Ukurasa Kuu Mapenzi yako yawe, YAHUVEH, Muumba wangu na Baba Yangu katika jina la YAHUSHUA, kwamba wakati huu uwe wakati wa Baraka mbele YAKO tunapofuata kuwasha kwa taa ya Chanukah, kama kumbusho ya kwamba nuru inayong’aa zaidi Uliyoituma hapa duniani, Mwana WAKO wa pekee YAHUSHUA MASIHI. Na kumbusho kuwa YEYE Alikuwa tumboni mwa mamake wakati wa Hanukkah (na kuzaliwa miezi tisa ifuatayo wakati wa Succot, Sikukuu ya Vibanda). Hii ndiyo sababu nyingine tunasherehekea sikukuu ya nuru. Taa za mafuta huzimwa baada ya siku nane. YAHUSHUA, nuru inayong’aa iliyotumwa hapa duniani, mafuta ya maisha ya kweli, Atadumu MILELE. Tunasherehekea muujiza huu wa taa zote mbili. YAHUSHUA Ndiye MENORAH INAYOISHI. MWANGAZA WA MILELE ambao HAUTAWAHI kuzimwa! Asante YAHUSHUA kwa kumpa Elisheva (Elisabeth) ufunuo huu Novemba 23, 2005. ‘Kwa kuwa ni Wewe YAHUVEH Utakayewasha taa yangu, katika jina la YAHUSHUA, Atakayemulika giza yangu.’ Tuma nuru YAKO na ukweli WAKO, kwa kuwa tunatafuta ukweli wako kupitia RUACH HA KODESH (Roho Mtakatifu), Atakayeniongoza mimi kuogopa na kupenda Majina Yenu Matakatifu, kusoma na kuweka na kufunza Torah Yenu Takatifu, Torah Iliyoandikwa, na Torah Iliyozungumzwa kama vile Neno Lililofanywa kuwa mwili, Mwana wako wa pekee, YAHUSHUA MASIHI. Na kwa bidii kuu kuheshimu Jina Lako lililobarikiwa na kuinuliwa, Jina la YAHUVEH na Mwana wako, YAHUSHUA. Kwa minajili ya taa za Chanukah, tufanye tuwe wenye hekima kupitia mwangaza unaoishi unaotuongoza, YAHUSHUA, Torah wako Anayeishi. Neno hili litimizwe, kama ilivyoandikwa: ‘“Haitapotea mdomoni mwako, mdomoni mwa watoto wako na kutoka mdomoni mwa watoto wa watoto wako”, ndivyo Asemavyo YAHUVEH, “kutoka sasa hadi milele”.’ Watoto wangu na wajukuu wangu watii Torah na wawe watu waaminifu, na uwape nguvu katika kutii Torah na kukutii wewe, inavyoambatana na mipango Yako mizuri. Nifanikiwe kuona watoto na wajukuu wakijihusisha kwa Torah na amri zako kwa ukweli. Fungua macho yetu ili tuweze kuelewa maajabu Yako ya Torah takatifu kuweza kueleza ukweli wa Torah na maajabu yake yote. Safisha mioyo yetu kwa kukutumikia Wewe, tuweke mbali na maovu na fikra chafu, macho yetu ione kurudi kwake Mwana wako mpendwa YAHUSHUA Atakayekuja na kutawala pale Yerusalemu kama Mfalme wa Wafalme na BWANA wa MABWANA. Ba-rucha-tah Adonai E-lo-hei-nu, Mel-ech ha-olam, Tunakubariki ewe YAHUVEH Mungu wetu, mfalme wa ulimwengu, Asher kideshanu be-mitzvotav, Uliyetutakasa kwa Neno lako, ve-tzivanu le-hadlik ner shel Chanukah. na kutuagiza tuwashe taa za Chanukah. Al Ha-Nissim (Inasemwa usiku zote nane) Ha-ne-roth hal-la-lu, a-nach-nu mad-li-kin al ha-nis-sim, Tunawasha hizi taa kwa ajili ya miujiza, v’al hat-shu-oth v’al ha-nif-la-oth she-o-see-ta la-avo-tei-nu, ukombozi na maajabu Wewe Umewatendea baba zetu wa kale, al y’de ko-ha-ne-cho, hak-k’do- shim. V’chol sh’-mo-nath y’may kupitia makuhani Wako watakatifu. Siku zote nane za chanu-kah, han-ne-roth hal-lo-lu ko-desh; v’ain lo-nu r’shuth Chanukah, taa hizi ni takatifu, haturuhusiwi kuzitumia vibaya l’hish-ta-mesh bo-hem el-lo lir-o-tom bil-vad. K’de l’ho-doth, lakini tunafaa kuziangalia tu, ili kutoa shukrani L’shim-cha al ni-se-cho, v’al y’shu-o-se-te-cho, v’al nif-l’o-te-cho Katika jina Lako kwa miujiza yako, ukombozi wako na maajabu yako. Ba-ruch a-tah Adonai E-lo-hei-nu, Mel-ech ha-olam, Tunakubariki ewe YAHUVEH, Mungu wetu, mfalme wa ulimwengu, she-a-sa si-sim la-a-avo-tei-nu ba-ya-mim ha-hem ba-ze-man ha-zeh Uliyetenda mambo ya ajabu kwa baba zetu katika nyakati za kale msimu huu. Katika usiku wa kwanza pekee: Shehekiyanu Ba-ruch a-tah Adonai E-lo-hei-nu, Mel-ech ha-olam, Tunakubariki ewe YAHUVEH Mungu wetu, mfalme wa ulimwengu, she-he-che-ya-nu ve-ki-ye-ma-nu ve-hi-gi-a-nu la-ze-man ha-zeh kwa kutupa maisha, kutuendeleza, na kutuwezesha kufika hadi msimu huu. Washa mshumaa wa kwanza. Sema Baraka iliyoko juu unapowasha mishumaa nyingine. Hapa chini kuna kumbusho la njia ambazo YAHUVEH Aliwakomboa Wayahudi wa kale kama ilivyoandikwa katika Maandiko Matakatifu. Ewe ngome kuu ya wokovu wangu, YAHUSHUA, kukusifu Wewe ndiyo furaha yangu. Uiregeshe Nyumba yangu ya Maombi na palepale tutaleta dhabihu ya shukrani. Utakapoyatayarisha mauaji kwa wale maadui wanaokutukana, Basi nitamalizia kwa wimbo kuwekwa wakfu madhabahu. II. Nafsi yangu imejawa na shida, nguvu yangu imemalizwa kwa huzuni. Wamehuzunisha maisha yangu na magumu, kwa utumwa wa ufalme wa ndama. Lakini katika nguvu Yake kuu Aliwaokoa waliothaminiwa, Jeshi la Farao na watoto wake wote walienda chini kama jiwe lililotumbukizwa majini. III. Hadi kwake patakatifu pa Neno Lake Alinileta mimi. Lakini pale, pia, sikuwa na pumziko Na mnyanyasaji akaja na kunihamisha. Kwa kuwa nilikuwa ninawatumikia Wageni, Na nikalewa kwa mvinyo wao wa mauti. Hata sikuwa nimeenda mbali Katika mwisho wa Babeli Zerubabel akaja. Katika mwisho wa miaka sabini niliokolewa. IV. Kuukata mti mkubwa wa cypress ndivyo alivyotaka huyu Mwagagi, wana wa Hamedatha, Lakini ikawa [mtego na] kizuizi kwake na kiburi chake kikakatizwa. Mkuu wa Benyamini Wewe Ulimwinua na adui, jina lake Ukalifuta Kizazi chake – mali yake – kwenye mti Ulimnyonga. V. Wagiriki walikusanyika dhidi yangu siku zile za Hasmonea. Walivunja kuta za minara yangu na kuchafua mafuta yote; Na kutoka chupa moja iliyoponea muujiza ukatokea kwa maua. Wanaume wa ufahamu – siku nane zikaanzishwa kwa wimbo na furaha. VI. Inua mkono Wako mtakatifu, YAHUVEH, na Uharakishe Mwisho kwa wokovu - Lipiza kisasi ya damu ya watumishi Wako Kutoka kwa taifa la uovu. Kwa kuwa ushindi umecheleweshwa sana kwetu sisi, na hakuna mwisho kwa siku za uovu, Mfukuze yule mwovu katika vivuli vya mbali na tuanzishie sisi wachungaji saba. Wema wa YAHUVEH, katika jina la YAHUSHUA, uwe juu yetu, azithibitishe kazi za mikono yetu kwetu sisi--naam, azithibitishe kazi za mikono yetu kwa Utukufu Wako. Zaburi 91:1-16 Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu sana, atadumu katika uvuli wake Mungu Mwenye Nguvu zote. Nitasema kuhusu YAHUVEH, “'Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu, ambaye ninamtumaini.’’ Hakika Yeye Atakuokoa na mtego wa mwindaji na maradhi ya kuambukiza ya kufisha. Atakufunika kwa manyoya yake, chini ya mabawa Zake utapata kimbilio, uaminifu Wake utakuwa ngao na kinga yako. Hutaogopa vitisho vya usiku, wala mshale urukao mchana, wala maradhi ya kuambukiza yanayonyemelea gizani, wala tauni iharibuyo adhuhuri. Ijapo watu elfu wataangukia kando yako, kumi elfu mkono wako wa kuume, lakini haitakukaribia wewe. Utatazama tu kwa macho yako na kuona adhabu ya waovu. Kama ukimfanya Aliye Juu kuwa makao yako--hata YAHUVEH ambaye ni kimbilio langu, basi hakuna madhara yatakayokupata wewe, wala maafa hayataikaribia hema yako. Kwa kuwa Atawaagiza malaika zake kwa ajili yako, wakulinde katika njia zako zote. Mikononi mwao Atakuinua juu, ili usijikwae mguu wako kwenye jiwe. Utawakanyaga simba na nyoka wakali, simba mkubwa na nyoka utawaponda kwa miguu. YAHUVEH Asema, “Kwa kuwa ananipenda Nitamwokoa, Nitamlinda kwa kuwa amelikubali jina langu.’’ Ataniita, Nami Nitamjibu, Nitakuwa pamoja naye katika taabu, Nitamwokoa na kumheshimu. Kwa siku nyingi Nitamshibisha na kumwonyesha wokovu wangu. Zaburi 67:1-8 {Wimbo Wa Kushukuru (Kwa Mwimbishaji: Na Ala Za Nyuzi Za Muziki. Zaburi. Wimbo.)} YAHUVEH uturehemu na kutubariki na kutuangazia nuru za uso wako, ili njia zako zijulikane duniani, wokovu wako katikati ya mataifa yote. Ee YAHUVEH, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu. Mataifa yote wafurahi na kuimba kwa shangwe, kwa kuwa unatawala watu kwa haki na kuongoza mataifa ya dunia. Ee Mungu, mataifa na wakusifu, mataifa yote na wakusifu. Ndipo nchi itatoa mazao yake, naye Mungu, Mungu wetu, atatubariki. YAHUVEH atatubariki na miisho yote ya dunia itamcha Yeye. Wale naoishi mbali sana wanaogopa maajabu yako, kule asubuhi ipambazukiapo na kule jioni inakofifilia umeziita nyimbo za furaha. Tunakuomba! Katika nguvu za mkono Wako mkuu wa kulia, niachilie huru kutokana na mzigo wa dhambi. Kubali ombi la taifa Lako; tupe nguvu, tusafishe, Ewe YAHUVEH wa Ajabu. Tafadhali Ewe YAHUVEH wa Ajabu – wale wanaotambua Umoja wako, wachunge kama mboni ya jicho. Wabariki, wasafishe, waonee huruma, utakatifu Wako uwafuate. YAHUVEH mwenye nguvu, na uzuri wako mwingi linda shirika lako. Katika jina la YAHUSHUA, rudia taifa Lako, inayosimamia utakatifu Wako. Kubali ombi letu na sikia kilio chetu, Ewe Unayejua mambo yote… Baraka kwa Jina la ufalme wa YAHUVEH, wenye utukufu, milele na milele. Zaburi 30:1-13 {Maombi Ya Shukrani Utenzi Wa Kuweka Wakfu Hekalu (Zaburi Ya Daudi).} Nitakutukuza Wewe, Ee YAHUVEH, kwa kuwa umeniinua na hukuacha adui zangu washangilie juu yangu. Ee YAHUVEH Mungu wangu, nilikuita unisaidie na wewe umeniponya. Ee YAHUVEH, umenitoa kuzimuni, umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti. Mwimbieni YAHUVEH enyi watakatifu wake, lisifuni jina lake takatifu, kwa kumbukumbu la utakatifu wake. Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi, bali upendo wake hudumu siku zote, inawezekana kilio kikawepo usiku kucha, lakini asubuhi kukawa na furaha. Nilipofanikiwa nilisema, ‘‘Sitatikiswa kamwe.’’ Ee YAHUVEH, uliponijalia, uliuimarisha mlima wangu, lakini ulipouficha uso wako nilifadhaika. Kwako Wewe, Ee YAHUVEH, niliita, kwa YAHUVEH niliomba rehema: “Kuna faida gani katika kuangamia kwangu? Katika kushuka kwangu shimoni? Je, mavumbi yatakusifu? Je, yatatangaza uaminifu wako? Ee YAHUVEH, unisikie na kunihurumia, Ee YAHUVEH, uwe msaada wangu.’’ Uligeuza maombolezo yangu kuwa kucheza, ulinivua nguo za gunia ukanivika furaha, ili moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya. Ee YAHUVEH wangu, nitakushukuru milele. Zaburi 133:1-3 {Sifa Za Pendo La Udugu (Wimbo Wa Kwenda Juu, Wa Daudi).} Tazama jinsi ilivyo vema na kupendeza wakati ndugu wanapoishi pamoja katika umoja! Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani, yakitiririka kwenye ndevu, yakitiririka kwenye ndevu za Aroni, mpaka kwenye upindo wa mavazi yake. Ni kama vile umande wa Hermoni unavyoanguka juu ya Mlima Sayuni. Kwa maana huko ndiko YAHUVEH alikoamuru baraka yake, naam, hata uzima milele. Zaburi 33:1-22 Mwimbieni YAHUVEH kwa furaha, enyi wenye haki, inawapasa wanyofu wa moyo kumsifu. Msifuni YAHUVEH kwa kinubi, mwimbieni sifa kwa zeze la nyuzi kumi. Mwimbieni wimbo mpya, pigeni kwa ustadi, pigeni kelele za furaha. Maana neno la YAHUVEH ni haki na kweli, ni mwaminifu kwa yote atendayo. Hupenda uadilifu na haki, dunia imejaa upendo wake usiokoma. Kwa neno la YAHUVEH mbingu ziliumbwa, jeshi lao la angani kwa pumzi ya kinywa chake. Ameyakusanya maji ya bahari kama kwenye mtungi, vilindi vya bahari ameviweka katika ghala. Dunia yote na imwogope YAHUVEH watu wote wa dunia wamche. Kwa maana alisema, na ikawa, aliamuru na ikasimama imara. YAHUVEH huzuia mipango ya mataifa, hupinga makusudi ya mataifa. Lakini mipango ya YAHUVEH inasimama imara milele, makusudi ya moyo wake vizazi vyote. Heri taifa ambalo YAHUVEH ni Mungu wao, watu ambao aliwachagua kuwa urithi wake. Kutoka mbinguni YAHUVEH hutazama chini na kuwaona wanadamu wote, Kutoka maskani mwake huwaangalia wote wakaao duniani--Yeye ambaye huumba mioyo yao wote, ambaye huangalia kila kitu wanachokitenda. Hakuna mfalme aokokaye kwa ukubwa wa jeshi lake, hakuna shujaa aokokaye kwa wingi wa nguvu zake. Farasi ni tumaini bure kwa wokovu, licha ya nguvu zake nyingi hawezi kuokoa. Lakini macho ya YAHUVEH yako kwa wale wamchao, kwa wale ambao tumaini lao ni katika upendo wake usio na kikomo, ili awaokoe na mauti na kuwahifadhi wakati wa njaa. Sisi tunamngojea YAHUVEH kwa matumaini, yeye ni msaada wetu na ngao yetu. Katika Yeye mioyo yetu hushangilia, kwa maana tunalitumainia jina lake takatifu. Upendo wako usio na mwisho ukae juu yetu, Ee YAHUVEH, kama vile tunavyoweka tumaini letu kwako.
USIKU 1: Mose alipomaliza kuisimamisha maskani ya YAHUVEH, aliitia mafuta na kuiweka wakfu pamoja na samani zake zote. Pia alitia madhabahu mafuta na kuweka wakfu pamoja na vyombo vyake vyote. Ndipo viongozi wa Israeli, wakuu wa jamaa waliokuwa viongozi wa kabila wasimamizi wa wale waliohesabiwa, wakatoa sadaka. Walizileta kama matoleo yao mbele za YAHUVEH magari sita ya kukokotwa yaliyofunikwa pamoja na maksai kumi na wawili, yaani, maksai mmoja kutoka kwa kila kiongozi na gari moja la kukokotwa kutoka kwa kila viongozi wawili. Haya waliyaleta mbele ya maskani ya YAHUVEH. YAHUVEH akamwambia Mose, “Vikubali vitu hivi kutoka kwao, ili viweze kutumika katika kazi kwenye Hema la Mkutano. Wapatie Walawi kama kazi ya kila mtu itakavyohitaji.’’ Hivyo Mose akachukua yale magari ya kukokotwa pamoja na maksai na kuwapa Walawi. Aliwapa Wagershoni magari mawili ya kukokotwa na maksai wanne, kama walivyohitaji kwa kazi yao, pia aliwapa Wamerari magari manne ya kukokotwa na maksai wanane, kama kazi yao ilivyohitaji. Wote walikuwa chini ya maelekezo ya Ithamari mwana wa kuhani Aroni. Lakini Mose hakuwapa Wakohathi chochote kati ya hivyo, kwa sababu walitakiwa kubeba vitu vitakatifu mabegani mwao, kwa kuwa walikuwa wanawajibika. Wakati madhabahu ilipotiwa mafuta, viongozi walileta sadaka zao kwa ajili ya kule kuwekwa wakfu kwake na kuziweka mbele ya madhabahu. Kwa maana YAHUVEH alikuwa amemwambia Mose, “Kila siku kiongozi mmoja ataleta sadaka yake ili kuwekwa wakfu madhabahu.’’ Yule ambaye alileta sadaka yake siku ya kwanza alikuwa Nashoni mwana wa Aminadabu wa kabila la Yuda. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, lililojazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Nashoni mwana wa Aminadabu. Mwanzo 1:2-5 Sasa Dunia ilikuwa haina umbo tena ilikuwa tupu, giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji, naye Roho wa Mungu alikuwa ametanda juu ya maji. Mungu akasema, “Iwepo nuru’’ nayo nuru ikawepo. Mungu akaona ya kuwa nuru ni njema, ndipo Mungu akatenganisha nuru na giza. Mungu akaiita nuru “mchana’’ na giza akaliita “usiku.’’ Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya kwanza. Mwanzo 1:14-18 Mungu akasema, “Iwepo mianga kwenye nafasi ya anga ili itenganishe mchana na usiku, nayo iwe alama ya kutambulisha majira mbali mbali, siku na miaka, nayo iwe ndiyo mianga kwenye nafasi ya anga itoe nuru juu ya dunia.’’ Ikawa hivyo. Mungu akafanya mianga miwili mikubwa. Mwanga mkubwa utawale mchana na mwanga mdogo utawale usiku. Pia Mungu akafanya nyota. Mungu akaiweka katika nafasi ya anga iangaze dunia, itawale mchana na usiku na ikatenganishe nuru na giza. Mungu akaona kuwa hili ni jema. Yohana 1:1-13 Hapo mwanzo, alikuwako Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Tangu mwanzo huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu. Vitu vyote viliumbwa kwa Yeye, wala pasipo Yeye hakuna chochote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa. Ndani Yake ndimo ulimokuwa uzima na huo uzima ulikuwa nuru ya watu. Nuru hung’aa gizani nalo giza halikuishinda. Alikuja mtu mmoja aliyetumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana. Alikuja kama shahidi apate kuishuhudia hiyo nuru, ili kwa kupitia yeye watu wote waweze kuamini. Yeye mwenyewe hakuwa ile nuru, bali alikuja kuishuhudia hiyo nuru. Nuru halisi, imwangaziayo kila mtu ilikuwa inakuja ulimwenguni. Alikuwepo ulimwenguni na ingawa ulimwengu uliumbwa kwa Yeye, haukumtambua. Alikuja kwa walio Wake, lakini wao hawakumpokea. Bali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio Jina Lake--Hawa watoto wamezaliwa si kwa damu wala kwa mapenzi ya mwili au kwa mapenzi ya mtu, bali kwa mapenzi ya Mungu.
USIKU 2: Siku ya pili yake Nethaneli mwana wa Suari, kiongozi wa kabila la Isakari, alileta sadaka yake. Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikawa kimejazwa unga laini uliochanganywa na la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi likiwa limejazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana- kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana- kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Nethaneli mwana wa Suari. Isaiah 5:20-24 Ole wao wanaoita ubaya ni wema na wema ni ubaya, wawekao giza badala ya nuru na nuru badala ya giza, wawekao uchungu badala ya utamu na utamu badala ya uchungu. Ole wao walio na hekima machoni pao wenyewe na kujiona wenye akili machoni pao wenyewe. Ole wao walio mashujaa kwa kunywa mvinyo nao walio hodari katika kuchanganya vileo, wale wanaoachilia wenye hatia kwa kupokea hongo, lakini huwanyima haki wasio na hatia. Kwa hiyo, kama ndimi za moto zirambavyo nyasi na kama vile majani makavu yazamavyo katika miali ya moto, ndivyo mizizi yao itakavyooza na maua yao yatakavyopeperushwa kama mavumbi, kwa kuwa wameikataa sheria ya YAHUVEH Mwenye Nguvu na kulisukumia mbali neno la Aliye Mtakatifu wa Israeli. Matthew 6:22-23 ‘‘Jicho ni taa ya mwili. Kama jicho lako ni nyofu, mwili wako wote utakuwa na nuru. Lakini kama jicho lako ni ovu, mwili wako wote utajawa na giza. Kwa hiyo basi, kama nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza, hilo ni giza kuu namna gani! ”
USIKU 3: Siku ya tatu, Eliabu mwana wa Heloni, kiongozi wa kabila la Zabuloni, alileta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana- kondoo wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana- kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Eliabu mwana wa Heloni. Zaburi 115:5-7 Zina vinywa, lakini haziwezi kusema, macho, lakini haziwezi kuona, zina masikio, lakini haziwezi kusikia, pua, lakini haziwezi kunusa, zina mikono, lakini haziwezi kupapasa, miguu, lakini haziwezi kutembea, wala koo zao haziwezi kutoa sauti. Ayubu 24:13 “Wako wale wanaoiasi nuru, wasiofahamu njia zake wala hawakai katika mapito yake. Ayubu 24:17 Kwa wote hawa, giza nene ndiyo asubuhi yao, hujifanya rafiki na vitisho vya gizani. Ayubu 18:5-6 ‘‘Taa ya mwovu imezimwa, nao mwali wa moto wake umezimika. Mwanga hemani mwake umekuwa giza, taa iliyokaribu naye imezimika. Ayubu 12:25 Hupapasa gizani pasipokuwa na mwanga, huwafanya wapepesuke kama walevi. Yeremia 25:10 Nitawaondolea sauti ya shangwe na furaha, sauti ya bibi na bwana arusi, sauti ya mawe ya kusagia na mwanga wa taa. Ezekieli 32:8 Mianga yote itoayo nuru angani nitaitia giza juu yako, nitaleta giza juu ya nchi yako, asema YAHUVEH Mwenyezi. Isaya 42:18 ‘‘Sikieni, enyi viziwi, tazameni, enyi vipofu mpate kuona! Marko 8:14-21 Wanafunzi walikuwa wamesahau kuleta mikate ya kutosha. Walikuwa na mkate mmoja tu kwenye mashua. Yesu akawaonya: ‘‘Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na ya Herode.’’ Wakaanza kujadiliana wao kwa wao wakasema, ‘‘Anasema hivi kwa kuwa hatukuleta mikate.’’ Yesu akifahamu majadiliano yao, akawauliza: ‘‘Mbona mnazungumzia kuhusu kutokuwa na mikate? Bado hamtambui wala kuelewa? Je, mbona mioyo yenu ni migumu kiasi hicho? Mna macho lakini mnashindwa kuona, mna masikio lakini mnashindwa kusikia? Je, hamkumbuki? Nilipoimega ile mikate mitano kuwalisha watu elfu tano, mlikusanya vikapu vingapi vilivyojaa vya masazo?’’ Wakamjibu, “Kumi na viwili.’’ ‘‘Je, nilipomega ile mikate saba kuwalisha watu 4,000, mlikusanya vikapu vingapi vilivyojaa vya masazo?’’ Wakamjibu, “Saba.’’ Ndipo akawaambia, Akawauliza, ‘‘Je, bado tu hamwelewi?’’ Ukurasa Kuu |
www.allmightywind.com | www.almightywind.com Please go to the other if one is off line. We are Sabbath-Keepers, Not Seventh-Day Adventists Click Here For More Info Mailing and Email Addresses |