Bonyeza kwenye mshumaa juu ya sanduku zenye nambari, na vuta na kuuweka kwenye Menorah kwa SIKU ya 5. Mishumaa inawekwa kutoka upande wa kulia hadi kushoto |
SIKU ya 5
Mapenzi yako yawe, YAHUVEH, Muumba wangu na Baba Yangu katika jina la YAHUSHUA, kwamba wakati huu uwe wakati wa Baraka mbele YAKO tunapofuata kuwasha kwa taa ya Chanukah, kama kumbusho ya kwamba nuru inayong’aa zaidi Uliyoituma hapa duniani, Mwana WAKO wa pekee YAHUSHUA MASIHI. Na kumbusho kuwa YEYE Alikuwa tumboni mwa mamake wakati wa Hanukkah (na kuzaliwa miezi tisa ifuatayo wakati wa Succot, Sikukuu ya Vibanda). Hii ndiyo sababu nyingine tunasherehekea sikukuu ya nuru. Taa za mafuta huzimwa baada ya siku nane. YAHUSHUA, nuru inayong’aa iliyotumwa hapa duniani, mafuta ya maisha ya kweli, Atadumu MILELE. Tunasherehekea muujiza huu wa taa zote mbili. YAHUSHUA Ndiye MENORAH INAYOISHI. MWANGAZA WA MILELE ambao HAUTAWAHI kuzimwa! Asante YAHUSHUA kwa kumpa Elisheva (Elisabeth) ufunuo huu Novemba 23, 2005. ‘Kwa kuwa ni Wewe YAHUVEH Utakayewasha taa yangu, katika jina la YAHUSHUA, Atakayemulika giza yangu.’ Tuma nuru YAKO na ukweli WAKO, kwa kuwa tunatafuta ukweli wako kupitia RUACH HA KODESH (Roho Mtakatifu), Atakayeniongoza mimi kuogopa na kupenda Majina Yenu Matakatifu, kusoma na kuweka na kufunza Torah Yenu Takatifu, Torah Iliyoandikwa, na Torah Iliyozungumzwa kama vile Neno Lililofanywa kuwa mwili, Mwana wako wa pekee, YAHUSHUA MASIHI. Na kwa bidii kuu kuheshimu Jina Lako lililobarikiwa na kuinuliwa, Jina la YAHUVEH na Mwana wako, YAHUSHUA. Kwa minajili ya taa za Chanukah, tufanye tuwe wenye hekima kupitia mwangaza unaoishi unaotuongoza, YAHUSHUA, Torah wako Anayeishi. Neno hili litimizwe, kama ilivyoandikwa: ‘“Haitapotea mdomoni mwako, mdomoni mwa watoto wako na kutoka mdomoni mwa watoto wa watoto wako”, ndivyo Asemavyo YAHUVEH, “kutoka sasa hadi milele”.’ Watoto wangu na wajukuu wangu watii Torah na wawe watu waaminifu, na uwape nguvu katika kutii Torah na kukutii wewe, inavyoambatana na mipango Yako mizuri. Nifanikiwe kuona watoto na wajukuu wakijihusisha kwa Torah na amri zako kwa ukweli. Fungua macho yetu ili tuweze kuelewa maajabu Yako ya Torah takatifu kuweza kueleza ukweli wa Torah na maajabu yake yote. Safisha mioyo yetu kwa kukutumikia Wewe, tuweke mbali na maovu na fikra chafu, macho yetu ione kurudi kwake Mwana wako mpendwa YAHUSHUA Atakayekuja na kutawala pale Yerusalemu kama Mfalme wa Wafalme na BWANA wa MABWANA. Ba-rucha-tah Adonai E-lo-hei-nu, Mel-ech ha-olam, Tunakubariki ewe YAHUVEH Mungu wetu, mfalme wa ulimwengu, Asher kideshanu be-mitzvotav, Uliyetutakasa kwa Neno lako, ve-tzivanu le-hadlik ner shel Chanukah. na kutuagiza tuwashe taa za Chanukah. Al Ha-Nissim (Inasemwa usiku zote nane) Ha-ne-roth hal-la-lu, a-nach-nu mad-li-kin al ha-nis-sim, Tunawasha hizi taa kwa ajili ya miujiza, v’al hat-shu-oth v’al ha-nif-la-oth she-o-see-ta la-avo-tei-nu, ukombozi na maajabu Wewe Umewatendea baba zetu wa kale, al y’de ko-ha-ne-cho, hak-k’do- shim. V’chol sh’-mo-nath y’may kupitia makuhani Wako watakatifu. Siku zote nane za chanu-kah, han-ne-roth hal-lo-lu ko-desh; v’ain lo-nu r’shuth Chanukah, taa hizi ni takatifu, haturuhusiwi kuzitumia vibaya l’hish-ta-mesh bo-hem el-lo lir-o-tom bil-vad. K’de l’ho-doth, lakini tunafaa kuziangalia tu, ili kutoa shukrani L’shim-cha al ni-se-cho, v’al y’shu-o-se-te-cho, v’al nif-l’o-te-cho Katika jina Lako kwa miujiza yako, ukombozi wako na maajabu yako. Ba-ruch a-tah Adonai E-lo-hei-nu, Mel-ech ha-olam, Tunakubariki ewe YAHUVEH, Mungu wetu, mfalme wa ulimwengu, she-a-sa si-sim la-a-avo-tei-nu ba-ya-mim ha-hem ba-ze-man ha-zeh Uliyetenda mambo ya ajabu kwa baba zetu katika nyakati za kale msimu huu. Siku ya tano Shelumieli mwana wa Surishadai, kiongozi wa watu wa Simeoni, alileta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kwa kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi likiwa limejazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, pamoja na maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Shelumieli mwana wa Surishadai. Zaburi 13:4 Adui yangu atasema, ‘‘nimemshinda,’’ adui zangu watashangilia nitakapoanguka. Zaburi 139:12 Hata giza halitakuwa giza kwako, usiku utang'aa kama mchana, kwa kuwa giza ni kama nuru kwako.’’ Danieli 9:17 Basi YAHUVEH wetu, sasa sikia maombi na dua ya mtumishi wako. Ee YAHUVEH, kwa ajili yako tuangalie kwa huruma kuhusu ukiwa wa mahali pako patakatifu. Zaburi 43:3 Tuma hima nuru yako na kweli yako na viniongoze, vinilete mpaka mlima wako mtakatifu, mpaka mahali unapoishi. Zaburi 36:10 Ongeza upendo wako kwa wale wanaokujua wewe, haki yako kwa wale walio wanyofu wa moyo. Zaburi 18:29 Kwa msaada wako nitashinda jeshi, nikiwa pamoja na YAHUVEH wangu nitaweza kuruka ukuta. Mithali 20:27 Taa ya YAHUVEH huchunguza roho ya mwanadamu, huchunguza utu wake wa ndani. Zaburi 56:13 Kwa kuwa umeniokoa toka kwenye mauti na miguu yangu kwenye kujikwaa, ili kwamba niweze kuenenda mbele za YAHUVEH katika nuru ya uzima. Ayubu 33:29-30 ‘‘YAHUVEH hufanya haya yote kwa mwanadamu--mara mbili, hata mara tatu--ili aigeuze nafsi yake toka shimoni, ili nuru ya uzima imwangazie. Yohana 9:1-7 YAHUSHUA alipokuwa akipita, akamwona mtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa. Wanafunzi Wake wakamwuliza, “Rabi, ni nani aliyetenda dhambi, ni huyu mtu au wazazi wake hata azaliwe kipofu?’’ YAHUSHUA akawajibu, “Huyu mtu wala wazazi wake hawakutenda dhambi. Alizaliwa kipofu ili kazi za Mungu zidhihirishwe katika maisha yake. Yanipasa kuzifanya kazi zake Yeye aliyenituma wakati bado ni mchana, kwa kuwa usiku waja ambapo hakuna mtu awezaye kufanya kazi. Wakati niko ulimwenguni, Mimi ni nuru ya ulimwengu.’’ Baada ya kusema haya, akatema mate ardhini, akatengeneza tope kwa mate na kumpaka yule mtu kipofu machoni. Kisha akamwambia, “Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu.” (Siloamu, maana yake ni aliyetumwa.) Ndipo yule kipofu akaenda, akanawa, naye akarudi akiwa anaona.
Rudi kwa Ukurasa wa Hanukkah |
Ukurasa Kuu
|
www.allmightywind.com | www.almightywind.com Please go to the other if one is off line. We are Sabbath-Keepers, Not Seventh-Day Adventists Click Here For More Info Mailing and Email Addresses |