Ukurasa 1    Ukurasa 2    Ukurasa 3    Ukurasa 4
Ukurasa Kuu






USIKU 4:

Hesabu 7:30-36
Siku ya nne Elisuri mwana wa Shedeuri, kiongozi wa kabila la Reubeni alileta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, lililojazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano,mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wenye mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Elisuri mwana wa Shedeuri.

Isaya 42:5-7
Hili ndilo asemalo Mungu, YAHUVEH--yeye aliyeziumba mbingu na kuzitanda, aliyeitandaza dunia na vyote vitokavyo humo, awapaye watu wake pumzi na uzima kwa wale waendao humo. “Mimi, YAHUVEH, nimekuita katika haki, nitakushika mkono wako, nitakulinda na kukufanya kuwa agano kwa ajili ya watu na nuru kwa Mataifa, kuwafungua macho wale wasioona, kuwaacha huru kutoka kifungoni waliofungwa jela, na kuwafungua kutoka gerezani wale wanaokaa gizani.

Isaya 45:6-7
Mimi ninaumba nuru na kuhuluku giza, ninaleta mafanikio na kusababisha maafa, Mimi, YAHUVEH, hufanya vitu hivi vyote.

Isaya 42:16
Nitawaongoza vipofu kwenye njia ambayo hawajaijua, kwenye mapito wasiyoyazoea nitawaongoza, nitafanya giza kuwa nuru mbele yao na kufanya mahali palipoparuza kuwa laini. Haya ndiyo mambo nitakayofanya, mimi sitawaacha.

Luka 2:25-35
Basi alikuwako huko Yerusalemu mtu mmoja jina lake Simeoni, ambaye alikuwa mwenye haki na mcha Mungu, akitarajia faraja ya Israeli na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake. Roho Mtakatifu alikuwa amemfunulia kuwa hatakufa kabla hajamwona Kristo wa YAHUVEH. Simeoni akiwa ameongozwa na Roho “YAHUVEH Mungu Mwenyezi, kama ulivyoahidi, sasa wamruhusu mtumishi wako aende zake kwa amani. Kwa maana macho yangu yameuona wokovu Wako, ulioweka tayari machoni pa watu wote, nuru kwa ajili ya ufunuo kwa watu Mataifa na kwa ajili ya utukufu kwa watu wako Israeli.” Naye Yosefu na mama yake mtoto wakastaajabu kwa yale yaliyokuwa yamesemwa kumhusu huyo mtoto. Kisha Simeoni akawabariki, akamwambia Maria mama yake, “Mtoto huyu amewekwa kwa makusudi ya kuanguka na kuinuka kwa wengi katika Israeli. Atakuwa ishara ambayo watu watanena dhidi yake, ili mawazo ya mioyo mingi yadhihirike na upanga utauchoma moyo wako.




USIKU 5:

Hesabu 7:36-41
Siku ya tano Shelumieli mwana wa Surishadai, kiongozi wa watu wa Simeoni, alileta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kwa kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi likiwa limejazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, pamoja na maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Shelumieli mwana wa Surishadai.

Zaburi 13:4
Adui yangu atasema, ‘‘nimemshinda,’’ adui zangu watashangilia nitakapoanguka.

Zaburi 139:12
Hata giza halitakuwa giza kwako, usiku utang'aa kama mchana, kwa kuwa giza ni kama nuru kwako.’’

Danieli 9:17
Basi YAHUVEH wetu, sasa sikia maombi na dua ya mtumishi wako. Ee YAHUVEH, kwa ajili yako tuangalie kwa huruma kuhusu ukiwa wa mahali pako patakatifu.

Zaburi 43:3
Tuma hima nuru yako na kweli yako na viniongoze, vinilete mpaka mlima wako mtakatifu, mpaka mahali unapoishi.

Zaburi 36:10
Ongeza upendo wako kwa wale wanaokujua wewe, haki yako kwa wale walio wanyofu wa moyo.

Zaburi 18:29
Kwa msaada wako nitashinda jeshi, nikiwa pamoja na YAHUVEH wangu nitaweza kuruka ukuta.

Mithali 20:27
Taa ya YAHUVEH huchunguza roho ya mwanadamu, huchunguza utu wake wa ndani.

Zaburi 56:13
Kwa kuwa umeniokoa toka kwenye mauti na miguu yangu kwenye kujikwaa, ili kwamba niweze kuenenda mbele za YAHUVEH katika nuru ya uzima.

Ayubu 33:29-30
‘‘YAHUVEH hufanya haya yote kwa mwanadamu--mara mbili, hata mara tatu--ili aigeuze nafsi yake toka shimoni, ili nuru ya uzima imwangazie.

Yohana 9:1-7
YAHUSHUA alipokuwa akipita, akamwona mtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa. Wanafunzi Wake wakamwuliza, “Rabi, ni nani aliyetenda dhambi, ni huyu mtu au wazazi wake hata azaliwe kipofu?’’ YAHUSHUA akawajibu, “Huyu mtu wala wazazi wake hawakutenda dhambi. Alizaliwa kipofu ili kazi za Mungu zidhihirishwe katika maisha yake. Yanipasa kuzifanya kazi zake Yeye aliyenituma wakati bado ni mchana, kwa kuwa usiku waja ambapo hakuna mtu awezaye kufanya kazi. Wakati niko ulimwenguni, Mimi ni nuru ya ulimwengu.’’ Baada ya kusema haya, akatema mate ardhini, akatengeneza tope kwa mate na kumpaka yule mtu kipofu machoni. Kisha akamwambia, “Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu.” (Siloamu, maana yake ni aliyetumwa.) Ndipo yule kipofu akaenda, akanawa, naye akarudi akiwa anaona.


Ukurasa 1    Ukurasa 2    Ukurasa 3    Ukurasa 4
Ukurasa Kuu








ALPHA & OMEGA ALMIGHTYWIND RUACH HA KODESH WILDFIRE LAST CHANCE MINISTRY



www.allmightywind.com  |   www.almightywind.com
Please go to the other if one is off line.

We are Sabbath-Keepers, Not Seventh-Day Adventists
Click Here For More Info


Mailing and Email Addresses


By Faith Enoch was translated that he should not see death: and was not found, because YAHUVEH had translated him: for before his translation he had this testimony, that he pleased YAHUVEH. Hebrews 11:5

By Faith Enoch was translated that he should not see death: and was not found, because YAHUVEH had translated him: for before his translation he had this testimony, that he pleased YAHUVEH. Hebrews 11:5