Unabii wa 119
2011 Mwito wa Kutubu au Kufa,
YAH Ana Nambari Yako!!!
Imeandikwa/Imezungumzwa katika upako
wa RUACH ha KODESH
kupitia Mtume Elisabeth Sherrie
Elijah Nikomia
Disemba 24, 2010
Ilitolewa Januari 1, 2011
(Kutoka
Unabii wa 105, YAHUVEH alisema ujumbe huu uwekwe katika kila unabii kutoka
sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth kutoita huduma hii kwa jina la mwanaume au
mwanamke hata kabla kuwepo na huduma. Niliiweka ndani ya roho yako kwa kuwa
hakuna lolote kwa haya lililofanyika kwa mkono wako au lililotoka kwenye kinywa
chako. Ilitoka kwenye kinywa cha YAHUVEH aliyeizalisha. Ilitoka kwenye kinywa
cha YAHUSHUA, MASHIACH wako aliyeizalisha. Ilitoka kwenye kinywa cha RUACH ha
KODESH, IMMAYAH wako aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa
imefeli kitambo. Ni kwa upepo wa SHKHINYAH GLORY inayovuma kote duniani, upepo
Takatifu wa uamsho, sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8))
*******
Elisabeth aongea kwenye kinaza sauti:
Niliamka na nikasikia simu inalia, ikilia ring, ring,
na nikasikia simu. Mara ya kwanza ilivyofanyika hivi ni jana na ilikuwa siku
inayoitwa solstice ya baridi siku ya 22. Kwa hivyo nilisikia simu hiyo ikilia
siku ya 22 Disemba. Na Niko alisema ya kwamba hakukuwa na simu yoyote iliyokuwa
inalia.
Hata hivyo hapa ndipo nilipokuwa leo (23 Dis.)
nilipoamshwa mara ya pili kwa sauti ya ring, ring, ring na wakati huu, salaaala,
simu haikuacha kulia. Nilimwambia Niko simu yako inalia nilimwamsha na akasema
kuwa simu yake hailii. Nikasema bado naisikia ikilia hata hivi nikikuongelesha
wewe na ikalia, salaaala, mara nyingi hata nikiwa ninaongea ilikuwa bado inalia
kutokatika.
Ilikuwa kweli sana na Niko alisema kuwa simu yangu
iko humu ndani chumbani mwa kulala na sikuweza kuelewa haya alafu, salaaala,
nikahisi kuwa ilikuwa kwenye ulimwengu wa kiroho, Mungu alikuwa anajaribu kuwasiliana
nami. Kwa hivyo nilirudi kulala na nilipoamka nilikuwa nikimwambia Niko ya kuwa
– mimi huwa naamka saa nne kamili asubuhi – na ninamwambia Niko kuhusu hio simu
na kuomba kwa sauti ya juu, ninasema unajua haya yatakuwa mambo yasiyo ya kawaida
duniani. Ninasikia kilio cha simu, ni nini, unalojaribu kuniambia mimi Baba wa
Mbinguni? Alafu nikayasikia haya.
Ni kilio ambacho hamna yeyote anayetaka kujibu, na
hili ndilo lililofanyika na kwa hivyo nikaanza kutubu na nikaanza…... ngoja
nilisema, kilio ambacho hamna yeyote aliyejibu, na nikasema kwa hivyo ni kilio
cha aina gani? Niliuliza, nimekufeli kwa njia yoyote na nikasikia ya kwamba ni
kilio cha kutubu dhambi. O Abba YAH, Ndio, Ndio mimi ninatubu, pole sana kwa
vile ninajua ya kuwa mimi sio kamili, ninajua mimi hufeli nyakati zingine. Nilikuwa
ninajaribu kufikiria ni nini kibaya nilichokuwa nimefanya ambacho Mungu aliweza
kusema ya kuwa sikuwa nimekitubu.
Mimi huwa na wasiwasi sana kuhusu kitu hiki na
Youtube, mimi huwa na wasiwasi kuwa roho yangu imekuwa wapi, baridi kuu hunikumba
rohoni wakati mwingine. Watu hawa ni wanyama na imekuwa ikiendelea kwa muda
kupita mwaka na mimi huwa na wasiwasi kuwa nyongo imeniingia kwa sababu Mungu amekubali
na maadui wananikejeli na kucheka na wanasema, waona, yeye sio Nabii bado
ninasimama hapa na bado niko hai na hakuna ambacho kimefanyika. Kwanza huyu
Molly na mimi nilisoma kuwa mwanamke huyu alikuwa anakejeli kwenye akaunti yake
bandia hata sijui jina lake. Siwajui watu hawa. Kwa hivyo nilipokuwa ninatubu
na nilikuwa na wasiwasi kwa sababu ya kile nilichokuwa ninakiombea mara ya pili
kabla sijarudi kulala, ni baraka ngapi zilizojitokeza na kufikia watu na ujumbe
wa Wokovu na Unabii, lakini ninahisi ni kama nimejiumiza mwenyewe kwa njia fulani.
Kwa hivyo kweli hii Youtube imekuwa upanga wenye makali mawili, hata kama imekuwa baraka kubwa
pia imeleta taabu, lakini nilipokuwa nikifikiria na kuomba kuhusu haya yote na
kufikiri kuwa hii ndio sababu Mungu alikuwa amekasirika akisema kuwa hakuna
ambaye ameshika simu, kilio cha kutubu.
Halafu nikamsikia YEYE akisema,
Neno la Unabii linaanza hapa:
“Sio wewe Elisabeth; sio wewe ninayezungumzia.” YEYE
alisema, “Ni wale ambao hawajibu. Ni (wale walio ndani ya) dunia waliokataa
kujibu kilio cha kutubu, wakijua kuwa Nimewapa onyo. Ni wale tu watakaohesabika
ndio watakaoepuka Siku ya Dhiki Kuu. Ni wale wanaojua wanachofanya na kunikera
MIMI na bado wanaendelea katika dhambi zao, wanaosema wana Roho Mtakatifu ndani
yao lakini wanaendelea kwa dhambi zao, (wale) wanaotoa visingizio wakijua kuwa
MIMI huona kila kitu wanachofanya iwe filamu za ngono au iwe ushoga, iwe pombe
au iwe zini, usherati, ulevi, madawa za kulevya, laana, wanajua kuwa MIMI
huona, wanajua wanafaa kuwa mfano, wanadai jina la Yesu Kristo, hata YAHUSHUA
na kumbe MIMI niko mbali nao. Roho Mtakatifu hawezi kukaa katika Hema ya
dhambi, lakini bado wao hunijaribu MIMI mara kwa mara.
Nilitoa mwito wa
kutubu dhambi, ni wachache ambao wamesikia. Ni kama simu inayolia na kulia na
hakuna anayejibu. Nilikuweka kwenye mtandao mbali na pana, MIMI Nilikuweka pale
ili kuonyesha kuwa MIMI ni Mungu wa hukumu na pia huruma, MIMI sidanganyi. Lakini
wanamtukana Nabii, wanasema kuwa huduma YANGU ni ya uovu, wananijaribu MIMI na
wananikejeli na kusema, hakuna chochote kitakachotufanyikia, Elisabeth nenda
mbali. Wanasema ni kwa neema yote imefanyika kwenye msalaba. Sasa ninaweza
kufanya dhambi nitakavyo, waona, roho yangu haijapotea. Ni wewe, wewe unaoishi
katika sheria, unafikiri kuwa ni lazima umtii Mungu huyu unayosema na sisi
tunasema kuwa hakuna kitu kama dhambi imetolewa kabisa.
Wanakuchukia wewe (Elisabeth) kwa dhati:
wanachukia wote wanaohubiri kuepukana na dhambi. Wanachukia wote wanoaonya.
Wewe ulitoa mwito, MIMI nilikutuma kule Amightywind kuwaonya wale watu
wanaojiita Wakristo kutubu dhambi zao. Nimesema mara kwa mara kwa mara. Ni
wachache watakaosikia.
Nilituma Huduma ya Amightywind kwa YouTube na kile
walichokufanyia wewe wananifanyia MIMI na bado wao hudai Jina LANGU Takatifu na
kumbe MIMI niko mbali nao. Wao hutaja Maneno YANGU, wao huzitumia kama silaha
kwako na watu wengine wote wanaowaonya kutubu na kutafuta uso wa YAHUSHUA kabla
Hajawaondoa kabisa duniani kwa ghadhabu ZAKE.
Wanasahau ya kwamba Nilikuwa yule Mwana Kondoo
aliyechinjwa mara moja tu. Wanasahau kuwa Ninakuja na moto machoni MWANGU.
Wanasahau ni ghadhabu ya Mwana Kondoo. Wanasahau kuwa dhambi MIMI huchukia.
Wanatoa visingizio kufanya dhambi na wale watakaowajibika zaidi wale wanaotukana,
dharau, chukia na kupaka uchafu Huduma hii Niliyoiita Amightywind.
Kwa hivyo Elisabeth Ninakuacha usikie simu ikilia,
Ninataka uwaonye tena. Ni wachache sana walioshika simu ya kutubu na kuepuka
dhambi. Ni wachache watakaookolewa wakati Siku ya Dhiki Kuu itakapoanza.
Haitoshi kusema tu tubu, lazima kuwe na vitendo
vinavyotekeleza maneno hayo. Lazima kuwe na kurarua (rarua- kuharibu kabisa) na
kuharibu kwa mavazi yako, lakini sio kwa njia ya kimwili. Nimesema tubu. Nimeiweka
Huduma hii Takatifu hapo ndio wote duniani waone kama wamechagua pia na bado
wengi wao wamefunga masikio yao na kupofua macho yao, wanasema sisi hatuoni,
sisi hatukusikii na ni huduma ya Amightywind na wewe Nabii Elisabeth Elijah ndio
tunaowachukia. Sisi ndio jamii ya Wakristo na hata useme nini, chukua Huduma
yako ya Amightywind na chukua Unabii zako mbali kwa kuwa tutaendelea kwa dhambi
zetu na utaona, bado tuko hai na haijalishi kama Huduma ya Amightywind
tunaichukia kwa sababu Mungu wenu bado hajatuua. Mungu wenu hata hajatushika
kwa hivyo huyo Mungu wenu sio Mungu wetu kwa sababu Mungu wetu anasema tunaweza
kutenda dhambi. Mungu wetu asema tunaweza kukuchukia. Mungu wetu asema tunaweza
haribu Amightywind. Mungu wetu asema wewe ni nabii bandia na hakuna haja ya
kutubu dhambi zetu.
O, lakini nyinyi watu wajinga, wajinga huyu ni
MIMI, YAHUSHUA, anayeongea kupitia chombo hiki cha udongo. Mmenijaribu MIMI na kunijaribu
MIMI na kunijaribu MIMI na MIMI nimeitumia Huduma hii kwa mwito wa kutubu
dhambi na bado mnasema ni shetani ambaye ametumwa. Mnasahau nilichoufanyia ule mti.
Mnasahau kuwa ilikuwa MIMI, YAHUSHUA Niliyeulaani kwa
sababu ulikataa kuzaa matunda mazuri. Mnasahau kwamba ulinyauka na kufa. Mnasahau kuna aliyelaumiwa ambaye MIMI Ninachukia.
Ule mti unawakilisha wewe mwenye moyo mgumu kama jiwe, wewe unayetumia Maneno
YANGU, wewe unayetumia Jina LANGU, wewe unayeiita Huduma hii ovu kwa sababu
uliisikia neno tubu na epuka mbali na dhambi zako. Unachukia ya kwamba Nimenena
na unamwita Nabii bandia kwa sababu unafikiri kuwa wewe unao ujuzi wote na bado
MIMI Ninakuambia, wewe ni mjinga kwa vile maono yanapewa kwake huyu Nabii,
lakini wewe unadhani unajua mambo yote. Bado, MIMI Ninakuita msomi mjinga wa bibilia kwa
sababu unalitumia neno liuwalo tu na hamna roho katika yote unayosema na
unaitumia Neno Takatifu na kusema ni Bibilia ya King James (KJV) pekee
inayofaa, ondokeni mbali NAMI nyinyi nyote wengine, mmeiongezea vitabu vingine
na hapana, hata hatutaziangalia.
Wajinga, wajinga nyinyi, MIMI ninatingiza kichwa
changu nikiangalia maisha yenu. Nyinyi ndio msipotubu na kuepuka mbali na
dhambi kwa uhakika, nyinyi ndio nitakaowaambia ondoka mbali na MIMI enyi
wafanyakazi wa uovu kwa kuwa MIMI sijawahi kuwajua. Kwa sababu tu umesema ombi
la wokovu, lazima pia vitendo vyako vitekeleze maneno yako, huwezi tu kusema
kwamba unanipenda MIMI na ukose kunitii MIMI. Huu ni uongo kutoka kule Jehanamu.
Huu ni uongo na kwa sababu Huduma hii ndiyo inayowaambia na pia kila Huduma
nyingine inayotembea katika utakatifu WANGU na kukataa kuafikiana na dhambi na
watenda dhambi. Nyinyi mnaojiita Wakristo hakuna utakatifu wowote ndani yenu na
mnachukia yeyote ambaye huja kwenu na Roho ya Utakatifu na upako WANGU katika nyuso
zao na jambo hili halijabadilika kutoka siku za kale. Mnachukia yeyote anayeongea
Maneno YANGU, walio na upako na wajasiri na kwa hivyo nimempa Elisabeth ishara
mnapokaribia kuingia mnayoita mwaka mwingine. Kumekuwa na mwito wa kutubu na lo, ni wachache,
wachache ambao wanasikiliza au hata kusikia simu hio ikilia.
Bado hamuelewi? Bado hamuelewi? Njia ya pekee ya
kuingia mbinguni ni kwa kuchukua simu hio. Ni lazima usikie simu hio ikilia. Ni
lazima uujibu mwito huo wa kutubu na kuepuka mbali na dhambi, acheni kutunga
visingizio kwa sababu hivi karibuni mtapata mmechelewa.
Uhukumu kali utakuja kwa wale ambao wametesa Huduma hii ambayo MIMI nimeiweka kwenye vyombo
vya habari vilivyo na macho mengi na masikio nyingi na mmejua kuihusu na hamjaitetea
na mmemchukia kwa sababu MIMI Nilisema kwa nguvu na uwazi TUBU, TUBU na muepuke
mbali na dhambi zenu.
Mtachagua kadha wa kadha unabii hizi na kutumia akili
yenu ya binadamu lakini MIMI Nimewaonya mara kwa mara ni kupitia Roho Mtakatifu
pekee ndipo mtakapoelewa kuwa Maneno yaliyonenwa sio ya kutafasiriwa na akili ya
binadamu. Kila Unabii bila kuzitenga zinasababisha watu kutubu dhambi. Zinasababisha
watu kuja katika mikono YANGU ya upendo. Zinawaelekeza watu na kuwafunza
Utakatifu. Haya sio Maneno ya mwanamke au mwanamume. MIMI hutumia chombo hiki cha
udongo pekee, huyu mmoja ambaye mmechukia na kumtusi, mmesema tutakuangamiza,
tutakuaibisha, tutaongea maneno yetu ya chuki kwa sababu tunaweza. Hata tutaiba
na kulichafua jina la Huduma ya Amightywind kwa sababu unathubutu kutuita sisi
watenda-dhambi na unathubutu kuonyesha dhambi zetu kwa sababu sisi hatuwezi kuvumilia
Utakatifu ulio usoni mwako au nyuso za wafanya kazi wanaofanya kazi kando yako,
kwa hivyo tunaambia kila mtu ili kuhakikisha kuwa
wao pia wakuchukie na wasisikilize Unabii Takatifu kwa kuwa ni uongo na kwa
hivyo mnawafunga macho enyi wanafiki na kwa hivyo mnawaziba masikio.
Enyi mliokataliwa, MIMI Nitawaonyesha ni nini MIMI hufanya
kwa sababu ya chuki yenu. Hamna Roho Mtakatifu ndani yenu. Nyinyi ni watoto
wake shetani na MIMI Nimekuwa mvumilivu nanyi kwa muda mrefu sana. MIMI Niliiweka
Huduma hii ya Nafasi ya Mwisho kabla ya kuja kwa siku za taabu na kumbukeni,
chochote mmemfanyia mmenifanyia MIMI pia. Mtasimama mbele YANGU katika Mahakama
ya Sheria inayotoka mbinguni na mtasimama mbele ya uso WANGU na MIMI Nitakukumbusha
maneno yako ya chuki na MIMI Nitasema, ondoka mbali NAMI wewe mfanyakazi wa
uovu kwa kuwa MIMI sijawahi kukujua, MIMI sijawahi kukujua. Ni aidha Roho WANGU
Mtakatifu alikuacha kitambo au hakuwa ndani yako hata.
Kwa hivyo Elisabeth, MIMI hukuwezesha kusikia simu
ikilia. Nilikuacha usikie ni kwa muda gani imekuwa ikilia, ishara yake tu, mara
nane. Kuna wale watakaoisikia na itakuwa kwao mwanzo mpya na kwa kweli watatubu
na watajua kwa kweli kuwa Huduma ya Amightywind ni Takatifu na ni Huduma ambayo
Mungu alituma.
Kwa wale wote watakaonyenyekea na kuepukana na dhambi
zao na akili, mwili, moyo na roho zao kwa kweli, watatubu kwelikweli. Kwa
kweli, watatubu kwelikweli. Haya ndiyo maneno Ninayo ya kusema kwenu, jibu
mwito huo, enyi Watakatifu wa kutubu, kila siku. Hata wewe Elisabeth, ulisema,
ni nini ambayo sijajibu? Ni kwa njia gani ambayo sijatubu? O tafadhali nisamehe
kwa njia yoyote ambayo mimi nimekufeli kwa kuwa mimi sio kamili. Nilikuambia,
Elisabeth sio wewe, kwa sababu wewe husikia mwito WANGU na ulijibu simu YANGU
na wale wote wengine ambao hufanya kazi kando yako na wale wote ambao wanajua
kuwa Huduma ya Amightywind huongea ukweli na haijadanganya. Wamejibu mwito wa
kutubu dhambi, lakini kuna wale ambao wanajua kuwa kuna ukweli kwenye Huduma
hii na bado, wananijaribu MIMI na wanaamini kuwa imetosha tu kukujua. Wanaamini
kuwa imetosha tu kusoma Unabii. Wanaamini kuwa MIMI siku zote Nitakuwa na
huruma na hakutakuwa na matokeo ya dhambi. Hawa ndio MIMI Nitawapa hukumu kali
zaidi kwa sababu hawaoni ya kwamba wanawajibika kwa dhambi Ninazozichukia.
Kwa hivyo waambie Binti YANGU, wanataka Neno jipya litokezee.
Waambie Nilivyofurahia MIMI na wale ambao hujitahidi, ambao bali na kunitii
MIMI kila siku, huamini na kuzungumza na kusambaza yale Maneno MIMI husema. Hawaogopi
kumwudhi binadamu yeyote kwa kuwa nia yao pekee rohoni ni kinifurahisha MIMI
YAHUSHUA, kwa kuwa wanajua zawadi zao zitatoka Mbinguni.
Kwa hivyo waambie Binti YANGU, wewe kuwa yule Eliyah
wa Upya ambaye Nimempa upako na kazi ya kufanya.
Waambie Binti WANGU, hata kama watatema kwenye uso wako,
wewe waonye Binti WANGU, hivi karibuni wataangamizwa.
Waambie Binti WANGU, o MIMI Naja tena. MIMI Naja tena,
lakini wakati huu itakuwa Nikiwa na moto machoni MWANGU na siongei kuhusu Nitakapomchukua
Bibi Arusi WANGU kuwa NAMI, Ninaongea kuhusu wale maadui ambao wako kama ule
mti, Nitaulaumu na utanyauka na kufa kwa wote kuona.
Waambie Binti WANGU, kuwa yule Nabii mjasiri. Acha
kushugulika na wanachosema wanawake na wanaume.
Wewe waambie Binti WANGU, wewe waambie kwa niaba YANGU
kwa kuwa huo ndio mlio wa simu. Wewe una mwito wa kuwa Nabii. Uliijibu kitambo
sana. MIMI sitakuacha ukose kuchukua simu hiyo. Ni mwito wa maisha yako ambao
huwezi kuutoroka kwa sababu ni MIMI Nimekuita Binti WANGU kuonya binadamu wote
kabla ya Siku Kuu ya Dhiki kufika, wakati wa Shida ya Yakobo. O na kwa wengi
sana, sana, watakuwa wamechelewa.
Haya ndiyo Maneno Ninayo ya kusema. Tena maadui
watakutumia kejeli na chuki. Jua tu
hivi, wao sio WANGU. Jua tu hivi, MIMI sijawatuma. Jua tu hivi, wao ni watoto
wa shetani, bibi arusi wa shetani, waliokataliwa, wafanyakazi wa uovu na
watalipa na roho zao na Jehanamu na Ziwa la Moto, hatima yao inawadia.
Usiyaweke maneno hayo ya chuki, nipe MIMI. Ninayaweza,
wewe hauyawezi. Haya sio yenu enyi Watakatifu kushughulikia, maneno haya ya
chuki ni ya kwangu MIMI. Hizi kejeli, matusi yanayosemwa ni ya kwangu MIMI. Hawawezi
kuona ule Upako na Utakatifu Niliouweka juu yenu WOTE ambao ni WANGU sanasana
Bibi Arusi WANGU wanaokazana kila siku kunitii MIMI na hunitumikia MIMI na kuniabudu
MIMI na kuniita MIMI MWENYEZI MUNGU na BWANA, KIONGOZI wa maisha yao, MKUBWA,
MWOKOZI, wao hunikiri MIMI. Hawa ndio Bibi Arusi WANGU. Wao huchukua matusi,
huchukua chuki, wanalaumiwa, wanapakwa matope, wanaongelewa maovu. Hawa ndio
Bibi Arusi WANGU na o Nitawachukua kwa haraka kuwa karibu NAMI. Mnajijua.
Mnakubali ukweli unaojitokeza. Mnajijua. Mnayafahamu matunda mazuri yaliyomo
kwenye Huduma hii ya Amightywind kwa vile upepo mkuu unaenea kote duniani. Na
sasa Ninaipeleka kote katika lugha nyingi tofauti na kuna zingine zaidi
zinazokuja.
Mnajijua o Bibi Arusi WANGU Ninaowathamini. Je mnajuaje?
Kwa sababu mmechukiwa, mmetukanwa, mmedharauliwa, mmetupwa mbali kama waovu.
Bali kila mfanyalo ni kunifurahisha MIMI kwa kila njia na kuwaambia
watenda-dhambi kutubu na kuepuka na dhambi na mmetukanwa kwa sababu ya hayo. Mnajijua,
lakini hamwongei tu kuhusu Utakatifu, mnaishi maisha ya Utakatifu na hata hamfikirii
kutenda dhambi kabla ya kuifanya. Nyinyi ndio Bibi Arusi WANGU. Nyinyi ndio Matunda
YANGU ya Kwanza. Nyinyi ni wachache Ninapoangalia duniani humu, lakini nyinyi
ndio Bibi Arusi WANGU na ni nyinyi Ninaowapenda na kuwathamini. Maadui wenu ni
maadui WANGU, kama vile Esau Ninawachukia.
Wewe chukua maneno haya Elisabeth, wewe waonye ya kuwa
simu inalia. Nimekutuma kama Nabii kwao kuwaambia. Ni wangapi wamesikia na hata
hivyo wamekataa kukubali ya kuwa wameisikia. Kwa hivyo Ninakuambia, o Nabii
WANGU, waambie watubu dhambi, waambie Nilichokuwezesha usikie na kutakuwa na
wale watakaotubu dhambi na kuepukana na dhambi zao. Na ukiwaambia kuwa simu
inalia, watasikia. Watasikia na watasamehewa na kama namba 8 inavyosema (Vilio
8 kwa simu) tutakuwa na mwanzo mpya kwa sababu Nina Nabii aliye tayari kukejeliwa
na kuchukiwa kwa ajili ya jina LANGU akitoa kilio kuu, jibu mwito huu wa kutubu
dhambi, simu inalia kutoka Mbinguni, kwa kuwa Ninawapenda sana kuwaonya kupitia
Eliyah WANGU wa Upya, hata jina lako Eliyah linachukiwa. Kumbuka tu ile Roho ya
Jezebel ilimfukuza Eliyah wa Kitambo na je unatarajia jambo lipi lingine? Je,
Nabii Mtakatifu yeyote anaweza tarajia jambo lipi lingine? Je, Bibi Arusi wa
YAHUSHUA anaweza tarajia jambo lipi lingine? Kwa sababu kama wangenikubali
MIMI, kama wote wangenikubali MIMI kwa upendo wangekuwa pia wanakukubali,
lakini ukiangalia dunia hii na hata MIMI hutuma baridi kunyeshea nyoyo za mawe
na bado hawatubu, bado hawaepuki. Wanasema kuwa MIMI tu ni Mungu wa upendo na
huruma na MIMI siwashtaki kuhusu dhambi, lakini wataona hiyo ndiyo sababu
kutakuwa na kile kinachoitwa Siku ya Dhiki Kuu.
Asante Elisabeth kwa kujibu mwito kwa kuwa
ungekuwa unaishi katika dhambi hatya haungesikia simu hii ikilia, lakini
ulisikia na ililia mara 8 kwa sababu wengi, wengi watakasikiza na hii itakuwa
kwao mwanzo mpya.”
Imezungumzwa katika Upako wa RUACH ha KODESH
kwake Mtume Elisabeth (Elisheva) Sherrie Elijah
Nikiwaudhi wengi, na baraka kwa wengine. Mtoto, Shujaa, Bibi Arusi wa
YAHUSHUA ha MASHIACH/YESU KRISTO
www.allmightywind.com
www.almightywind.com