Ombi
La Wokovu.
Jinsi
ya Kuirithi Zawadi BURE ya Uzima wa Milele.
Je,
Ubatizo ni Jambo Muhimu Kwa Kupata Wokovu?
*******
YAHUSHUA
Mpendwa,
Nakukubali
sasa kama BWANA na MWOKOZI wangu, Wewe ndiye
Mungu ninayependa. Naamini ya kwamba ulilipa gharama ya dhambi zangu pale
Kalvari, ulikufa na kufufuka katika siku ya tatu. Nauliza uje moyoni mwangu,
nisamehe dhambi zangu, nioshe niwe msafi wa udhalimu wote. Pole kwa kutenda
dhambi, na nageuka kutoka kwa dhambi hizo. Asante kwa kunijaza na Roho
Mtakatifu wako, na kunipa hamu ya kukutumikia siku zote za maisha yangu, na
uishi maisha yako ndani yangu YAHUSHUA, ili Utukuzwe! Asante kwa kunipa hamu ya kusoma
Bibilia, na kunipa hekima niielewe. Asante kwa Kunipenda na Kuokoa roho
yangu, ikisababisha Imani yangu kukua, ili siku moja nitakuwa na WEWE Mbinguni.
Nijaze na Roho Mtakatifu wako sasa na niokoe kutoka kwa yule muovu katika jina
lako YAHUSHUA Naomba! Nisaidie YAHUSHUA kukumbuka wote wametenda dhambi na
kupungukiwa na Utukufu wa YAHUVEH, na ulikuja kutuokoa sisi watenda dhambi,
ndio sababu wewe huitwa MWOKOZI wetu. Amina.
*******
Soma
ombi hili alafu isome tena, wakati huu BILA maarifa ya kichwa lakini na moyo
wako wote, iamini kwa IMANI, na kumbuka YAHUSHUA SI Mungu Pekee, lakini YEYE ni
rafiki wako wa dhati! Anakujali sana, Anakupenda
sana. Jinsi
vile ulivyo. Anachukia Dhambi, lakini Anakupenda WEWE, mtenda dhambi!
YAHUSHUA
alilipa gharama ya dhambi zako, sasa hufai kujisikia kama
mwenye hatia au aliyehukumiwa tena! Ungama dhambi zako kwa YAHUSHUA. Zitaje,
alafu mwambie pole, muulize akusamehe! Dhambi zako zote za zamani na sasa.
Dhambi ni kitu chochote ulichofanya au unachofanya kinchomchukiza YAHUVEH
Mtakatifu. Hakuna mtu aliye bora zaidi kushinda mwingine! Kumbuka haya!
Soma
Agano Jipya ili upate kujua YAHUSHUA ni nani. (Yohana 3:16) Bibilia husema
lazima umwungame Yeye kama BWANA na Mwokozi
ili Akuungame mbele yake Baba. Usione aibu kumjua YAHUSHUA, kwani Yeye HAONI
aibu kukujua WEWE. Ambia mtu ya kwamba umemkubali YAHUSHUA wa Kalvari na
Nazareti, siku hii na malaika wote mbinguni wanashangilia.
Turuhusu
tushangilie nawe. Kama unahitaji Mchungaji,
tuna wengi zaidi ya mmoja. Karibu katika Familia ya YAHUSHUA! TUNA MATUMAINI YA
KWAMBA TUTAKUTANA NAWE MBINGUNI, KAMA SI HAPA DUNIANI!
Tuma
Barua Pepe kwa Elisabeth na umueleze juu ya zawadi ya uzima wa milele ambayo
umerithi kutoka kwa YAHUSHUA Masihi wetu Mpendwa!
[email protected]
*******
Rudi
Kwa Ukurasa Wa Wokovu
Je,
Ubatizo ni Jambo Muhimu Kwa Kupata Wokovu?
Ubatizo,
Mto wa Yordani
Mbatizwe.
(Ona Matendo ya Mitume 2:38, 39)
Kubatizwa
inamaanisha kutumbukizwa kwenye maji. Wakati mwingine, mtu husimama ndani ya
maji alafu hutumbukizwa majini (na Mkristo mwenzake) kisha huinuliwa kutoka
majini na kusimama tena. Umuhimu wa kitendo hiki unaonekana katika Kitabu cha
Warumi 6:1-7 na zoezi hili hupatikana katika Kitabu cha Matendo ya Mitume
8:26-39.
Watu
wengine hufikiria ya kwamba ubatizo si moja ya vitendo ambavyo ni ishara ya
kumkubali YAHUSHUA. Hata hivyo, jambo moja ni wazi katika Bibilia. Imani na
ubatizo huwa pamoja kila wakati, hazijatenganishwa. Kwa hivyo, ni wazi ya
kwamba Ubatizo ni ishara ya kumkubali YAHUSHUA. Tunawahimiza wote mtafute
sababu za ubatizo katika Bibilia. Mkristo yeyote wa kweli anaweza kukubatiza.
Kubatizwa
na maji ni njia moja. YAHUSHUA alisema, “Yohana alibatiza na maji lakini
YAHUSHUA hubatiza na MOTO wa ROHO MTAKATIFU!” Baada ya kubatizwa na maji,
ULIZIA kujazwa kwa MOTO wa ROHO MTAKATIFU! Hivi ndivyo zawadi za ROHO MTAKATIFU
hupatikana! Kwa hivyo, usiamini ya kwamba KAMA
hauna hizi zawadi au huwezi kuzungumza katika ndimi takatifu, hautaenda
Mbinguni! Hili ni funzo la uongo! Jambo hili lingekuwa kweli, basi YAHUVEH
angesema vivyo hivyo kwa uwazi ya kwamba wote ambao hawawezi kuzungumza katika
ndimi takatifu HAWATAOKOLEWA! Tena, lingekuwa kweli, hakungekuwa na haja ya
YAHUSHUA kupeana maisha yake na kumwaga damu pale Kalvari! Ni Damu yake
YAHUSHUA Pekee inayoosha dhambi zote kwa wale wanaokubali ZAWADI hii kwa IMANI!
Kanisa
zingine hufunza KAMA mtu hajabatizwa, hata
mtoto mdogo, basi huyo mtu hataenda Mbinguni! Jambo hili lingekuwa kweli, kwa
nini basi YAHUSHUA alijitolea pale Kalvari? Ubatizo ni ishara wazi kwa wote
kuona ya kwamba tunamfuata YAHUSHUA! Watoto wadogo hawawezi kuyaelewa haya
vizuri, kwa hivyo HAIFAI kuwabatiza mpaka watakapoweza kuelewa gharama ambayo
mtu anafaa kulipa ili kumfuata YAHUSHUA. Inafaa watoto wachanga waletwe mbele
yake Baba wanapozaliwa, SI kuwabatiza, kwa sababu lazima waamue wenyewe wakiwa
wamekua.
Kwa
hivyo, badala ya kuangalia ubatizo kama kitu ambacho LAZIMA ufanye, bali na
kumkubali YAHUSHUA kama Bwana na Mwokozi wao,
ili waokolewe… lazima mtu ATAKE kufanya jambo hili, ili kuruhusu kujazwa
kwa Roho Mtakatifu na kuonyesha kila mtu ya kwamba wana uhusiano na kifo na
kufufuka kwa Mwokozi wao, YAHUSHUA Ha Mashiach!