Unabii wa 24 Sehemu ya 1
Jihadharini, Mlango wa Safina na Kitabu Cha Mataifa Kinafungwa!
Imezungumzwa na Kuandikwa katika upako wa RUACH ha KODESH kupitia Mtume Sherrie Elijah (Elisheva Sherrie Eliyahu)
Novemba 15, 1998
Haya maneno yanatoka kwenye Unabii wa 105, YAHUVEH alisema yaongezwe kwenye Unabii zote kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva], kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke. Hata kabla kuwepo na Huduma, Niliiweka ndani ya roho yako. Kwa kuwa hakuna lolote lililofanyika kwa mikono yako. Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASHIACH wako aliyeizalisha. Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako aliyeizalisha. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO. Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)
Katika mwezi wa Julai 2010, MUNGU YAHUVEH pia Alisema kuongezwe yafuatayo mbele ya Unabii zote kutoka Kitabu cha pili cha Mambo ya Nyakati:
2 Mambo ya Nyakati 36:16, “Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi Ghadhabu ya BWANA juu ya Watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.”
* * * * * * *
Ingieni sasa, Mlango wa Safina na Kitabu cha Mataifa kinafungwa. Njooni katika Safina. Njooni katika mikono YANGU ambamo kuna usalama. Kwa wale wanaoniita MIMI Mpendwa NAMI huwaita Bibi Arusi Wapendwa WANGU, Watoto WANGU. Njooni mwamini tena katika TUMAINI LENU LENYE BARAKA, MUNGU MWENYEZI, BWANA, MWOKOZI na BWANA ARUSI. Amini katika TUMAINI LENYE BARAKA. Nitawaokoa kutoka kwa ghadhabu zinazokuja. Kwa wale wanaokataa TUMAINI LENYE BARAKA, kukuja KWANGU kwa Bibi Arusi WANGU Mpendwa, kuenda naye usiku wa manane. Mnanitusi MIMI kusema kuwa MIMI Nitamsababisha kuangamizwa na Ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Yeye ni mpendwa WANGU, je, kwa nini Nimpige Bibi Arusi WANGU? MIMI sio mpigaji wa wanawake.
Tayari mmejaribiwa na kupatikana kama wanaostahili kuwa Bibi Arusi WANGU, au singekuwa naja kuwanyakua NAMI. Kwa hivyo acheni kunitusi MIMI na amini kuwa MIMI ni mtenda wema kwa wale wanaonitafuta MIMI kwa bidii na hutafuta kukuja KWANGU na hutamani kukuja KWANGU tena. Kama ilivyokuwa katika Nyakati za Nuhu, Nilimwonya Nuhu kuwa mvua utakuja. Ingawa Nuhu hakujua mafuriko ni nini aliniamini MIMI. Nilimwambia Nuhu ajenge Safina ingawa kazi ilikuwa ngumu na kejeli na mateso yalikuwa makuu. Ingawa kazi ilichukua miaka mingi kukamilika, kile Nilichotaka Nuhu kutimiza kwa sababu ya kutii kwake, nyinyi mko hapa leo. Wanyama aliowaokoa, isipokuwa wale ambao mliowamaliza, walijaza dunia. Nilijua mbeleni ni nani Niliyemwumba kuwa na ujasiri wa kunena jumbe, na nguvu za RUACH ha KODESH (ROHO MTAKATIFU) WANGU na upako unaothibitisha nyoyo za wale na masikio ya kiroho ya kusikia na macho ya kuona.
Nuhu HAKUWA na shaka, pia Manabii WANGU wa leo hawafai kuwa na shaka. Lakini wengi huwa na shaka, hata kama MIMI huzungumza maneno YANGU ya moto na kutumia midomo yao kuzungumza na mikono kuandika na bado, wao huthubutu kuwa na shaka na hushangaa kama wanasikia kutoka Mbinguni. Nuhu hakuwa na shaka. Yeremia hakuwa na shaka, Yona hakuwa na shaka, Eliya hakuwa na shaka, Ezekieli hakuwa na shaka, Danieli hakuwa na shaka, mbona basi Manabii WANGU wa leo wananishuku MIMI? Nitaimarisha maneno Ninayoyasema. Msiwasikize wanaokejeli kama ilivyokuwa katika siku ya Nuhu na Lutu na Musa, itakuwa vivyo hivyo tena. Mvua unakuja lakini ni utawala wa hofu YANGU Takatifu ya ghadhabu na hukumu za Mungu Mkuu “MIMI NIKO”.
Mafuriko yaja, lakini sio mafuriko ya maji tu, lakini mafuriko ya bakuli za laana zinazomwagwa. Nitajaza dunia hii na mafuriko ya ghadhabu zangu kutoka wakati wa dhambi ya Adamu na Hawa dhidi YANGU. Nilivyokuwa na Nuhu kuonya juu ya mafuriko, Musa kuonya juu ya laana na Lutu kuonya kuwa moto wa Mbinguni utaanguka, kwa hivyo Nitafanya vivyo hivyo tena, Ninaonya sasa kupitia handmaiden WANGU. Itakuwa bora zaidi kwenu kusoma kila neno Ninalozungumza na kuandika kupitia kwake. Daima huwa kuna mabaki watakaonisikiza na kusikia sauti YANGU. Daima kuna wengi watakaokejeli kama vilevile wapagani walivyomkejeli Nuhu, Musa na Lutu. Kama vilevile maangamizi na ghadhabu zilivyokuja kama mafuriko, laana na moto kwa ghadhabu na hukumu ya Mungu Mkuu ‘MIMI NIKO’, itakuwa vivyo hivyo tena.
Kwa hivyo mtafanya vyema kuyasikia maneno anayonena huyu handmaiden WANGU Eliya [kwa Kiebrania Eliyahu]. Haya sio maneno yake lakini ni maneno kutoka mdomoni mwa Muumba wenu. Mliomba ujumbe kutoka KWANGU. Nitazungumza sasa. Haya maneno yatawakasirisha maadui WANGU na kuwasababisha watoto WANGU na Bibi Arusi kushangilia na kuwa na furaha tele na iliyojawa na Utukufu. Jehanamu nzima ilijaribu kumzuia Sherrie Elijah [Elisheva Sherrie Eliyahu] kuyasikia maneno YANGU Ninayoyazungumza sasa lakini walimzuia tu na hawakuweza kufanya MIMI Nisizungumza na yeye kusikia. Haya maneno humfanya shetani kutetemeka, kwa wengi, NDIO, Ninasema mamilioni wataisikia sauti YANGU na kukimbia kwenye mikono ya kuokoa ya Wokovu ya Mwana WANGU YAHUSHUA. Ni kupitia tu kwa Damu ya YAHUSHUA iliyomwagwa ndio yeyote anaweza kuokolewa kutokana na yale yajayo. Nitamwaga HASIRA ZANGU! Nyinyi mnaosikia au mnaosoma haya aidha mtaokolewa na kuja KWANGU tena au mtaishi kuyapitia ghadhabu ZANGU!
Mnachofanya sasa kwa utukufu WANGU na mlichofanya kwa utukufu WANGU pekee kitasababisha Mwana WANGU kuwaokoa kutokana na vitisho vya ghadhabu na hukumu YANGU ijayo. Mlango wa Safina YANGU unafunga; ingieni kwa haraka kama bado mwaweza. Katika Nyakati za Nuhu wapagani waliugonga mlango wa Safina ili kuingia kwa usalama lakini wakati ulikuwa ushapita baada ya ghadhabu kuanza kuanguka. Wapagani waliyapuuza manyunyu kama wanavyofanya sasa hivi, lakini fungueni macho yenu, tayari ghadhabu zimekuwa zikianguka kote duniani lakini kwa kiwango kidogo kuliko itakavyokuwa. Njooni haraka kwake YAHUSHUA. Mkubalini kama Bwana, Mwokozi na Mungu. Je, mnajua njia ya kuepuka, mwangoja nini? Safina ni kama Safina ya Agano LANGU. Safina ni ahadi YANGU ya usalama. Ni Mwana WANGU YAHUSHUA tu Ndiye Safina ya usalama.
Nitajibu maombi yenu tu katika Jina la YAHUSHUA ha MASHIACH! Hamwezi kuomba kwa majina yenu wenyewe, katika ujasiri wenu au nguvu zenu. Msithubutu kuguza kiti CHANGU cha enzi kwa majina yenu kwa kuwa hamna jina la kuomboleza kwa niaba yenu ila la Mwana WANGU Mpendwa YAHUSHUA. Msithubutu kuvaa nguo zenu za utakatifu kwa kuwa Ninajua ni nani aliye na ALAMA YANGU iliyowekwa kwao. Wale waliokombolewa kwa kweli kupitia kazi ya Mwana WANGU YAHUSHUA pale Kalvari. Njooni KWANGU katika Jina la YAHUSHUA, kupitia Damu YAKE iliyomwagwa; Simama katika Nguo ZAKE za Utakatifu. Ndiposa mnapofanya hivi Nasema, “Njooni kwa ujasiri mbele ya Mungu Mkuu “MIMI NIKO”, Mungu WENU YAHUVEH. Mtakapojaribu kuja katika jina lingine lile NITAWARUSHA NJE! Hamtaokolewa kwa njia nyingine kutokana na mafuriko ya ghadhabu YANGU, moto utakaoanguka, laana, mapigo, ila tu kwa kumkubali YAHUSHUA sasa kama MASIHI, Mwokozi wako, Mungu wako, kabla wakati haujaisha.
Buddha hawezi kukuokoa, hakuweza kujiokoa. Allah, Mohammed, Ghandi, hawawezi kukuokoa; hawakuweza kujiokoa wenyewe, WOTE WALIKUFA! Wote wapo katika Hukumu kwa kuwasababisha wengine kuwaabudu. Sun Moon hawezi kuwaokoa; hawezi kujiokoa kutokana na Hukumu ijayo. Maitreya hawezi kukuokoa! Kuna jina tu moja ambalo linaweza kukuokoa na ni Jina la YAHUSHUA ha MASHIACH. Kama mtamwita YAHUSHUA au YAHSHUA haijalishi, iteni tu Jina LAKE. Nyinyi mnaojiita Wayahudi sikizeni kwa makini. Hamwezi kuingia Mbinguni kwa kuabudu tu na kuamini Jina la YAHUVEH, ingawa hilo ni Jina LANGU, YAHUSHUA Ndiye MASIHI wa pekee.
Gharama Mwana WANGU alilipa Kalvari ilikuwa kwa Wokovu wenu, nyote Wayahudi na Mataifa. YAHUSHUA alisulubiwa na kuteswa na alikufa na kufufuka kwa sababu yenu. Alilipa fidia kwa dhambi zenu. Nyote Wayahudi na Mataifa Nisikizeni MIMI; hamna Mwokozi mwingine ila YAHUSHUA. YEYE Ndiye Mwokozi wenu, njia ya pekee ya kuepuka ghadhabu ZANGU zinazokuja. Watoto WANGU Niliowaumba waliozaliwa kama Wayahudi Nisikizeni MIMI. Mnamngoja Mwokozi mwingine, kumbe mwangoja bure. Hamna mwingine ila Mwana WANGU YAHUSHUA. Yule ambaye mmefunzwa kumchukia Ndiye Safina pekee ya usalama. Hauwezi kunipenda MIMI na tena kumchukia Mwana WANGU Mpendwa. YAHUSHUA Ndiye Niliyemtuma duniani kulipa fidia kwa dhambi zenu.
Hii ndiyo sababu Israili na Yerusalemu hawana amani, kila taifa ambalo humkataa YAHUSHUA kama MASIHI HALITAKUWA NA AMANI. NISIKIZENI MIMI TENA! JUENI YAHUSHUA NA MTAKUWA NA AMANI! YAHUSHUA huleta amani zaidi ya kuelewa. YAHUSHUA Ndiye Mkuu wa Amani. Je, wawezaje kuwa na amani na kumkataa Mkuu wa pekee wa Amani. Kama zilivyokuwa nyakati za Nuhu, kazi ilikuwa ngumu kwa kujenga ile safina. Wakati ulikuwa mrefu wa kujenga safina na kuwakusanya wanyama. Kama ilivyokuwa ngumu kwa manabii wa kale na manabii wa leo, sio rahisi kuyanena Maneno YANGU! Inahitaji ujasiri na utawakera wengi kuliko kuwabariki. YAHUSHUA aliwakera wengi. Kwa hivyo Manabii WANGU wasiozungumza maneno ambayo ni ya masikio ya utafiti, lakini huzungumza maneno ambayo yanathibitisha na kunena siri ZANGU, wakiwaonya kutubu, na pia huwapa matumaini na huruma daima.
Kazi ya manabii na mitume sio rahisi wala ya kupendelewa. Manabii WANGU hukatishwa tamaa wanapojaribu kuwafanya watu wasikie wakijua kuwa haya maneno sio yao. Wao hutoa hela zao kuhubiri jumbe za kinabii kwa kuwa kamwe nina mabaki watakaosikia sauti YANGU na kutii. Kamwe MIMI huwa na mabaki wanao hamu ya kusikia yale ambayo manabii wanazungumza. Lakini, Ninavyo huzuni kwa sababu wachache sana wapo tayari kujitoa kufanya kazi na Manabii WANGU kando yao, wakisaidiana kubeba mzigo. Je, si Neno LANGU husema, “Mwamini Nabii na utafanikiwa,” Sasa Ninawaambia, “Bariki nabii na utapokea tuzo sawa kama wao katika Ufalme wa Mbinguni na hapa duniani.” Wakati fedha ya karatasi itakuwa karatasi bure na haina thamani tena, Nitakumbuka kama uliwasaidia Manabii WANGU au haukuwasaidia na mahitaji yao.
Kumbukeni mjane wa Sarepta, kama mna shaka. Je, si Nilijua ni nani ambaye atakayetaka kumsaidia Eliya wa Kale katika shida zake? Je, Nilimtoa mwanamke wa mali kumsaidia Eliya? Hapana, Nilimtumia mtu ambaye pia alikuwa na mahitaji kama yeye. Wote walikuwa na njaa, au sio? Wote hawakuwa na mali au vipi na bado Nilichagua huyo Mjane Mdogo wa Sarepta kwa kuwa Nilijua moyo wake. Hakuwa mchoyo na ingawa alikuwa na wasiwasi, ilikuwa chakula chake na mwanaye cha mwisho na baadaye yeye na mwanaye wafe. Lakini alimwamini yule nabii na kwa hayo, hakukosa tena. Aliweka mahitaji ya nabii mbele ya mahitaji yake. Kumbukeni Nilivyozidisha mkebe wake wa mafuta na haukukauka. Kumbukeni Nilivyozidisha pipa lake la unga ili isibaki tupu.
Kumbukeni Nilivyomwuliza atumie imani yake kutoa mwisho wa alicho nacho. Kumbukeni Watoto WANGU, alilazimishwa kuomba vyungu na kopo kutoka majirani wake na walipomwuliza anachoenda kuweka ndani alisema kuwa Mungu atawajazia vyombo vyao vitupu. Kama Nilvyomfanyia Nitayafanya haya tena. Amini pekee! Imani bila matendo imekufa. Nitayafanya haya kwa wale wanaoamini kuwa Nitawashughulikia kama Nilivyomfanyia yule mjane wa Sarepta kwa wale wanobariki Manabii WANGU. Mtataka Niwabariki wakati pesa zenu za karatasi na kadi hazina maana. Nitakumbuka sasa kama ulitoa fungu la kumi au ulitoa sadaka pale Nilipokuambia utoe. Si Neno LANGU lasema, “Wekeni hazina zenu Mbinguni ambapo wezi hawawezi kuiba wala kutu kuharibu.” Wekeni baraka zenu kama vile mnavyoweka hazina zenu. Mahali moyo wako upo, kile unachokiamini, ndicho Mungu wako.
Nawaambia haya; yeyote aliyesaidia Nuhu aliokolewa. Lakini nani alifanya kazi na Nuhu? Familia yake pekee! Kwa hivyo itakuwa vivyo hivyo tena. Ni watoto WANGU wa kweli ambao watakuwa na hamu ya kuwasaidia manabii kunena na sio kuwanyamazisha manabii au kufunga miguu ya dume wanaposukuma jembe. Ombeeni manabii sanasana huyu handmaiden anayezungumza. Shetani anataka kunyamazisha sauti YANGU katika dunia hii kwa kuwa manabii daima huonya kabla sijatuma ghadhabu ZANGU au kabla shetani hajashambulia. Ni Manabii WANGU ambao MIMI huwapa siri ZANGU. Kamwe sijatuma ghadhabu ZANGU na hukumu mpaka Niwatume manabii kuzungumza na kuonya TUBUNI! Shetani sanasana huwachukia manabii. Ofisi ya nabii si rahisi. Hakuna yeyote aliye nabii isipokuwa wao wanaojua mateso. Wameteseka kupata upako wa kutabiri.
Kwa hivyo sasa Nasema, “Bariki Manabii WANGU na Nitawabariki.” Walinde Manabii WANGU na Nitawalinda. Fanyeni kazi na Manabii WANGU na makuu yatakuwa baraka zenu sanasana unapokuwa na mahitaji. Jitoeni kwa kuwaficha Manabii WANGU na Nitawaficha. Toa ulicho nacho kwa Manabii WANGU na Ninawaahidi kuwa hamtabaki njaa wala kukosa makao.” Wakati umefika ambapo ni hatari kujiita nabii. Inazidi kuwa hatari YAHUSHUA anapokaribia kuwajia Bibi Arusi WAKE. Sio lazima Niwaambie Nilichosema, mwafaa kuyajua haya. Aibu kwenu nyote kwa kutofanya kile mnajua Nimeizungumzia kwa Roho yenu kufanya. Wakati mwingi Nimesema, “Wasaidie,” na bado mmekataa. Je, mwawezaje kusema kuwa mwanipenda MIMI wakati hamnitii MIMI? Ingieni katika Safina ya Mwana WANGU YAHUSHUA ha MASHIACH.
Amini kuwa MIMI ni Mungu anayewatuza wale wanaonitafuta MIMI kwa bidii. Kama waamini kuwa utateswa na ghadhabu zilizo karibu kujaza dunia hii, basi utateswa na ghadhabu na hukumu. Kama waamini kuwa MIMI ni Mungu anayewatuza wale wanaonitafuta MIMI kwa bidii, wanaosikia sauti YANGU kwa makini na hufanya mapenzi YANGU na sio yenu, wanaotembea Nikisema tembea, wanaokimbia Ninaposema kimbia, wanaosimama Ninaposema simama, wanaozungumza Ninaposema zungumza, wanaonyamaza Nisiposema chochote au wasiofanya chochote hadi wasikie kutoka Mbinguni. Mwanajeshi huwa hafuati amri zake; yeye hungoja mkubwa wake kunena amri. Kwa hivyo ngojeni, ingawa jibu LANGU linachukua wakati kufika, litakuja. Vita vilivyo Angani vinaendelea. Sauti zake zimezuiliwa hadi sasa. Je, Manabii WANGU wangewezaje kuongea kama hizo sauti hazingezuiliwa, wote wangekuwa wamekwisha. Ni kwa ajili yenu Nimeacha vita hivi vya Angani viendelee. Mhuri wa waliokombolewa umetiwa mhuri kama shetani pia alivyoweka alama kwa wale walio wake.
Kwa hivyo, MIMI Baba yenu YAHUVEH Nimeweka alama kwa wale walio WANGU. Wanaompenda Mungu watakuwa Watakatifu zaidi. Waovu watakuwa waovu zaidi. Ole kwa ardhi hii kwa kuwa inatetemeka na kutikisika. YAHUSHUA anavyokaribia ardhi, sio anga tu inayotikisika lakini ardhi inatikisika pia kwa hofu kwa kuwa inajua maovu ambayo imetenda. Mitetemeko ya ardhi ni ardhi inayotikisika kwa hofu na itazidi na dhoruba zitazidi kuwa kali na lava iliyo milimani itamwagika kwa kuwa lava hiyo inapashwa moto na ghadhabu ZANGU! Inachemka vikali dhidi ya wapagani wa ardhi hii wanaokataa amri YANGU, wanaokataa tuzo la YAHUSHUA la pale Kalvari na wanaochukia yote ambayo ni Takatifu. Ardhi itatikisika tena sana Mwana wa Mungu anavyokaribia. Anga inatikisika na hasira za shetani na vita vinavyoendelea Angani. Anga ina maumivu kama mwanamke anayejifungua. Itakuwa ni kama nyota zinaanguka kutoka angani. Mkuu wa uwezo wa anga anatikisa anga, kwa kuwa shetani anajua.
“YAHUSHUA ANAWAJIA BIBI ARUSI WAKE, YAHUSHUA ANARUDI TENA!” Shetani lazima ayafanye maovu yake haraka kwa kuwa anajua wakati wake ni mfupi sana sasa. Anataka kuchukua nafsi nyingi kama atakavyoweza kwa kuwa anajua hii ndiyo njia ya pekee ya kumkwaza YAHUSHUA! Kwa kuwa Mwana WANGU alilipa gharama pale Kalvari ili shetani asikupeleke jehanamu naye. Marekani, ndio, kunakuja vita kwenye pwani zenu na nchi. Lakini Nimewalinda hadi sasa. Nimengoja Marekani KUTUBU na bado nchi hii inanihuzunisha MIMI. Inanikasirisha MIMI! Viongozi wa siasa hawana aibu au huruma na wanazidi kuwa waliolaumiwa. Watu wanaopigia kura hawa viongozi wa aibu hawana huruma wala aibu.
Badala ya kuzungumza kwa niaba ya utakatifu, wanapiga kura na kuwaingiza ofisini wapagani waovu. Marekani mnaye mliompigia kura. Wanaompenda Mungu na watakatifu wachache waliokuwa ofisini waliaibishwa mbele ya wote. Waliachwa uchi na kazi zao kuibwa kwa sababu walithubutu kuzungumza dhidi ya nabii bandia wa nchi hii na kwa sababu walisimamia maadili na utakatifu. Ole wao waliokuwa na chaguo la kupigia kura Watu wa Mungu lakini wakachagua wapagani na roho za mpinga kristo. Niliwaokoa Watu WANGU walioondolewa ofisini waliosimamia utakatifu ili wasiwe pale kwenye ikulu (white house) wakati taabu itakapotokea mahali hapo na ghadhabu ZANGU Nitazionyesha kwa wale wanasiasa waliolaumiwa. Kahaba, kumbukeni Sodoma na Gomora, ipo kwenye ikulu (White House). Nitawabariki wale waliopiga kura dhidi ya waovu walio pale Washington D.C. na Nitawalaani waliopiga kura kwa maovu ya usherati na kura zao.
Nitawaibisha Marekani mbele ya dunia nzima. Viongozi wenu watalia kwa uwazi kwa yale ambayo Nitayafanya. Lakini sio Watoto WANGU, mtajua nini cha kufanya wakati utakapofika. Sababu kuu kuwa hamjui bado ni kwa sababu bado wakati haujafika. MIMI huwa siji mbele ya wakati wala sichelewi, MIMI Bwana Mungu wenu huwa nafika kwa masaa kamili, nyinyi hufikiria tu Nimechelewa. Masaa YANGU ni kamili. Hamwezi kuenda mbele YANGU wala nyuma YANGU lakini lazima muwe kando YANGU. Watoto WANGU wote walio wa YAHUSHUA wanatamani kurudi KWAKE kote duniani, wananisikia MIMI, sauti ya Muumba wenu, Mungu mkuu “MIMI NIKO.” Kwa niaba yenu Nitatuma miujiza kama vile hamjawahi kuiona mpaka sasa. Kwa kuwa mwaona Mwana WANGU YAHUSHUA MASIHI wenu anakaribia ardhi hii, kama vile huyu handmaiden Sherrie Elijah [Elisheva Sherrie Eliyahu] amewaambia hapo awali, Ninarudia tena.
Ni kweli kuwa Gabrieli tayari amepuliza tarumbeta yake. Sauti yake imezuiliwa na vita vilivyo Angani lakini tarumbeta yake Gabrieli itasikika na sauti yake kuachiliwa. Miili yenu itabadilishwa ghafla, kufumba na kufumbua. Waliokufa katika YAHUSHUA (Kristo) watafufuka kwanza na nyinyi mliobaki mtakusanyika kukutana naye YAHUSHUA hewani. Lakini mtatembea kwenye miili yenu yenye utukufu mkihubiri kwa niaba YANGU, mkionya WASICHUKUE Alama ya Mnyama kwa siku 40. Basi mtakua mashahidi WANGU wakuu kwa Neno LANGU. Lakini kwa wale ambao hawatabadilika watakuwa na huzuni kwa sababu watajua kuwa lazima wapitie Dhiki Kuu.
Alafu mtakuja NAMI kunikuta MIMI hewani na pamoja tutakutana hewani. Bibi Arusi WANGU hawatapatwa na ghadhabu ZANGU. Shetani atatupwa papa hapa ardhini kwa hasira kuu pamoja na mapepo yake wakianguka kutoka angani. Ole wao watakaokuwa hapa ardhini. BIBI ARUSI WANGU WATAFURAHIA KWA KUONEKANA KWANGU! Wale waaminifu waliozungumza na kuamini kuwa YAHUSHUA hatawaokoa BIBI ARUSI WAKE kabla ya Dhiki Kuu watashangaa YAHUSHUA atakapokuja wakati wasiotarajia Bwana Arusi kuwajia Bibi Arusi WAKE! Wale ambao wameamua kuwa lazima wapitie Dhiki Kuu watakuwa wamelala Mwana WANGU YAHUSHUA atakapokuja na kuenda na Bibi Arusi wake usiku wa manane, miili yao ya binadamu ikibadilishwa kuwa miili isiyokufa.
Alafu hawa, waliokuwa wanalala na wana uhakika kuwa walikuwa sawa, wataona kuwa walikosea. Watalia na kuomboleza kuwa njia yao ya kuepuka ghadhabu zinazokuja imepita. Lazima watangojea miili yenye utukufu. Wapagani watakasirika na kumlaani Mungu Mwenyezi na chuki kuu itainuka dhidi ya waaminifu wa YAHUSHUA! Kwa kuwa baada ya siku 40 ya Watakatifu wenye Utukufu kuhubiri na kuonyesha walichokosa, huzuni kuu na hasira kuu itainuka. Ombeni sasa kuwa mtapatikana kustahili kuitwa Bibi Arusi wa Mwana WANGU YAHUSHUA. Ombeni kuwa mtapatikana kustahili kuepuka saa hii ya jaribio hili la kuchukua Alama ya Mnyama.
Niiteni MIMI sasa katika Jina la YAHUSHUA. MIMi ni Baba wa Mbinguni ambaye hatawafukuza wale wanaosikia maneno haya na kuyapokea na kuyatii. Kwa utukufu WANGU pekee Nimezungumza nanyi, kwa hivyo hamwezi kusema kuwa sikuwaonya. Kuna tu mwombezi mmoja, Safina moja tu ya usalama na ni Jina la YAHUSHUA ha MASHIACH! Kama Nuhu alivyokuwa juu ya maji ya ghadhabu ZANGU, kwa hivyo amini na nyinyi pia mtakuwa juu ya ghadhabu ZANGU mkitazama kutoka Mbinguni salama kutokana na Dhiki Kuu. Wale wanaosisitiza kunijaribu MIMI na kuamini sitawaokoa Bibi Arusi WANGU kabla ya Dhiki Kuu, wakiamini kuwa sitampata yeyote anayestahili kuepuka saa hii ya jaribio, kuna matumaini kwako wewe pia. Amini kuwa Nitawalinda kama Lutu na MNITII MIMI na pia nyinyi mtaona Mbinguni.
Ninawaonya kwamba katika wakati huo mtatembea kwa imani na sio kwa kuona, zaidi kushinda wakati mwingine katika historia. Hakuna yeyote aliye vuguvugu katika imani atakayeweza kustahimili ghadhabu ZANGU. Kama mwaona vigumu sana sasa kuwa na imani, je, si itakuwa vigumu zaidi kwenu nyinyi kuniamini kuwa Nitawaokoa na imani kubwa itakufa na watapeana maisha yao kama shahidi, watapendelea haya kuliko kuendelea kuishi kwa imani pekee. Watakatwa vichwa kwa imani yao na kupendelea kifo kuliko kuteswa. Lakini wale watakaokataa Alama ya Mnyama katika Dhiki Kuu wataokolewa.
* * * * * * *
Imezungumzwa katika upako wa RUACH ha KODESH, aliyeaminiwa na neno hili, Mtoto wa YAHUSHUA, Shujaa, Bibi Arusi, Mhubiri Sherrie Elijah (Elisheva Sherrie Eliyahu) Tarehe 11/15/98 Saa 12:00 mchana, Jumapili.
Enda Kwenye Sehemu Ya Pili Ya Unabii Huu
Someni Kuhusu Cloning Hapa
* * * * * * *
|