Bonyeza kwenye mshumaa juu ya sanduku zenye nambari, na vuta na kuuweka kwenye Menorah kwa SIKU ya 8. Mishumaa inawekwa kutoka upande wa kulia hadi kushoto |
USIKU 8:
Mapenzi yako yawe, YAHUVEH, Muumba wangu na Baba Yangu katika jina la YAHUSHUA, kwamba wakati huu uwe wakati wa Baraka mbele YAKO tunapofuata kuwasha kwa taa ya Chanukah, kama kumbusho ya kwamba nuru inayong’aa zaidi Uliyoituma hapa duniani, Mwana WAKO wa pekee YAHUSHUA MASIHI. Na kumbusho kuwa YEYE Alikuwa tumboni mwa mamake wakati wa Hanukkah (na kuzaliwa miezi tisa ifuatayo wakati wa Succot, Sikukuu ya Vibanda). Hii ndiyo sababu nyingine tunasherehekea sikukuu ya nuru. Taa za mafuta huzimwa baada ya siku nane. YAHUSHUA, nuru inayong’aa iliyotumwa hapa duniani, mafuta ya maisha ya kweli, Atadumu MILELE. Tunasherehekea muujiza huu wa taa zote mbili. YAHUSHUA Ndiye MENORAH INAYOISHI. MWANGAZA WA MILELE ambao HAUTAWAHI kuzimwa! Asante YAHUSHUA kwa kumpa Elisheva (Elisabeth) ufunuo huu Novemba 23, 2005. ‘Kwa kuwa ni Wewe YAHUVEH Utakayewasha taa yangu, katika jina la YAHUSHUA, Atakayemulika giza yangu.’ Tuma nuru YAKO na ukweli WAKO, kwa kuwa tunatafuta ukweli wako kupitia RUACH HA KODESH (Roho Mtakatifu), Atakayeniongoza mimi kuogopa na kupenda Majina Yenu Matakatifu, kusoma na kuweka na kufunza Torah Yenu Takatifu, Torah Iliyoandikwa, na Torah Iliyozungumzwa kama vile Neno Lililofanywa kuwa mwili, Mwana wako wa pekee, YAHUSHUA MASIHI. Na kwa bidii kuu kuheshimu Jina Lako lililobarikiwa na kuinuliwa, Jina la YAHUVEH na Mwana wako, YAHUSHUA. Kwa minajili ya taa za Chanukah, tufanye tuwe wenye hekima kupitia mwangaza unaoishi unaotuongoza, YAHUSHUA, Torah wako Anayeishi. Neno hili litimizwe, kama ilivyoandikwa: ‘“Haitapotea mdomoni mwako, mdomoni mwa watoto wako na kutoka mdomoni mwa watoto wa watoto wako”, ndivyo Asemavyo YAHUVEH, “kutoka sasa hadi milele”.’ Watoto wangu na wajukuu wangu watii Torah na wawe watu waaminifu, na uwape nguvu katika kutii Torah na kukutii wewe, inavyoambatana na mipango Yako mizuri. Nifanikiwe kuona watoto na wajukuu wakijihusisha kwa Torah na amri zako kwa ukweli. Fungua macho yetu ili tuweze kuelewa maajabu Yako ya Torah takatifu kuweza kueleza ukweli wa Torah na maajabu yake yote. Safisha mioyo yetu kwa kukutumikia Wewe, tuweke mbali na maovu na fikra chafu, macho yetu ione kurudi kwake Mwana wako mpendwa YAHUSHUA Atakayekuja na kutawala pale Yerusalemu kama Mfalme wa Wafalme na BWANA wa MABWANA. Ba-rucha-tah Adonai E-lo-hei-nu, Mel-ech ha-olam, Tunakubariki ewe YAHUVEH Mungu wetu, mfalme wa ulimwengu, Asher kideshanu be-mitzvotav, Uliyetutakasa kwa Neno lako, ve-tzivanu le-hadlik ner shel Chanukah. na kutuagiza tuwashe taa za Chanukah. Al Ha-Nissim (Inasemwa usiku zote nane) Ha-ne-roth hal-la-lu, a-nach-nu mad-li-kin al ha-nis-sim, Tunawasha hizi taa kwa ajili ya miujiza, v’al hat-shu-oth v’al ha-nif-la-oth she-o-see-ta la-avo-tei-nu, ukombozi na maajabu Wewe Umewatendea baba zetu wa kale, al y’de ko-ha-ne-cho, hak-k’do- shim. V’chol sh’-mo-nath y’may kupitia makuhani Wako watakatifu. Siku zote nane za chanu-kah, han-ne-roth hal-lo-lu ko-desh; v’ain lo-nu r’shuth Chanukah, taa hizi ni takatifu, haturuhusiwi kuzitumia vibaya l’hish-ta-mesh bo-hem el-lo lir-o-tom bil-vad. K’de l’ho-doth, lakini tunafaa kuziangalia tu, ili kutoa shukrani L’shim-cha al ni-se-cho, v’al y’shu-o-se-te-cho, v’al nif-l’o-te-cho Katika jina Lako kwa miujiza yako, ukombozi wako na maajabu yako. Ba-ruch a-tah Adonai E-lo-hei-nu, Mel-ech ha-olam, Tunakubariki ewe YAHUVEH, Mungu wetu, mfalme wa ulimwengu, she-a-sa si-sim la-a-avo-tei-nu ba-ya-mim ha-hem ba-ze-man ha-zeh Uliyetenda mambo ya ajabu kwa baba zetu katika nyakati za kale msimu huu. Siku ya nane Gamalieli mwana wa Pedasuri, kiongozi wa watu wa Manase, alileta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, lililojazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mmoja mume kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Gamalieli mwana wa Pedasuri. Siku ya tisa Abidani mwana wa Gideoni kiongozi wa watu wa Benyamini, alileta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, lililojazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mmoja mume kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Abidani mwana wa Gideoni. Siku ya kumi Ahiezeri mwana wa Amishadai, kiongozi wa watu wa Dani, alileta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli mia moja na thelathini na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, lililojazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Ahiezeri mwana wa Amishadai. Siku ya kumi na moja Pagieli mwana wa Okrani, kiongozi wa watu wa Asheri, alileta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta, kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, lililojazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Pagieli mwana wa Okrani. Siku ya kumi na mbili Ahira mwana wa Enani, kiongozi wa watu wa Naftali, alileta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila moja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, lililojazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja, kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Ahira mwana wa Enani. Hizi zilikuwa ndizo sadaka za viongozi wa Israeli madhabahu ilipowekwa wakfu wakati ilipotiwa mafuta, sahani kumi na mbili za fedha, bakuli kumi na mbili za fedha za kunyunyizia na masinia kumi na mawili ya dhahabu. Kila sahani ya fedha ilikuwa na uzito wa shekeli 130, na kila bakuli la fedha la kunyunyizia lilikuwa na uzito wa shekeli sabini. Masinia kumi na mawili yalikuwa na uzito wa shekeli 2,400 kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. Sahani kumi na mbili za dhahabu zilizojazwa uvumba zilikuwa na uzito wa shekeli kumi kila moja kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. Zote kwa pamoja, sahani za dhahabu zilikuwa na uzito wa shekeli 120. Jumla ya wanyama waliotolewa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, walikuwa fahali kumi na wawili wachanga, kondoo waume kumi na wawili, na wana-kondoo waume kumi na wawili wa mwaka mmoja, pamoja na sadaka zao za nafaka. Mbuzi waume kumi na wawili walitolewa kwa ajili ya sadaka za dhambi. Jumla ya wanyama kwa ajili ya dhabihu ya sadaka ya amani walikuwa maksai ishirini na wanne, kondoo waume sitini, mbuzi waume sitini na wana-kondoo waume wa mwaka mmoja sitini. Hizi zilikuwa ndizo sadaka zilizoletwa kwa ajili ya kuwekwa wakfu kwa madhabahu baada ya kutiwa mafuta. Mose alipoingia kwenye Hema la Mkutano kuzungumza na YAHUVEH, alisikia sauti ikisema naye kutoka kati ya wale makerubi wawili waliokuwa juu ya kile kiti cha rehema, juu ya sanduku la Ushuhuda. Mose akazungumza naye. YAHUVEH akamwambia Mose, “Sema na Aroni umwambie, ‘Wakati utakapoziweka zile taa saba, zinatakiwa kuangaza eneo lililo mbele ya kinara cha taa.’ ’’ Aroni akafanya hivyo, akaziweka zile taa ili zielekee mbele kwenye kinara cha taa, kama vile YAHUVEH alivyomwamuru Mose. Hivi ndivyo kinara cha taa kilivyotengenezwa: Kilitengenezwa kwa dhahabu iliyofuliwa, kuanzia kwenye kitako chake hadi kwenye maua yake. Kinara cha taa kilitengenezwa sawasawa kabisa na kielelezo ambacho YAHUVEH alikuwa amemwonyesha Mose. Isaya 30:26 Mwezi utaangaza kama jua, nao mwanga wa jua utang’aa mara saba zaidi, kama nuru ya siku saba, wakati YAHUVEH atakapoyafunga majeraha ya watu wake na kuponya vidonda alivyowatia. Zekaria 14:6-7 Siku hiyo hakutakuwepo nuru, baridi wala theluji. Itakuwa siku ya kipekee, isiyo na mchana wala usiku, siku ijulikanayo na YAHUVEH. Jioni inapofika nuru itakuwepo. Isaya 60:19-20 Luka 1:67-79 Zekaria, baba yake, akajazwa na Roho Mtakatifu, naye akatoa unabii akisema: “Ahimidiwe YAHUVEH, Mungu wa Israeli, kwa kuwa amewajilia Watu wake na kuwakomboa. Naye ametusimamishia pembe ya wokovu katika nyumba ya Daudi mtumishi Wake, kama alivyonena kwa vinywa vya manabii wake watakatifu tangu zamani, kwamba atatuokoa kutoka kwa adui zetu na kutoka mikononi mwao wote watuchukiao, ili kuonyesha rehema kwa baba zetu na kukumbuka agano lake takatifu, kiapo alichomwapia baba yetu Abrahamu: kutuokoa kutoka mkononi mwa adui zetu, tupate kumtumikia Yeye pasipo hofu katika utakatifu na haki mbele Zake, siku zetu zote. Nawe mtoto wangu, utaitwa nabii wa Aliye Juu, kwa kuwa utamtangulia YAHUVEH na kuandaa njia kwa ajili Yake, kuwajulisha watu Wake juu ya wokovu utakaopatikana kwa kusamehewa dhambi zao, kwa ajili ya wingi wa rehema za Mungu wetu, nuru itokayo juu itatuzukia ili kuwaangazia wale waishio gizani na katika uvuli wa mauti, kuiongoza miguu yetu katika njia ya amani.”
Rudi kwa Ukurasa wa Hanukkah |
Ukurasa Kuu
|
www.allmightywind.com | www.almightywind.com Please go to the other if one is off line. We are Sabbath-Keepers, Not Seventh-Day Adventists Click Here For More Info Mailing and Email Addresses |