Ukurasa Kuu
USIKU 6: Hesabu 7:42-47 Siku ya sita Eliasafu mwana wa Deueli, kiongozi wa watu wa Gadi, akaleta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kwa kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, lililojazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Eliasafu mwana wa Deueli. Zaburi 27:1 {Zaburi Ya Daudi} YAHUVEH ni nuru yangu na wokovu wangu, nimwogope nani? YAHUVEH ni ngome ya uhai wangu--nimhofu nani? Zaburi 104:1-2 Ee YAHUVEH, wangu, wewe ni mkuu sana, umejivika utukufu na enzi. Amejifunika katika nuru kama vile kwa vazi, amezitandaza mbingu kama hema. Zaburi 119:105 {Nun} Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga katika njia yangu. Zaburi 19:9 Kumcha YAHUVEH ni utakatifu, nalo ladumu milele. Amri za YAHUVEH ni za hakika, nazo zina haki. Mithali 6:23-24 Kwa maana maagizo haya ni taa, mafundisho haya ni mwanga na maonyo ya maadili ni njia ya uzima, yakikulinda na mwanamke mwovu, kutokana na maneno laini ya mwanamke mpotovu. Yohana 9:1-7 YAHUSHUA alipokuwa akipita, akamwona mtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa. Wanafunzi Wake wakamwuliza, “Rabi, ni nani aliyetenda dhambi, ni huyu mtu au wazazi wake hata azaliwe kipofu?’’ YAHUSHUA akawajibu, “Huyu mtu wala wazazi wake hawakutenda dhambi. Alizaliwa kipofu ili kazi za Mungu zidhihirishwe katika maisha yake. Yanipasa kuzifanya kazi zake Yeye aliyenituma wakati bado ni mchana, kwa kuwa usiku waja ambapo hakuna mtu awezaye kufanya kazi. Wakati niko ulimwenguni, Mimi ni nuru ya ulimwengu.’’ Baada ya kusema haya, akatema mate ardhini, akatengeneza tope kwa mate na kumpaka yule mtu kipofu machoni. Kisha akamwambia, “Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu.” (Siloamu, maana yake ni aliyetumwa.) Ndipo yule kipofu akaenda, akanawa, naye akarudi akiwa anaona.
Siku ya saba Elishama mwana wa Amihudi, kiongozi wa watu wa Efraimu alileta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, lililojazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano, na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Elishama mwana wa Amihudi. Mithali 4:18 Njia ya wenye haki ni kama nuru ya kwanza ya mapambazuko, ambayo hung’aa zaidi na zaidi mpaka mchana mkamilifu. Zaburi 97:11-12 Nuru huangaza wenye haki na furaha kwa watu wanyofu wa moyo. Furahini katika YAHUVEH, ninyi mlio wenye haki, lisifuni jina lake takatifu. Isaya 9:1-2 Hata hivyo, hapatakuwepo huzuni zaidi kwa wale waliokuwa katika dhiki. Wakati uliopita aliidhili nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, lakini katika siku zijazo ataiheshimu Galilaya ya Mataifa, karibu na njia ya bahari, kando ya Yordani-- Watu wanaotembea katika giza wameona nuru kuu, wale wanaoishi katika nchi ya uvuli wa mauti, nuru imewazukia. Kutoka 10:23 Hakuna mtu yeyote aliyeweza kumwona mwenzake, wala kuondoka mahali alipokuwa kwa muda wa siku tatu. Lakini Waisraeli wote walikuwa na mwanga katika maeneo yao waliyokuwa wanaishi. Isaya 60:1 “Ondoka, angaza, kwa kuwa nuru yako imekuja na utukufu wa YAHUVEH unaangaza juu yako. Isaya 2:5 Njooni, Enyi nyumba ya Yakobo, sisi na tutembee katika nuru ya YAHUVEH. Mathayo 4:12-17 YAHUSHUA aliposikia kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa ametiwa gerezani, alirudi Galilaya. Akaondoka Nazareti akaenda kuishi Kapernaumu ulioko karibu na bahari, katika mipaka ya nchi ya Zabuloni na ya Naftali, ili kutimiza unabii wa nabii Isaya, kama alivyosema: “Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, kwenye njia ya kuelekea baharini, ng'ambo ya Yordani, Galilaya ya watu Mataifa, watu wale waliokaa gizani wameona nuru kuu nao wale waliokaa katika nchi ya uvuli wa mauti, nuru imewazukia.’’ Tangu wakati huo, YAHUSHUA alianza kuhubiri akisema: “Tubuni, kwa maana Ufalme wa Mbinguni umekaribia.’’ * * * * * * * * * * * * * * Maandiko spesheli ya Sabato wakati wa Hanukkah. Hesabu 7:1-11 Mose alipomaliza kuisimamisha maskani ya YAHUVEH, aliitia mafuta na kuiweka wakfu pamoja na samani zake zote. Pia alitia madhabahu mafuta na kuweka wakfu pamoja na vyombo vyake vyote. Ndipo viongozi wa Israeli, wakuu wa jamaa waliokuwa viongozi wa kabila wasimamizi wa wale waliohesabiwa, wakatoa sadaka. Walizileta kama matoleo yao mbele za YAHUVEH magari sita ya kukokotwa yaliyofunikwa pamoja na maksai kumi na wawili, yaani, maksai mmoja kutoka kwa kila kiongozi na gari moja la kukokotwa kutoka kwa kila viongozi wawili. Haya waliyaleta mbele ya maskani ya YAHUVEH. YAHUVEH akamwambia Mose, “Vikubali vitu hivi kutoka kwao, ili viweze kutumika katika kazi kwenye Hema la Mkutano. Wapatie Walawi kama kazi ya kila mtu itakavyohitaji.’’ Hivyo Mose akachukua yale magari ya kukokotwa pamoja na maksai na kuwapa Walawi. Aliwapa Wagershoni magari mawili ya kukokotwa na maksai wanne, kama walivyohitaji kwa kazi yao, pia aliwapa Wamerari magari manne ya kukokotwa na maksai wanane, kama kazi yao ilivyohitaji. Wote walikuwa chini ya maelekezo ya Ithamari mwana wa kuhani Aroni. Lakini Mose hakuwapa Wakohathi chochote kati ya hivyo, kwa sababu walitakiwa kubeba vitu vitakatifu mabegani mwao, kwa kuwa walikuwa wanawajibika. Wakati madhabahu ilipotiwa mafuta, viongozi walileta sadaka zao kwa ajili ya kule kuwekwa wakfu kwake na kuziweka mbele ya madhabahu. Kwa maana YAHUVEH alikuwa amemwambia Mose, “Kila siku kiongozi mmoja ataleta sadaka yake ili kuwekwa wakfu madhabahu.’’ Hesabu 7:12-59 Yule ambaye alileta sadaka yake siku ya kwanza alikuwa Nashoni mwana wa Aminadabu wa kabila la Yuda. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumic, lililojazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Nashoni mwana wa Aminadabu. Siku ya pili yake Nethaneli mwana wa Suari, kiongozi wa kabila la Isakari, alileta sadaka yake. Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikawa kimejazwa unga laini uliochanganywa na la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi likiwa limejazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana- kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana- kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Nethaneli mwana wa Suari. Siku ya tatu, Eliabu mwana wa Heloni, kiongozi wa kabila la Zabuloni, alileta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana- kondoo wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana- kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Eliabu mwana wa Heloni. Siku ya nne Elisuri mwana wa Shedeuri, kiongozi wa kabila la Reubeni alileta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, lililojazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano,mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wenye mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Elisuri mwana wa Shedeuri. Siku ya tano Shelumieli mwana wa Surishadai, kiongozi wa watu wa Simeoni, alileta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kwa kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi likiwa limejazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, pamoja na maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Shelumieli mwana wa Surishadai. Siku ya sita Eliasafu mwana wa Deueli, kiongozi wa watu wa Gadi, akaleta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kwa kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, lililojazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Eliasafu mwana wa Deueli. Siku ya saba Elishama mwana wa Amihudi, kiongozi wa watu wa Efraimu alileta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, lililojazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano, na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Elishama mwana wa Amihudi. Siku ya nane Gamalieli mwana wa Pedasuri, kiongozi wa watu wa Manase, alileta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, lililojazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mmoja mume kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Gamalieli mwana wa Pedasuri. Zekaria 2:13 - 4:7 Tulieni mbele za YAHUVEH, enyi watu wote, kwa sababu ameinuka kutoka makao yake matakatifu.” Kisha akanionyesha Yoshua kuhani mkuu akiwa amesimama mbele ya malaika wa YAHUVEH, naye Shetani amesimama upande wake wa kuume ili amshitaki. YAHUVEH akamwambia Shetani, “YAHUVEH akukemee Shetani! YAHUVEH, ambaye ameichagua Yerusalemu, akukemee! Je, mtu huyu siyo kijinga kinachowaka kilichonyakuliwa kwenye moto?’’ Wakati huu, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu alipokuwa amesimama mbele ya malaika. Malaika akawaambia wale waliokuwa wamesimama mbele yake, ‘‘Mvueni nguo zake chafu.’’ Kisha akamwambia Yoshua, ‘‘Tazama, nimeiondoa dhambi yako, nami nitakuvika mavazi ya kitajiri.’’ Kisha nikasema, “Mvike kilemba kilicho safi kichwani mwake.’’ Kwa hiyo wakamvika kilemba safi kichwani na kumvika yale mavazi mengine, wakati malaika wa YAHUVEH akiwa amesimama karibu. Malaika wa YAHUVEH akamwamuru Yoshua: “Hivi ndivyo asemavyo YAHUVEH Mwenye Nguvu: ‘Ikiwa utakwenda katika njia zangu na kushika masharti yangu, basi utaitawala nyumba yangu na kuwa na amri juu ya nyua zangu, nami nitakupa nafasi miongoni mwa hawa wasimamao hapa. ‘‘ ‘Sikiliza, Ee Yoshua kuhani mkuu, pamoja na wenzako walioketi mbele yako, ambao ni watu ishara ya mambo yatakayokuja: Ninakwenda kumleta mtumishi wangu, Tawi. Tazama, jiwe nililoliweka mbele ya Yoshua! Kuna macho saba juu ya jiwe lile moja, nami nitachora maandishi juu yake,’ asema YAHUVEH Mwenye Nguvu, ‘nami nitaiondoa dhambi ya nchi hii kwa siku moja. “ ‘Katika siku hiyo kila mmoja wenu atamwalika jirani yake akae chini ya mzabibu wake na mtini wake,’ asema YAHUVEH Mwenye Nguvu.’ Kisha malaika aliyezungumza nami akarudi na kuniamsha, kama mtu aamshwavyo kutoka katika usingizi wake. Akaniuliza, “Unaona nini?’’ Nikajibu, “Ninaona kinara cha taa cha dhahabu tupu, nacho kina bakuli juu yake na taa zake saba juu yake, tena iko mirija saba ya kuleta mafuta, kwenye taa zote zilizo juu yake. Pia kuna mizeituni miwili karibu yake, mmoja upande wa kuume wa bakuli na mwingine upande wa kushoto.’’ Nikamuuliza malaika aliyezungumza nami, “Hivi ni vitu gani, YAHUVEH wangu?’’ Akanijibu, “Hujui kuwa hivi ni vitu gani?’’ Nikajibu, “Hapana, YAHUVEH wangu.’’ Kisha akaniambia, “Hili ni neno la YAHUVEH kwa Zerubabeli: ‘Si kwa nguvu, wala si kwa uwezo, bali ni kwa Roho yangu,’ asema YAHUVEH Mwenye Nguvu. ‘‘Wewe ni kitu gani, Ee mlima mkubwa sana? Mbele ya Zerubabeli wewe utakuwa ardhi tambarare. Kisha ataweka jiwe la juu kabisa la mwisho na watu wakipiga kelele wakisema, ‘YAHUVEH libariki! YAHUVEH libariki!’’
Hesabu 7:54 - 8:4 Siku ya nane Gamalieli mwana wa Pedasuri, kiongozi wa watu wa Manase, alileta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, lililojazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mmoja mume kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Gamalieli mwana wa Pedasuri. Siku ya tisa Abidani mwana wa Gideoni kiongozi wa watu wa Benyamini, alileta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, lililojazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mmoja mume kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Abidani mwana wa Gideoni. Siku ya kumi Ahiezeri mwana wa Amishadai, kiongozi wa watu wa Dani, alileta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli mia moja na thelathini na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, lililojazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Ahiezeri mwana wa Amishadai. Siku ya kumi na moja Pagieli mwana wa Okrani, kiongozi wa watu wa Asheri, alileta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta, kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, lililojazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Pagieli mwana wa Okrani. Siku ya kumi na mbili Ahira mwana wa Enani, kiongozi wa watu wa Naftali, alileta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila moja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, lililojazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja, kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Ahira mwana wa Enani. Hizi zilikuwa ndizo sadaka za viongozi wa Israeli madhabahu ilipowekwa wakfu wakati ilipotiwa mafuta, sahani kumi na mbili za fedha, bakuli kumi na mbili za fedha za kunyunyizia na masinia kumi na mawili ya dhahabu. Kila sahani ya fedha ilikuwa na uzito wa shekeli 130, na kila bakuli la fedha la kunyunyizia lilikuwa na uzito wa shekeli sabini. Masinia kumi na mawili yalikuwa na uzito wa shekeli 2,400 kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. Sahani kumi na mbili za dhahabu zilizojazwa uvumba zilikuwa na uzito wa shekeli kumi kila moja kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. Zote kwa pamoja, sahani za dhahabu zilikuwa na uzito wa shekeli 120. Jumla ya wanyama waliotolewa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, walikuwa fahali kumi na wawili wachanga, kondoo waume kumi na wawili, na wana-kondoo waume kumi na wawili wa mwaka mmoja, pamoja na sadaka zao za nafaka. Mbuzi waume kumi na wawili walitolewa kwa ajili ya sadaka za dhambi. Jumla ya wanyama kwa ajili ya dhabihu ya sadaka ya amani walikuwa maksai ishirini na wanne, kondoo waume sitini, mbuzi waume sitini na wana-kondoo waume wa mwaka mmoja sitini. Hizi zilikuwa ndizo sadaka zilizoletwa kwa ajili ya kuwekwa wakfu kwa madhabahu baada ya kutiwa mafuta. Mose alipoingia kwenye Hema la Mkutano kuzungumza na YAHUVEH, alisikia sauti ikisema naye kutoka kati ya wale makerubi wawili waliokuwa juu ya kile kiti cha rehema, juu ya sanduku la Ushuhuda. Mose akazungumza naye. YAHUVEH akamwambia Mose, “Sema na Aroni umwambie, ‘Wakati utakapoziweka zile taa saba, zinatakiwa kuangaza eneo lililo mbele ya kinara cha taa.’ ’’ Aroni akafanya hivyo, akaziweka zile taa ili zielekee mbele kwenye kinara cha taa, kama vile YAHUVEH alivyomwamuru Mose. Hivi ndivyo kinara cha taa kilivyotengenezwa: Kilitengenezwa kwa dhahabu iliyofuliwa, kuanzia kwenye kitako chake hadi kwenye maua yake. Kinara cha taa kilitengenezwa sawasawa kabisa na kielelezo ambacho YAHUVEH alikuwa amemwonyesha Mose. Isaya 30:26 Mwezi utaangaza kama jua, nao mwanga wa jua utang’aa mara saba zaidi, kama nuru ya siku saba, wakati YAHUVEH atakapoyafunga majeraha ya watu wake na kuponya vidonda alivyowatia. Zekaria 14:6-7 Siku hiyo hakutakuwepo nuru, baridi wala theluji. Itakuwa siku ya kipekee, isiyo na mchana wala usiku, siku ijulikanayo na YAHUVEH. Jioni inapofika nuru itakuwepo. Isaya 60:19-20 Luka 1:67-79 Zekaria, baba yake, akajazwa na Roho Mtakatifu, naye akatoa unabii akisema: “Ahimidiwe YAHUVEH, Mungu wa Israeli, kwa kuwa amewajilia Watu wake na kuwakomboa. Naye ametusimamishia pembe ya wokovu katika nyumba ya Daudi mtumishi Wake, kama alivyonena kwa vinywa vya manabii wake watakatifu tangu zamani, kwamba atatuokoa kutoka kwa adui zetu na kutoka mikononi mwao wote watuchukiao, ili kuonyesha rehema kwa baba zetu na kukumbuka agano lake takatifu, kiapo alichomwapia baba yetu Abrahamu: kutuokoa kutoka mkononi mwa adui zetu, tupate kumtumikia Yeye pasipo hofu katika utakatifu na haki mbele Zake, siku zetu zote. Nawe mtoto wangu, utaitwa nabii wa Aliye Juu, kwa kuwa utamtangulia YAHUVEH na kuandaa njia kwa ajili Yake, kuwajulisha watu Wake juu ya wokovu utakaopatikana kwa kusamehewa dhambi zao, kwa ajili ya wingi wa rehema za Mungu wetu, nuru itokayo juu itatuzukia ili kuwaangazia wale waishio gizani na katika uvuli wa mauti, kuiongoza miguu yetu katika njia ya amani.” Ukurasa Kuu |
www.allmightywind.com | www.almightywind.com Please go to the other if one is off line. We are Sabbath-Keepers, Not Seventh-Day Adventists Click Here For More Info Mailing and Email Addresses |