Bonyeza kwenye mshumaa juu ya sanduku zenye nambari, na vuta na kuuweka kwenye Menorah kwa SIKU ya 2. Mishumaa inawekwa kutoka upande wa kulia hadi kushoto |
SIKU ya 2
Mapenzi yako yawe, YAHUVEH, Muumba wangu na Baba Yangu katika jina la YAHUSHUA, kwamba wakati huu uwe wakati wa Baraka mbele YAKO tunapofuata kuwasha kwa taa ya Chanukah, kama kumbusho ya kwamba nuru inayong’aa zaidi Uliyoituma hapa duniani, Mwana WAKO wa pekee YAHUSHUA MASIHI. Na kumbusho kuwa YEYE Alikuwa tumboni mwa mamake wakati wa Hanukkah (na kuzaliwa miezi tisa ifuatayo wakati wa Succot, Sikukuu ya Vibanda). Hii ndiyo sababu nyingine tunasherehekea sikukuu ya nuru. Taa za mafuta huzimwa baada ya siku nane. YAHUSHUA, nuru inayong’aa iliyotumwa hapa duniani, mafuta ya maisha ya kweli, Atadumu MILELE. Tunasherehekea muujiza huu wa taa zote mbili. YAHUSHUA Ndiye MENORAH INAYOISHI. MWANGAZA WA MILELE ambao HAUTAWAHI kuzimwa! Asante YAHUSHUA kwa kumpa Elisheva (Elisabeth) ufunuo huu Novemba 23, 2005. ‘Kwa kuwa ni Wewe YAHUVEH Utakayewasha taa yangu, katika jina la YAHUSHUA, Atakayemulika giza yangu.’ Tuma nuru YAKO na ukweli WAKO, kwa kuwa tunatafuta ukweli wako kupitia RUACH HA KODESH (Roho Mtakatifu), Atakayeniongoza mimi kuogopa na kupenda Majina Yenu Matakatifu, kusoma na kuweka na kufunza Torah Yenu Takatifu, Torah Iliyoandikwa, na Torah Iliyozungumzwa kama vile Neno Lililofanywa kuwa mwili, Mwana wako wa pekee, YAHUSHUA MASIHI. Na kwa bidii kuu kuheshimu Jina Lako lililobarikiwa na kuinuliwa, Jina la YAHUVEH na Mwana wako, YAHUSHUA. Kwa minajili ya taa za Chanukah, tufanye tuwe wenye hekima kupitia mwangaza unaoishi unaotuongoza, YAHUSHUA, Torah wako Anayeishi. Neno hili litimizwe, kama ilivyoandikwa: ‘“Haitapotea mdomoni mwako, mdomoni mwa watoto wako na kutoka mdomoni mwa watoto wa watoto wako”, ndivyo Asemavyo YAHUVEH, “kutoka sasa hadi milele”.’ Watoto wangu na wajukuu wangu watii Torah na wawe watu waaminifu, na uwape nguvu katika kutii Torah na kukutii wewe, inavyoambatana na mipango Yako mizuri. Nifanikiwe kuona watoto na wajukuu wakijihusisha kwa Torah na amri zako kwa ukweli. Fungua macho yetu ili tuweze kuelewa maajabu Yako ya Torah takatifu kuweza kueleza ukweli wa Torah na maajabu yake yote. Safisha mioyo yetu kwa kukutumikia Wewe, tuweke mbali na maovu na fikra chafu, macho yetu ione kurudi kwake Mwana wako mpendwa YAHUSHUA Atakayekuja na kutawala pale Yerusalemu kama Mfalme wa Wafalme na BWANA wa MABWANA. Ba-rucha-tah Adonai E-lo-hei-nu, Mel-ech ha-olam, Tunakubariki ewe YAHUVEH Mungu wetu, mfalme wa ulimwengu, Asher kideshanu be-mitzvotav, Uliyetutakasa kwa Neno lako, ve-tzivanu le-hadlik ner shel Chanukah. na kutuagiza tuwashe taa za Chanukah. Al Ha-Nissim (Inasemwa usiku zote nane) Ha-ne-roth hal-la-lu, a-nach-nu mad-li-kin al ha-nis-sim, Tunawasha hizi taa kwa ajili ya miujiza, v’al hat-shu-oth v’al ha-nif-la-oth she-o-see-ta la-avo-tei-nu, ukombozi na maajabu Wewe Umewatendea baba zetu wa kale, al y’de ko-ha-ne-cho, hak-k’do- shim. V’chol sh’-mo-nath y’may kupitia makuhani Wako watakatifu. Siku zote nane za chanu-kah, han-ne-roth hal-lo-lu ko-desh; v’ain lo-nu r’shuth Chanukah, taa hizi ni takatifu, haturuhusiwi kuzitumia vibaya l’hish-ta-mesh bo-hem el-lo lir-o-tom bil-vad. K’de l’ho-doth, lakini tunafaa kuziangalia tu, ili kutoa shukrani L’shim-cha al ni-se-cho, v’al y’shu-o-se-te-cho, v’al nif-l’o-te-cho Katika jina Lako kwa miujiza yako, ukombozi wako na maajabu yako. Ba-ruch a-tah Adonai E-lo-hei-nu, Mel-ech ha-olam, Tunakubariki ewe YAHUVEH, Mungu wetu, mfalme wa ulimwengu, she-a-sa si-sim la-a-avo-tei-nu ba-ya-mim ha-hem ba-ze-man ha-zeh Uliyetenda mambo ya ajabu kwa baba zetu katika nyakati za kale msimu huu. Hesabu 7:18-23 Siku ya pili yake Nethaneli mwana wa Suari, kiongozi wa kabila la Isakari, alileta sadaka yake. Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikawa kimejazwa unga laini uliochanganywa na la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi likiwa limejazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana- kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana- kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Nethaneli mwana wa Suari. Isaiah 5:20-24 Ole wao wanaoita ubaya ni wema na wema ni ubaya, wawekao giza badala ya nuru na nuru badala ya giza, wawekao uchungu badala ya utamu na utamu badala ya uchungu. Ole wao walio na hekima machoni pao wenyewe na kujiona wenye akili machoni pao wenyewe. Ole wao walio mashujaa kwa kunywa mvinyo nao walio hodari katika kuchanganya vileo, wale wanaoachilia wenye hatia kwa kupokea hongo, lakini huwanyima haki wasio na hatia. Kwa hiyo, kama ndimi za moto zirambavyo nyasi na kama vile majani makavu yazamavyo katika miali ya moto, ndivyo mizizi yao itakavyooza na maua yao yatakavyopeperushwa kama mavumbi, kwa kuwa wameikataa sheria ya YAHUVEH Mwenye Nguvu na kulisukumia mbali neno la Aliye Mtakatifu wa Israeli. Matthew 6:22-23 ‘‘Jicho ni taa ya mwili. Kama jicho lako ni nyofu, mwili wako wote utakuwa na nuru. Lakini kama jicho lako ni ovu, mwili wako wote utajawa na giza. Kwa hiyo basi, kama nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza, hilo ni giza kuu namna gani! ”
Rudi kwa Ukurasa wa Hanukkah |
Ukurasa Kuu
|
www.allmightywind.com | www.almightywind.com Please go to the other if one is off line. We are Sabbath-Keepers, Not Seventh-Day Adventists Click Here For More Info Mailing and Email Addresses |