Rudi kwa Ukurasa wa Hanukkah  |   Ukurasa Kuu  |   Menorah iliyo kwenye Mtandao Ukurasa 1

Menorah Yako
Kutumika Siku Nane za Hanukkah!
Shalom!


SIKU ya 7


Hanukkah candle
Menorah iliyo kwenye Mtandao Ukurasa Kuu

Bonyeza kwenye mshumaa juu ya sanduku zenye nambari,
na vuta na kuuweka kwenye Menorah kwa
SIKU ya 7.
Mishumaa inawekwa kutoka upande wa kulia hadi kushoto


SIKU ya 7


Maombi yanayosemwa wakati menorah inapowashwa:

Mapenzi yako yawe, YAHUVEH, Muumba wangu na Baba Yangu katika jina la YAHUSHUA, kwamba wakati huu uwe wakati wa Baraka mbele YAKO tunapofuata kuwasha kwa taa ya Chanukah, kama kumbusho ya kwamba nuru inayong’aa zaidi Uliyoituma hapa duniani, Mwana WAKO wa pekee YAHUSHUA MASIHI. Na kumbusho kuwa YEYE Alikuwa tumboni mwa mamake wakati wa Hanukkah (na kuzaliwa miezi tisa ifuatayo wakati wa Succot, Sikukuu ya Vibanda).

Hii ndiyo sababu nyingine tunasherehekea sikukuu ya nuru. Taa za mafuta huzimwa baada ya siku nane. YAHUSHUA, nuru inayong’aa iliyotumwa hapa duniani, mafuta ya maisha ya kweli, Atadumu MILELE. Tunasherehekea muujiza huu wa taa zote mbili. YAHUSHUA Ndiye MENORAH INAYOISHI. MWANGAZA WA MILELE ambao HAUTAWAHI kuzimwa!

Asante YAHUSHUA kwa kumpa Elisheva (Elisabeth) ufunuo huu Novemba 23, 2005. ‘Kwa kuwa ni Wewe YAHUVEH Utakayewasha taa yangu, katika jina la YAHUSHUA, Atakayemulika giza yangu.’

Tuma nuru YAKO na ukweli WAKO, kwa kuwa tunatafuta ukweli wako kupitia RUACH HA KODESH (Roho Mtakatifu), Atakayeniongoza mimi kuogopa na kupenda Majina Yenu Matakatifu, kusoma na kuweka na kufunza Torah Yenu Takatifu, Torah Iliyoandikwa, na Torah Iliyozungumzwa kama vile Neno Lililofanywa kuwa mwili, Mwana wako wa pekee, YAHUSHUA MASIHI. Na kwa bidii kuu kuheshimu Jina Lako lililobarikiwa na kuinuliwa, Jina la YAHUVEH na Mwana wako, YAHUSHUA.

Kwa minajili ya taa za Chanukah, tufanye tuwe wenye hekima kupitia mwangaza unaoishi unaotuongoza, YAHUSHUA, Torah wako Anayeishi. Neno hili litimizwe, kama ilivyoandikwa: ‘“Haitapotea mdomoni mwako, mdomoni mwa watoto wako na kutoka mdomoni mwa watoto wa watoto wako”, ndivyo Asemavyo YAHUVEH, “kutoka sasa hadi milele”.’ Watoto wangu na wajukuu wangu watii Torah na wawe watu waaminifu, na uwape nguvu katika kutii Torah na kukutii wewe, inavyoambatana na mipango Yako mizuri. Nifanikiwe kuona watoto na wajukuu wakijihusisha kwa Torah na amri zako kwa ukweli.

Fungua macho yetu ili tuweze kuelewa maajabu Yako ya Torah takatifu kuweza kueleza ukweli wa Torah na maajabu yake yote. Safisha mioyo yetu kwa kukutumikia Wewe, tuweke mbali na maovu na fikra chafu, macho yetu ione kurudi kwake Mwana wako mpendwa YAHUSHUA Atakayekuja na kutawala pale Yerusalemu kama Mfalme wa Wafalme na BWANA wa MABWANA.



Baraka za Mshumaa

Ba-rucha-tah Adonai E-lo-hei-nu, Mel-ech ha-olam,

Tunakubariki ewe YAHUVEH Mungu wetu, mfalme wa ulimwengu,

Asher kideshanu be-mitzvotav,

Uliyetutakasa kwa Neno lako,

ve-tzivanu le-hadlik ner shel Chanukah.

na kutuagiza tuwashe taa za Chanukah.

Al Ha-Nissim

(Inasemwa usiku zote nane)

Ha-ne-roth hal-la-lu, a-nach-nu mad-li-kin al ha-nis-sim,

Tunawasha hizi taa kwa ajili ya miujiza,

v’al hat-shu-oth v’al ha-nif-la-oth she-o-see-ta la-avo-tei-nu,

ukombozi na maajabu Wewe Umewatendea baba zetu wa kale,

al y’de ko-ha-ne-cho, hak-k’do- shim. V’chol sh’-mo-nath y’may

kupitia makuhani Wako watakatifu. Siku zote nane za

chanu-kah, han-ne-roth hal-lo-lu ko-desh; v’ain lo-nu r’shuth

Chanukah, taa hizi ni takatifu, haturuhusiwi kuzitumia vibaya

l’hish-ta-mesh bo-hem el-lo lir-o-tom bil-vad. K’de l’ho-doth,

lakini tunafaa kuziangalia tu, ili kutoa shukrani

L’shim-cha al ni-se-cho, v’al y’shu-o-se-te-cho, v’al nif-l’o-te-cho

Katika jina Lako kwa miujiza yako, ukombozi wako na maajabu yako.

Ba-ruch a-tah Adonai E-lo-hei-nu, Mel-ech ha-olam,

Tunakubariki ewe YAHUVEH, Mungu wetu, mfalme wa ulimwengu,

she-a-sa si-sim la-a-avo-tei-nu ba-ya-mim ha-hem ba-ze-man ha-zeh

Uliyetenda mambo ya ajabu kwa baba zetu katika nyakati za kale msimu huu.


USIKU 7:

Hesabu 7:48-53
Siku ya saba Elishama mwana wa Amihudi, kiongozi wa watu wa Efraimu alileta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, lililojazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano, na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Elishama mwana wa Amihudi.

Mithali 4:18
Njia ya wenye haki ni kama nuru ya kwanza ya mapambazuko, ambayo hung’aa zaidi na zaidi mpaka mchana mkamilifu.

Zaburi 97:11-12
Nuru huangaza wenye haki na furaha kwa watu wanyofu wa moyo. Furahini katika YAHUVEH, ninyi mlio wenye haki, lisifuni jina lake takatifu.

Isaya 9:1-2
Hata hivyo, hapatakuwepo huzuni zaidi kwa wale waliokuwa katika dhiki. Wakati uliopita aliidhili nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, lakini katika siku zijazo ataiheshimu Galilaya ya Mataifa, karibu na njia ya bahari, kando ya Yordani-- Watu wanaotembea katika giza wameona nuru kuu, wale wanaoishi katika nchi ya uvuli wa mauti, nuru imewazukia.

Kutoka 10:23
Hakuna mtu yeyote aliyeweza kumwona mwenzake, wala kuondoka mahali alipokuwa kwa muda wa siku tatu. Lakini Waisraeli wote walikuwa na mwanga katika maeneo yao waliyokuwa wanaishi.

Isaya 60:1
“Ondoka, angaza, kwa kuwa nuru yako imekuja na utukufu wa YAHUVEH unaangaza juu yako.

Isaya 2:5
Njooni, Enyi nyumba ya Yakobo, sisi na tutembee katika nuru ya YAHUVEH.

Mathayo 4:12-17
YAHUSHUA aliposikia kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa ametiwa gerezani, alirudi Galilaya. Akaondoka Nazareti akaenda kuishi Kapernaumu ulioko karibu na bahari, katika mipaka ya nchi ya Zabuloni na ya Naftali, ili kutimiza unabii wa nabii Isaya, kama alivyosema: “Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, kwenye njia ya kuelekea baharini, ng'ambo ya Yordani, Galilaya ya watu Mataifa, watu wale waliokaa gizani wameona nuru kuu nao wale waliokaa katika nchi ya uvuli wa mauti, nuru imewazukia.’’ Tangu wakati huo, YAHUSHUA alianza kuhubiri akisema: “Tubuni, kwa maana Ufalme wa Mbinguni umekaribia.’’

* * * * * * * * * * * * * *

Maandiko spesheli ya Sabato wakati wa Hanukkah.

Hesabu 7:1-11
Mose alipomaliza kuisimamisha maskani ya YAHUVEH, aliitia mafuta na kuiweka wakfu pamoja na samani zake zote. Pia alitia madhabahu mafuta na kuweka wakfu pamoja na vyombo vyake vyote. Ndipo viongozi wa Israeli, wakuu wa jamaa waliokuwa viongozi wa kabila wasimamizi wa wale waliohesabiwa, wakatoa sadaka. Walizileta kama matoleo yao mbele za YAHUVEH magari sita ya kukokotwa yaliyofunikwa pamoja na maksai kumi na wawili, yaani, maksai mmoja kutoka kwa kila kiongozi na gari moja la kukokotwa kutoka kwa kila viongozi wawili. Haya waliyaleta mbele ya maskani ya YAHUVEH. YAHUVEH akamwambia Mose, “Vikubali vitu hivi kutoka kwao, ili viweze kutumika katika kazi kwenye Hema la Mkutano. Wapatie Walawi kama kazi ya kila mtu itakavyohitaji.’’ Hivyo Mose akachukua yale magari ya kukokotwa pamoja na maksai na kuwapa Walawi. Aliwapa Wagershoni magari mawili ya kukokotwa na maksai wanne, kama walivyohitaji kwa kazi yao, pia aliwapa Wamerari magari manne ya kukokotwa na maksai wanane, kama kazi yao ilivyohitaji. Wote walikuwa chini ya maelekezo ya Ithamari mwana wa kuhani Aroni. Lakini Mose hakuwapa Wakohathi chochote kati ya hivyo, kwa sababu walitakiwa kubeba vitu vitakatifu mabegani mwao, kwa kuwa walikuwa wanawajibika. Wakati madhabahu ilipotiwa mafuta, viongozi walileta sadaka zao kwa ajili ya kule kuwekwa wakfu kwake na kuziweka mbele ya madhabahu. Kwa maana YAHUVEH alikuwa amemwambia Mose, “Kila siku kiongozi mmoja ataleta sadaka yake ili kuwekwa wakfu madhabahu.’’

Hesabu 7:12-59
Yule ambaye alileta sadaka yake siku ya kwanza alikuwa Nashoni mwana wa Aminadabu wa kabila la Yuda. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumic, lililojazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Nashoni mwana wa Aminadabu.

Siku ya pili yake Nethaneli mwana wa Suari, kiongozi wa kabila la Isakari, alileta sadaka yake. Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikawa kimejazwa unga laini uliochanganywa na la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi likiwa limejazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana- kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana- kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Nethaneli mwana wa Suari.

Siku ya tatu, Eliabu mwana wa Heloni, kiongozi wa kabila la Zabuloni, alileta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana- kondoo wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana- kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Eliabu mwana wa Heloni.

Siku ya nne Elisuri mwana wa Shedeuri, kiongozi wa kabila la Reubeni alileta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, lililojazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano,mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wenye mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Elisuri mwana wa Shedeuri.

Siku ya tano Shelumieli mwana wa Surishadai, kiongozi wa watu wa Simeoni, alileta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kwa kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi likiwa limejazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, pamoja na maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Shelumieli mwana wa Surishadai.

Siku ya sita Eliasafu mwana wa Deueli, kiongozi wa watu wa Gadi, akaleta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kwa kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, lililojazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Eliasafu mwana wa Deueli.

Siku ya saba Elishama mwana wa Amihudi, kiongozi wa watu wa Efraimu alileta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, lililojazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano, na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Elishama mwana wa Amihudi.

Siku ya nane Gamalieli mwana wa Pedasuri, kiongozi wa watu wa Manase, alileta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, lililojazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mmoja mume kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Gamalieli mwana wa Pedasuri.

Zekaria 2:13 - 4:7
Tulieni mbele za YAHUVEH, enyi watu wote, kwa sababu ameinuka kutoka makao yake matakatifu.” Kisha akanionyesha Yoshua kuhani mkuu akiwa amesimama mbele ya malaika wa YAHUVEH, naye Shetani amesimama upande wake wa kuume ili amshitaki. YAHUVEH akamwambia Shetani, “YAHUVEH akukemee Shetani! YAHUVEH, ambaye ameichagua Yerusalemu, akukemee! Je, mtu huyu siyo kijinga kinachowaka kilichonyakuliwa kwenye moto?’’ Wakati huu, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu alipokuwa amesimama mbele ya malaika. Malaika akawaambia wale waliokuwa wamesimama mbele yake, ‘‘Mvueni nguo zake chafu.’’ Kisha akamwambia Yoshua, ‘‘Tazama, nimeiondoa dhambi yako, nami nitakuvika mavazi ya kitajiri.’’ Kisha nikasema, “Mvike kilemba kilicho safi kichwani mwake.’’ Kwa hiyo wakamvika kilemba safi kichwani na kumvika yale mavazi mengine, wakati malaika wa YAHUVEH akiwa amesimama karibu.

Malaika wa YAHUVEH akamwamuru Yoshua: “Hivi ndivyo asemavyo YAHUVEH Mwenye Nguvu: ‘Ikiwa utakwenda katika njia zangu na kushika masharti yangu, basi utaitawala nyumba yangu na kuwa na amri juu ya nyua zangu, nami nitakupa nafasi miongoni mwa hawa wasimamao hapa. ‘‘ ‘Sikiliza, Ee Yoshua kuhani mkuu, pamoja na wenzako walioketi mbele yako, ambao ni watu ishara ya mambo yatakayokuja: Ninakwenda kumleta mtumishi wangu, Tawi. Tazama, jiwe nililoliweka mbele ya Yoshua! Kuna macho saba juu ya jiwe lile moja, nami nitachora maandishi juu yake,’ asema YAHUVEH Mwenye Nguvu, ‘nami nitaiondoa dhambi ya nchi hii kwa siku moja. “ ‘Katika siku hiyo kila mmoja wenu atamwalika jirani yake akae chini ya mzabibu wake na mtini wake,’ asema YAHUVEH Mwenye Nguvu.’

Kisha malaika aliyezungumza nami akarudi na kuniamsha, kama mtu aamshwavyo kutoka katika usingizi wake. Akaniuliza, “Unaona nini?’’ Nikajibu, “Ninaona kinara cha taa cha dhahabu tupu, nacho kina bakuli juu yake na taa zake saba juu yake, tena iko mirija saba ya kuleta mafuta, kwenye taa zote zilizo juu yake. Pia kuna mizeituni miwili karibu yake, mmoja upande wa kuume wa bakuli na mwingine upande wa kushoto.’’ Nikamuuliza malaika aliyezungumza nami, “Hivi ni vitu gani, YAHUVEH wangu?’’ Akanijibu, “Hujui kuwa hivi ni vitu gani?’’ Nikajibu, “Hapana, YAHUVEH wangu.’’ Kisha akaniambia, “Hili ni neno la YAHUVEH kwa Zerubabeli: ‘Si kwa nguvu, wala si kwa uwezo, bali ni kwa Roho yangu,’ asema YAHUVEH Mwenye Nguvu. ‘‘Wewe ni kitu gani, Ee mlima mkubwa sana? Mbele ya Zerubabeli wewe utakuwa ardhi tambarare. Kisha ataweka jiwe la juu kabisa la mwisho na watu wakipiga kelele wakisema, ‘YAHUVEH libariki! YAHUVEH libariki!’’









ALPHA & OMEGA ALMIGHTYWIND RUACH HA KODESH WILDFIRE LAST CHANCE MINISTRY



www.allmightywind.com  |   www.almightywind.com
Please go to the other if one is off line.

We are Sabbath-Keepers, Not Seventh-Day Adventists
Click Here For More Info


Mailing and Email Addresses




By Faith Enoch was translated that he should not see death: and was not found, because YAHUVEH had translated him: for before his translation he had this testimony, that he pleased YAHUVEH. Hebrews 11:5