikwa.

23Kule kuzimu alipokuwa akiteseka, alitazama juu, akamwona Abrahamu kwa mbali, naye Lazaro alikuwa karibu yake.

24Hivyo yule tajiri akamwita, Baba Abrahamu, nihurumie na umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake ndani ya maji aupoze ulimi wangu, kwa sababu nina maumivu makuu kwenye moto huu.

25Lakini Abrahamu akamjibu, Mwanangu, kumbuka kwamba wakati wa uhai wako ulipata mambo mazuri, lakini Lazaro alipata mambo mabaya. Lakini sasa anafarijiwa hapa na wewe uko katika maumivu makuu.

26Zaidi ya hayo kati yetu na ninyi huko, kumewekwa shimo kubwa, ili wale wanaotaka kutoka huku kuja huko wasiweze, wala mtu ye yote asiweze kuvuka kutoka huko kuja kwetu.

27Akasema, Basi, nakuomba, umtume Lazaro aende nyumbani kwa baba yangu,

28maana ninao ndugu watano. Awaonye, ili wasije nao wakafika mahali hapa pa mateso.

29Abrahamu akamjibu, Ndugu zako wana Mose na Manabii, wawasikilize hao.

30Yule tajiri akasema, Hapana, baba Abrahamu, lakini mtu kutoka kwa wafu akiwaendea, watatubu.

31Abrahamu akamwambia, Kama wasipowasikiliza Mose na manabii, hawataweza kushawishiwa hata kama atafufuka mtu kutoka kwa wafu.

 

Matayo 19:24

 

24        Nawaambia, tena, Ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu ya sindano, kuliko tajiri kuingia katik ufalme wa Mungu.