UNABII WA 4
MSIWE NA SHAKA WAKATI
AMBAPO HAMNIHISI KANDO YENU!
Alipewa Rev. Sherrie Elijah Februari
5, 1997
*******
Leo
tu nilisema “YAHUVEH, ni nini kinachofanyika
hadi siwezi kuhisi kuwepo kwako
Hatufuati hisia zetu, hisia hutudanganya,
lazima tufuate imani yetu. Kwa kuwa wale walio
wema wataishi kwa imani pekee, sio hisia. Lilikuwa jambo kuu tulipokubaliwa
kuhisi kuwepo kwake, lakini kuna kitu kinachobadilika katika eneo ya kiroho na
ingawa YAHUSHUA bado yupo nasi, ni kama amelala kwenye mashua, na tunaangamizwa
na dhoruba za maisha na sisi ndio wanafunzi wanaosema, “YAHUSHUA, amka kabla
tuangamie”. Alafu YAHUSHUA huamka na
kusema, “Enyi mlio na imani kidogo” na kukemea dhoruba. Bado ninamngoja akemee
dhoruba nzito ambazo nimekabiliana nazo kwa muda mrefu sasa inaonekana. Tunajua
kuwa kuna wakati uliotengwa kwa ukombozi wetu. Ninavyonakili haya ninapata
upako. Nimeacha na kuomba katika Roho na nitafanya jambo hili wakati mwingine,
baada ya kuchukua mamlaka juu ya shetani. Kama YAHUVEH kweli anataka kuzungumza
kupitia mimi tena, atafanya vivyo hivyo. Nakupa mikono yangu YAHUSHUA na akili
yangu, masikio yangu ya kiroho na macho yangu ya kiroho.
Tafadhali zungumza nami sasa ili niwape neno
la kumpa moyo ndugu yangu mdogo. Katika jina lako YAHUSHUA nauliza na kwa nguvu
za RUACH ha KODESH, kupitia damu ya YAHUSHUA ha MASHIACH wa Kalvari. Je, kuna
neno ambalo unataka kuzungumza kwa watu wako? Kama ndivyo RUACH ha KODESH paka
mafuta mikononi mwangu sasa kama ulivyozungumza kupitia upako huu usio wa
kawaida katika jumbe (3) za unabii zilizopewa mbeleni. Kwa kuwa unawajali watu
walio katika Mtandao ambao hawana njia nyingine ya kusikia ujumbe wako kwa
uwazi ili waelewe na ghasia zisiwakamate katika udhibiti wa shetani. Upako
unanijia katika mikono yangu sasa na tena sauti ya YAHUSHUA inazungumza nami. Sifa
kwake YAHUSHUA!
******
Waambie mtoto WANGU; waambie siwezi tena
kushikilia hasira za Baba YANGU. Nimejaribu. Nimelilia huruma kwa wale
wanaochafua yote yaliyo Takatifu kwa makusudi; wale wanaokataa kufahamu kuwepo
kwa jambo kama dhambi. Wale walio katika mimbari wanaotoa visingizio kwa ajili
ya dhambi, je, hata kisingizio bora kinawezaje kufunika uweusi wa dhambi? Lakini
bado Ninapowaomba watubu, wageuke kutoka kwa dhambi, wananikejeli MIMI na
kusema YAHUVEH hajali, Anaelewa. Wanaambia Manabii na Mitume WANGU wanyamaze na
kuwaacha, wayaweke maneno yao kati ya wao wenyewe. Hawatawaruhusu kuongea
katika kanisa, na kuruhusu roho za ibada ya pepo chafu kuingia katika kanisa
hadi nabii hayuko salama akiomba. Hizi pepo mbaya hungoja, zikijua manabii waja
kutoa onyo ZANGU, na wanazuiwa na ndio, wengine hata huumizwa. Onyo likiwa kuu,
upinzani mkuu utatoka kwa adui.
Shetani anajaribu sana kuwanyamazisha
Manabii na Mitume WANGU na wale ambao wameambiwa waonye watu. Waonye juu ya
MUNGU katika Nahumu 1 inayosema YEYE huongea katika dhoruba na mitetemeko ya
ardhi. Waonye kuwa YAHUVEH ni MUNGU aliye na wivu na hataruhusu miungu nyingine
mbele YAKE. Waonye, kuwa ghadhabu yake YAHUVEH haifurahishwi virahisi. WAONYE!
Bado MIMI YAHUSHUA huwatuma Wajumbe WANGU kuwaonya na kama katika bibilia
wanapigwa na wengine hata wanauliwa. Nimezungumza kuhusu wapelelezi wa shetani
waliomo katika kanisa: hakuna yeyote anayesikiliza.
Ni wachache sana hata wanaodhubutu
kuwafichua. Nimewaonya kuwa shetani yumo katika makanisa na anapigania funzo la
uongo, roho za uasi, roho ya kudanganya kanisa kuwa dhambi si dhambi. Lakini
MIMI ni MUNGU MTAKATIFU na Ninadai nyote muwe watakatifu kama MIMI Nilivyo
MTAKATIFU. Nimeweka Roho YANGU ndani yenu ili mjue lipi ni ukweli na lipi ni
uongo. Dhambi ni nyeusi, sio kijivu, Utakatifu ni nyeupe na sio rangi nyingine.
Wengine sasa watamruhusu shetani kuyachukua haya na kutengeneza matusi ya
kirangi. Acheni jambo hili sasa, mnajua ni nini Ninachomaanisha. Ni nyekundu
pekee itakayoosha dhambi hii kutoka kwa akili zenu, na hii ni Damu ya YAHUSHUA
ha MASHIACH hapo Kalvari. Ninaonya sasa kuwa linalosababisha kuwepo KWANGU
kutohisiwa kama hapo awali ni kwa sababu Ninaomboleza. Ninalia kwa yale ambayo
lazima Nifanye hivi karibuni.
Je, walimsikiza huyu Nabii ambaye sasa
Ninamtumia wakati Niliwaonya kabla ya wakati kuwa uchina utaonja hasira ZANGU
kupitia mitetemeko ya ardhi, mtetemeko mkubwa zaidi bado haujatokea lakini
waja. Wamewaua Watoto WANGU wengi sana, na kuwatesa na kuwaweka jela Watoto
WANGU, Wajumbe WANGU, kwa haya, serikali italipa vikuu na nchi hii itararuliwa
na mitetemeko ya ardhi huku wakijaribu kuwagawanya Watu WANGU na kuwaongoza
mbali NAMI kwa hofu ya kuabudu kwa uwazi MUNGU ambaye hapo awali walimtumikia
na sasa wanaogopa kumtumikia kwa uwazi. Kama walivyogawanya Watu WANGU ndivyo
Nitakavyogawa ardhi yao.
Ninawalinda wale ambao ni WANGU, na
Ninajua nani ni WANGU. Hata Nimetingiza milango ya jela kama katika nyakati za
kale, ili wafungwa waliohubiri injili, kwa kuwa hili ndilo lililokuwa hatia yao
pekee, wakuwe huru. Naja kwa njia kuu na mwaka huu ingawa vituo vya habari vya
nyumbani kwenu vinakataa kukubali ule uharibifu na hasira ambayo MIMI Nishaonyesha mwaka huu. Nitaanza kuwaonyesha kwa njia ambazo
hawataweza tena kudharau. Wanalaumu mama ardhi. Kuna Muumbaji mmoja tu na MIMI
ndiye Baba wa viumbe vyote. MIMI NIKO AMBAYE NIKO. Hakuna mwingine. MIMI sigawi utukufu WANGU na mtu
yeyote kama vile mama ardhi. Nimetuma onyo katika vipindi vya televisheni,
ndio, mwamba amelia, lakini je wanasikiliza, ni wachache sana, wachache sana. Msifikirie
kuwa Ninafurahia kwa haya ambayo lazima Nifanye kwa sababu Sijafurahia, lakini
lazima Niyafanye, kwa kuwa watoto wanafikiria sasa wanatawala mzazi.
Volkano kadhaa zitalipuka wakati mmoja,
itakuwa moto WANGU nyekundu itakayomwagika na kuonyesha
hasira ZANGU. Ni wachache ambao wanajaribu kuwa Watakatifu. Wanadhani
kuwa MIMI Nitaafikiana na dhambi zao. Kama tu wangeweza kutubu. Kama tu
wangefahamu kuwa MIMI ni MUNGU ambaye habadiliki. Mimi niko sawa jana, leo na
milele. Ni lazima nyinyi mbadilike, sio MIMI NIKO AMBAYE NIKO’ MKUU, ‘MIMI NIKO
AMBAYE NIKO’ na siombi msamaha kwa lolote Ninalofanya. Simpi majibu yeyote.
YAHUVEH mkuu amekasirika na hata Mwana WANGU, yule Niliyewapa kama Mwokozi
hawezi kuzuia hasira ZANGU tena. Nipo karibu kuonyesha hasira ZANGU,
jihadharini nyote mlionikejeli MIMI na neno la YAHUSHUA na kuwanyamazisha wale
walio na upako wa wajumbe WANGU na kuwatusi, kuwatesa na kuwaweka jela katika
jela za binadamu. NIMEKASIRIKA! Niliwaonya Sodoma na Gomora na Ninawaonya sasa
tena. Dunia hii ni Babeli wa kisasa, dunia hii. MIMI ni Muumbaji anayeamuru
Utakatifu; Niliweka ndani ya kila binadamu mahali panapotamani Utakatifu na
uhusiano na Muumbaji wao.
Sitatuma tu volkano zitakazolipuka moja
baada ya nyingine, lakini Nitatingiza ardhi hii kama mzazi anavyotingiza mtoto
mtundu. Sitatingiza tu sehemu moja ya ardhi hii moja kwa moja, lakini sehemu
nyingi za ardhi wakati mmoja. Nitatuma miguu YANGU yatakayokanyaga ardhi kwa
hasira. Kwa kuwa hasira zangu ni kuu kwa wale waasi walionitingizia ngumi zao usoni
MWANGU, na kusema wanakataa kutii kitabu na sheria zilizoandikwa elfu za miaka
kale. Kwa wale wanaotumia JINA LANGU kama tusi. Kwa wale wanaokejeli Damu ya
MWANANGU iliyomwagwa kwa sababu yao pale kalvari. Nitatuma vimbunga kuonyesha
machozi iliyonitoka juu ya watoto WANGU wasiotubu na juu ya wale Niliowaumba
waliofaa kuwa Watoto WANGU lakini wakakataa kunikubali MIMI kama Baba.
Wale waliojiingiza katika mambo yasiyo
takatifu, na hata hawakujaribu kunifurahisha MIMI au kunisaka MIMI. Mafuriko
yatakuja na kufunika sehemu zote za ardhi wakati mmoja. Hii itakuwa ishara ya machozi YANGU, kwa kuwa
wengi wamechagua Jehanamu juu ya Mbinguni. Wale waliochagua shetani juu ya
YAHUSHUA. Nitazituma tufani na itakuwa ngumi YANGU inayotuma upepo unaopepea. Sitayaonyesha
haya katika sehemu moja tu, mkiziona zote zikija pamoja mtajua Ninaongea na
Nimekasirika na hasira ZANGU hazifurahishwi virahisi.
Kumekuwa na mitetemeko ya ardhi, mafuriko,
tufani, vimbunga hapa na pale duniani lakini mkiziona moja baada ya nyingine
zikifuatana kwa mtindo huu, nyingi kwa wakati mmoja basi mtajua huu ndio wakati
Niliowaonya juu yake. TUBU SASA, kabla wakati haujaisha. Nimekuwa
nikizishikilia hasira ZANGU kwa muda mrefu sasa. Kwa sababu ya MWANANGU na
maombi YAKE kwenu nyinyi watu, Nimeshikilia ghadhabu YANGU. Lakini shetani
ananikejeli MIMI na kunidharau MIMI kwa sababu Sijawaadhibu. Anatumia viumbe
vyangu kunikejeli na kunidharau MIMI. Midomo Nilizoumba. Midomo nilizozipa
upako wakati mmoja. Ndio, hata katika kanisa ZANGU Ninakejeliwa huku neno
Takatifu linabadilishwa kufuata umbo la mwanadamu. Sio umbo la MUNGU Mtakatifu.
Wanafunza kuwa ushoga umetoka KWANGU,
SIO DHAMBI, ni kosa la YAHUVEH, ni kasoro ya kuzaliwa.
Roho za kudanganya na kuchanganyisha zinatoka
kwa wale walio na umbo la utakatifu, lakini hawana utakatifu ndani yao. Nitapambana
MIMI Mwenyewe nao hawa wachungaji waovu kwa njia ambazo zitawaonyesha watu kuwa
MIMI sio MUNGU wa kukejeliwa. MIMI sio MUNGU wa kukasirishwa ovyo. Nitapambana
vikali na utawaona wakianguka wakifa mimbarini, wale wanaokubali vitu hivi na
kutoa mimba. Niliwajua nyote kabla muwe tumboni mwa mama zenu. Niliumba na kuunda
na kupanga vile Nilivyotaka maisha yenu yawe. Ilikuwa chaguo lako kuwa vile
MIMI nilivyotaka. Usinilaumu MIMI, kwa kuwa Nilikutakia mazuri tu. Hata nyinyi
mlioteseka, na kuishi maisha yaliyokaa ni kama hayakuwa yamebarikiwa,
Nitawatumia na Nimewatumia kwa Utukufu WANGU, katika mateso yako umenipa MIMI
Utukufu wengine wakiona kuwa bado unanisifu MIMI, kunitumikia MIMI na kuniabudu
MIMI. Upako WANGU unamwagwa katika maisha yenu, hata kushinda wale wanaoishi
maisha yao yaliyo na matatizo machache. Maisha yako hayajapewa baraka za
wengine, lakini si kwa sababu Sikupendi kama wengine, ni kwa sababu kama
YAHUSHUA alivyowekwa katika ardhi hii kuteseka juu ya wengine, kwa hivyo hata
wewe pia, na tuzo zako zitakuwa kuu mbinguni kama utabaki mwaminifu mpaka
mwisho.
Watoto WANGU wengine wamejawa nyongo
wanavyoona wapagani, wale ambao hawajawahi kupiga goti, au kuomba wakinipa MIMI
asante, na Watoto WANGU husema huyu ni MUNGU wa aina gani? Nawaambia, msiwaonee
wivu matajiri ambao hawanikubali MIMI, au waovu. Inakaa ni kama wanazo baraka
zote maishani kwa kuwa haya ndiyo yote ambayo watawahi kupata, na alafu itakuwa
laana ya milele, na jehanamu ya milele na mateso. Walitupilia mbali maisha ya
milele Mbinguni kwa miaka michache hapa ardhini ambapo walitenda dhambi za kila
aina, sanasana dhambi ya kufikiria kwamba hawahitaji Mwokozi.
Lakini wewe, ukibaki mwaminifu utaona
Mbinguni na kwa wakati mfupi kwenye ardhi utaona mateso, chuki na matusi,
lakini usijawe na nyongo, usiende mbali NAMI. Ni heri uje KWANGU. Angalia
Nilivyo Baba aliye na upendo. Nimewaonya mapema ili wakati vitu hivi
vitakavyokuja kwenye ardhi mtakuwa mshaonywa mapema, ili muweze kutubu na
kuwaonya wengine kabla hasira ZANGU hazijaonekana. MIMI hutuma Manabii WANGU
kuonya kabla Sijatuma uharibifu. Lakini nyinyi mnaonipenda, kunitumikia MIMI
kwa uaminifu na kujiosha katika Damu ya YAHUSHUA ha MASHIACH ili mbaki
watakatifu mbele YANGU, hamna chochote cha kuogopa katika wakati huu,
hamtapatikana kama hamko tayari.
Nitalinda yote ambayo ni YANGU, na
Ninajua yapi ni YANGU. Ninajua kila moja ya nyoyo zenu zote, na Ninazo roho
zenu mikononi MWANGU kwa kuwa mmenipa MIMI maisha yenu na roho zenu
mlipomkubali YAHUSHUA kama Bwana na Mwokozi. Mmeleta miili zenu kama dhabihu
hai kwa utukufu WANGU. Sijawakasirikia. Ninawapenda, na Nitawafunika na
kuwalinda. Ndio, hata mkiona dunia imetingizwa katika hasira YANGU, Nililie
MIMI. Nitakuwa papo hapo kuwakumbatia.
Sababu linalofanya wengi wenu msihisi
kuwepo KWANGU sasa, si kwa sababu yenu. Ndio, hata huyu Ninayemtumia kuzungumza
maneno haya na hajui ni nini ataandika kutoka neno moja hadi lingine
linalofuata, ana tatizo kuhisi kuwepo KWANGU tangu Nilipomtumia kuwaonya watu
WANGU mwisho. Nimempa upako huu usio wa kawaida kushika tahadhari ya watu
WANGU, ambao hangekuwa na njia nyingine ya kuwaongelesha, kwa kuwa
Nimewatawanya kote duniani. Manabii WANGU na Wajumbe watasikia, na wanazo masikio
za kiroho na macho na mdomo jasiri kuwaonya watu ambao hawasikii.
Nawaambia tena Manabii na Watoto WANGU,
msiwe na shaka na kufikiria Nimewaacha wakati ambapo hamwezi kunihisi MIMI
kando yenu. Sijaenda pahali popote, bado Nipo hapa; Nimekimya tu kwa kuwa huu ndio
utulivu kabla ya dhoruba. MIMI huwa kimya kabla Niachilie hasira ZANGU kwa kuwa
Ninajaribu kushikilia ghadhabu zangu, lakini tangu mafuriko ya Noah imekuwa
ikipanda na tena Nina huzuni wakati Ninapoona yote Niliyoyafanya, hata kumpa
MWANANGU wa pekee kama Dhabihu. Abrahamu alikuwa na dhabihu nyingine; Niliwapa
MWANANGU, kuwa Mwokozi wenu. Ni wachache sana ambao watamkaribisha YEYE.
NIMEKASIRIKA! Niliwapa Mwili WAKE ili mponywe. Ni wachache sana ambao wataamini
kuwa kuna uponyaji kwa sababu ya vile viboko viliyolazwa kwenye Mwili WAKE. Niliwapa
Damu YAKE, ili msamehewe. Ni wachache sana ambao watakubali zawadi hii pale
Kalvari. Niliwapa maisha YAKE, ili mwokolewe. O, hii ndiyo sababu inayofanya
mhisi upungufu wa kuwepo KWANGU. Hamjawahi kukasirika na watoto wenu hadi
mkapoteza hamu ya kuongea, kwa hofu ya hasira zako mwenyewe? Hamjawahi kuhuzunishwa
sana hadi mkataka tu kuwa kimya au kukasirika sana hadi mwataka tu kuwa kimya. Ukiogopa
kuachilia hasira zako kwa hofu ya mambo ambayo yanaweza kutokea. NIPO HAPO!
Sijawakasirikia wale wanaotamani kuhisi
kuwepo KWANGU. Nimewakasirikia wale ambao hawajahisi kuwa Niko kimya, na kuwepo
KWANGU hautamanwi. Kwa wale ambao mnahisi kuwepo
KWANGU haupo, na mna huzuni kwa sababu ya haya, na mnatubu na kushangaa ni nini
kibaya mlichofanya, sasa Ninazungumza kupitia
Handmaiden WANGU na kuwaambia nyinyi, mmefanya yote ambayo ni sawa, ndio sababu
mnahisi kukimya KWANGU na hamhisi kuwepo KWANGU. Sizungumzi na wale walio
katika dhambi na hawajawahi kunijua MIMI au kunitamani MIMI, kutoka mwanzoni. Mnajua
ni nani Ninaowazungumzia. Ni Watoto WANGU tu ambao wataelewa. Kwa wale kati
yenu, ambao mlikuwa Watoto WANGU lakini mkawa na uvuguvugu, rudini sasa
Nawaomba. Nitamani MIMI na kuweni na hamu ya kuisikia sauti YANGU tena. Sijawaacha,
ni nyinyi mliotenda haya.
Tubuni kufunza uongo. Tubuni kufunza kuwa,
dhambi sio ukosefu wa utakatifu na kuwa hamna kitu kama dhambi, kwa kuwa
YAHUVEH anayependa wote atawasamehe kwa kila mtakachofanya. Hakuna haja ya
kutubu, au kugeuka kutoka kwa dhambi. Hamwoni kuwa huu ni uongo wa shetani. Shetani
husema, “hauhitaji Mwokozi, zawadi YANGU, MWANANGU mpendwa YAHUSHUA.” Hamwoni,
Ninalia Ninapofikiria gharama Mpendwa WANGU aliyolipa kwa sababu yenu? Mkisema ya
kwamba hamna kitu kama dhambi, na kila kitu kinakubaliwa NAMI kwa kuwa MIMI ni
MUNGU ambaye hajali tena ni nani ulalaye naye au nini ulalacho nacho.
Ni damu ya nani asiye na hatia inayomwagwa?
Hata wale ambao hawajazaliwa, ‘si dhambi kuwaua kama hauwezi kuwaona’. Hata
wakati mnapoweza kuwaona kama wanawaua watoto hawa wasio na hatia ili kuokoa
maisha ya wengine, haijalishi, wao ni muhimu kwa kitu fulani. Huu ni uuaji na
hii ni dhambi. Wahubiri mtanijibu MIMI nyinyi wenyewe kwa kuwa mmesema,
mnanifanyia kazi MIMI, lakini mmekuwa mkifanya kazi dhidi YANGU. Ushoga ni
DHAMBI! Kutoa mimba ni DHAMBI! Uuaji ni DHAMBI! Uasi ni DHAMBI! Uchawi ni
DHAMBI! Nyote mnajua DHAMBI ni nini! Someni amri 10. Wahubiri, Mitume, Manabii,
Walimu, Wainjilisti, rudini kufunza kuwa dhambi ni dhambi. Ni mtenda dhambi
aliyetubu tu ndiye atakayesamehewa.
Hamna tena, kila mtu fungeni macho yenu
hatutaki kumwaibisha mtu yeyote, ili waweze kuinua mikono yao na kumkubali
YAHUSHUA ha MASHIACH kama Mwokozi wao. Je, mnaelewa vipi jambo hili lilivyonikasirisha?
Tangu lini ikawaje ni aibu kuja kwake YAHUSHUA kwa kusamehewa kwa dhambi zenu. Hakuwezi
kuwa na Wokovu bila kuungama dhambi zako kwa wengine. Kukiri kwa dhambi
hubadilika kuwa wokovu. Nawaambia msiponiungama MIMI mbele ya binadamu,
YAHUSHUA hatawaungama mbele YANGU, Baba. Watoto WANGU, Wainjilisti WANGU,
Manabii, Wachungaji, Walimu na Mitume wamefanya hivi.
O, uchungu huu. Huzuni niliouvumilia juu
ya haya. Mnafikiria hawa watu ambao walikuwa na aibu kuu ya kusimama na
kuungama kuwa wanahitaji Mwokozi, watabaki waaminifu kwa muda mgani? Papo hapo
adui ataiba lile mbegu ndogo lililopandwa. Wale kati yenu, mliofanya haya,
TUBUNI! Kataa kufanya haya tena kwa uwazi. Kwa kuwa mtajibu kwa zile roho
zilizopotea ambazo zingekuwa zimeokolewa. Wale kati yenu mlionifanya MIMI kukaa
kama MUNGU wa mchanganyiko mnaposema wanaweza kuinua mikono yao kisiri na
kusema YAHUSHUA njoo moyoni mwangu, bila kuwafunza kwanza lazima walie na
kutubu dhambi zao, na kugeuka kutoka kwa dhambi hizo. Kubali kumweka YAHUSHUA
kwanza maishani mwao, na kufuata Utakatifu, sio ukosefu wa utakatifu. Mtanijibu
MIMI mwenyewe pia, na kwa wale wote waliofikiria, kuwa ukishaokolewa
umeokolewa, sasa tunaweza kufanya chochote kile tunachotaka kwa sababu dhambi
zetu zote zimefunikwa. Hamkuwafunza, ‘kwa nini mnasema mnanipenda MIMI na
hamnitii MIMI?’
Wale kati yenu mliotumia roho za
udanganyifu kupata watu kuinua mikono yao kama macho ya kila mtu imefungwa
alafu kuwaita waje wasimame mbele ya watu baada ya kuwafanya waamini kuwa
wanaweza kufanya haya kisiri. Mmewaonyesha kuwa YAHUVEH ni MUNGU wa
mchanganyiko na udanganyifu. MIMI SIO! Kwa haya mtalipa, msipotubu. Ndio, kabla
ardhi haijaanza kutingizika, hata sasa Ninatingiza na kuwagawa wasio waaminifu
na walio waaminifu katika zile zinazofaa kuwa Kanisa ZANGU, Hekalu ZANGU. Ninazungumzia
sehemu za kukusanyika sasa kwa kuwa Kanisa na Hekalu za Kweli ni watu WANGU.
Lakini katika mijengo ya kanisa mtaona ni
nini kinachofanyika kwa wale wanaowachanganya Kondoo WANGU. Au wale waliotaka
kuwa kondoo lakini wakabadilishwa kuwa mbuzi, kwa kuwa mchungaji mwovu ni mbwa
mwitu aliyetumwa kati ya Kondoo WANGU kuwaangamiza kwa ukosefu wa maarifa na
utambuzi. NIMEKASIRIKA! Katika mijengo ya kanisa mshaona mgawanyo ukianza.
Ninafichua adui kati ya kambi zenu. Tahadhari, simama, angalia, na sikiza sauti
ya RUACH ha KODESH. Tena endeleeni kuniita MIMI na kusema ninatamani kuwepo KWAKO
kwa kuwa hawa ndio wale waliozoea kuhisi kuwepo KWANGU na waliozoea kusikia
sauti YANGU kila siku na sasa wanahisi kunyamaza KWANGU.
Lakini Sitabaki kimya wakati wote
Wapendwa WANGU, ni kwa muda mfupi tu ambapo mtahisi huzuni WANGU, na lazima msifuate
hisia zenu kwa kuwa hayo ni ya mwili. Lazima mfuate imani yenu kwa kuwa hii ni ya
Roho. Siku hii Nimechagua kuzungumza kupitia huyu Handmaiden, msigombane kati
yenu na kusema, “Kwa nini YAHUVEH alizungumza kupitia mwanamke au kuweka upako
mikononi mwake.” Nawaacha na haya, Nachagua kumtumia yeyote Ninayechagua
kumtumia, na sijibu binadamu yeyote na kama Ningeweka upako mdomoni mwake pekee
kama alivyozoea, na singeweka upako mikononi mwake kwenye kibodi, je, mngekuwa
mmenisikia MIMI Nikizungumza ujumbe huu kupitia kwake siku hii? Mmejijibu
maswali yenu.
Sasa tafadhali onya watu, ingawa katika
nyakati za Noah wengi hawakusikiza. Bado, msiwe na damu mikononi mwenu kama Ezk
3:17-21 husema, “Msiwache damu ipatikane mikononi mwenu.” ONYA WATU! Bado kuna
muda mfupi uliobaki, kwa ajili ya MWANANGU Nimekuwa na huruma kwa watu, lakini
wakati wa kulipiza kisasi na wa hukumu unakaribia haraka. Waonye, na mnitafute
MIMI kama bado Ninaweza kupatikana. Tia maanani tarehe hii na mwangalie matukio
katika dunia, 2/25/1997. Nimemkataza Handmaiden WANGU, Sherrie Elijah,
kubadilisha hata neno moja Nililolizungumza. Ingawa anajua si wote
watakaokubali yote Niliyoyazungumza.
Tena, Ninawaonya wale walio maadui WANGU
lakini hujifanya kuwa hao ni rafiki ZANGU, akina Yuda jihadharini, kwa kuwa
mnapotafuta kumwumiza huyu mjumbe mnamwumiza yule aliyemwumba na kumpa upako. Mtakuwa
wa kwanza watakaohisi ghadhabu YANGU na mtajua kuwepo KWANGU kwa njia ambazo
hamngependa kujua. NIMEKASIRIKA, na nyinyi mlioniomba MIMI kuzungumza mmesikia
sauti ya upendo, uhakika, huzuni, na hasira kuu. Mmesikia sauti ya YAHUVEH
Mkuu, ‘MIMI NIKO’ akizungumza kupitia chombo kilichopasuka cha udongo siku hii.
Ombea wale wote ambao umejaribu kuzifikia nyoyo zao, na bado hunisukuma MIMI
mbali. Omba watubu leo kwa kuwa kesho wakati unaweza kuwa umepita.
Alipewa Rev. Sherrie Elijah katika siku
ya 2/5/1997
*******
Ndugu Noel, nimemsomea mwanangu mwasi
haya, na nikasema kutakuwa na watu kote duniani watakaokuwa wakiomba na
kumtafuta YAHUVEH kuona kama nilichoandika ni ya YAHUVEH. Je, kweli ilikuwa
YAHUVEH Baba aliyezungumza kupitia kwangu katika upako wa RUACH ha KODESH? Haya
yatajaribiwa na kuthibitishwa na manabii, wachungaji, mitume, walimu,
wainjilisti. Kabla wathibitishe jumbe zile zingine za kiunabii za mwaka huu
alizonipa YAHUVEH, sasa nakuuliza mwanangu, hii ilikuwa sauti ya YAHUVEH
iliyozungumza kupitia kwangu? Na thibitisho bora kwangu mimi ilikuwa wakati
ambapo mwanangu alisema, “Ndio.”
Sifa kwake YAHUSHUA! Nilimwambia kuwa
bado kuna matumaini. Kwa kuwa hata kijana mwenye uasi anaweza kusikia sauti ya
YAHUVEH. Hii ilikuwa jaribio kuu na sina shaka kuwa YAHUVEH mwenyewe
alizungumza maneno haya ili niyaandike siku hii. Tafadhali nakili haya na itume
kwa kila mtu RUACH ha KODESH atakuambia umtumie. Ipeleke katika kanisa yako,
hata kama hawatasikiza.
www.allmightywind.com
www.almightywind.com
Contact AmightyWind