Chag Hanukkah Sameach!! Ukurasa 1 Ukurasa 2 Ukurasa 3 Ukurasa 4 Ukurasa Kuu Kuleta Hanukka nne pamoja nasi Jumapili tarehe 7 Desemba, kwa Jumapili tarehe 15 Desemba, 2023
Hapa unaweza kuwasha mishumaa ya Menorah kwenye mtandao, na kusherehekea Hanukkah nasi Huduma ya Amightywind Hanukkah Njema kutoka Mtume/Nabii Elisheva Eliyahu (Elisabeth Sherrie Elijah)!!!
Hanukkah—pia inaandikwa kama Chanukah. Hanukkah—inamaanisha “kuwekwa wakfu” na inajulikana kama “Sikukuu ya Nuru”, ni sikukuu ya Kiyahudi inayoanza Tarehe 25 ya Kiebrania ya mwezi wa Kislev na huendelea kwa muda wa siku nane, hadi siku ya 2 ya mwezi wa Tevet. Mwaka huu wa 2014 unalingana na…
Hanukkah ni makumbusho ya ushindi wa Maccabees (ulioongozwa na Yuda) dhidi ya Wahelenisti wa Syria katika vita vilivyotokea muda wa 165 BCE. (nakala: Wayahudi hutumia BCE---Before Common Era na CE---Common Era badala ya BC na AD). Vita hivi vyenyewe viliaminiwa kuwa muujiza, lakini hadithi ya Kiyahudi hutoa maelezo zaidi ya matambiko ya Hanukkah, kama ilivyoelezwa hapa chini. Baada ya Hekalu Mlimani pale Yerusalemu kurejeshwa tena, ilibidi Hekalu iwekwe wakfu tena. Katika hadithi, ni kopo moja tu la mafuta ya sakramenti lililopatikana, iliyotosha siku moja tu. Kwa muujiza, mafuta hayo yalitumika kutoa mwanga siku nane, ndiposa siku nane za Hanukkah. Tambiko muhimu zaidi ya Hanukkah ni kuwasha mshumaa. Wayahudi huwasha mshumaa kwa kifaa spesheli ya kushikilia mshumaa kinachoitwa “Menorah” au “hanukkiah”. Kila usiku, mshumaa mmoja huongezwa. Mshumaa ulioko katikati, unaitwa “shamash”, unatumika kuwasha mishumaa ile nyingine na unawashwa kila usiku. Basi, usiku wa kwanza wa Hanukkah, mishumaa miwili inawashwa (shamash na mshumaa wa usiku wa kwanza) na katika usiku wa mwisho, kuna mishumaa tisa iliyowashwa. Ni mila kula vyakula vilivyokarangwa kwenye mafuta wakati wa Hanukkah. Vyakula vinavyoliwa sanasana ni kama potato latkes (viazi) na “sufganiot” (donut ya jeli). | ||||||
Mila nyingine ni kucheza mchezo wa “dreidel”. Dreidel (au “sivivon”) ni kidude kilicho na pande nne. Katika pande zote kuna herufi tofauti ya Kiebrania: nun (nun), gimel (gimel), heh (heh) na peh (peh), inayolingana na maneno katika sentensi “nes gadol haya po” (“Muujiza mkuu ulifanyika hapa”). Bila shaka, muujiza huu ulifanyika Israeli, kwa hivyo nje ya Israeli, herufi ya peh (peh) inabadilishwa na shin (shin) inayosema “nes gadol haya sham” (Muujiza mkuu ulifanyika kule”). Dreidel inatumika kwa mchezo wa kamari ambapo kila herufi inawakilisha kiasi tofauti ya pesa (au chochote…) iliyoshindwa au kupotezwa. | ||||||
Huko Israeli, Hanukkah ni wakati wa sherehe. Shule huwa zimefungwa kwa muda wa wiki moja na huwa kuna sherehe nyingi na matukio spesheli kote nchini. Tunaimba nyimbo za Hanukkah (kama wimbo unaocheza kwenye usuli), kula vyakula vingi na kufurahia sana! Ukurasa Kuu |
www.allmightywind.com | www.almightywind.com Please go to the other if one is off line. We are Sabbath-Keepers, Not Seventh-Day Adventists Click Here For More Info Mailing and Email Addresses |