Rudi kwa Ukurasa wa Hanukkah  |   Ukurasa Kuu  |   Menorah iliyo kwenye Mtandao Ukurasa 1

Menorah Yako
Kutumika Siku Nane za Hanukkah!
Shalom!


SIKU ya 6


Hanukkah candle
Menorah iliyo kwenye Mtandao Ukurasa Kuu

Bonyeza kwenye mshumaa juu ya sanduku zenye nambari,
na vuta na kuuweka kwenye Menorah kwa
SIKU ya 6.
Mishumaa inawekwa kutoka upande wa kulia hadi kushoto


SIKU ya 6


Maombi yanayosemwa wakati menorah inapowashwa:

Mapenzi yako yawe, YAHUVEH, Muumba wangu na Baba Yangu katika jina la YAHUSHUA, kwamba wakati huu uwe wakati wa Baraka mbele YAKO tunapofuata kuwasha kwa taa ya Chanukah, kama kumbusho ya kwamba nuru inayong’aa zaidi Uliyoituma hapa duniani, Mwana WAKO wa pekee YAHUSHUA MASIHI. Na kumbusho kuwa YEYE Alikuwa tumboni mwa mamake wakati wa Hanukkah (na kuzaliwa miezi tisa ifuatayo wakati wa Succot, Sikukuu ya Vibanda).

Hii ndiyo sababu nyingine tunasherehekea sikukuu ya nuru. Taa za mafuta huzimwa baada ya siku nane. YAHUSHUA, nuru inayong’aa iliyotumwa hapa duniani, mafuta ya maisha ya kweli, Atadumu MILELE. Tunasherehekea muujiza huu wa taa zote mbili. YAHUSHUA Ndiye MENORAH INAYOISHI. MWANGAZA WA MILELE ambao HAUTAWAHI kuzimwa!

Asante YAHUSHUA kwa kumpa Elisheva (Elisabeth) ufunuo huu Novemba 23, 2005. ‘Kwa kuwa ni Wewe YAHUVEH Utakayewasha taa yangu, katika jina la YAHUSHUA, Atakayemulika giza yangu.’

Tuma nuru YAKO na ukweli WAKO, kwa kuwa tunatafuta ukweli wako kupitia RUACH HA KODESH (Roho Mtakatifu), Atakayeniongoza mimi kuogopa na kupenda Majina Yenu Matakatifu, kusoma na kuweka na kufunza Torah Yenu Takatifu, Torah Iliyoandikwa, na Torah Iliyozungumzwa kama vile Neno Lililofanywa kuwa mwili, Mwana wako wa pekee, YAHUSHUA MASIHI. Na kwa bidii kuu kuheshimu Jina Lako lililobarikiwa na kuinuliwa, Jina la YAHUVEH na Mwana wako, YAHUSHUA.

Kwa minajili ya taa za Chanukah, tufanye tuwe wenye hekima kupitia mwangaza unaoishi unaotuongoza, YAHUSHUA, Torah wako Anayeishi. Neno hili litimizwe, kama ilivyoandikwa: ‘“Haitapotea mdomoni mwako, mdomoni mwa watoto wako na kutoka mdomoni mwa watoto wa watoto wako”, ndivyo Asemavyo YAHUVEH, “kutoka sasa hadi milele”.’ Watoto wangu na wajukuu wangu watii Torah na wawe watu waaminifu, na uwape nguvu katika kutii Torah na kukutii wewe, inavyoambatana na mipango Yako mizuri. Nifanikiwe kuona watoto na wajukuu wakijihusisha kwa Torah na amri zako kwa ukweli.

Fungua macho yetu ili tuweze kuelewa maajabu Yako ya Torah takatifu kuweza kueleza ukweli wa Torah na maajabu yake yote. Safisha mioyo yetu kwa kukutumikia Wewe, tuweke mbali na maovu na fikra chafu, macho yetu ione kurudi kwake Mwana wako mpendwa YAHUSHUA Atakayekuja na kutawala pale Yerusalemu kama Mfalme wa Wafalme na BWANA wa MABWANA.



Baraka za Mshumaa

Ba-rucha-tah Adonai E-lo-hei-nu, Mel-ech ha-olam,

Tunakubariki ewe YAHUVEH Mungu wetu, mfalme wa ulimwengu,

Asher kideshanu be-mitzvotav,

Uliyetutakasa kwa Neno lako,

ve-tzivanu le-hadlik ner shel Chanukah.

na kutuagiza tuwashe taa za Chanukah.

Al Ha-Nissim

(Inasemwa usiku zote nane)

Ha-ne-roth hal-la-lu, a-nach-nu mad-li-kin al ha-nis-sim,

Tunawasha hizi taa kwa ajili ya miujiza,

v’al hat-shu-oth v’al ha-nif-la-oth she-o-see-ta la-avo-tei-nu,

ukombozi na maajabu Wewe Umewatendea baba zetu wa kale,

al y’de ko-ha-ne-cho, hak-k’do- shim. V’chol sh’-mo-nath y’may

kupitia makuhani Wako watakatifu. Siku zote nane za

chanu-kah, han-ne-roth hal-lo-lu ko-desh; v’ain lo-nu r’shuth

Chanukah, taa hizi ni takatifu, haturuhusiwi kuzitumia vibaya

l’hish-ta-mesh bo-hem el-lo lir-o-tom bil-vad. K’de l’ho-doth,

lakini tunafaa kuziangalia tu, ili kutoa shukrani

L’shim-cha al ni-se-cho, v’al y’shu-o-se-te-cho, v’al nif-l’o-te-cho

Katika jina Lako kwa miujiza yako, ukombozi wako na maajabu yako.

Ba-ruch a-tah Adonai E-lo-hei-nu, Mel-ech ha-olam,

Tunakubariki ewe YAHUVEH, Mungu wetu, mfalme wa ulimwengu,

she-a-sa si-sim la-a-avo-tei-nu ba-ya-mim ha-hem ba-ze-man ha-zeh

Uliyetenda mambo ya ajabu kwa baba zetu katika nyakati za kale msimu huu.


USIKU 6:

Hesabu 7:42-47
Siku ya sita Eliasafu mwana wa Deueli, kiongozi wa watu wa Gadi, akaleta sadaka yake. Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kwa kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kila kimoja kikiwa kimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, lililojazwa uvumba, fahali mmoja mchanga, kondoo mume mmoja na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mbuzi mume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, maksai wawili, kondoo waume watano, mbuzi waume watano na wana-kondoo waume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa ndiyo sadaka ya Eliasafu mwana wa Deueli.

Zaburi 27:1
{Zaburi Ya Daudi} YAHUVEH ni nuru yangu na wokovu wangu, nimwogope nani? YAHUVEH ni ngome ya uhai wangu--nimhofu nani?

Zaburi 104:1-2
Ee YAHUVEH, wangu, wewe ni mkuu sana, umejivika utukufu na enzi. Amejifunika katika nuru kama vile kwa vazi, amezitandaza mbingu kama hema.

Zaburi 119:105
{Nun} Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga katika njia yangu.

Zaburi 19:9
Kumcha YAHUVEH ni utakatifu, nalo ladumu milele. Amri za YAHUVEH ni za hakika, nazo zina haki.

Mithali 6:23-24
Kwa maana maagizo haya ni taa, mafundisho haya ni mwanga na maonyo ya maadili ni njia ya uzima, yakikulinda na mwanamke mwovu, kutokana na maneno laini ya mwanamke mpotovu.

Yohana 9:1-7
YAHUSHUA alipokuwa akipita, akamwona mtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa. Wanafunzi Wake wakamwuliza, “Rabi, ni nani aliyetenda dhambi, ni huyu mtu au wazazi wake hata azaliwe kipofu?’’ YAHUSHUA akawajibu, “Huyu mtu wala wazazi wake hawakutenda dhambi. Alizaliwa kipofu ili kazi za Mungu zidhihirishwe katika maisha yake. Yanipasa kuzifanya kazi zake Yeye aliyenituma wakati bado ni mchana, kwa kuwa usiku waja ambapo hakuna mtu awezaye kufanya kazi. Wakati niko ulimwenguni, Mimi ni nuru ya ulimwengu.’’ Baada ya kusema haya, akatema mate ardhini, akatengeneza tope kwa mate na kumpaka yule mtu kipofu machoni. Kisha akamwambia, “Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu.” (Siloamu, maana yake ni aliyetumwa.) Ndipo yule kipofu akaenda, akanawa, naye akarudi akiwa anaona.









ALPHA & OMEGA ALMIGHTYWIND RUACH HA KODESH WILDFIRE LAST CHANCE MINISTRY



www.allmightywind.com  |   www.almightywind.com
Please go to the other if one is off line.

We are Sabbath-Keepers, Not Seventh-Day Adventists
Click Here For More Info


Mailing and Email Addresses




By Faith Enoch was translated that he should not see death: and was not found, because YAHUVEH had translated him: for before his translation he had this testimony, that he pleased YAHUVEH. Hebrews 11:5