UNABII 54
SASA NDIO WAKATI!
�Kaza Fikira (kaa fokasi), Tii Mkuu Wako NA Fuata Amri Zangu Sasa!�
Ujumbe Ulipokelewa Aprili 5, 2002
Umeandikwa/ Umesemwa chini ya upako wa RUACH ha KODESH kupitia Mtume Elisabeth Elijah (Elisheva Eliyahu)
Hii inatoka Unabii 105, YAHUVEH Alisema ujumbe huu uwekwe katika kila Unabii kutoka sasa: Nilikuonya kitambo Elisabeth(Elisheva) kutoita Huduma baada ya jina la mwanaume au mwanamke hata kabla kuwepo na huduma. Niliweka ndani ya roho yako kwa kuwa hakuna lolote kwa haya ambalo limefanyika kwa mkono wako, hakuna lolote kwa haya ambalo limetoka kwenye kinywa chako. Limetoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH ambaYE amezaa. Limetoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASHIACH wako ambaYE amezaa. Limetoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako ambaYE amezaa. Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo. Ni kwa upepo wa SH�KHINYAH GLORY unaovuma kote duniani, Upepo Takatifu wa Uamsho, sio kwa pumzi yako au ingekuwa imefeli. (Isaya 42:8)
Julai 2010 MUNGU YAHUVEH pia alisema yaongezwe haya kutoka Mambo ya Nyakati ya 2 kabla ya kila Unabii:
2 Mambo ya Nyakati 36:16, �Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii WAKE, hata ilipozidi ghadhabu ya BWANA juu ya watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.�
*******
Hili ni somo watoto WANGU ambalo inapaswa mujifunze. Hili ni somo ambalo ni bora mujifunze vyema. Ninapomuambia (mtoto aliye na fokasi) kufanya kitu, anakifanya, na anakifanya mara moja (Waeb 12:9). Haangalii upande wa kushoto; haangalii upande wa kulia (Kumb 30:17-18; Is 30:21). Anabaki amekaza fikira kwa kazi iliyopo mbele yake. Hiki Mwanangu [Elisabeth (Elisheva) na watoto WANGU wote], hiki ndicho mnachopaswa kujifunza. Ninapokuambia ufanye kitu, sasa ndio wakati. Sio katika saa yako, sio katika dakika yako, sio katika sekunde yako, ni katika wakati WANGU. Ilichukua muda gani kuweka unabii wa Pasaka juu? Inachukua muda gani kuweka Neno lililonenwa juu? Sasa leo ninapeana ujumbe mwingine na itachukua muda gani kuiweka juu?
Nakuambia hili, Ninategemea kwako, Ninategemea Maneno ninayosema kupitia wewe kufikia Watu WANGU, kutia moyo Watu WANGU. Hivyo mnaNIuliza ni nini mnapaswa kujifunza. Ni lazima mjifunze kufanya vitu katika muda WANGU na sio katika muda wenu. Ni lazima mjifunze kutokengeushwa. NImeiweka ndani (2 Wakor 4:7). Kwa sababu yeye �[mwana aliyekomaa (Warum 8:17)] � anajua kazi iliyo mbele yake na anakaza fikira kwa moja na vikengeusha-fikira vinapokuja kwa upande wa kushoto au kulia, anajua kuvikemea (2 Tim 2:12-13; Waebr 3:12-13). Anajua sio MIMI ninaYEvituma. Kwa hivyo hili ndilo somo, Wanangu, mnalopaswa kujifunza. Endeleeni kuNIomba, kweli, lakini lazima mujifunze kutii.
Na mwanaume ambaye nilituma njia yenu, yeye ni Mwislamu aliyegeuka Mkristo. Alikuwa ni mmoja ambaye anatafuta. Nawauliza hili swali: Vipi unavyokomboa mbegu mbaya? Vipi unavyokomboa tendo baya? Ni kuipanda kwenye mchanga mzuri. Msifukuze wale ambao NInawatuma hata kama mnafikiri wao ni walaghai. Kuna somo la kujifunza katika hili. Wakati ujao ipeleke kwa watatu na sio kwa mmoja [k.m. pata thibitisho.]
Nawaambia hili, lazima muwape wengine nafasi ya kuwabariki. Ni wangapi hawajui kwamba mko katika ukosefu? Mnajuaje kwamba sitawainua [wawasaidie]? Kuna wale ambao Nimewatumia hapo nyuma. Yule mjane wa Sarefati angejuaje kuwa Eliya wa Kale [kwa Kiebrania, Eliyahu] alikuwa na njaa ikiwa SIngemtuma kwake kumwambia. Na yule mjane wa Sarefati hangebarikiwa. Yule mjane wa Sarefati na mwanaye hawangeishi. Kama singemtuma nabii WANGU na hitaji ili [mjane] awe na fursa ya kulijaza, ili NIWE na fursa ya kudhihirisha kuwa MIMI ni YAHUVEH, MUNGU YULE YULE, jana, leo na milele. Sio kwamba uende kwao na kuomba. Ni Baraka kwao kuweza kupokea thawabu ambazo huja kwa wale husaidia hii huduma. Ni laana juu ya vichwa vyao Ninapowatuma kwao na maombi na mahitaji yenu na wanafunga maskio. Ni wao ambao siku moja wataingia uoga wanapoona hakuna yeyote katika wakati wao wa hitaji. Nimeiweka kwenye moyo wa Mwanangu na leo hamungesikia. Lakini leo sasa NInaisema. Wale ambao NItakuambia uwaambie. Hata dada yako Olga angesaidia. Wale wote hawangewaacha mwe bila maskani. Nawauliza hili, Watoto WANGU, YAHUSHUA Alipolisha wale 5,000, si Alisema, �Kuna nini karibu?� Na kukawa na yule mtoto wa uvuvi. Haikubidi wanafunzi [wa YAHUSHUA] waende na kumwomba yule kijana ashiriki chakula chake cha mchana? Na hakuItumia kuzidisha na kulisha wale 5,000 hata zaidi? Kwa hivyo ni mabaki ngapi yaliyobaki?
Msifanye kiburi sana cha kutosema hitaji lenu. Neno LANGU kwani halisemi, �Pea na itapewa kwako, iliyoshindiliwa na kutikiswa, ambapo watu wanalimbikiza hazina juu ya kifua chako?� Lakini watafanyaje hivi, Watoto WANGU, ikiwa hamuwaambii hitaji lenu? Mtajua ni nani wa kuamini. Na ikiwa hawatajibu, huu sio wajibu wenu. Wamelimbikiza laana juu ya vichwa vyao. Sikuwaambia WANANGU, kuwa hii huduma ni ya kipekee? Wanavyo wafanya ndivyo wanavyo NIfanya MIMI. Sio watu wanao waandalia mahitaji yenu. Lakini ni MIMI NInaongea kupitia watu. NInaongea na watu na shetani anaongea na watu.
Hili ni jaribio. Watafanya nini Nitakapokutuma? Je! Neno LANGU halisemi, �Kama utatoa japo maji ya kunywa kwa nabii, basi kuna Baraka.� Kwa hivyo nawatuma na mahitaji ya hii huduma. Nawatuma kuwajaribu wao. Je, watasikia sauti YANGU? Ikiwa hawatasikia, katika wakati wao wa hitaji, NItafanya kiziwi masikio YANGU kwa sauti yao. Nawatuma kwa wajane wa Sarefati ingawa wanajua wao sio mjane. Nawatuma kwa wale ambao wana njaa, ingawa hawajui wana njaa. Nawatuma kwa wale ambao wana kiu ingawa hawajui kuwa wana kiu. Iwapo hawajali kuwa unaenda njaa, basi Sitajali watakapokuwa wakienda njaa. Iwapo hawajali kama utakosa makao, basi Sitajali watakapo kosa makao.
Nitainua njia, lakini Nawaambia hili, Watoto WANGU, lazima mnyenyekee na kuifanya njia YANGU na sio njia yenu. NInapowaambia kufanya kazi, mnapaswa kuifanya mara moja. Hamuruhusiwi vikengeusha-fikira zaidi. Lakini mnaona, Nimekuwa nawajaribu kuona mlivyokaza fikira. [Kwa kiongozi] hukaa kwa kazi iliyo mbele yake- haachi akili yake kutangatanga mbele na nyuma. Tena Nawaambia, jifunzeni. Kwa maana hili sio hata jambo lolote anajisifu nalo [yaani hili sio jambo kiongozi anaweza jisifia (1 Wakor 1:31)] � hii ni zawadi YANGU NImetoa. Lakini ni chaguo lake kama atatii-na leo-[unapohisi] huzuni wa moyo WANGU, hiyo sio ari ya chini huo ni kuhuzunika kwa ROHO YANGU (Waebrania 3:12-15).
Tii na tii sasa. NIliwaambia mbeleni; nguvu iko katika neno lililosemwa, sio lililoandikwa pekee yake. Ni mara ngapi lazima NIseme jambo lile lile? Nakasirika wakati NInapo lazima kurudia. NAwasamehe, Watoto WANGU, mnapokosea. Lakini tu tubuni na muifanye njia YANGU na sio yenu. Kumbukeni, hakuna anayekuja kwenye hii huduma isipokuwa NImewatuma. Yule mwanamme NIliMtuma � kuna somo la kujifunza na mmejifunza leo. Sasa ombeni kwamba NIikomboe alafu muifanye njia YANGU.
[Yule ambaye ametiwa mafuta kulinda] hata yuajua wakati Elisabeth [Elisheva] yumo hatarini kabla yeye [Elisheva] kujua. Wakati mwingine anabishana na kuhangaika. Anajifunza kutambua anaweza amini NIliyetuma � hadi Farao muovu azamishwe na usikie huo ujumbe, ni lazima aendelee kumulinda kutokana na mashambulizi ambayo yaja tena. Wanakasirika saana, kwa vile kila kitu wanachofanya kinafeli na hamufai kuhisi bila nguvu. Kwa sababu nguvu zenu haziwezi kukomboa, lakini mkono wa YAHUVEH na YAHUSHUA wakomboa.
Kwa sasa watoto, baada ya kutii, leteni haya maombi tena hii leo. Kwa maana hakuna kitu kizuri NItakachowazuia. Je! Mnafikiri sijui mahitaji yenu? Na bado lazima muwe kama yule mwanamke ambaye alienda mbele ya hakimu, na wakati mwingine mNIombe zaidi ya mara moja. Muendelee kugonga hadi NIjibu. Muendelee kutafuta hadi mpate. Sababu kwa nini? Sina wajibu wowote wa kuwaeleza.
Kumbukeni MUNGU ni nani. MIMI NDIYE Mfinyanzi, nyinyi ndio udongo. Nawafinyanga, Nawavunja, Nawarejesha [kwa hali nzuri], Nawafinyanga njia YANGU. Najua ni kipimo kipi cha joto kinachohitajika. SItatia moto saana tanuru, hata hivyo Najua kipimo cha joto ambacho lazima kiwe ili mwe na imani ya kuNIamini. Kile ambacho mmepitia sasa kinahusu siku zijazo. Kama hamuwezi NIamini sasa, je, vipi mtaNIamini wakati huo? Je, mtafunza vipi wengine kuNIamini? Kuna sababu ya mambo ambayo yametendeka.
Shikilia kwa nguvu imani yenu Watoto WANGU na hata kutukie nini, msiachilie kwa maana kamwe SItawaacha na SItawatelekeza kamwe. Simama juu ya Neno LANGU, halitawaangusha. Wekeni kumbukumbu zenu kwenye Neno LANGU, halitawaangusha. Ficha Neno LANGU, halitawaangusha. Penda Neno LANGU, halitawaangusha. Amini Neno LANGU, halitawaangusha. Nena na milima ya deni na kusema, �Jizoeni katika Jina la MWANANGU YAHUSHUA. Amini na msitie shaka. Jifunzeni somo vema.
Kwa hivyo SIhitaji kurudia, kwa maana nyinyi pia mnajaribiwa, Watoto WANGU. SIiti waliohitimu, Nastahilisha walioitwa na mmeitwa. Pelekeni mahitaji yenu kwa [ndungu zenu]. Pelekeni mahitaji yenu kwa [dada zenu]. Pelekeni mahitaji yenu kwa Olga. Wapeni nafasi wawe Baraka. NItawaeleza [nyinyi] wale wengine. Ha[i]maanishi muifanye katika wakati wenu, hiyo inamaanisha ifanyeni katika wakati WANGU.
Kuanzia sasa lazima msikie haya maneno, sasa ndio Wakati. NInapopeana amri, ni kama jenerali anapopeana amri kwa mwanajeshi. Wakati wanajeshi wanasema, � Nitaifanya katika wakati wangu, katika njia yangu,� musidhubutu. Kwa hivyo jinsi gani zaidi mnapaswa kutubu kwa kuthubutu kuambia MUNGU wa Ulimwengu, �Subiri, Bwana, hadi nitakapokuwa na wakati.� Tena, Nasema, wanajeshi wanachukua amri; wanajeshi hawapeani amri. Nyinyi ni Watoto WANGU, lakini nyinyi ni wanajeshi WANGU. Nyinyi ni vyombo VYANGU ambavyo Natumia kufikia wengine. Sasa ndio Wakati! Sasa ndio Wakati! Kazia fikira kazi iliyo mbele yenu, hatua moja kwa wakati. Sasa ndio wakati! Sio dakika baada ya sasa! Sasa ndio wakati!
Mwisho wa Neno
Mtume Elisabeth Elijah (Elisheva Eliyahu)
Msamaha wetu, hasa kutoka kwa meneja wa tovuti [sasa, wa zamani], kwa maana sehemu za huu ujumbe awali zilikuwa zimeondolewa ambazo sasa zimerejeshwa katika huu ujumbe. Meneja wa tovuti [sasa, wa zamani] ameadhibiwa na YAHUSHUA kwa kufanya hili.